UJUMBE WA UISLAMU KWA ULIMWENGU MZIMA
Makala hii imekwisha kutafsiriwa katika
Jamii ya vilivyomo
Full Description
- UJUMBE WA UISLAMU KWA ULIMWENGU MZIMA
- KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU.
- UTANGULIZI:
- VYANZO VYA MSINGI KATIKA DINI YA KIISLAMU.
- UPANDE WA KIROHO KATIKA UISLAMU.
- FAIDA ZINAZO PATIKANA KATIKA KUWAAMINI MALAIKA:
- FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUVIAMINI VITABU:
- FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUWAAMINI MITUME:
- FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUIAMINI SIKU YA MWISHO:
- FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUIAMINI QADARI:
- IBADA ZA KIMANENO NA VITENDO KATIKA UISLAMU (NGUZO ZA UISLAMU):
- Mtazamo wa Uislamu kuhusu uchumi:
- Mtazamo wa Uislamu kuhusu hali ya kijamii:
- Miongoni mwa haki za raia zinazo mpasa mtawala kuzitekeleza ni :-
- Ama kuhusiana na wajibu na haki zinazo wahusu watu wote;
- Upande wa tabia katika Uislamu.
- Baadhi ya adabu za Kiislamu:-
- Adabu za mazungumzo.
- HITIMISHO:
UJUMBE WA UISLAMU KWA ULIMWENGU MZIMA
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU.
UTANGULIZI:
Shukurani zote zinamsitahiki Mwenyezi Mungu,na rehma na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad,na ahli zake na maswahaba zake wote.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Sema; Enyi watu mlio pewa kitabu (cha Mwenyezi Mungu.Mayahudi na Manaswara)! njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu; ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu,wala tusimshirikishe (Mwenyezi Mungu)na chochote,wala baadhi yetu tusiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu (au pamoja na Mwenyezi Mungu).wakikengeuka ,semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni waislamu,(tumenyenyekea amri za Mwenyezi Mungu".[1]
Kwa hakika dini ya uislamu ndiyo dini ya haki,kwa kuwa ndio dini ya kimaumbile iliyo sahihi,dini iliyo wazi ambayo hakuna ndani yake ugumu wowote wala uficho wa aina yeyote, kila mtu katika uislamu ana haki ya kuuliza chochote kinacho mtatiza ,au jambo lolote linalo msumbua katika akili yake, lakini uislamu haukutoa haki ya kujibu maswali haya yanayo fungamana na mambo ya dini kwa kila mtu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “ Sema (uwaambie): “Mola wangu ameharamisha (haya:Ameharamisha) mambomachafu, yaliyodhihirika na yaliyo fichika,na dhambi na kutoka katika utii (wa wakubwa) pasipo haki,na kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika ambacho hakukiteremshia dalili (ya kusema kishirikishwe naye)na (ameharamisha)kusema juu ya Mwenyezi mungu msiyo yajua".[2]
Bali uislamu umetoa haki ya kujibu mambo yanayo fungamana na dini kwa watu wenye elimu ya kisheria, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Basi waulizeni wenye kumbukumbu (za vitabu vya Mwenyezi Mungu vya kale) ikiwa nyinyi hamjui'[3]
Na Mtume wetu Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amebainisha athari mbaya zinazo tokana na kuuliza na kutaka kupata maarifa ya mambo ya dini kwa watu ambao hawaja makinika kielimu,akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu hatoiondoa elimu kwa kuingo`a katika vifua vya waja wake wenye elimu,lakini ataiondoa elimu kwa kuwaondoa (kuwafisha) wanazuoni,mpaka itakapo fikia hakuna mwanazuoni yeyote alie bakia,basi watu watawafanya wale wasiojua kitu (kuwa ndio wajuzi) wataulizwa (juu ya mambo ya dini) nao watatoa fat-wa bila ya elimu,watapotea na kuwapoteza watu".[4]
Katika uislamu hakuna mambo ambayo ni ya ndani kabisa tunayo takiwa kuyaamini halafu tusiruhusiwe kuuliza (kwa lengo la kutaka kuyafahamu),ispokuwa mambo ambayo akili ya mwanadamu haiwezi kuyadiriki (kuyafahamu) kama vile mambo ya ghaibu (yasiyo onekana),ambayo Mwenyezi Mungu hakutubainishia,kutoka na kwamba hakuna faida yoyote kwa wanadamu kuyafahamu mambo hayo,ama yale ambayo kuna faida kwa wanadamu kuyajua katika mambo ya ghaibu basi Mola wetu Mtukufu katubainishia kupitia Mtume wake Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake.
Na sisi kama wanadamu inampitia kila mmoja wetu akilini mwake maswali ambayo anataka kupata majibu yake, basi uislamu umekuwa ni wenye kutoa majibu ya maswali haya kwa njia nyepesi, tena yenye kukinaisha. Kwa mfano:
Kama mtu atauliza kuhusu asili yake ni nini? Basi atapata jawabu katika kauli yake Mwenyezi Mungu “Na kwa yakini tulimuumba mwanadamu kwa udongo ulio safi.Kisha tukamuumba kwa tone la manii,(mbegu ya uzazi) lililo wekwa katika makao yaliyo hifadhika. Kisha tukalifanya tone hilo kuwa pande la damu,na tukalifanya pande la damu hilo kuwa pande la nyama,kisha tukalifanya pande la nyama hilo kuwa mifupa,na mifupa tukaivika nyama, kisha tukamfanya kiumbe kingine,basi ametukuka Mwenyezi Mungu m-bora wa waumbaji".[5]
Na kama mtu atataka kujua ni ipi nafasi yake na daraja yake katika ulimwengu huu kati ya viumbe vya Mwenyezi Mungu ambavyo ni vingi kabisa, basi atalikuta jawabu katika kauli yake Mwenyezi Mungu “Na hakika tumewatukuza wanadamu ,na tumewapa vya kupanda barani na baharini,na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri,na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tulio waumba,kwa utukufu ulio mkubwa (kabisa).[6]
Na kama atauliza ni upi msimamo wake kuhusu viumbe alivyo viumba Mwenyezi Mungu katika ulimwengu huu, atalikuta jawabulipo katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Mwenyezi Mungu ndie aliye kutiishieni bahari ,ili humo zipite merikebu kwa amri yake,na ili mtafute fadhila yake na mpate kushukuru.Na amekutiishieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini,vyote vimetoka kwake;bila shaka katika haya zimo alama (kubwa za neema kubwa za Mwenyezi Mungu juu yenu)kwa watu wanao fikiri".[7]
Na endapo atauliza kuhusu sababu ya kuumbwa kwake na kuletwa katika ulimwengu huu,basi atalikuta jawabu katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu. Sitaki kwao rizki wala sitaki wanilishe.Kwa yakini Mwenyezi Mungu ndie mtoaji wa rizki,Mwenye nguvu madhubuti" [8]
Na kama atauliza kuhusu huyu muumbaji ambaye kaumba ulimwengu huu,na ambaye ibada zote ni lazima zielekezwe kwake peke yake,basi atalikuta jawabu katika kauli yake Mwenyezi Mungu “Sema;Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja (tu).Mwenyezi Mungu(tu)ndiye anaye stahiki kukusudiwa (na viumbe vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea).Hakuzaa wala hakuzaliwa.Wala hana anaye fanana naye hata mmoja “.[9]
Na pia katika kauli yake Mwenyezi Mungu “Yeye ndiye wa mwanzo na ndiye wa mwisho naye ndie wa dhahiri na wa siri,naye ndie mjuzi wa kila kitu".[10]
Na kama atauliza kuhusu njia itakayo mpelekea kupata utulivu wa kiroho,na raha ya nafsi,na utulivu wa mawazo,basi jawabu atalipata katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Wale walio muamini Mwenyezi Mungu na nyoyo zao zikatulia katika kumtaja Mwenyezi Mungu,tambueni (kuwa)kwa kumtaja Mwenyezi Mungu nyoyo hupata utulivu" .[11]
Na kama atauliza kuhusu njia itakayo mpeleka katika mafaniko na kufaulu,na kupata maisha yaliyokuwa bora,basi atalikuta jawabu katika kauli ya Mwenyezi Mungu “ Watakao fanya matendo mema,wakiwa ni wanaume au wanawake,hali ya kuwa ni waumini,basi tutawapa maisha mazuri (hapa duniani) na tutawalipa malipo yao kwa mema waliyokuwa wakiyatenda".[12]
Na kama atauliza kuhusu hali ya wale wasio muamini Mwenyezi Mungu na yale aliyoyateremsha,atalipata jawabu katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu :“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu (hayo),basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki,na siku ya kiyama tutamfufua hali ya kuwa ni kipofu. Aseme; “ Ewe Mola wangu! mbona umenifufua kipofu,na hali nilikuwa nikiona? (Mungu)Atasema; “ndiyo vivyo hivyo, zilikujia aya zetu ukazisaha, (ukazipuuza),na kadhalika leo utasahauliwa (utapuuzwa) “.[13]
Na kama atauliza kuhusu dini iliyo kamilika,iliyo kusanya sheria zote zenye kuweza kuitengeneza jamii,na kuiweka sawa hali ya mtu mmoja mmoja,katika dunia yake na akhera yake,basi jawabu atalikuta katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “ Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema zangu,na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu.."[14]
Na endapo akiuliza kuhusu dini ya haki ambayo anatakiwa kuifuata,na njia sahihi itakayo mfikisha kwa Mwenyezi Mungu,na kumfikisha katika pepo,basi atalipata jawabu katika kauli yake Mwenyezi Mungu : “ Na anaye taka dini isiyo kuwa ya Kiislamu,basi haitakubaliwa kwake,naye akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa) “.[15]
Na endapo atauliza kuhusu mahusiano yake na binadamu wenzie yaweje? basi atalikuta jawabu katika kauli yake Mwenyezi Mungu : “Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (Yule) mwanamume(mmoja;Adamu)na(Yule)mwanamke(mmoja;Hawa) Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mpate kujuana (tu basi,sio mkejeliane).Hakika ahishimiwaye (mbora wenu) sana mbele ya Mwenyezi Mungu ni Yule amchae Mungu zaidi katika nyinyi".[16]
Na kama atauliza awe na msimamo gani kuhusu elimu? basi atalipata jawabu katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Mwenyezi Mungu atawainua wale walio amini miongoni mwenu,na wale walio pewa elimu watapata daraja zaidi.."[17]
Na endapo atauliza kuhusu mwisho wake katika maisha haya ya kidunia,basi atalikta jawabu katika kali yake Mwenyezi Mungu: “Kila nafsi itaonja mauti,na bila shaka mtapewa ujira wenu kamili siku ya kiyama,na aliye wekwa mbali na Moto na akaingizwa peponi,basi amefuzu (amefaulu kweli kweli),na maisha ya dunia(hii)si kitu ila starehe idanganyayo(watu) “.[18]
Na endapo atauliza kuhusu uwezekano wa kufufuliwa baada ya kufa,na kurudi kuwa na uhai tena,basi jawabu atalipata katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na akatupigia mfano,na akasahau kuumbwa kwake kwa (manii) akasema: "Nani atakaye huisha mifupa na hali imesagika?".Sema: Ataihuisha Yule aliye iumba mara ya kwanza,naye ni mjuzi wa kila (namna ya )kuumba. Ambaye amekufanyieni moto katika mti mbichi,mkawa nanyi kwa (mti)huo mnauwasha.Je Yule aliye ziumba mbingu na ardhi (mnaona) hana uweza wa kuumba(mara ya pili) mfano wao(wanadamu)?Kwanini? Naye ni Muummbaji Mkuu, Mjuzi (wa kila jambo).Hakika amri yake anapo taka chochote(kile kitokee)ni kukiambia: 'Kuwa' ,basi mara huwa".[19]
Na endapo atauliza kuhusu matendo yenye kukubaliwa mbele za Mungu baada ya kufufuliwa kwake,basi jawabu atalipata katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Kwa yakini hao walio amini na wakafanya vitendo vizuri,makaazi yao yatakuwa hizo pepo za Firdaws".[20]
Na kama atataka kujua mambo yatakuwaje baada ya kufufuliwa viumbe,basi atalikuta jawabu lenye kumbainishia wazi wazi kwamba,baada ya kufufuliwa maisha yatakuwa ni ya milele,na njia ni mbili tu hakuna ya tatu,ima mtu ataingia peponi au ataingia Motoni, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Bila shaka wale walio kufuru miongoni mwa watu walio pewa kitabu na washirikina,wataingia katika Moto wa Jahannamu,wakae humo milele; hao ni viumbe waovu. Hakika wale walio amini na kutenda mema ,basi hao ndio viumbe wema. Malipo yao mbele ya Mola wao ni mabustani ya daima, ambayo mito inapita mbele yake,wakae humo milele; Mwenyezi Mungu amewaridhia, nao wameridhika. (Malipo) hayo ni kwa Yule anaye muogopa Mola wake".[21]
Mpendwa msomaji:
Kwa yakini kabisa mimi ninahakikisha kwamba katika uislamu ndiko kunapatikana ufumbuzi wa matatizo yote ambayo yanautatiza ulimwengu wetu leo hii, na kwamba kuufuata uislamu na kuutekeleza ipasavyo ndio ufumbuzi pekee wa matatizo hayo. Na ulimwengu umekwisha jaribu nidhwam na njia zote ambazo zimewekwa na wanadamu, na wamethibitisha wenyewe kwamba nidhamu hizo zimeshindwa kuleta ufumbuzi wa matatizo tuliyo nayo, sasa kwanini ulimwengu usijaribu kutekeleza uislamu?, amesema (F.Filweas)[22] : “Yameandika magazeti hivi karibuni kwamba wanafalsafa na waandishi wa Nchi za kimagharibi wanadai kwamba hizi dini zilizopo hivi sasa zimekwisha pitwa na wakati…na kwa hiyo kuna haja sasa ya kuachana nazo, maneno haya yanatubainishia ni tabu kiasi gani wanayo ipata waandishi na wana falsafa wa kimagharibi, kwa sababu ya magumu wanayo pambana nayo katika dini ya kikristo, lakini watu hawa wanakosea,kwa sababu Uislamu ambao ndio jawabu na ufumbuzi pekee wa matatizo yote hayo bado upo, na uko tayari kutatua matatizo yao, kwa nini basi hawataki kuujaribu"?!.
Naamini kuwa sitakuwa ni mwenye kukosea nikisema kuwa waislamu wengi katika zama hizi wako mbali kabisa na kufuata na kutekeleza mafundisho sahihi ya Uislamu, kwa sababu mambo wanayoyafanya wengi katika waislamu katika maisha yao ya kila siku yako mbali kabisa na mafundisho ya Uislamu, na malengo yake. Maana uislamu sio kama wanavyo dhani baadhi ya watu kwamba ni ibada maalumu ambazo hutekelezwa katika nyakati maalumu tu basi, bali Uislamu ni itikadi, na ni sheria, na ni muongozo wa kiibada, na matendeano na watu,Uislamu ni dini na ni Dola kwa maana yake halisi.
Amesema mseaji mmoja: “Utukufu ulioje wa dini ya Kiislamu lau ingelikuwa na watu wenye kutekeleza misingi yake na mafundisho yake, na wakafuata maamrisho yake na wakajitenga na makatazo yake, na wakaifikisha kwa mataifa mengine kwa mujibu wa maelekezo ya Mwenyezi Mungu yanayo sema: “Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na kwa mawaidha yaliyo mazuri, na ujadiliane nao kwa njia nzuri".[23]
Amesema (J.S.restler)[24] katika utangulizi wa kitabu chake alicho kiita: Utamaduni wa Waarabu. “ Hakika neno Uislamu linaweza kuchukuliwa katika maana tatu tofauti: Maana ya kwanza ni Dini, na maana ya pili ni Dola, na maana ya tatu ni Utamaduni. Kwa kifupi ni utamaduni wa kipekee".
Hakika Uislamu kwa itikadi yake na ibada zake,na matangamano na watu,na mafundisho yake, tangu ulipoteremka (Uislamu) kwa Mtume Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake mpaka leo hii bado haujabadilika wala kugeuka, lakini walio badilika na kugeuka ni Waislamu, hivyo basi pindi mtu anaye jinasibisha na Uislamu anapokosea na kufanya jambo linalo katazwa kisheria, haimaanishi kwamba mafundisho ya Uislamu yanamuamrisha kufanya hivyo, au yanakubaliana na jambo hilo, na ili kufafanua zaidi maneno haya hebu tupige mfano mwepesi tu, unao weza kutusaidia kulielewa vizuri jambo hili. Lau kama tukimpa mtu flani Ala (chombo) ambacho kimeachanishwa, kisha tukampa kitabu cha maelekezo ambacho kimeandaliwa na mtu aliye itengeneza Ala hiyo, kinachoelezea njia sahihi ya kukiunganisha kifaa hicho, endapo mtu huyo atakosea katika zoezi la kukiunga tena,au akakiunga kwa njia nyingine tofauti na maelekezo yaliyoko katika kijitabu hicho,je tutasema kuwa maelekezo yaliyoko katika kile kitabu sio sahihi au tutasemaje?! Bila shaka kutakuwa na majibu ya aina tatu:
1. Kwamba mtu huyu hakufuata utaratibu aliouelekeza mtengenezaji wa chombo hicho.
2. Au kwamba hakufuatilia vizuri hatua alizo elekezwa katika kitabu cha maelekezo.
3. Au kwamba hakufahamu maelekezo yaliyomo katika kile kitabu cha maelekezo.
Na katika hali hii ya tatu inamlazimu arejee katika kampuni iliyo tengeneza ili wambainishie vizuri njia sahihi ya kuunganisha kifaa kile, na matumizi sahii. Mfano huu ndio mfano wa Uislamu, inampasa mwenye kutaka kuujua Uislamu auchukue kutoka katika vyanzo vyake vilivyo sahihi, kwa sababu kuijua dini ni lazima uisome kwa watu
wanao ifahamu vizuri, huu ndio utaratibu sahihi. Ndio maana mtu anapo ugua anakwenda kwa Daktari, na anaye taka kujenga anamtafuta Mhandisi, vivyo hivyo katika kila kitu ni lazima kichukuliwe mahala pake.
Ombi langu kwa kila atakaye soma kitabu hiki,namuomba ajiepushe na ushabiki wa kidini na mtazamo alio nao katika fikra zake, aipe uhuru akilii yake, akisome kitabu hiki kwa usomaji wa mtu anaye kusudia kuifikia haki na kuijua, na sio usomaji wa mtu anaye kusudia kutafuata wapi muandishi kateleza ili amtoe makosa,na kumtia kasoro, akisome usomaji wa mtu anaye taka kuipa nafasi akili yake ihukumu, na sio mapenzi ndio yahukumu, ili asije akawa ni miongoni mwa watu ammbao Mwenyezi Mungu kawataja kwa sifa mbaya, pale alipo sema katika kitabu chake kitukufu: “Na pindi wanapo ambiwa yafuateni yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu,wao husema: Bali sisi tunafuata yale tuliyo wakuta nayo baba zetu, je hata kama baba zao walikuwa hawajui chochote wala hawakuongoka (watawafuata ntu)? “.[25]
Mwanadamu yeyote ambaye kaendelea, ambaye kastaarabika ni yule mwenye kuitumia akili yake vizuri, ni yule ambaye haazimi akili yake kwa wengine, ni yule ambaye hakubaliani na jambo lolote ispokuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina, na pindi anapo kinaika basi hufanya haraka kulifanyia kazi jambo ambalo amekinaika nalo,pia hawi ni mwenye kuyafanyia ubakhili mambo aliyokinaika nayo, bali huyaeneza na kuyatangaza kwa watu mambo ambayo kayafanyia utafiti na uchunguzi wa kina, kwa kumuelimisha asie yajua, na kumrekebisha ambaye kafahamu tofauti.
Na mimi kwa hakika siwezikusema kwamba maudhui hii nimeielezea kwa mapana na marefu katika kitabu changu hiki, na hii ni kutokana na maelezo niliyo yatanguliza kwamba Uislamu ni nidhamu ambayo imepangilia utaratibu wa maisha yetu ya hapa Duniani pamoja na Akhera,na ili kuyabainisha yote hayo yanahitaji kitabu kikubwa sana, na sio katika kijitabu kidogo kama hiki, na ndio maana nimetosheka na kuashiria tu baadhi ya mambo, na tabia ambazo ndio za msingi , na mwenendo wa kiislamu ,ili iwe ni kama ufunguo kwa mwenye kutaka kufanya utafiti na uchunguzi zaidi juu ya ukweli wa dini ya Kislamu.
Lakini inawezekana mtu akasema kuwa katika nidhwamu na kanuni zilizopo katika jamii mbali mbali katika ulimwengu wetu hivi sasa, yako mabo yanayo fanana na nidhamu zilizo letwa na Uislamu!
Lakini jawabu la swali hili ni kwamba, ni kipi kilicho tangulia,Uislamu au hizi nidhamu za kibinadamu? Bila shaka sheria za Kiislamu zimetangulia, sheria za kiislamu zimekuwa zikitumika zaidia ya karne kumi na nne(14)zilizo pita, hivyo nidhamu yoyote katika nidhamu hizi za kibinadamu inayoonekana kufanana na nidhamu ya Kiislamu na sheria zake basi imechukuliwa katika sheria na nidhamu za Uislamu, hasa ukizingatia kwamba kulikuwa na watafiti mbali mbali wasio kuwa waislamu walio jaribu kutafiti kuhusu Uislamu tangu kudhihiri kwake, ingawaje nia zao zilikuwa tofauti tofauti. Wako walio kusudia kujua haki iko wapi ili waifuate, pia wako walio tafiti kwa malengo ya kuizuia haki na kupambana nayo.
Kimeandikwa na:
Dr. Abdulrahman Al-sheha
Falme za kiarabu Saudi Arabia
S.L.P.59565
Riyadh 11535
VYANZO VYA MSINGI KATIKA DINI YA KIISLAMU.
Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipokuwa katika viwanja vya Mina katika Hijja yake ya kuaga alisema: “Je mnajua leo hii ni siku gani"? maswahaba wakamjibu kwa kusema: (Mungu na Mtume wake ndio wajuao),Akasema: “Siku hii ni siku tukufu, je mnajua huu ni mji gani"? wakasema ;( Mungu na Mtume wake ndio wajuao) ,akasema: “Ni mji mtukufu, je mnajua ni mwezi gani huu"? wakasema; ( Mungu na Mtume wake ndio wajuao), akasema: “Ni mwezi mtukufu" kisha akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu ameziharamisha kwenu damu zenu, na mali zenu, na heshima zenu, kama alivyo iharamisha (itukuza) siku yenu hii, katika mwezi wenu huu,katika mji wenu huu.."[26]
Hivyo basi miongoni mwa vyanzo vya msingi kabisa katika dini ya Kiislamu ni kuhifadhi na kuzilinda nafsi za watu,na heshima zao,na mali zao,na akili zao,na vizazi vyao,na kumhifadhi na kumlinda mnyonge na mtu asiye jiweza:-
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu uharamu wa kuifanyia uadui nafsi ya mwanadamu: “Wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza (kuiua) isipokuwa kwa haki (akahukumu hakimu kuwa mtu huyo anastahiki kuuawa na akatoa amri ya kuuawa) “.[27]
Na akasema vile vile Mwenyezi Mungu: “wala msiziue nafsi zenu, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye huruma kwenu".[28]
Na amsema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu uharamu wa kuwavunjiia watu heshima: “Wala msikaribie zinaa,hakika hiyo zinaa ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa) “.[29]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu uharamu wa kuzifanyia uadui mali za watu: “Wala msiliane mali zenu kwa batili.."[30]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu uharamu wa kuiharibu akili :“Enyi mlio amini ! bila shaka ulevi ,na kamari,na kuabudiwa (na kuombwa)asiye kuwa Mwenyezi Mungu,na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli (na kwa njia zinginezo); (yote haya) ni uchafu (ni) katika kazi za shetani,basi jiepusheni navyo ili mpate kufaulu".[31]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu uharamu wa kuangamiza kizazi: “Na wanapo ondoka wanakwenda huku na huko katika ardhi kufanya uharibifu humo na kuangamiza mimea na roho (za watu), na Mwenyezi Mungu hapendi uharibifu".[32]
Na kuhusu haki za wanyonge, Mwenyezi Mungu anasema:
1. Kuhusu haki za wazazi wawili: “Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yeyote ila yeye tu. Na (ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa)wazazi wawili, kama mmoja wao akifikia uzee,(naye yuko) pamoja nawe,au wote wawili, basi usiwambie hata Ah! Wala usiwakemee, na useme nao kwa msemo wa heshima (kabisa) ,na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa (njia ya kuwaonea) huruma (kwa kuwaona wamekuwa wazee). Na useme: “Mola wangu! Warehemu (wazee wangu) kama walivyo nilea katika utoto" .[33]
Na kuhusu haki za yatima, anasema Mwenyezi Mungu: “Basi usimuonee yatima"[34].
Na kuhusu kuhifadhi mali yake,akasema: “Wala msiikaribie (msiiguse ) mali ya yatima ispokuwa kwa njia iliyo bora (kwa hao mayatima)"[35].
Na kuhusu haki za watoto, Mwenyezi Mungu anasema: “Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umaskini, sisi tutakupeni riziki nyinyi na wao pia"[36]
Na kuhusu haki za wagonjwa, Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anasema: “Wakomboeni mateka, na walisheni wenye njaa, na watembeleeni wagonjwa"[37]
Na kuhusu haki za wanyonge, amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake “Si miongoni mwetu asiye waheshimu wakubwa, na kuwahurumia wadogo, na akaamrisha mema na kukataza mabaya" .[38]
Na kuhusu haki za wenye matatizo Mwenyezi Mungu amesema: “Ama mwenye kuomba usimkemee".[39]
Na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amesema: “Mtu mwenye kujali haja za ndugu zake ,basi Mwenyezi Mungu huzijali haja zake".[40]
UPANDE WA KIROHO KATIKA UISLAMU.
Hakika Dini (sheria) ya Kiislamu ni kama zilivyo dini nyingine alizo ziteremsha Mwenyezi Mungu kabla yake , Imekuja na vyanzo, na itikadi zinazo wawajibisha wafuasi wake kuziamini, na kuziitakidi, na kuzieneza, na kuzilingania bila ya kuwalazimisha watu. Na hii ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini,uongofu umekwisha pambanuka na upotofu, basi anaye mkataa shetani na akamwamini Mwenyezi Mungu, bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichokuwa na kuvunjika, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia (na) Mwenye kujua".[41]
Na Uislamu umewaamrisha wafuasi wake ulinganiaji wao katika dini uwe ni kwa njia nzuri, kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri , na jadiliana nao kwa njia iliyo nzuri"[42].
Swala la kukinaika ni swala la msingi sana katika uislamu, kwa sababu imani inayokuwa katika misingi ya kulazimishwa inamfanya mtu atamke kwa ulimi wake maneno yaliyotofauti na itikadi iliyoko moyoni mwake, na huu ndio unafiki ambao uislamu umetahadharisha sana na kuutaja (unafiki) kuwa ni mbaya kuliko ukafiri. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini (kabisa) katika moto(wa Jahanam).[43]
Kwa upande wa kiibada :-
Uislamu umekuja na ibada mbali mbali za kimaneno, na za kivitendo, na za kiitikadi, ambazo katika uislamu zinaitwa nguzo za imani, ambazo ni hizi:-
1. Kumuamini Mwenyezi Mungu:
Na kumuamini Mwenyezi Mungu kunamtaka mtu ampwekeshe Mwenyezi Mungu katika mambo matatu:
Kumpwekesha katika sifa yake ya uumbaji, yaani kuitakidi na kukiri kuwa yupo, nayeye peke yake ndiye muumba wa Ulimwengu na vyote vilivyomo, na Yeye ndiye mwenye kuvimiliki na kuviendesha atakavyo, yeye ndiye mtendaji pekee ambaye hakuna wa kumzuia katika jambo lolote, haliwi katika ulimwengu huu ila alitakalo yeye. Kasema Mwenyezi Mungu mtukufu: "Fahamuni: kuumba (ni kwake tu Mwenyezi Mungu) na amri zote ni zake (Mwenyezi Mungu). Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote".[44]
Na kwa hakika Mwenyezi Mungu amebainisha hoja na dalili zinazo onyesha kwamba yeye ndiye Muumbaji pekee aliposema: "Mwenyezi Mungu hakujifanyia mtoto, wala hakukuwa na mungu mwingine pamoja naye, ingekuwa hivyo basi kila mungu angewachukua alio waumba; na baadhi yao wangeliwashinda wengine (maana lazima wangepigana; kwani fahari wawili hawakai zizi moja). Mwenyezi Mungu ametakasika na sifa wanazo msifu nazo (zisizo kuwa ndizo)[45].
Kumpwekesha katika sifa yake ya uungu, yaani kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu wa kweli,hakuna Mungu wa kweli ispokuwa Yeye, na hakuna anaye stahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Yeye tu, hakuna anaye stahiki kutegemewa ila Yeye, na hakuna wa kuombwa ila Yeye, na hawekewi nadhiri ila Yeye, na hakuna ruhusa ya kuelekeza aina yoyote ile ya ibada ispokuwa kwake tu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu :"Na hatukumtuma kabala yako Mtume yoyote ila tulimfunulia ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mimi, basi niabuduni".[46]
Kumpwekesha katika majina yake na sifa zake; yaani kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu anayo majina mazuri mazuri na sifa tukufu, na kwamba ametakasika na kila upungufu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu ;" Na Mwenyezi Mungu anayo majina mazuri mazuri; basi muombeni kwayo, na waacheni wale wano pindisha (utakatifu wa ) Majina yake, karibuni hivi watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda".[47]
Kwa hiyo tunayathibitisha yale ambayo Mwenyewe kajithibitishia katika kitabu chake (Qur-ani) au kayathibitisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na kwamba hafanani katika majina hayo na yeyote katika viumbe wake, tunayathibitisha bila kutafuta kujua namna yake, au kuyageuza, au kuyafananiza na kuyashabihisha. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: "Hakuna chochote mfano wake; naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona".[48]
2. Kuwaamini Malaika:
Nako ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu anao Malaika wengi, hakuna ajuaye idadi yao ila Mwenyezi Mungu, wanatekeleza matakwa ya Mwenyezi Mungu katika kuendesha na kuchunga ulimwengu huu na vilivyomo kwa mujibu wa maamuzi ya Mwenyezi Mungu[49], wamepewa majukumu ya mbinguni na ardhini, na kila harakati inayotokea ulimwenguni ni katika utendaji wao kwa mujibu wa matakwa ya Mwenyezi Mungu mtukufu, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu; " Na niaapa kwa Malaika wenye kupangilia mambo (mbinguni na ardhini kwa idhini ya Mola wao) "[50]
Na akasema tena katika sura nyingine; "Naapa kwa Malaika wenye kuyagawa mambo na kuyaendesha kwa idhini ya Mwenyezi Mungu"[51]
Na Malaika wameumbwa kwa nuru. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Malaika wameumbwa kwa nuru, na wameumbwa Majini kwa moto, na akaumbwa mwanadamu kutokana na kile mlichoelezwa"[52]
Nao Malaika ni katika vitu vya ghaibu (visivyo onekana), japokuwa wameumbwa kwa nuru, lakini Mwenyezi Mungu kawapa uwezo wa kujigeuza katika maumbile tofauti tofauti ili waonekane, kama alivyo tueleza Mola wetu kuhusu Malaika Jibrilu kwamba alimuendea Mama Maryam katika sura ya kibinadamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na (Maryam) akaweka pazia kujikinga nao, tukampelekea Roho wetu (Jibril) akajimithilisha kwake (kwa sura ya ) binadamu aliye kamili. (Maryam) akasema: Hakika mimi najikinga kwa (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa Rehma aniepushe nawe. Ikiwa unamuogopa Mwenyezi Mungu ( basi ondoka nenda zako). (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mjumbe wa Mola wako; ili nikupe mwana mtakatifu"[53]
Na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alimuona Malaika Jibrilu katika umbile lake halisi akiwa na mbawa mia sita, hali kalifunika anga kutokana na ukubwa wake.[54]
Na Malaika wameumbwa na mbawa, wako wenye mbawa mbili ,wako wenye tatu, wako wenye zaidi ya hizo, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu: " Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi, aliye wafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili mbili na tatu tatu na nne nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo.."[55]
Ama kuhusu hali zao zingine hilo ni katika elimu ya Mwenyezi Mungu peke yake. Muda wao wote huutumia katika kumtaja Mwenyezi Mungu na kumsifu na kumtukuza ; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu : " Wanamtukuza Mwenyezi Mungu usiku na mchana wala hawachoki"[56] Mwenyezi Mungu kawaumba ili wamuabudu. Amesema: " Masihi (Nabii Issa) hataona unyonge kuwa Mja wa Mwenyezi Mungu wala Malaika walio kurubishwa (na Mwenyezi Mungu hawataona unyonge kuwa waja wa Mwenyezi Mungu"[57]
Na hao Malaika wanakuwa ni wajumbe baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake katika wanadamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu; " Ameyateremsha haya Roho mwaminifu (Jibril). Juu ya moyo wako ili uwe miongoni mwa waonyaji. Kwa lugha ya kiarabu iliyo wazi (fasihi) "[58]
Na wanatekeleza majukumu anayo waamrisha Mwenyezi mungu kuyatekeleza. Amesema Mwenyezi Mungu: "Wanamuogopa Mola wao aliye juu yao, na wanatenda wanayo amrishwa".[59]
Na hao Malaika sio watoto wa Mwenyezi Mungu, lakini tunawajibika kuwaheshimu na kuwapenda. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu : "Na makafiri wanasema (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehma amejifanyia mtoto ,ametakasika (Mwenyezi Mungu) Bali (hao Malaika) ni waja (wa Mwenyezi Mungu) walio tukuzwa . Hawamtangulii kwa neno (lake analosema), nao wanafanya amri zake (zote) ".[60]
Wala wao hawana ushirika na Mwenyezi Mungu katika sifa zake za uungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " wala hatakuamrisheni kuwafanya Malaika na Manabii kuwa waungu. Je, atakuamrisheni ukafiri baada ya kuwa nyinyi Waislamu? ".[61]
Miongoni mwa hao Malaika wamo ambao Mwenyezi Mungu katueleza majina yao na kazi zao kwa mfano;
- Jibril: Yeye kapewa majukumu ya kuteremsha Wahyi (ufunuo). Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Ameyateremsha haya Roho mwaminifu (Jibril). Juu ya moyo wako ili uwe miongoni mwa waonyaji"[62]
- Mikail: Amepewa majukumu ya mvua na mimea. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu : " Anaye mfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail (anatafuta kuangamia) kwani Mwenyezi Mungu atakuwa adui wa makafiri hao "[63]
- Malaika wa mauti: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Sema : Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa kwenu, kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu".[64]
- Israafil : Kapewa majukumu ya kupuliza parapanda kwa ajili ya kufufuliwa viumbe ili kuhesabiwa. Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu : " Basi litakapo pulizwa para panda, (baragumu), hapo hautakuwepo ujamaa baina yao siku hiyo wala hawataulizana".[65]
- Maalik :Yeye ni milnzi wa Moto. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Nao watapiga kelele (kumwambia yule Malaika anaye waadhibu waseme): Ewe Malik! Naatufishe Mola wako, Malik atasema: Bila shaka mtakaa humuhumu ".[66]
- Zabania: Hao ni Malaika walio pewa majukumu ya kuwaadhibu watu wa Motoni. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Basi na awaite wanachama wenzake (wamsaidie). Na sisi tutawaita Zabania (Malaika wa Motoni wamuadhibu) ".[67]
- Na kila mwanadamu amepewa Malaika wawili, mmoja anasajili mema yake, na mwingine anasajili maovu yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu : " Wanapo pokea wapokeaji wawili, anaye kaa kuliani na (anaye kaa) kushotoni (yaani Malaika). Hatoi kauli yoyote ispokuwa karibu yake yuko mngojeaji tayari (kuandika) "[68]
- Ridhwan: Yeye ni milinzi wa pepo. Na wako Malaika walio pewa jukumu la kumchunga na kumhifadhi mwanadamu…na wengi wengineo ambao wametajwa katika Qur-ani na katika Sunna, pia wako wengine wengi ambao hatukuelezwa lakini inatulazimu kuwaamini wote.
FAIDA ZINAZO PATIKANA KATIKA KUWAAMINI MALAIKA:
1. Tunapata kujua utukufu wa Mwenyezi Mungu mtukufu na uwezo wake na kwamba kakizunguka kila kitu kwa elimu yake, maana utukufu wa viumbe ni dalili juu ya utukufu wa aliye viumba.
2. Kuwaamini Malaika kunatuhamasisha katika kufanya mambo ya kheri na kujitenga na mabaya, katika hali ya siri na uwazi, pindi pale Mwislamu anapo tambua kuwa kuna Malaika wanao sajili maneno yake na vitendo vyake, na kwamba kila alifanyalo litakuwa ima la kheri kwake au dhidi yake.
3. Kuwaamini Malaika kunatusaidia kujitenga na mambo ya uzushi, na itikadi batili walizonazo wasio amini ghaibu (mambo yasiyo onekana).
4. Tunapata kujua huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kwa kule kuwawekea Malaika wanao wahifadhi na kuyaendesha mambo yao.
5. Kuviamini vitabu.
Ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu kateremsha vitabu kutoka kwake, kaviteremsha kwa Mitume wake, ili wavifikishe kwa watu, na kwamba vitabu hivyo vimebeba haki, na kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uungu wake na uumbaji wake na katika majina na sifa zake .Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili za waziwazi na tukaviteremsha vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu"[69]
Na Mwislamu anatakiwa kuviamini vitabu vyote vilivyo teremshwa kabla ya Qur-ani, na kuamini kuwa vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, lakini hawajibiki kuvifanyia kazi na kuvifuata baada ya kushuka qur-ani, kwa sababu vitabu hivyo vimete-remshwa kwa muda maalumu na kwa watu maalumu. Miongoni mwa vitabu hivyo ambavyo Mwenyezi Mungu kavieleza ni:
v Swahifa za Ibrahimu na Musa: Na Qur-ani imetubainishia baadhi ya sheria zilizo kuja katika suhuf hizo, akasema Mwenyezi Mungu: " Au hakuambiwa yaliyomo katika vitabu vya Mussa ?. Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi (ya Mwenyezi Mungu) .Kwamba haichukui nafsi dhambi za nafsi nyingine. Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyo yafanya. Na kwamba amali yake itaonekana. Kisha atalipwa malipo yaliyo kamilika".[70]
v Taurati: Hiki ni kitabu kitakatifu alicho teremshiwa Nabii Mussa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Hakika tuliteremsha taurati yenye uongofu na nuru; ambayo kwayo Manabii walio jisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu) waliwahukumu Mayahudi, na watawa na maulamaa pia (walihukumu kwa hiyo Taurati), kwa sababu walitakiwa kuifadhi kitabu (hicho) cha Mwenyezi Mungu; nao walikuwa mashahidi juu yake. Basi (nyinyi Waislamu) msiwaogope watu, bali niogopeni (Mimi). Wala msibadilishe Aya Zangu kwa thamani chache (ya duniani). Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri ".[71]
Na quur-ani tukufu imebainisha baadhi ya yaliyo kuja katika Taurati, miongoni mwa hayo ni kutaja baadhi ya sifa za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ambazo wale wasio taka haki miongoni mwao wanajitahidi sana kuzificha. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makfiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (pamoja) wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi (Yake). Alama zao zi katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika taurati".[72]
Pia Qur-ani imebainisha baadhi ya hukumu za kisheria zilizotajwa ndani ya Taurati. Akasema Mwenyezi Mungu: " Na humo (katika Taurati) tuliwaandikia ya kwamba mtu (huuawa) kwa mtu, najicho (hutolewa) kwa jicho, na pua (hukatwa) kwa pua, na sikio (humeguliwa) kwa sikio, na jino ( hung`olewa)kwa jino, na itakuwa kulipiziana kisasi katika kutiana majeraha. Lakini atakaye samehe basi itakuwa kafara kwake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu " .[73]
v Zaburi: Hiki ni kitabu kilicho teremshwa kwa Nabii Daudi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Daudi tukampa Zaburi "[74]
v Injili: Na hiki ni kitabu kitakatifu kilicho teremshwa kwa Nabii Issa (Yesu). Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na Tukawafuatishia (Mitume hao) Isa bin Maryam kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na Tukampa Injili iliyomo ndani yake uongofu na nuru na isadikishayo yaliyo kuwa kabla yake, na uongozi na mawaidha kwa wamchao Mwenyezi Mungu (wanao muogopa) ".[75]
Na kwa hakika Qur-ani tukufu imebainisha baadhi ya mambo yaliyo kuja katika Taurati na Injili, ikiwa miongoni mwa hayo ni kubashiri ujio wa Nabii Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake,
amesema Mwenyezi mungu Mtukufu : " Na rehma yangu inaweza kukienea kila kitu. Lakini nitawaandikia (kweli kweli kabisa) wale wanao jikinga na yale niliyo wakataza, na wanatoa zaka, na wanaziamini aya Zetu. Ambao wanamfuata Mtume Nabii aliye Ummy (asiye jua kusoma wala kuandika, na juu ya hivi atafundisha mafundisho hayo ya ajabu ya Uislamu) ambaye wanamuona ameandikwa kwao katika Taurati na Injili, ambaye anawaamrisha mema na anawakataza yaliyo mabaya, na kuwahalalishia vilivyo vizuri, na kuwaharamishia vibaya, na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao.."[76]
Na miongoni mwa yaliyo kuja katika vitabu hivyo ni kuhimiza watu kuipigania dini ya Mwenyezi Mungu ili neno la Mwenyezi Mungu liwe ndilo liko juu. Hivyo basi Jihadi haikuja katika sheria ya Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake peke yake bali ilikuwepo hata katika vitabu vilivyo tangulia kabla ya Qur-ani. Amesema Mwenyezi Mungu : " Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waislamu nafsi zao na mali zao (watoe nafsi zao na mali zao katika kupigania Dini yake) ili na Yeye awape Pepo, wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu; wanaua na wanauawa. Hii ndio ahadi aliyo jilazimisha Mwenyezi Mungu ) katika Taurati na Injili na Qur-ani, na ninani atekelezaye zaidi ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye (Mwenyezi Mungu) , na huko ndiko kufuzu kukubwa".[77]
v Qur-ani tukufu: Ni wajibu kuamini kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu, ambayo kashuka nayo Malaika Jibrilu kwa Mtume Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake yakiwa katika lugha ya kiarabu iliyo fasaha. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu : " Ameteremsha haya Roho muaminifu, (Jibril). Juu ya moyo wako ili uwe miongoni mwa waonyaji. Kwa lugha ya kiarabu wazi wazi (fasihi) ".[78]
Nayo Qur-ani tukufu inatofautiana na vitabu vilivyo itangulia katika mambo yafuatayo:
1. Kwamba Qur-ani ndicho kitabu cha mwisho katika vitabu vilivyo teremshwa, kikiwa kinavisadikisha vitabu vilivyo tangulia, ambavyo havikugeuzwa wala kubadilishwa kutoka katika kulingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na uwajibu wa kumtii, na kumuabudu Yeye peke yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "
Na tumekuteremshia Kitabu kwa (ajili ya kubainisha) haki, kinacho sadikisha vitabu vilivyo kuwa kabla yake, na kuvihukumia (kama haya ndiyo yaliyo haribiwa ama ndiyo yaliyo salimika) ".[79]
2. Mwenyezi Mungu amefuta kupitia Qur-ani vitabu vilivyo tangulia, kwa sababu Qur-ani imekusanya mafundisho ya Mwenyezi Mungu yote ambayo ni yenye kudumu , yanayo faa kwa kila zama na kila mahali. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu".[80]
3. Qur-ani imeteremshwa kwa ajili ya watu wote, sio kwamba ni kitabu kinacho wahusu baadhi ya watu tu kama vitabu vilivyo tangulia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " (Hiki ni) kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatoe watu katika giza uwapeleke katika nuru kwa idhini ya Mola wako.."[81]
Ama vitabi vilivyo tangulia hata kama vinakubaliana katika asili ya Dini, lakini sheria zake zilikuwa ni kwa watu maalumu, katika zama maalum tu. Kwa mfano Nabii Issa (Yesu) alisema: "Sikutumwa ispokuwa kwa kondoo wa izraeli walio potea"[82]
4. Kwamba Qur-ani ni kitabu ambacho kukisoma ni ibada, na pia kukihifadhi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Mwenye kusoma herufi moja tu katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi huandikiwa kwa herufi hiyo jema moja, na hilo jema moja malipo yake nisawa na mema kumi, kisha akafafanua kwa kusema: Simaanishi kwamba (Alif,Laam,Miim) ati ndio herufi moja, bali Alif ni herufi , na Lam ni herufi, na Mim ni herufi ".[83]
5. Kwamba Qur-ani imekusanya sheria zote ambazo ndio sababu ya kusimamisha jamii iliyokuwa bora. Amesema (J.S.Restler)[84] katika kitabu chake alicho kiita Utamaduni wa kiarabu: " Hakika qur-ani inatoa ufumbuzi wa matatizo yote, na inaelekeza mafungamano baina ya kanuni za dini na kanuni za kitabia, na imetilia maanani sana swala la kuweka nidhamu na umoja katika jami, na kupunguza uovu na upweke, na dhana potofu, na imetilia maanani sana swala la kuwajali wanyonge,na inausia wema, na inaamrisha kuoneana huruma…na kwa upande wa sheria zake imeweka ufafanuzi wa ndani sana wa kila jambo linalo husu maisha ya kila siku, na ikaweka nidhamu katika maswala ya mafungamano na mirathi, na kwa upande wa kifamilia ikapam-banua majukumu ya kila mmoja .Kwa mfano namna ya kuishi na watoto, watumwa, wanyama, mambo ya kiafya, mavazi n.k "
6. Qur-ani ni kama ushahidi wa kihistoria unao bainisha mfululizo wa kuteremka Dini kwa Manabii na Mitume , na mambo yaliyo wasibu kutoka kwa watu wao, kuanzia kwa Nabii Adamu mpaka kufikia kwa Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ambaye ndio wa mwisho wao.
7. Mwenyezi Mungu ameilinda kutokana na kuchezewa kwa nama yoyote, ima kwa kuongeza jambo lolote, au kupunguza, au kubadili au kugeuza, ili ibakie kwa watumpaka siku ambayo Mwenyezi Mungu atairithi ardhi na vilivyomo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Hakika sisi ndio tulio teremsha mauidha haya (hii Qur-ani); na hakika sisi ndio tutakao yalinda ".[85] Ama vitabu vingine Mwenyezi mungu hakuchukua ahadi ya kuvilinda, kwasababu viliteremshwa kwa ajili ya watu maalumu na kwa zama maalumu, na ndio maana vikabadilishwa na kugeuzwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu ugeuzaji walioufanya Mayahudi katika Taurati :" Mnatumaini (nyinyi waislamu) ya kwamba watakuaminini (hao Mayahudi); na hali baadhi yao walikuwa wanasikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wanayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua ? "[86]
Na kuhusu ubadilishaji wa wakristo katika Injili amesema Mwenyezi Mungu: "Na kwa wale walio sema: "Sisi ni Manasara" tulichukua ahadi kwao, lakini wakaacha sehemu (kubwa) ya yale waliyo kumbushwa, kwahiyo tukaweka baina yao (wenyewe kwa wenyewe) uadui na bughdha mpaka siku ya Qiyama. Na Mwenyezi Mungu atawaambia waliyo kuwa wakiyafanya. Enyi watu wa kitabu! Amekwisha kufikieni Mtume wetu, anaye kudhihirishieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika kitabu, na husamehe mengi. Bila shaka imekwisha kufikieni nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kitabu kinacho bainisha kila (jambo) ".[87]
Na miongoni mwa uzushi wa Mayahudi na Wakristo waliouingiza katika dini yao, ni madai ya Mayahudi kwamba Uzair ni mwana wa Mungu, na madai ya Wakristo kuwa Yesu ni mwana wa Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Mayahudi wanasema: Uzair ni mwana wa Mungu, na Manasara wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima), wanayaiga maneno ya wale walio kufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize, wanageuzwa namna gani hawa! ".[88]
Qur-ani tukufu imewarudi na kusahihisha hizo itikadi zao potofu. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu. Mwenyezi Mungu (tu) ndiye anaye stahiki kukusudiwa (na viumbe vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea). Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja) .[89]
Ndugu msomaji! Kutokana na maelezo yaliyotangulia tunapata kufahamu kwamba Injili zilizopo hivi sasa mikononi mwa watu sio katika Maneno ya Mwenyezi Mungu, wala sio katika maneno ya Nabii Issa (Yesu), bali hayo ni katika maneno ya wafuasi wake na wanafunzi wake, ambao wamechanganya ndani yake historia yake, na mawaidha yake, na wasia wake, na wakayageuza mengi sana na kuyabadilisha mafundisho yake sahihi kwa malengo yao na maslahi binafsi. Amesema Kasisi:T.J.[90]Taakir :" Kwa hiyo zikatolewa Injili ili kuweka wazi na kubainisha matakwa ya kikundi ambacho ziliandikwa kwa ajili yake, na kwa hakika ilitumika historia sahihi katika kuziandaa,ila hatukusita kugeuza au kubadilisha kwa kuongeza au kupunguza kila ilipo bidi kulingana na malengo ya muandishi".
FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUVIAMINI VITABU:
Tunapata kutambua huruma na mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kwa kuwateremshia vitabu vinavyo waelekeza katika njia sahihi itakayo wafikisha katika radhi zake, wala hakuwaacha hivi hivi wakitapatapa huku wakipotezwa na shetani pamoja na matamanio yao.
Tunapata kutambua kuwa Mwenyezi Mungu ni mweye hekima, maana kila watu kawawekea sheria zinazo lingana na hali zao.
Kupitia imani hii wanajitenga waumini wa kweli na wasio wakweli katika kudai kwao imani, kwa sababu mwenye kukiamini kitabu alichoteremshiwa Mtume anaye mfuata, imani hiyo inamlazimisha kuviamini pia vitabu walivyoteremshiwa Mitume wengine, ambavyo ndani yake mnakuwa na bishara ya vitabu vingine na Mitume wengine.
Kuviamini vitabu ni sababu ya kupata malipo makubwa mbele za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa sababu mwenye kukiamini kitabu chake na vitabu vingine vilivyo teremshwa baada yake hupata malipo mara mbili.
Kuwaamini Mitume:
Nako ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu kawachagua baadhi ya wanadamu akawafanya ni Mitume na Manabii, akawatuma kwa viumbe wake wakaja na sheria zake ili kuitekeleza ibada ya Mwenyezi Mungu na kuisimamisha Dini yake, na kumpwekesha katika sifa yake ya Uumbaji na Kuabudiwa, na wampwekeshe katika majina yake na sifa zake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na hatukumtuma kabla yako Mtume yoyote ila tulimfunulia ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mimi, basi niabuduni ".[91]
Na akawaamrisha kuzifikisha sheria zake kwa watu, ili wasije kuleta hoja yoyote baada ya kuwa wamefikiwa na Mitume, kwahiyo wao wanambashiri kuipata radhi ya Mwenyezi Mungu na Pepo yake kila atakaye waamini na akayaamini waliyo kuja nayo, na wanamuonya kutokana na ghadhabu za Mwenyezi Mungu kila atakaye wapinga na akayapinga waliyo kuja nayo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na hatutumi Mitume ila huwa ni watoaji wa habari njema na waonyaji. Na wenye kuamini na kufanya wema haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. Na wale waliokadhibisha Aya zetu itawagusa (itawapata) adhabu kwa sababu ya kule kuasi kwao".[92]
" Na kwa yakini tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimlia (majinayao na habari zao), na wengine hatukukusimlia.." [93]
Ni lazima kuwaamini Mitume wote, na kwamba wao ni wanadamu, hawana jambo lolote linalo watoa katika sifa ya uanadamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: " Hatukuwatuma (hatukuwapa utume) kabla yako ila wanaume (wa kibinadamu, si Malaika); tulio wafunulia, (tulio waletea Wahyi). Basi waulizeni wenye kumbu kumbu (ya mambo ya zamani) ikiwa nyinyi hamjui. Wala hatukuwajaalia (hao Mitume kuwa) miili isiyokula chakula, wala hawakuwa wenye kuishi milele (wasife) ".[94]
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Mtume Muhamad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Wambie: Bila shaka mimi ni binadamu kama nyinyi (ispokuwa nimeletewa wahyi tu, ndio tofauti yangu). Ninaletewa wahyi ya kwamba Mungu wenu ni Mungu mmoja tu. Anayependa kukutana na (jazaaya) Mola wake na afanye vitendo vizuri wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake ".[95]
Na akasema Mwenyezi Mungu kuhusu Nabii Isa (Yesu): " Masihi bin Maryam si chochote ila ni Mtume (tu). (Na) bila shaka Mitume wengi wamepita kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. (Na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na wakienda choo. Basi waungu gani wanao kula na kwenda choo)?! Tazama jinsi tunavyo wabainishia aya , kisha tazama jinsi wanavyo geuzwa (kuacha haki) ".[96]
Na wao hawamiliki sifa yoyote miongoni mwa sifa za uungu, hawana uwezo wa kumnufaisha yeyote, wala kumdhuru yeyote, wala hawana sifa ya kuuendesha ulimwengu n.k. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Sema: Sina mamlaka ya kujipa nafuu wala kujiondolea madhara ila apendavyo Mwenyezi Mungu, na lau kama ningelijua ghaibu ningejizidishia mema mengi; wala yasingelinigusa madhara."[97]
Na hao Mitume wameitekeleza amana na wakayafikisha yale waliyo tumwa kuyafikisha, nao ni wakamilifu katika viumbe, kielimu na kimatendo. Na Mwenyezi Mungu kawalinda na uongo na khiyana na kuwa wazembe katika kufikisha ujumbe wake. Amesema Mwenyezi Mungu : " Na haiyumkini kwa Mtume kuleta miujiza ispokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu".[98]
Na inatupasa kuwaamini wote, mwenye kuwaamini baadhi yao na asiwaamini wengine, basi huyo anakuwa kakufuru na ametoka katika Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu " Hakika wale wanao mkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume yake, na wanataka kutenga baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume yake, kwa kusema: wengine tunawaamini na wengine tunawakataa, na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya (si ya kiislamu khasa wala ya kikafiri). Basi hao ndio makafiri kweli, na tumewaandalia makafiri adhabu idhalilishayo ".[99]
Na Qur-ani tukufu imetutajia majina ya Mitume ishirini na tano(25). Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na hizi ndizo (baadhi ya) hoja Zetu tulizo mpa Ibrahimu juu ya watu wake, tunamnyanyua katika vyeo yule tumtakaye (kwa kuwa anakwenda mwendo tunao utaka) .Hakika Mola wako ndiye Mwenye hekima (na) ndiye ajuaye. Na tukampa ( Ibrahimu mtoto anaye itwa) Is-haq na (mjukuu anaye itwa) Yaaqubu, wote tukawaongoa. Na Nuhu tulimuongoa zamani (kabla ya kuja Nabii Ibrahimu ulimwenguni). Na katika kizazi chake (Nuhu, tulimuongoa) Daudi na Suleymani na Ayubu na Yusufu na Musa na Haruni. Na hivi ndivyo tuwalipavyo wafanyao mema. Na ( tukamuongoa) Zakaria na Yahya na issa na Ilyas wote (walikuwa) miongoni mwa watu wema. Na (tukamuongoa) Ismail na Alyasaa na Yunus na Luti, na wote tukawafadhilisha juu ya walimwengu (wote katika zama zao) ".[100]
Na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu Adamu " Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adamu na Nuhu na kizazi cha Ibrahimu na kizazi cha Imrani (babake Musa, na Imrani Mwengine aliye baba yake Maryam) juu ya walimwengu wote(wa zama zao).[101]
Na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu Huud; " Na kwa kina Adi tuliwapelekea ndugu yao Hud, akasema :Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu nyinyi hamna Mungu ispokuwa Yeye .Hamkuwa nyinyi ila ni watungao uongo tu (katika kusema masanu kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu).[102]
Na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu Swaleh: " Na kwa Thamud tukampeleka ndugu yao Swaleh akasema: Enyi watu wangu muabuduni Mwenyezi Mungu; nyinyi hamna Mungu ila Yeye".[103]
Na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu Shuaib : " Na kwa watu wa Madyan (tulimpeleka) ndugu yao Shuaib, akasema: Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye".[104]
Na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu Idris " Na (mtaje )Ismail na idris, na Dhul kifli, wote walikuwa miongoni mwa wanao subiri ".[105]
Na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu Muhammad akieleza kuwa Yeye ndiye wa Mwisho, na hakuna Nabii wala Mtume baada yake mpaka siku ya Qiyama : " Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na mwisho wa mitume"[106]
Hivyo Dini yake Muhamad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ni yenye kutimiliza Dini zilizo tangulia, na ndio ya mwisho na kwahiyo itakuwa ndio Dini iliyo kamilika na ya kweli ambayo inampasa kila mtu kuifuata, na ndiyo yenye kubakia mpaka siku ya Qiyama.
Na katika hao Mitume wako ambao walipata matatizo makubwa sana katika kuwafikishia watu wao ujumbe wa Mwenyezi Mungu, na wakawa ni wavumilivu sana katika hilo, nao ni: Nuhu, Ibarahimu, Musa, Isa(Yesu), na Muhamad-rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwaendee wote. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na wakumbushe tulipochukua ahadi kwa Manabii (wote) na kwako wewe, na Nuhu na Ibrahi na Musa na Isa mwana wa Maryam, naTulichukua kwao ahadi ngumu".[107]
FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUWAAMINI MITUME:
Tunapata kutambua huruma ya Mwenyezi Mungu na mapenzi yake kwa waja wake, kwa kuwatumia Mitume watokanao na wao ili wawafikishie sheria zake, na wawe ni kiigizo katika kuwalingania watu.
Kupitia kuwaamini Mitume wanapata kujitenga waumini wa kweli na wasio wakweli ,kwa sababu mwenye kumuamini Mtume aliye tumwa kwake inamlazimu kuwaamin wengine ambao wamebashiriwa katika kitabu chao.
Tunapata kutambua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa waja wake walio waamini Mitume wake wote malipo maradufu.
5. Kuiamini siku ya mwisho (Qiyama).
Ni kuwa naitikadi kwamba maisha haya ya kidunia iko siku yatakwisha na Dunia kumallizika. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Kila kilichoko juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka .Inabaki Uso wa Mola wako (tu mwenyewe) Mwenye Utkufu na Hishima ".[108]
Pindi Mwenyezi Mungu atakapo taka Dunia hii imalizike atamuamrisha Malaika Israfil kupuliza Parapanda, hapo watakufa viumbe wote, kisha atamuamuru kupuliza tena mara ya pili na hapo watu watainuka kutoka makaburini mwao wakiwa hai na viwiliwili vyao vitajikusanya kutoka katika ardhi, tangia kwa baba yetu Adamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na litapigwa baragumu watoke roho wote waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila yule amtakaye Mwenyezi Mungu. Kisha litapigwa kwa mara nyingine, hapo watafufuka (wote) wawe wanatazama (lipi litatokea) ".[109]
Na kuiamini siku ya mwisho ni pamoja na kuyaamini yote aliyoyaeleza Mola wetu Mtukufu, na aliyo yaeleza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katika mambo yanayo tokea baada ya kufa, kama vile:
1. Kuyaamini maisha ya kaburini. Na kipindi hiki kinaanza baada ya kufa mwanadamu mpaka siku ya Qiyama, na kwamba waumini wananeemeshwa humo makaburini mwao, na makafiri walio yakanusha mafundisho ya Mola wao wanaadhibiwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na adhabu mbaya ikawazunguka hao watu wa Firauni pamoja naye. Adhabu za Motoni wanadhihirishiwa (makaburini mwao) asubuhi na jioni. Na siku itakapo tokea kiyama (kutasemwa) waingizeni watu wa Firaun katika adhabu kali zaidi (kuliko hii waliyo ipata kaburini) ".[110]
2. Na kuamini kwamba kuna kufufuliwa ; Yaani kuwa na yakini kwamba Mwenyezi mungu Mtukufu atawafufua katika siku hiyo viumbe wote, watoke makaburini mwao wakiwa hawakuvaa nguo, tena wako peku peku, hali yakuwa hawakutahiriwa (wakiwa katika maumbile yao kamili kama siku walipo zaliwa). Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu: "Walio kufuru wanadaikuwa hawatafufuliwa, sema: Kwanini? kwa haki ya Mola wangu, nyinyi lazima mtafufuliwa, kisha lazima mtajulishwa mliyo yatenda (na mlipwe kwayo). Na hayo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu".[111]
Na kwa kuwa jambo la kufufliwa ni jambo ambalo watu wengi wanalikanusha, Mwenyezi Mungu kaleta mifano mingi sana katika Qur-ani akibainisha uwezekano wa kufufuliwa, na akazirudi na kuzibatilisha hoja za wanao lipinga jambo hili, miongoni mwa mifano hiyo ni :
- Mwenyezi Mungu Kawataka wafikirie pale anapo ihuisha ardhi iliyokuwa maiti (isiyoweza kuotesha chochote). Akasema Mwenyezi mungu: " Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake inataharaki na kukua na kuotesha kila namana ya mimea mizuri . Hayo ni kwa sababu Mwenyezi mugnu yuko,na kwamba Yeye huwahuisha wafu, na kwamba Yeye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu . Na kwamba Kiyama kitakuja, hapana shaka ndani yake, na kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini".[112]
- Wafikiri juu ya kuumbwa mbingu na ardhi, ambavyo ndio viumbe vikubwa kuliko mwanadamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Je! hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi na hakuchoka kwa kuziumba ana uwezo wa kuwafufua wafu? Naam, hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu ".[113]
- Wafikirie kitendo cha mtu kulala usingizi na kuamka, hakika kitendo hicho ni kama kuwa hai baada ya kuwa alikuwa kafariki, na ndio maana usingizi ukaitwa kifo kidogo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Mwenyezi Mungu hutakabadhi roho wakati wa mauti yao, na zile (roho) zisizo kufa (bado pia Mwenyezi Mungu anazitabadhi) katika usingizi wao, basi huzizuia zile alizo zikidhia mauti, (alizo zihukumu kufa), na huzirudisha zile zingine mpaka(ufike)wakati ulio wekwa, bila shaka katika hayo yamo mzingatio kwa watu wanao tafakari".[114]
- Wafikirie katika umbile la mwanzo la mwanadamu; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na akatupigia mfano na akasahau kuumbwa kwake (kwa manii) akasema: Nani atakaye huisha mifupa na hali imesagika?. Sema; Ataihuisha Yule Aliye iumba mara ya kwanza, Naye ni Mjuzi wa kila (namna ya) kuumba".[115]
3.Na kuamini kuwa kutakuwa na kufufuliwa; Yaani kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua viumbe wote kwa ajili ya kuonyeshwa matendo yao waliyo yatenda duniani na ili waweze kulipwa kulingana na matendo yao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na wakumbushe siku tutakayo iendesha milima (angani inaruka kama sufi), na utaiona ardhi iwazi (imenyooka moja kwa moja,haikuzibwa kwa milima wala miti walavinginevyo). Nasi (siku hiyo) Tutawafufua (viumbe wote) wala Hatutamwacha hata mmoja kati yao. Na watahudhurishwa mbele ya Mola wako safu safu, (na wataambiwa); Bila shaka mmetujia kama Tulivyo kuumbeni mara ya kwanza".[116]
4.Na kuamini kwamba viungo vya mwanadamu vitamtolea ushahidi. Amesema Mwenyezi Mungu: "Hata watakapoujia (huo Moto), hapo ndipo masikio yao na macho yao na ngozi zao(na viungo vyao vingine) zitakapotoa ushahidi juu yao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. Na wao waziambie (hizi) ngozi zao; Mbona mnatushuhudia? Nazo ziwaambie Mwenyezi Mungu aliye kitamkisha kila kitu ndiye aliye tutamkisha, naye ndiye aliye kuumbeni mara ya kwanza. Na kweli (hivi sasa) mnarudishwa. Na hamkuwa mnajificha hata masikio yenu na macho yenu na ngozi zenu (na viungo vyenu vingine) zisiweze kutoa ushahidi juu yenu, bali mlidhani ya kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika (hayo) mnayo yafanya".[117]
5. Na kuamini kwamba kuna kuulizwa na kuhojiwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wasimamisheni (hapo) hakika wataulizwa. (Waambiwe) Muna nini?mbona hamnusuriani?. Bali wao siku hiyo watadhalilika kabisa"[118]
6 .Kuamini kwamba kuna daraja (ambayo ni njia iliyopo juu ya moto wa Jahanam, na watu wote watapita katika njia hiyo, wasalimike wa kusalimika na waangamie katika Moto wa kuangamia) Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Wala hakuna yoyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia (hiyo Jahanam) ni wajibu wa Mola wako uliokwisha hukumiwa. Kisha tutawaokoa wale wamchao Mungu, na tutawaacha madhwalimu humo wamepiga magoti".[119]
7.Kuamini kwamba vitendo vya wanadamu vitapimwa katika mizani, na watalipwa walio fanya mema malipo sitahiki kutokana na mema yao, na imani zao, na kuwafuata kwao Mitume, na waovu nao wataadhibiwa ikiwa ni malipo ya uovu wao na kuwapinga kwao Mitume na kuwaasi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Nasi tutaweka mizani za uadilifu siku ya Qiyama, na nafsi yoyote haitadhulumiwa hata kidogo, na hata kama (jambo hilo lina) uzito mdogo wa chembe ya hardali nalo Tutalileta. Nasi tunatosha kuwa (wazuri kabisa) wa hisabu ".[120]
8. Kuamini kuwa watu watagawiwa vitabu vilivyo sajiliwa ndani yake matendo yao waliyo yatenda. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Ama atakaye pewa daftari lake katika mkono wake wa kulia. Basi yeye atahesabiwa hesabu nyepesi. Na atarudi kwa watu wake(peponi) na hali ya kuwa ni mwenye furaha. Lakini atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake. Basi yeye atayaita mauti (yamjie ili afe apumzike,wala hayatamjia). Na ataingizwa Motoni".[121]
9.Kuamini kuwa kuna malipo ya Pepo au Moto, na kwamba humo yatakuwa ni maisha ya milele. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Bila shaka wale walio kufuru miongoni mwa watu walio pewa kitabu, na washirikina wataingia katika Moto wa Jahanamu, wakae humo milele, hao ni waovu wa viumbe. Hakika wale walio amini na kutenda mema, basi hao ndio wema wa viumbe. Malipo yao kwa Mola wao ni Mabustani ya daima ambayo mito inapita mbele yake,wakae humo milele ;Mwenyezi Mungu amewaridhia, nao wameridhika. (Malipo ) hayo ni kwa yule anaye muogopa Mola wake".[122]
10. Kuamini kuwa kuna Mto Peponi ambao kapewa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na kwamba kutakuwa na uombezi, na mengine mengi aliyo yaeleza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuhusu siku hiyo ya Qiyama.
FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUIAMINI SIKU YA MWISHO:
Inamsaidia mtu kujiandaa na siku hiyo kwa kudumu katika kufanya matendo mema,na kuwa ni mwenye kufanya haraka kuliendea kila jambo la kheri kwa ajili ya kutarajia malipo mema,na anakuwa ni mwenye kuyaacha maasi na kujitenga mbali nayo kwa ajili ya kuziogopa adhabu za Mwenyezi Mungu katika siku hiyo ya Qiyama.
Kuiamini siku ya mwisho pia inakuwa ni kiliwazo chema kwa waumini kwa yale yanayo wapita hapa duniani, kutokana na malipo mema wanayo yatarajia kwa Mwenyezi Mungu siku ya mwisho.
Kuiamini siku ya Mwisho ni njia ya kupambanua baina ya waumini na wasio waumini.
6.Kuamini uwezo wa Mwenyezi ungu.
Nako ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu,alikijua kila kitu tangu mwanzo kabla hata ya kutokea kwake, na akajua kila kitakacho tokea, kisha akavifanya hivyo vitu vikawepo, kwa mujibu wa elimu Yake na makadirio Yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kiasi (chake makhsusi).[123]
Kwahiyo mambo yote yaliyo kwisha tokea, na yanayo tokea, na yatakayo tokea, katika ulimwengu huu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyajua kabla ya kutokea kwake kisha akayafanya yatokee kwa matakwa Yake na mipangilio Yake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Mja yoyote hawezi kuwa muumini wa kweli mpaka aamini uwezo na maamuzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ya kheri na ya shari, na kwamba jambo lolote linalo mfika basi lisingeweza kumkosa, na kwamba linalo muepuka basi halikuwa limekadiriwa kumfika".[124]
Lakini kuamini hivi hakupingani na mtu kufanya sababu zinazo kubalika: Kwa mfano mtu akitaka uzazi ni lazima afanye sababu zitakazo mpelekea kufikia lengo lake hilo, ambazo ni kuoa, lakini sababu hii inaweza kuleta natija anazo zitarajia (kizazi) na pia natija zaweza zisipatikane kulingana na matakwa ya Mwenyezi Mungu na uamuzi Wake, maana hizo sababu sio kwamba ndio kila kitu bali lazima atake Mwenyezi Mungu Mtukufu.Na hizi sababu tuzifanyazo pia ni katika makadirio yake Mwenyezi Mungu, na ndio maana Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema katika kuwabainishia Maswahaba wake pindi walipo muuliza wakaseama: Vipi kuhusu dawa tunazo zitumia kujitibu je zinaweza kuzuia jambo ambalo kaisha likadiria Mwenyezi Mungu? Akasema " Hizo dawa pia ni katika makadirio ya Mwenyezi Mungu".[125]
Na njaa ,kiu na baridi pia ni miongoni mwa vitu alivyo vikadiria Mwenyezi Mungu, lakini hata hivyo kila mtu hufanya kila awezalo ili kujikinga navyo kwa kutafuta chakula, kinywaji, na mavazi ya kuzuia baridi, kwahiyo wanaizuia Qadari ya Mwenyezi Mungu kwa Qadari ya Mwenyezi Mungu
FAIDA ZIPATIKANAZO KATIKA KUIAMINI QADARI:
- Inamfanya mtu awe ni mwenye kuridhika na kila litakalo mpata, kuifanya nafsi yake iwe ni yenye kutulia,na hawi ni mwenye masikitiko na unyonge kwa yanayo mfika ,au kwa anayo yakosa. Nadhani wote tunakubaliana kwamba kutokuwa na utulivu wa nafsi na mawazo, humpelekea mtu kupatwa na maradhi ya nafsi ambayo hufikia hatua ya kuuathiri hata mwili. Lakini kuiamini Qadari na maamuzi ya Mwenyezi Mungu kunamuepusha mtu na mambo yote haya. Amesema Mwenyezi Mungu Mutkufu: " Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kabla hatuja muumba. kwa yakini hilo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu. Ili msihuzunike sana kwa kitu kilicho kupoteeni (na kinacho kupoteeni), wala msifurahi sana kwa Alicho kupeni (na kwa Anacho kupeni), na Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye".[126]
- Kuiamini Qadari kunampelekea mtu kuwa na hima katika kutafuta elimu na uvumbuzi kuhusu mambo mbalimbali aliyoyaweka Mwenyezi Mungu Mtukufu katika ulimwengu huu; Maana yale mambo anayo yakadiria Mwenyezi Mungu yampate mwanadamu kama maradhi na matatizo mbalimbali yanamfaya aongeze juhudi katika kuyatafutia ufumbuzi kupitia vitu balimbali alivyo viumba Mwenyezi Mungu katika ulimwengu huu, hivyo anaweza kuiondoa Qadari ya kwanza kupitia qadari ya pili.
-Kupitia kuiamini Qadari anapata mtu kuliwazika kutokana na matatizo mbalimbali yanayo msibu; kwamfano mtu akipata hasara katika biashara zake, jambo hili kwake ni msiba, lau kama utaufuatishia huzuni, na masikitiko, basi anakuwa kapatwa na misiba miwili, msiba wa hasara, na msiba wa huzuni; Ama aliye iamini Qadari na kwamba kila kitu kinatokea kwa matakwa yake Mola, bila shaka ataridhika na hasara ya mwanzo kwasababu anaamini kuwa ilikwisha pangwa imfike na hakukuwa na njia ya kuiepuka .Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendwa na Mwenyezi Mungu kuliko muumini ambaye ni dhaifu, lakini kila mmoja kati yao ana ubora wake. Yapupie mambo yaliyo na manufaa kwako, na umtegemee Mwenyezi Mungu, wala usiwe ni mwenye kushindwa, na endapo litakufika jambo usiseme: Lau kama ninge fanya kadha basi ingelikuwa kadha, lakini useme hivi: Hivi ndivyo alivyo kadiria Mwenyezi Mungu, nae hufanya alitakalo. Kwa sababu neno "Lau…" hufungua njia ya shetani."[127] (yaani humpa shetrani njia ya kukutawala na hatimae kukuingiza mawazo yasiyo sahihi).
Na kuamini Qadari sio kama wanavyo dhania baadhi ya watu kwamba maana yake ni kuto kufanya sababu, bali ni kukaa na kungojea kwamba lililo kadiriwa litakuja tu! hapana. Na haya tunayapata kupitia majibu ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliyo mijbu mtu mmoja aliye muuliza kuhusu ngamia wake akasema: Je nimuache aende tu nitawakali kwa Mwenyezi Mungu? Akamwambia "Hapana, bali mfunge kisha utawakali kwa Mwenyezi Mungu".[128]
IBADA ZA KIMANENO NA VITENDO KATIKA UISLAMU (NGUZO ZA UISLAMU):
Na ibada hizi ndio msingi na kipimo cha Uislamu wa mtu.Na katika nguzo hizi ziko ambazo ni za kimaneno, nazo ni Shahada mbili, na ziko ambazo ni za kivitendo, ambazo ni Swala na Kufunga, na ziko ambazo ni za kimali, ambazyo ni kutoa Zaka, pia ziko ambazo zinajumuisha mwili pamoja na mali, ambayo ni Hijja. Lakini ni muhimu kutambua kwamba Uislamu haukusudii katika Ibada hizi tulizo zitaja kwamba watu wafanye vitendo tu peke yake, bali lengo kubwa katika Ibada hizi ni kuzitakasa nafsi na kuziweka katika muelekeo ulio sawa kupitia Ibada hizi. Uislamu unataka ibada hizi iwe ni sababu ya kutengenea kila mtu na hatimae jamii kwa ujumla. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Ibada ya swala: "Bila shaka Swala (ikisaliwa vilivyo) humzuilia( huyo mwenye kusali na) mambo machafu na maovu".[129]
Na akasema Mwenyezi Mungu kuhusu Ibada ya Zaka "Chukua sadaka katika mali zao uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao) ".[130]
Na akasema vilevile kuhusu Ibada ya Swaumu: " Enyi mlio amini ! mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyo lazimishwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu".[131]
Kwahiyo saumu ni malezi na mazoezi ya kujizuia na matamanio ya nafsi, nahii ndio tafsiri ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuhusu swaumu aliposema: " Mtu ambaye hakuacha kusema uongo na kuyaacha mambo ya kipuuzi, basi Mwenyezi Mungu hana haja ya kumuona akiacha chakula chake na kinywaji chake".[132] Yaani kufunga kwake hakuna faida yoyote, maana hakulifikia lengo la funga.
Na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu Ibada ya Hijja: " Hijja ni miezi maalumu, na anayekusudia kufanya Hijja katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu, wala asibishane katika hiyo Hijja".[133]
Hivyo basi Ibada katika uislamu zina nafasi kubwa sana katika kujenga tabia nzuri na kuzilinda. Na nguzo za Uislamu ni hizi zifuatazo:
Nguzo ya kwanza:Shahada mbili.
Nayo ni kushuhudia kwamba hakuna anaye stahiki kuabudiwa kwa haki Ispokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, na kushuhudia kwamba Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na nguzo hii, ambayo ni ya kimaneno kama tulivyo tanguliza ndio ufunguo wa kuingia katika Uislamu, ambao unafuatiwa na nguzo zingine zilizo bakia.
Maana ya shada ( LAA ILAAHA ILALLAHU ).
Hili ndilo neno la tauhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), kwa sababu ya neno hili Mwenyezi Mungu kawaumba viumbe, na akaumba Pepo na Moto. Amesema Mwenyezio Mungu Mtukufu: " Sikuwaumba Majini na watu ila wapate kuniabudu".[134]
Na huu ndio ulikuwa wito (ulingano) wa Mitume na Manabii wote kuanzia Nabii Nuhu mpaka kufikia kwa Mtume wa Mwisho Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na hatukumtuma kabla yako Mtume yoyote ila tuli mfunulia ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mimi, basi Niabuduni".[135]
Na maana yake ni kwamba:-
-Hakuna aliye umba ulimwengu huu ila Mwenyezi Mungu peke yake.
-Hakuna anaye miliki wala kuendesha ulimwengu huu ila Mwenyezi Mungu peke yake.
-Hakuna anaye sitahiki kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu Peke yake.
-Kwamba Mwenyezi Mungu anasifika kwa sifa za ukamilifu, na ametakasika na kila aina ya upungufu.
Mambo yanayo fungamana na shahada (LAA ILAAHA ILALLAHU).
1. Kutambua kwamba kila kinachoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu ni batili, maana hakuna anaye sitahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mwenyezi Mungu tu,Yeye ndiye anastahiki ibada zote zielekezwe kwake, kama vile swala, maombi, vichinjwa, nadhiri, na kadhalika. Hata kama ni Nabii au Malaika hawastahiki kuelekezewa aina yoyote miongoni mwa aina za Ibada. Na yoyote mwenye kuelekeza aina yoyote ile ya Ibada kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu basi huyo anakuwa kakufuru hata kama anatamka shahada mbili.
2. Kuwa na yakini isiyo na shaka yoyote ndani yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wenye kuamini kweli kweli ni wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; kisha wakawa si wenye shaka, na wakapigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, hao ndio wenye kuamini kweli".[136]
3. kulikubali tamko hili (shahada) bila ya kulipinga. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wao walipokuwa wakiambiwa hakuna aabudiwaye kwa haki ispokuwa Mwenyezi Mungu, walikuwa wakikataa".[137]
4. Kufanya matendo yanayo kubaliana na tamko hilo, pamoja na kunyeyekea, na kafuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kuacha makatazo yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na ajisalimishaye uso wake kwa Mwenyezi Mungu, na hali ya kuwa anawafanyia mema (viumbe wenzie) bila shaka amekwisha kamata fundo lililo madhubuti; na mwisho wa mambo yote ni kwa Mwenyezi Mungu".[138]
5. Awe ni mkweli katika hilo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Wanasema kwa ndimi zao (maneno) yasiyo kuwemo nyoyoni mwao" .[139]
6. Awe ni ni mwenye kumtakasia nia Mwenyezi Mungu katika ibada zake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala hawakuamrishwa ila kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, waache dini za upotofu na wasimamishe swala".[140]
7. Ampende Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na vipenzi wa Mwenyezi Mungu pamoja na waja wake wema, na awachukie na kujitenga na wale wanaomfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na awe ni mwenye kuyatanguliza yale ayatakayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake hata kama yanapingana na matakwa ya nafsi yake. Amesema Mwenyezi Mungu : " Sema: Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mlizo chuma na biashara mnazo ogopa kuharibikiwa, na majumba mnayo yapenda; (ikiwa vitu hivi) ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu waasi( njia iliyo nyooka).[141]
Na pia katika mambo yanayo fungamana na shahada ni kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye haki ya kuweka utaratibu wa kiibada, na kupangilia mambo ya waja wake kuanzia mtu mmoja mmoja mpaka ngazi ya jamii kwa ujumla, nayeye peke yake ndiye mwenye haki ya kuhalalisha na kuharamisha, kwa kupitia Mtume wake. Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu: "Na anacho kupeni Mtume basi kipokeeni, na anacho kukatazeni basi jiepusheni nacho".[142]
Ni kumtii kwa kila aliloliamrisha, na kumsadikisha katika kila alilo lieleza, na kujitenga na kila alilo likataza na kulikemea. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Mwenye kumtii Mtume amemtii Mwenyezi Mungu".[143] Na hii inamaanisha :
Kuukubali utume wake na kwamba yeye ndiye wa mwisho katika Mitume na Manabii, nayeye ndiye mbora wao. Amesema mwenyezi mungu Mtukufu: " Muhamad si baba wa yoyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu".[144]
Kukubali kwamba yote aliyo yaeleza yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, sio kwa matamanio ya nafsi yake. Amesema Mwenyezi Mungu: "Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya (anayo sema) ila ni Wahyi (ufunuo)ulio funuliwa (kwake) ".[145]
Ama katika mambo yake mengine ya kidunia Yeye ni kama watu wengine, katika maswala yake binafsi alikuwa akijitahidi na kutumia rai yake,kama alivyo sema: " Hakika mimi ni mwanadamu kama nyinyi, na hakika nyinyi mnashitakiana kwangu, na huenda mmoja wenu akawa ni fasaha katika kujieleza kuliko mwenzie, nami ninampa haki kulingana na jinsi nilivyo sikia, hivyo nitakaye mhukumia haki ya ndugu yake basi asiichukue, maana atambue nitakua nimemkatia kipande cha Moto".[146]
Kuitakidi na kukubali kwamba ujumbe alio kuja nao unawahusu watu wote pamoja na Majini, mpaka siku ya Qiyama. Amesema Mwenyezi Mungu: "Na hatukukutuma (hatukukuleta) ila kwa watu wote uwe mtoaji wa habari nzuri na muonyaji"[147]
Kuufuata mwenendo wake na kushikamana nao bila ya kuzidisha chochote. Amesema Mwenyezi Mungu : " Sema: ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni (hapo) Mwenyezi Mungu atakupendeni, na atakusameheni madhambi yenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye msamaha na Mwenye rehema".[148]
Nguzo ya pili: Kusimamisha Swala.
Hii ndio nguzo ya Dini, na mwenye kuiwacha anakufuru na kutoka katika Dini. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Kichwa cha mambo yote ni Uislamu, na muhimili wake ni swala, na kilele chake ni kupigania Dini ya Mwenyezi Mungu".[149]
Na hii swala ni maneno maalumu na vitendo maalumu ambavyo hufunguliwa kwa kupiga takbira na hufungwa kwa kutoa salamu. Ibada hii Mwislamu anaitekeleza kwa ajili ya kumtukuza na kumtii Mola wake, katika wakati huo anaachana na mambo yote ya kidunia kwa ajili ya kunong`ona na Mola wake kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana, kwa hiyo swala ni mawasiliano baina ya mja na Mola wake, maana kila Mwislamu anapo zama katika ladha za kidunia na nuru ya imani katika moyo wake ikaanza kufifia mara muadhini anaadhini kwa ajili ya swala na nuru ya imani inaangaza tena, kwa hiyo anakuwa ni mwenye mawasiliano na Mola wake kila wakati. Na hizi swala ni tano usiku na mchana, wanasizswali waislamu hali ya kujumuika pamoja miskitini, ispokuwa mwenye udhuru. Mkusanyiko huu unawafanya waweze kujuana, na wawe na mapenzi baina yao, na kujuliana hali zao, ambaye ni mgonjwa basi wanamtembelea, na mwenye matatizo wanamsaidia, na mwenye majonzi wanamliwaza, na mwenye kuwa na uzembe basi wanampa nasaha. Na hii swala ni njia ya kuondoa utabaka katika jamii, maana waislamu husimama kwa pamoja katika safu moja wakubwa kwa wadogo, maskini kwa tajiri, mtukufu (mheshimiwa) kwa mnyonge, wote wako sawa katika kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kunyenyekea, wameelekea sehemu moja, na vitendo vyao ndani ya swala ni vya aina moja, na usomaji wao ni wa aina moja, tena katika wakati mmoja.
Nguzo ya tatu: Kutoa Zaka.
Na hii zaka ni kiwango maalumu katika mali anatakiwa mwislamu mwenye uwezo kukitoa katika mali yake, hali yakuwa nafsi yake imeridhika, katika hali ya kumtii Mola wake na kutekeleza agizo lake katika kufanya hivyo, ana wapa ndugu zake mafakiri na masikini na wenye matatizo ili kutatua haja zao, na kuwaepusha na udhalili wa kuomba omba. Na zaka hii ni wajibu juu ya kila Muislamu ambaye kamiliki kiwango maalumu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Wala hawakuamrishwa ila kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawache dini za upotofu na wasimamishe swala na kutoa zaka, hiyo ndiyo Dini iliyo sawa"[150]
Mwenye kupinga uwajibu wake (kwamba si wajibu) anakuwa kakufuru, maana anakuwa kazuilia haki za wanyonge, na masikini na mafakiri. Na hii zaka sio kodi kwamba inachukuliwa na dola kama wanavyo dai wasio jua Uislamu, maana ingekuwa ni kodi basi ingekuwa ni lazima kwa kila anaye ishi katika dola ya Kiislamu, awe ni Muislamu au sio Muislamu, lakini ni wazi kwamba Zaka ina sharti zake. Na miongoni mwa sharti zake ni kuwa mwenye kuitoa awe ni Muislamu.
Na sharti za Zaka zilizo wekwa na sheria ni :
1- Mtoaji awe kamiliki mali inayofikia kiwango kilicho wekwa na sheria, ambacho thamani yake ni sawa na garmu (85) za Dhahabu.
2- Mali hiyo iwe imepitiwa na mwaka mzima. Na mali zinazotolewa zaka ni wanayama wafugwao, pesa, bidhaa za kibiashara. Ama nafaka zaka yake hutolewa pale zinapo komaa, na matunda pia hutolewa zaka yake yanapo kuwa tayari. Na Uislamu tayari umebainisha wanao sitahiki kupewa hizo Zaka pale alipo sema Mwenyezi Mungu " Sadaka hupewa (watu hawa); Mafakiri na masikini na wanao zitumikia, na wanao tiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislamu), na katika kuwapa uungwana watumwa, na katika kuwasaida wenye deni, na katika (kutengeneza) mambo aliyo amrisha Mwenyezi Mungu, na katika (kupewa) wasafiri (walio haribikiwa). Ni faradhi inayo toka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima".[151]
Na hii Zaka ni sawa na asilimia 2.5% ya mali. Uislamu umekusudia katika kuifaradhisha Zaka kuondoa ufakiri katika jamii, na kuzui hatari zinazo weza kusababishwa na ufakiri, kama wizi, uporaji, uadui, mauaji n.k pia umekusudia kuhuisha moyo wa ushirikiano na kusaidiana katika jamii kwa kukidhi haja za wenye matatizo. Na tofauti iliyopo kati ya zaka na kodi ni kwamba zaka Muislamu anaitoa kwa moyo mkunjufu bila ya kulazimishwa wala kusimamiwa, bali mwenyewe anajisimamia, maana anajua kuwa ni wajibu juu yake, pia anatambua kuwa anaitakasa nafsi yake kutokana na ubakhili, na tamaa, na inamtwaharisha kutokana na kuipenda dunia na kuzama katika matamanio kupita kiasi jambo ambalo linampelekea kusahau matatizo ya ndugu zake mafakiri na masikini. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wenye kuepushwa na ubakhili wa nafsi zao hao ndio wenye kufaulu".[152]
Pia Zaka hii inazisafisha nyoyo za mafakiri na masikini kutokana na chuki na husuda kwa matajiri, pale wanapo waona matajiri wakitoa yale aliyowawajibishia Mwenyezi Mungu katika mali zao, na wakiwafanyia ihsani na kuwajali na kuwaangalia. Na zimekuja dalili nyingi katika sheria zikiwatahadharisha matajiri kutokana na kuzuia Zaka. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: " Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyo wapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni bora kwao (kufanya ubakhili huko) la, ni vibaya kwao.Watafungwa kongwa (madude ya kunasa shingoni) za yale waliyo yafanyia ubakhli siku ya Qiyama".[153]
Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Mtu yeyote aliye miliki fedha au dhahabu na akawa hatoi haki yake basi atambue kuwa itakapo fika siku ya Qiyama zitayeyushwa (hizo dhahabu na fedha) katika Jahanamu kisha ababuliwe kwazo uso wake, na mgongo wake, kila zinapo poa zinayeyushwa tena, katika siku amabayo urefu wake ni sawa na miaka elfu hamsini, atakuwa katika hali hiyo mpaka itakapo pitishwa huku kwa viumbe, ndipo aione njia yake eidha ya kwenda Peponi au Motoni".[154]
Nguzo ya nne: kufunga mwezi wa ramadhani:
Nao ni mwezi mmoja tu katika mwaka mzima,wanaufunga Waislamu kwa kujizuia kula na kunywa, na kuwaingilia wake zao mchana, wanafanya hivyo kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mola wao, tangu kuchomoza kwa alfajiri mpaka kuzama jua. Na hii funga sio kwamba ni jambo jipya ambalo limekuja katika sheri ya Kiislamu peke yake,bali lilikuwepo hata katika sheria zilizo tangulia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini mmelazimishwa kufunga (swaumu) kama walivyo lazimishwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu".[155]
Lakini sio lengo la kufunga kwamba ni kujizuia na kula na kunywa tu na kufanya tendo la ndoa tu, bali ni lazima pia kujizuia kusema uongo, kuteta na kusengenya, kufanya udanganyifu na mambo mengine mabaya mfano wa haya, ingawaje sio kwamba mambo haya yanatakiwa kuyaacha katika Ramadhani peke yake, bali ni wajibu kuyaacha hata katika siku zingine zisizo kuwa ramadhani, lakini katika Ramadhani inakuwa ni zaidi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Mtu asiye acha kusema uongo na kufanya mambo ya kipuuzi basi Mwenyezi Mungu hana haja ya kumuona mtu huyo ameacha kula na kunywa (yaani funga yake haina manufaa yoyote kwake) ".[156]
Na swaumu ni mpambano baina ya nafsi na matamanio yake, inamnyanyua daraja Muislamu na kumtoa katika maneno machafu na matendo mabaya. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake :Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kila amali aifanyayo mwanadamu huwa ni yake, ispokuwa swaumu hiyo ni ya kwangu, na mimi ndiyo najua malipo yake. Na swaumu ni kinga, pindi atakapo kuwa mmoja wenu kafunga basi asifanye madhambi, na endapo mtu atamtukana au kumtafuta ugomvi basi aseme; Hakika mimi ni mwenye kufunga. Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad imo mikononi mwake, harufu ya kinywa cha mwenye kufunga mbele ya Mwenyezi Mungu ni nzuri kuliko harufu ya miski. Mwenye kufunga anazo furaha mbili, furaha ya kwanza ni pale unapo fika wakati wa kufuturu, na furaha ya pili ni siku atakapo kutana na Mola wake atafurahia swaumu yake".[157].
Na kupitia swaumu ndipo mtu anapata kujua haja za ndugu zake mafakiri na masikini na wenye matatizo, hali hiyo inampelekea kutekeleza haki zao na kukidhi haja zao.
Nguzo ya tano:Kwenda Maka kufanya hijja.
Nacho ni kitendo cha kwenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Maka, kwa ajili ya kufanya matendo maalumu, katika maeneo maalumu, katika wakati maalumu. Nguzo hii ni wajibu juu ya kila Muislamu, mwenye akili timamu, alie kwisha baleghe, wanaume kwa wanawake, ni wajibu mara moja tu katika umri, kwa sharti ya kuwa na uwezo wa kimwili, na kimali. Maana mtu kama ni mgonjwa ugonjwa ambao hautarajiwi kupona, basi ugonjwa unamzuia kufanya hijja hata kama ni tajiri, ispokuwa anatakiwa kutafuta mtu atakaye mfanyia Hijja. Vilevile atakaye kuwa ni fakiri hamiliki mali inayo muwezesha kukidhi mahitaji yake ya lazima na watu walio chini yake hawajibikiwi kwenda Hijja. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hija katika nyumba hiyo; yule awezaye kufunga safari kwenda huko, na atakaye kanusha (asende na hali ya kuwa anaweza) basi Mwenyezi Mungu si muhitaji kuwahitajia walimwengu".[158]
Inazingatiwa Hijja kuwa ndio mkusanyiko mkubwa wa Kiislamu , ambao unawakusanya Waislamu kutoka pande zote za Dunia katika sehemu moja kwa wakati maalumu wakimuomba Mungu mmoja, hali ya kuwa wamevaa vazi la aina moja, wakitekeleza ibada ya aina moja, na wote wakiita wito wa aina moja (Labaika Allaahuma labaika, labaika laashariika laka labaika, innal-hamda wan-niimata laka wal-mulku laashariika laka). Yaani: Tumeitika wito Ewe Mola wetu,huna mshirika ewe Mola wetu ,hakika sifa njema na neema na ufalme ni wako.
Hakuna tofauti kati ya mtukufu na mnyonge, au kati ya mweupe na mweusi, au kati ya mwarabu na asiye mwarabu, wote wako sawa mbele za Mwenyezi Mungu, tofauti yao ni ucha Mungu wao tu.
Miongoni mwa mazuri ya Dini ya Kiislamu:
Kwakuwa sheria ya Kiislamu (Dini) ndio ya mwisho kuteremka, hapana shaka kwamba itakuwa na mambo makhsusi, na mazuri amabayo hayakupatikana katika sheria (Dini) zilizo tangulia, na kwa sababu hizo inakuwa ni Dini ambayo inafaa kwa kila zama na kila mahala mpaka kitakapo simama Kiyama. Na kwa sababu ya mazuri haya imekuwa Dini ya Kiislamu ndio Dini pekee inayo weza kuwapatia furaha wanadamu hapa duniani na siku ya mwisho.
Miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo:-
Kwamba dalili zake zimekuja zikibainisha waziwazi kwamba Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni moja tu,na kwamba Mwenyezi Mungu aliwatuma Mitume tangu Nuhu mpaka kufikia kwa Muhamad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kila mmoja alikuwa anatimiliza aliyo kuja nayo mwenzake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Hakika mfano wangu mimi na Manabii walio nitangulia ni kama mfano wa mtu aliye jenga nyumba na akaipamba vizuri ispokuwa sehemu ya tofari moja katika sehemu ya pembeni ,wakawa watu wanaitembelea nyumba hiyo na kuisifu na huku wakimwambia mwenyewe; Kwa nini usinge malizia tofari hili moja? Basi mimi ndio tofari hilo, na mimi ndio Mtume wa mwisho".[159]
Ispokuwa Nabii Issa (Yesu) atateremshwa katika zama za mwisho ili aje kuleta uadilifu Duniani, wakati dunia itakapo kuwa imejaa dhulma na ujeuri, hataivo hatakuja na Dini mpya, bali atahukumu kwa sheria na kwa Dini ya Kiislamu aliyo kuja nayo Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, haya ni kwa mujibu wa maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipo sema : " Hakitasimama kiyama mpaka ateremke mwana wa Maryam kwa hukumu yenye uadilifu, atavunja misalaba, na kuua nguruwe, na kuweka kodi kwa wale wasio fuata sheria (Uislamu), na mali zitakuwa nyingi mpaka ifikie hakuna anaye kubali kupewa".[160] Mitume wote wito wao na ujumbe wao ulikuwa ni mmoja, nao ni kulingania katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasa na washirika, au kumfananisha na chochote. Na waliwalingania watu wamuabudu moja kwa moja bila kupitia kitu kingine baina yao na Mola wao, na walikuwa wakizitakasa nafsi za wanadamu,na kuzielekeza katika mambo yatayo waletea amani duniani na kesho mbele za Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "amekupeni sheria ya Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na Tuliyo kufunulia wewe, na Tuliyo wausia Ibrahimu na Musa na Isa, kwamba simamisheni Dini wala msifarikiane kwayo (kwa ajili ya Dini) ".[161]
Kupitia Uislamu Mwenyezi Mungu amefuta sheria (dini) zilizo tangulia, kwa hiyo Uislamu ndio Dini ya mwisho, na Mwenyeezi Mungu haridhiki kuabudiwa kupitia dini nyingine isiyo kuwa Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu: " Na tumekuteremshia kitabu kwa (ajili ya kubainisha) haki, kinacho sadikisha vitabu vilivyo kuwa kabla yake, na kuvihukumia (kamaya ndiyo yaliyo haribiwa ama ndiyo yaliyo salimika) ".[162]
Na kwakuwa ndio Dini ya mwisho Mwenyezi Mungu alichukua dhamana ya kuilinda mpaka siku ya mwisho, tofauti na dini (sheria) zilizo tangulia, Mungu hakuahidi kuzilinda kwa kuwa zilikuwa ni za muda maalumu na kwa watu maalumu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Hakika Sisi ndio tulio teremsha mauidha haya (hii qur-ani); na hakika Sisi ndio tutakao yalinda ".[163]
Na hii ni dalili wazi wazi kwamba Mtume Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ndio Mtume wa mwisho. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Muhamad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na mwisho wa Mitume".[164]
Lakini haimaanishi kwamba hatupaswi kuwasadikisha na kuwaamini Mitume walio tangulia pamoja na vitabu vyao, maana Isa (Yesu) alikuja kukamilisha aliyo kuja nayo Musa, na Muhamad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuja kukamilisha aliyo kuja nayo Isa (Yesu), na Muhamad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akawa ndio mwisho wa Manabii na Mitume. Na mwislamu ameamrishwa kuviamini vitabu vyote na mitume wote walio tangulia.Endapo mtu ataacha kumuamini hata mmoja kati yao basi anakuwa katoka katika Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Hakika wale wanao mkanusha mwenyezi Mungu na Mitume yake,na wanataka kutenga baina ya mwenyezi Mungu na Mitume yake kwa kusema: wengine tunawaamini na wengine tunawakataa, na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya (si ya kiislamu khasa wala ya kikafir). Hao ndio Makafir kweli, na Tume waandalia makafiri adhabu idhalilishayo" . [165]
Kwamba Dini ya Kiislamu imekamilika na kutimia kuliko sheria zilizo tangulia, maana sheria zilizo tangulia zilikuwa zinahusiana na misingi ya kiroho, na zikiwalingania wafuasi wake kuzitakasa nafsi zao, wala hazikuzungumzia mambo yanayo husiana na dunia yao na maisha kwa ujumla kwa kuyapambanua na kuyawekea taratibu, tofauti na Uislamu, maana umekuja kukamilisha na kupangiliamambo yote yanayo husiana na Dini pamoja na dunia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu".[166]
Na ndio maana Uislamu ikawa ni dini bora. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Nyinyi ndio Umma bora kuliko umma zote zilizo dhihirishiwa watu, (ulimwenguni) mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na kama wale walio pewa kitabu wangeliamini (kama walivyo amrishwa) ingelikuwa bora kwao (Lakini) miongoni mwao wako wanao amini, na wengi wao wanatoka katika twaa ya Mwenyezi Mungu".[167]
Kwamba dini ya Kiislamu ni dini ya watu wote ulimwengu mzima bila ya kubagua, sio kwamba ni ya jinsia flani peke yao, au umma flani tu, autaifa flani tu. Ni Dini inayo waunganisha watu wote sio kwa misingi ya rangi, au lugha, au utaifa, au ukoo, au zama, n.k bali ni kwa misingi ya itikadi maalumu ndio iliyowakusanya. Kila mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu kuwa ndie Muumba na kwamba Uislamu ndio dini sahihi, na kwamba Muhamad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ni Mtume wa Mwenyezi Mungu basi anakuwa kaingia na kujiunga chini ya bendera ya Uislamu, katika zama zozote, mahala popote. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na hatukukutuma (Hatukukuleta) ila kwa watu wote uwe mtoaji wa habari njema na muonyaji".[168] Lakini Mitume walio tangulia walikuwa wakitumwa kwa watu wao peke yao. Amesema Mwenyezimungu Mtukufu: " Tulimpeleka Nuhu kwa watu wake, naye akasema: Enyi watu wangu muabuduni Mwenyezi mungu nyinyi hamna Mungu ila Yeye ".[169]
Na amesema Mwenyezi Mungu: " Na kwa Adi (Tulimpeleka) ndugu yao Hudi, akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye".[170]
Na amesema Mwenyezi Mungu: " Na kwa Thamud (Tulimpeleka) ndugu yao Swaleh. Akasema: Enyi kaumu yangu!Muabuduni Mwenyezi Mungu,nyinyi hamn Mungu ila Yeye"[171]
Na amesema Mwenyezi Mungu:" Na (Tulimpeleka) Luti. Basi wakumbushe alipo waambia kaumu yake…".[172]
Na amesema Mwenyezi Mungu: " Na kwa watu wa Madyan (tulimpeleka) ndugu yao Shuaib…"[173]
Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kisha baada ya (Mitume hao) Tulimpeleka Musa na hoja zetu kwa Firauni na watu wake".[174]
Na amesema Mwenyezi mungu Mtukufu: (Na (wakumbushe ) aliposema (Nabii) Isa bin Maryam (kuwaambia Mayahudi); Enyi wana wa Israili! Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati…".[175]
Na kwakuwa Dini ya Kiislamu ni Dini ya ulimwengu mzima , na kwa watu wote katika zama zote, Waislamu wameamrishwa kufikisha ujumbe huu kwa watu wote. Amesema Mwenyezi Mung Mtukufu: "Na vivyo hivyo tumekufanyeni Umma wa kati na kati (kama Qibla chenu tulivyo kifanya bora) ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu".[176]
Dini ya Uislamu sheria zake na mafundisho yake yamemakinika na hayakubali kugeuzwa wala kubadilishwa maana yanatoka kwa Mwenyezi mungu, sio maneno ya kibinadamu ,maana ya binadamu hayakosi mapungufu na makosa na kubadilika kutokana na zama na mazingira, nahii ndio hali halisi katika nidhamu na sheria zinazo pangwa na wanadamu, haziwi katika hali moja, utakuta sheria na kanuni zinazofaa katika jamii Fulani hazifai katika jamii nyingine, na zinazofaa katika zama Fulani basi hazifai katika zama zingine, ilimradi kila mwenye kuweka kanuni na sheria anaziweka kulingana na hali halisi ilivyo kwa wakati ule. Bali wakati mwingine anaweza kuweka kanuni mtu Fulani, akaja mwengine na mtazamo tofauti na ule na hivyo akazibadilisha, eidha kwa kuzidisha au kupunguza. Lakini sheria ya Kiislamu kama tulivyo sema kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa viumbe wote, ajuaye mambo yao yote yanayowafaa kulingana na hali zao, hakuna yeyote katika wanadamu hata awe na elimukiasi gani, au cheo kiasi gani, hana haki ya kugeuza chochote katika sheria ya Mwenyezi Mungu, eidha kwa kuzidisha au kupunguza. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: " Je, wao wanataka hukumu za kijahili( ya zile siku za ujinga kabla ya kuletwa Mtume)? na nani aliye mwema zaidi katika hukumu kuliko Mwenyezi Mungu; (yanafahamika haya) kwa watu wenye yakini".[177]
Dini ya Uislamu ni Dini inayo kubaliana na maendeleo, na jambo hili ndilo linaifanya iwe ni Dini inayo faa katika kila zama na kila mahala, maana Uislamu umeweka misingi na kanuni madhubuti katika akida (itikadi), na katika ibada, kama vile Imani, swala na idadi yake, na idadi ya rakaa zake, na nyakati zake, na zaka na viwango vyake, na swaumu na wakati wake, na hija na wakati wake na namna yake na mipaka yake…na kadhalika. Mambo haya yamethibiti hayabadiliki kwa kubadilika zama au mahala. Ispokuwa yanapo zuka mambo mapya yanayo fungamana na Ibada hizi, basi yanapimwa katika mizani ya Qur-ani tukufu, yakikubaliana basi yanachukuliwa, na yanayo kwenda kinyume yanaachwa, na kama hayakupatikana katika Qur-ani basi hutazamwa katika mafundisho sahihi kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake yaliyo thibiti katika mapokezi sahihi, na kama hatukupata humo basi jukumu hili linakuwa ni la wanazuoni walio fikia viwango vya hali ya juu kielimu na kiucha Mungu katika kila zama na kila mahala, wana haki ya kujitahidi na kubainisha hukumu ya jambo hilo kulingana na hali halisi ya zama zile na jamii ilivyo .Lakini jitihada hizi sio kwa matamanio ya nafsi, bali ni lazima ziwe zimesimama katika mafuhumu ya Qur-ani na Suna za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, pia mambo haya mapya ambayo pengine yanaweza yasionekane wazi wazi katika Qur-ani au mafundisho ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake wanazuoni wameweka kanuni ambazo zinatokana na Qur-ani na Suna, ambazo ni kama vipimo, jambo lolote linalo onekana ni geni katika maswala ya kisheria basi hupimwa katika mizani hizo. Kwamfano miongoni mwa kanuni hizo ni kama hizi : (Asili ya vitu vyote ni halali, mpaka ipatikane dalili ya kuharamisha). (kanuni ya kuhifadhi na kuchunga maslani). (kanuni ya kuchunga wepesi katika mambo yote na kuondoa uzito). (kanuni ya kuondoa madhara). (kanuni ya kufanya baadhi ya yaliyo katazwa kwa ajili ya kuchunga maslahi flani). (dharura hukadiriwa kwa kiwango chake). (kuzuia madhara kunatangulizwa zaidi kuliko kuleta maslahi). (Madhara hayaondolewi kwa kusababisha madhara mengine). (huvumiliwa madhara ya mtu mmoja ili kuzuia madhara ya walio wengi). Hii ni mifano tu ya baadhi ya kanuni za kisheria, na kila kanuni miongoni mwa hizi tulizo zitaja na ambazo hatukuzitaja ina maana pana sana,wala mtu asiibebe kwa maana finyu na hatimaye akafahamu kinyume na makusudio yake.
Katika Uislamu watu wote ni sawa katika kutekeleza sheria, hakuna tofauti kati ya fakiri na tajiri, wala hakuna tofauti ya bwana mkubwa au mnyonge, wote ni sawa mbele ya sheria. Mfano hai ni kisa kilichotokea katika kabila la kikurasihi wakati mama mmoja katika ukoo wa banii makhzuum (ni miongoni mwa koo tukufu) alipo iba, wakataka apatikane mtu wa kumtetea mbele ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ili asitekelezewe hukumu, wakamchagua Usama bin Zaid ambaye alikuwa ni kipenzi sana kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, basi Usama akenda kumuombea msamaha, Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikasirika sana na kumkemea Usama kwa ukali akasema:" Unakuwa mtetezi katika hukumu miongoni mwa hukumu za Mwenyezi Mungu?!" kisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasimama na kuwahutubia akasema: "Enyi watu,kwa hakika kilicho waangamiza walio kuwa kabla yenu, nikwamba alipokuwa akiiba bwana mkubwa miongoni mwao wanamuacha, na akiiba ambaye ni mnyonge basi wanamsimamishia hukumu. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau kama aliyeiba ni Binti yangu Fatuma bint Muhamad, basi ningeliukata mkono wake".[178]
Uislamu ni Dini ambayo vyanzo vyake vya sheri vimesalimika na mapungufu, hakuna kuzidisha wala kupunguza au kugeuza; navyo ni Qur-ani tukufu pamoja na sunna tukufu. Qur-ani tukufu tangu ilipo teremshwa kwa Mtume Muhamad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake mpaka leo iko vilevile kwa herufi zake na aya zake na sura zake, haijapunguzwa au kuongezwa au kugeuzwa. Maana wakati inashuka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuwa na waandishi wake kama vile akina Aly, na Muawiya, na Ubayi bun Kaab, na Zaid bin Thaabit, ikawa inapoteremka aya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anawaamuru kuiandika, na anawaelekeza mahala pake katika sura husika, kwahiyo Qur-ani ikahifadhiwa kwa kuiandika pia ikahifadhiwa vifuani. Na Waislamu walikipupia sana kitabu cha Mwenyezi Mungu katika kukisoma na kukihifadhi kwa ajili ya kuyatafuta malipo aliyo yeleza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipo sema: "Mbora wenu ni yule aliye jifunza Qur-ani na akaifundisha".[179] Na wanazitoa nafsi zao na mali zao katika kukitumikia kitabu hiki na kukihifadhi, wanafanya hivyo kwakuwa hiyo ni ibada wanajikurubisha kwayo kwa Mola wao. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Mwenye kusoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu,basi huandikiwa jema moja, na hilo jema moja malipo yake ni sawa na mema kumi, sisemi :Alif Lam Mim kwamba ndiyo herufi moja, lakini (Alif) ni herufi, na (Lam) ni herufi, na (Mim) ni herufi ".[180]
-Na Suna tukufu za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ambazo ndizo zimeibainisha Qur-ani na kutafsiri hukumu zake,nayo imehifadhiwa na kulindwa kutokana na kuongezwa yasiyo kuwamo, maana Mwenyezi Mungu aliwaandaaa watu ambao walikuwa ni wakweli ,waadilifu wacha Mungu, wakautumia wakati wao na uhai wao katika kuzisoma hadithi za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na wakasoma mapokezi yake na wapokezi wake pia na kuwatambua walio kuwa na sifa zinazo wafanya mapokezi yao yakubalike na wasio kuwa na sifa hizo, hivyo wakazikusanya hadithi zote zilizo pokelewa kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na wakazichambua ambazo ni sahihi, na hivyo zikatufikia sisi hali ya kuwa ni sahihi hakuna ya uongo hata moja.Na mwenye kutaka kujua ni njia gani iliyo tumiwa katika kuihifadhi suna basi na arejee katika vitabu vya elimu ya sayansi ya hadithi,ambavyo vilitungwa kwa ajili ya kuzitumikia hadithi za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, atagundua kwamba kwa njia zilizo tumiwa ni wazi kabisa kwamba huwezi kutilia shaka juu ya hadithi zilizo tufikia toka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na ataona wazi ni juhudi kubwa kiasi gani walizo zitumia katika kuitumikia Suna.
Uislamu ni Dini iliyo weka usawa kwa viumbe wote katika asili ya kuumbwa,wanaume kwa wanawake, weusi kwa weupe, mwanadamu wa kwanza ambaye Mwenyezi Mungu kamuumba ni baba yetu Adamu, kisha akamuumba kutokana naye mkewe hawa, ambaye ndiye mama wa viumbe, na akajalia kizazi kiendelee kutokana na wawili hao, hivyo asili ya wanadamu wote ni moja .Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi watu! mcheni Mola wenu ambaye amekuummbeni katika nafsi (asili) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana. Na (muwatazame) jamaa".[181] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Hakika Mwenyezi Mungu kakuondoleeni kasoro za kijahiliya (zama za ujinga kabla ya kuja Mtume), na kujifakharisha kwenu kwa baba zenu, ima mtu atakuwa ni muumini mcha Mungu au ni muovu, na watu wote wanatokana na Adamu ,naye adamu ametokana na udongo".[182] Kwa hiyo mwandamu yeyote aliye kwisha patikana juu ya mgongo wa ardhi na watakao kuja wote ni katika kizazi cha Adamu. Na kizazi chake Adamu hapo mwanzo wote walikuwa na Dini moja na wakiongea lugha moja, lakini kila walipo ongezeka na wakazidi kusambaana katika sehemu mbali mbali za dunia hii ikawa ni sababu ya kutofautiana lugha zao na rangi zao, kulingana na mazingira ambayo yalipelekea hata fikra zao ziwe tofauti, na maisha yao pia kutofautiana, na hatimaye itikadi zao zikatofautiana . Amesema Mweyezi Mungu Mtukufu:" Wala watu hawakuwa (huko nyuma kabisa katika zama za Na bii Adamu) ila ni kundi moja, (wote wanafuata Dini ya haki). Kisha wakahitalifiana, na kama sio neno lililo tangulia kutoka kwa Mola wako (kuwa atawalipa siku ya kiyama, hawalipii hapa) ,bila shaka shauri lao lingekwisha katwa (mara moja) baina yao katika yale wanayo hitalifiana".[183]
Kwahiyo mafundisho ya Uislamu yamewaweka watu wote bila kujali jinsia zao, au rangi zao, au lugha zao katika daraja moja, wote wako sawa mbele za Mwenyezi Mungu, tofauti inakuja tu kutokana na jinsi gani mtu atajikurubisha kwa Mola wake kwa kufuata sheria na mafundisho yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Enyi watu! kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja: Adamu) na ( yule yule) mwanamke (mmoja; Hawa), na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali), ili mjuane (tu basi sio mkejeliane). Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi".[184]
Na kwa mujibu wa usawa huu ndio watu wote katika mtazamo wa sheria ya Kiislamu wanakuwa sawa katika uhuru ambao uko chini misingi ya Dini, hivyo kila mtu anakuwa na uhuru katika mambo mbali mbali kama vile:
1- Uhuru wa kufikiri na kutoa rai. Maana Uislamu unawahimiza wafuasi wake kusema ukwelii na kuelezea hisia zao na mawazo yao-yasiyo kuwa kinyume na sheria-na kwamba mtu asiogope lawama ya mwenye kulaumu maadamu yuko katika haki. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Jihadi iliyobora ni kusema ukweli mbele ya kiongozi au mtawala dhwalimu".[185]
Ndio maana Maswahaba walishindana katika kulitekeleza hilo, kama ilivyo pokewa kuwa mtu mmoja alisema kumwambia Umar bin alkhatwab (Radhi za Mwenyeezi Mungu zimuendee) kiongozi wa Waislamu: "Muogope Mwenyezi Mungu ewe kiongozi wa waislamu" kisha mtu mwingine akataka kumkemea na kumzuia: Vipi unathubutu kumwambia hivyo kiongozi wa Waislamu?. Ndipo Umar akamwambia: Mwache aseme maana kama hamtatwambia basi hamtakuwa na kheri yoyote, nasisi kama hatuta kusikilizeni na kukubali nasaha zenu hatutakuwa nakheri yoyote.
Na tukio lingine ni pale Aly bin Abitwalibu alipotoa hukumu katika jambo flani kwa rai yake kisha akaulizwa Umar, na wakati huo yeye ndiye alikuwa mtawala, akasema: Laiti ningeulizwa mimi juu ya jambo hilo aliloulizwa Aly basi mimi ninge hukumu tofauti nay eye. Alipo ulizwa kwa nini usibatilishe hukumu yake na wewe ni kiongozi? Akasema: Laiti hilo lingekuwa katika Qur-ani au Hadithi basi ningelimpinga, lakini hiyo ni rai binafsi, na katika rai watu wanashirikiana, na hakuna ajuaye ni rai gani ambayo ni sahihi mbele za Mwenyezi Mungu.
2-Uhuru wa kuchuma mali kwa njia halali na kumiliki. Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu: " Wala msitamani vile ambavyo Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu (kwa vitu hivyo) kuliko wengine, wanaume wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyo vichuma; na wanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyo vichuma".[186]
3-Pia kila mtu ana uhuru wa kupata elimu kusoma, bali Uislamu unalihesabu jambo hili ni katika wajibu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Kutafuta elimu ni wajibu kwa kila Muislamu".[187]
4-Kila mtu anayo haki na kunufaika na kheri mbali mbali alizo ziweka Mwenyezi Mungu katika uliwemngu huu, katika misingi inayo kubalika. Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu: " Yeye ndiye aliye ifanya ardhi iwe inaweza kutumika (kwa kila muyatakayo) kwa ajili yenu, basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika riziki zake,na kwake yeye ndio marejeo (yenu nyote) ".[188]
5-Kila mtu anayo haki ya kuwa mtawala katika jamii pindi atakapo kuwa na sifa na uwezo kubeba majukumu hayo. Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Yeyote atakaye tawalishwa jambo miongoni mwa mambo ya Waislamu ,kisha naye akamtawalisha mtu asiye sitahiki katika nafasi hiyo, basi zitamshukia laana za Mwenyezi mungu, na Mwenyezi Mungu hatakubali kutoka kwake amali yoyote, mpaka amuingize Motoni. Na mwenye kumpa yeyote mpaka katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi atakuwa kavunja mipaka ya Mwenyezi Mungu pasina haki na atakuwa amesitahiki laana ya Mwenyezi Mungu,au atatoka nje ya dhima ya Mwenyezi Mungu".[189]
Na Uislamu unakizingatia kitendo cha kumuweka katika madaraka mtu asiye sitahiki ni katika kupoteza amana, jambo ambalo ni miongoni mwa dalili za kuharibika ulimwengu na kusimama kiyama. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Pindi amana ikipotezwa, basi ngojeeni kiyama". Akaulizwa ni vipi kuipoteza amana ewe Mtume wa Mungu? Akasema: " Pindi watakapo pewa majukumu watu wasio na sifa za kubeba majuku yale ngojeeni kiyama".[190]
Katika Uislamu hakuna heshima maalumu iliyo beba maana ya kiibada kwa mtu kama ilivyo katika dini zingine, na hii ni kwa sababu Uislamu ulipokuja ulivunja na kuondoa mipaka na vizuizi baina ya Mwenyezi Mungu na waja wake, ukayakemea mambo waliyo kuwa wakiyafanya washirikina ya kujaalia washirika wa kati na kati katika ibada zao. Akasema Mwenyezi Mungu: " Wa kuitakidiwa Mola ni Mwenyezi Mungu tu, lakini wale wanao wafanya wengine kuwa ni waungu badala yake(husema): Sisi hatuwaabudu hawa ila wapate kutufikisha karibu kabisa na Mwenyezi Mungu".[191] Na Mwenyezi Mungu akabainisha kwamba hawa washirika hawawezi kumfaa mtu wala kumdhuru, bali wao ni viumbe tu kama wao. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Hakika wale mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni waja ( watumwa) kama nyinyi (bai nyinyi bora zaidi kuliko wao. Nyinyi mna midomo ya kusema wao hawana), hebu waiteni nao wakuitikieni ,ikiwa mnasema kweli (kama wao ni bora na wanayo haya) ".[192] Kwahiyo Uislamu ukaweka utaratibu wa njia ya kuwasiliana na Mola wake moja kwa moja, kupitia imani yake ya kisawa sawa kwa Mola wake, na kumlilia amuondolee na kumkidhia haja zake, na kumtaka msamaha, na kuomba msaada kwake moja kwa moja, bila kupitia kitu kingine. Hiyvo mtu anapo tenda dhambi moja kwa moja anamuelekea Mola wake na kumtaka msamaha, popote pale anapo kuwa na katika hali yoyote ile aliyopo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na mwenye kutenda uovu (wa kuwachukiza wenziwe) au akaidhulumu nafsi yake (kwa kufanya kosa la kumdhuru mwenyewe tu) kisha akaomba maghufira (msamaha) kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kughufiria na mwenye kurehemu".[193] Hivyo katika Uislamu hakuna watu maalumu wenye haki ya kuhalalisha jambo au kuharamisha jambo lolote, au kuwasamehe watu dhambi zao, na wao wakajiona kama vile ni mawakili wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake wanamsamehe wamtakaye na kumpa Pepo na kumnyima wamtakaye, bali hiyo ni haki ya Mweyezi Mung peke yake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katika kuifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu " Wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu"[194] hakika wao hawakuwa wakiwaabudu lakini walikuwa wanapo liharamisha jambo na wao huwafuata katika hilo, na wanapo lihalalisha jambo nao pia wanalihalalisha".[195]
Dini ya Kiislamu ni Dini ya kushauriana katika mabo yote ya kidini na kidunia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na wale walio muitikia Mola wao (kwa kila amri zake) na wakasimamisha swala, na wanashauriana katika mambo yao, na wanatoa katika yale tuliyo waruzuku".[196] Jambo la kushauriana ni jambo lililo himizwa katika sheria ya Kiislamu, na ndio maana hata Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kaamrishwa kufanya hivyo, ili awe mfano kwetu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu " Basi kwa rehma itokayo kwa Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao (Ewe Muhamad), na kama ungekuwa mkali na mwenye moyo mgumu, bila shaka wangelikukimbia, basi wasamehe wewe na uwaombee msamaha (kwa Mwenyezi Mngu), na ushauriane nao katika mambo".[197]
Na kushauriana ndio njia ya kufikia katika usahihi wa mambo na ndio maana Waislamu katika karne za nyuma walipokuwa wakitekeleza jambo hili katika mambo yao ya Dini na ya kidunia mambo yaliwaendea vizuri, na pindi walio badilika na kuliacha jambo hili ndipo walipo fika katika hali ya kufeli katika mambo yao yote kidini na kidunia.
Uislamu umeweka haki baina ya watu kulingana na daraja zao, ili maisha yao yawe sawa na mambo yao kidini na kidunia yaweze kwenda vizuri; wazazi wanazo haki na watoto pia wanazo haki, na ndugu na jamaa wanazo haki na majirani pia wana haki, na marafiki wanazo haki..n.k amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote, na wafanyieni ihsani wazazi wawili, na jamaa na mayatima na masikini,na jirani walio karibu na jirani walio mbali, na rafiki walio ubavuni (mwenu) na msafiri aliye haribikiwa, na wale iliyo wamiliki mikono yenu ya kuume. Bila shaka Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wajivunao".[198] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Msifanyiane husuda, wala msipunjane katika vipimo, wala msibughudhiane, wala msipeane migongo, wala baadhi yenu wasiuze juu ya biashara za baadhi yenu ( wasiharibiane biashara), kuweni enyi waja wa Mwenyezi Mungu ni ndugu ,Muislamu ni ndugu wa Muislamu, hamdhulumu, wala hamdhalilishi, wala hamdharau, ucha Mungu uko vifuani (akaashiria kifuani kwake mara tatu) yamtosha mtu kuwa ni mshari kwa kumdharau ndugu yake Muislamu, kila Muislamu ni haramu kwake damu ya ndugu yake Muislamu ,na mali yake na heshima yake ".[199] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Hawi muumini wa kweli mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake vile avipendavyo yeyekatika nafsi yake".[200] Mpaka maadui wa Uislamu pia wanazo haki katika Uislamu, anasimulia Abu azizi bin Umair,huyu ni ndugu yake na Swahaba mtukufu Mus-abu bin Umair,anasema: Nilikuwa miongoni mwa watu walio kamatwa mateka katika vita vya Badri,akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake :" Usianeni kuwatendea wema hawa mateka", na nilikuwa mimi katika kundi la Maanswari (watu wa Madina) ,walikuwa wanapo leta chakula chao cha mchana na cha usiku, basi wao wanakula tende, mimi wananipa mkate, kwa ajili ya kutekeleza wasia wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake juu yao".[201] Uislamu haukuishia hapo tu bali umewapa haki hata wanyama na kuzilinda haki zao. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake :" Atakaye muua ndege bila ya sababu yoyote (hakusudii kunufaika naye ,eidha kumla au kwa manufaa mengine) atakuja ndege huyo siku ya kiyama amwambie Mola wake, Ewe Mola wangu hakika fulani aliniua bila sababu yoyote".[202] Na imepokewa kutoka kwa Ibnu Umar- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwandee –aliwakuta vijana miongoni mwa vijana wa kikuraishi wakiwa wamemfunga ndege mahala kisha wanalenga shabaha zao, na wamemuwekea mmiliki wa yule ndege malipo Fulani kwa kila jiwe litakalo mkosa ,walipo muona Ibnu Umar wakatawanyika, akasema: Nani kafanya jambo hili? Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kufanya hivi, hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kamlaani kila atakaye kukifanya kitu chenye roho ni kitu cha kulengea shabaha".[203] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake wakati alipo mkuta ngamia kakonda kwa sababu ya njaa : " Mcheni Mwenyezi Mungu juu ya hawa wanyama wasio tamka, wapandeni kwa wema na waleni kwa wema".[204]
Uislamu umetoa haki hata kwa miti. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Atakaye ukata mkunazi Mwenyezi Mungu atamtupa Motoni" alipo ulizwa Abudawuud kuhusu maana ya hadithi hii,akasema: Hadithi imepokewa kwa ufupi ,na maana yake ni kwamba : Atakaye ukata mti bila ya haki yoyote, mahala ambapo wapita njia wananufaika na kivuli chake, na wanyama pia wananufaika na kivuli chake, basi Mwenyezi Mungu atamtupa Motoni.
Na Uislamu umeweka haki za kijamii juu ya mtu mmoja mmoja,na haki zilizo juu ya kila mtu kwa jamii yake,hivyo kila mtu anatakiwa kutekeleza haki za jamii na jamii pia inatakiwa kutekeleza haki za kila mtu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Muumini kwa Muumini mwenzie ni kama jengo moja ambalo limeshikana vizuri na likawa imara" kisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akashikamanisha vidole vyake katika kuweka wazi maana ya hadithi hii.[205] Na pindi ikishindikana kutekeleza haki za mtu mmoja mmoja na haki za jamii kwa wakati mmoja, basi hutangulizwa maslahi ya jamii kwanza; Kwamfano: Kama nyumba ya mtu iliyoko karibu na njia ikawa na dalili za kuanguka na inahofiwa kuwa inaweza kusababisha madhara kwa watu,basi inaruhusiwa kuibomoa kwa ajili ya kulinda maslahi ya walio wengi. Au kama mtu atajenga njiani inaruhusiwa kuibomoa nyumba yake na kumhamisha kwa ajili ya maslahi ya njia.
Dini ya Uislamu ni Dini ya upole na huruma, mafundisho yake yanalingania kuacha tabia za ukali na roho mbaya. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Wenye huruma Mwenyezi Mungu huwahurumia, wahurumieni walioko ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni".[206] Na katika kulingania katika upole na huruma auislamu haukuishia kwa watu peke yake bali jambo hili lina takikana hata kwa wanyama, na ndio maana kuna mama mmoja aliingia Motoni kwa sababu ya mnyama. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Aliadhibiwa mwanamke mmoja kwa sababu ya paka ambaye alimfungia mpaka akafa, ikawa ni sababu ya yeye kuingia Motoni, hakumpa chakula wala maji,wala hakumuacha akajitaftie mwenyewe".[207] Na Uislamu umelifanya jambo la kuwahurumia wanyama ni sababu ya kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu na ni sababu ya kuingia Peponi. Amesema Mtume(.Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Mtu mmoja alikuwa akitembea njiani akawa amepatwa na kiu kikali sana, mara akakuta kisima cha maji akateremka kismani na kunywa maji,kisha akatoka ,mara akamuona mbwa akiwa na kiu kikali mpaka anakula mchanga kutokana na kiu, yule mtu akasema: Hakika mbwa huyu kapatwa na kiu mithili ya kiu iliyo nipata mimi, akateremka tena kisimani akateka maji kwa kutumia kiatu chake na akamnywesha yule mbwa, Mungu akamsamehe dhambi zake", maswahaba wakamuuliza MtuemRehma na amani za Allah ziwe juu yake: Hivi kuna malipo hata katika kuwasaidia wanyama? Akawajibu kwa kusema: "Ndio, kila kiumbe kilicho na mapafu kuna ujira katika kukisaidia".[208]
Ikiwa Uislamu umewahurumia wanyama kiasi hikii vipi mwanadamu ambaye Mwenyezi Mungu kamfanya bora na akamtukuza kuliko viumbe wote!. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na hakika tumewatukuza wanadamu na tumewapa vya kupanda barani na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tulio waumba kwa utukufu ulio mkubwa (kabisa) ".[209]
Katika Uislamu hakuna utawa na mtu kujiharamishia vilivyo halali kwake ambavyo kavihalalisha Mwenyezi Mungu na kaviumba kwa ajili ya waja wake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "..Msijitilie uzito msije mkajisababishia yaliyo mazito, maana kuna watu walio jitilia uzito na Mwenyezi Mungu akawatilia uzito, na mabaki yao mnayaona katika mahekalu na majumba yao, kisha akasoma aya hii: "Na utawa (wanaume kutooa na wanawake kutoolewa) wameubuni (wenyewe), Sisi hatukuwaandikia hayo (wenyewe waliyafanya haya) ili kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu.."[210]
Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Kuleni na kunyweni,na mtoe sadaka, lakini msifanye israfu,wala msijivune, hakika Mwenyezi Mungu anapenda kuziona athari za neema yake kwa mja wake pindi anapo mneemesha".[211] Lakini pia Uislamu sio Dini inayo lingania katika kuielekea dunia na matamanio yake moja kwa moja ,bali inamtaka mtu asichupe mipaka ,awe kati na kati, ndio maana una mtaka Mwislamu anapo kuwa katika hali ya kushughulishwa na dunia akumbuke pia kuwa ni mwenye haja na akhera, kwa kutekeleza aliyowajibishiwa na mola wake. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu : "Enyi mlio amini! kutakapo nadiwa kwa ajili ya swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi mkamtaje Mwenyezi Mungu na acheni biashara. kufanya hivi ni bora kwenu ikiwa mnajua (hivi basi fanyeni).[212] Na akatakiwa Muislamu anapokuwa kazama katika ibada pia akumbuke kuwa kuna mahitaji muhimu ya kidunia ambayo yanamtaka akatafute riziki.Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:"Na itakapo kwisha swala, tawanyikeni katika ardhi mkatafute fadhila za Mwenyezi Mungu..".[213]
Na Uislamu amewasifu walio kusanya sifa mbili hizi.Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:"Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi (hakuwasahaulishi) kumkumbuka Mwenyezi Mungu,na kusimamisha swala na kutoa Zaka,wanaiogopa siku ambayo nyoyo zitadahadari na macho pia".[214]
Na Uislamu umekuja na misingi yenye kuhifadhi haki za akili na nafsi ya mwanadamu, kama ilivyo kuwa Muislamu anatakiwa kuichunga nafsi yake na kuihesabu kutokana na matendo yake kama alivyo sema Mwenyezi Mungu :" Basi anaye fanya wema (hata) wa kiasi cha uzito wa mdudu chungu ataona jazaa yake. Na anayefanya uovu(hata) wa kiasi cha uzito wa mdudu chungu ataona jazaa yake ".[215] vile vile hatakiwi kuitesa nafsi yake na kuinyima vile vizuri alivyo ihalalishia Mwenyezi Mungu,katika vyakula na vinywaji,na kuvaa vizuri na kuoa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Sema: Ni nani aliyeharamisha mapambo ya Mwenyezi mungu ambayo amewatolea waja wake".[216] Uislamu haukuharamisha ispokuwa vilivyo vibaya vyenye madhara kwa mwanadamu na akili yake au mwili wake au mali yake, au jamii yake.Roho ya mwanadamu kwa mtazamo wa Uislamu Mwenyezi Mungu kaiumba na kumtawalisha mwanadamu katika Dunia hii kwa lengo la kufanya na kutekeleza sheria za Mola wake,na hakuna mweye haki ya ya kuifanyia uadui nafsi ya mwanadamu ispopkuwa kwa haki ya Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwa hakika tumemuumba mwanadamu katika umbile lililo bora kabisa". Ndio maana Mwenyezi Mungu akaamrisha kuuhifadhi mwili huu kwa mambo yafuatayo:-
1. Kujitwahirisha: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanao jitakasa".[217] Uislamu ukajaalia miongoni mwa masharti ya swala anayo itekeleza Muislamu kila siku mara tano ni kutawadha. Akaseema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake; "Haikubaliki swala ya mmoja wenu bila ya twahara,na haikubaliki swadaka ya mtu aliye ficha ngawira".[218] Pia Uislamu umewajibisha kuoga baada ya mtu kupatwa na janaba(baada ya kufanya tendo la ndoa).Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: "Na mkiwa na janaba basi ogeni".[219] Na ukafanya jambo la kuoga ni katika mambo yaliyo himizwa sana katika baadhi ya ibada kama vile swala ya Ijumaa na Eid mbili,na katika Hija na Umra ..n.k
2. Kushikamana na swala la usafi,kama vile:-
- Kuosha mikono kabla na baada ya kula. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Baraka ya chakula ni pamoja na kunawa kabla ya kula na baada ya kula".[220]
- Kunawa mdomo baada ya kula, na kusafisha meno.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katika kuhimiza mswaki : " Laiti nisingechelea uzito kwa umati wangu basi ningewaamrisha wapige mswaki kila wanapo tawadha kwa ajili ya swala".[221]
- Kusafisha na kuondoa uchafu ambao unaweza kuwa ni sababu ya Bakteria.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Mambo matano ni ya kimaumbile ;Kutahiri,na kunyoa nywele zilizo sehemu za siri,na kuondoa nywele za kwapani,na kupunguza masharubu,na kukata kucha".[222]
3. Kula pamoja na kunywa katika vilivyo vizuri. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni,na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa mnamuabudu Yeye peke yake".[223] Lakini pia katika kutumia vitu hivi vilivyo halalishwa,kukawekwa sharti ambalo ni kutokufanya israfu(ufujaji na uharibifu).Akasema Mwenyezi Mungu: "Na kuleni(vizuri)na kunyweni(vizuri),lakini msipite kiasi tu,hakika Yeye Mwenyezi Mungu hawapendi wapitao kiasi(wapindukiao mipaka) ".[224] Na utaratibu sahihi wa kula kaubainisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alippo sema : "Hajapata mwanadamu kujaza chombo ambacho ni shari kwake kuliko tumbo lake,inakutosha ewe mwanadamu kula kiasi tu ili upate kuishi,na ikiwa hakuna budi ni lazima ule sana basi ligawe tumbo lakosehemu zifuatazo;theluthi kwa ajili ya chakula,na theluthi nyingine kwa ajili ya maji,na theluthi nyingine kwa ajili ya kupumua".[225]
4. Uislamu umeharamisha kutumia kila kitu ambacho ni kibaya katika vyakula na vinywaji ,kama vile mizoga,damu,nyama ya nguruwe,pombe,madawa ya kulevya,sigara n.k. yote haya ni kwa ajili ya kulinda usalama wa mwili wa mwanadamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu; " Yeye amekuharamishieni mizoga na damu na nyama ya ngueuwe na kilicho tajiwa katika kuchinjwa kwake jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu.Lakini atakaye fikwa na dharura(ya kula vitu hivi) bila kutamani wala kupita kiasi,yeye hana dhambi,hakika Mwenyezi mungu ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu".[226] Na amesema tena Mwenyezi Mungu: "Enyi mlio amini! Bila shaka ulevi na kamari,na kuabudiwa (na kuombwa) asiyekuwa Mwenyezi Mungu,na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli (na kwa vinginevyo) yote haya ni uchafu ni katika matendo ya shetani.basi jiepusheni navyo ili mpate kufaulu. Hakika shetani anataka kukutieni uadui na bughudha baina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari, na anataka kukuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na (kukuzuilieni) kusali,basi je mtaacha (mabaya haya)?[227]
5. Uislamu umeruhusu kucheza michezo yenye faida kama vile myeleka,hata Mtume mwenyewe alishikana myeleka na bwana mmoja anaitwa rukana,Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamshinda.[228] Na pia kushindana mbio.Imepokewa kutoka kwa Bibi Aisha Mke wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakeamesema: Siku moja tulishinda mbio na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake nikamshinda,tukakaa muda mpaka nilipo nenepa,kisha tukashindana tena akanishinda,akasema; Namimi nimekulipa ule ushindi wako wa mwanzo".[229]
Na michezo kama kuogelea na kutupa mishale na vitu vinginevyo,na kupanda farasi,michezo yote hii imepokewa katika athari kwamba Umar bin Khatwab ambaye ni kiongozi wa pili wa waislamu baada ya kufa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwamba amesema: "Wafunzeni watoto wenu kutupa mishale,na kuogelea na kupanda farasi".
6. Uislamu pia umeamrisha kuujali mwili kwa kuutibu pindi upatwapo na maradhi.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Hakika Mwenyezi Mungu kateremsha maradhi na kateremsha tiba,na akajaalia kila ugonjwa una dawa yake,basi jitibuni enyi waja wa Mwenyezi Mungu lakini msijitibu kwa vitu alivyo viharamisha".[230]
7.Ukaamrisha Uislamu kutekeleza ibada ambazo ni sawa na chakula cha roho,ili iweze kusalimika na maradhi ya wasi wasi ambayo yanapelekea kuuathiri mwili na hatimaye kupatwa na maradhi. Amesema Mwenyezi Mungu: "Wale walio amini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi mungu nyoyo hutulia". [231]
Na Uislamu ukalizingatia swala la kuupuuza mwili na kutoupa haki yake ya chakula,kuupumzisha,kukidhi haja za kimaumbile kwa njia zilizo halali na mengineyo ni katika mambo yaliyo katazwa kisheria. Imepokewa kutoka kwa Swahaba mtukufu Anasi bun Malik- Mungu amuwie radhi- amesema : Walikuja watu watatu katika nyumba za wake wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake wakiwauliza kuhusu ibada za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anazo zifanya awapo nyumbani,pindi walipo elezwa kama kwamba waliziona ni chache,kisha wakasema :Hata hivyo Yeye sio sawa na sisi,maana Yeye kasamehewa madhambi yake;hapo mmoja wao akasema:Ama mimi nitaswali usiku muda wa maisha yangu yote,na mwingine akasema:Mimi nitafunga maisha yangu yote,na mwingine akasema: Mimi nitajitenga na wanawake sitaoa maisha yangu yote.Akaja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akawauliza : "Nyinyi ndio mlio sema kadha wakadha?!Naapa kwa Mwenyezi Mungu,hakika mimi ni mcha Mungu zaidi yenu,na ninamuogopa zaidi yenu,lakini mimi ninafunga na wakati mwingine ninakula,na nina swali na nina lala usingizi,na ninaoa,yoyote atakaye kwenda kinyume na mwenendo wangu basi huyo hayuko pamoja nami"[232]
Dini ya Uislamu ni Dini ya elimu na maarifa inawalingania watu kutafuta elimu.Amesema Mwenyezi MunguMtukufu: " Sema:je wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasio jua?".[233] Na ikawataja kwa ubaya watu wajinga .Akasema Mwenyezi Mungu katika kuelezea kisa cha Nabii Musa na watu wake kuhusu kisa cha ng`ombe:"Akasema:Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa wajinga".[234] Na ukajaalia katika elimu iko ambayo kuitafuta ni lazima kwa kila muislamu,kama vile mambo ambayo ni ya msingi kuyajua kila Muislamu yanayo husiana na Dini yake na maisha yake na nyingine sio lazima kwa kila mtu bali wakiwa nayo baadhi inatosha.Na Mweyezi Mungu hajapata kumuamrisha Mtume wake kujizidishia kitu miongoni mwa vitu vya kidunia ispokuwa elimu,na hii inaonyesha umuhimu wa elimu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na (uombe)useme;Mola wangu nizidishie elimu".[235] Na Uislamu umeiheshimu sana elimu na wenye elimu.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Si katika umati wangu asiye waheshimu wakubwa na kuwahurumia wadogo,na asiye tambua haki za wenye elimu".[236] Na uislamu ukampa mwenye elimu cheo na daraja kubwa kabisa.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Ubora wa mwenye elimu kati yenu ni sawa na ubora wangu kwenu nyinyi".[237] Na ili kuhimiza juu ya kutafuta elimu na kueleza ubora wake uislamu umejaalia kazi ya kutafuta elimu na kuifundisha ni jihadi kubwa ambayo mtu anaandikiwa malipo makubwa kwa Mwenyezi Mungu na ni njia ya kuipata Pepo .Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Mwenye kutoka kwa ajili ya kutafuta elimu anahesabiwa kuwa yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakapo rejea".[238] Na akasema vile vile " Hakuna mtu yeyote anaye shika njia kwa ajili ya kutafuta elimu ispokuwa Mwenyezi Mungu humrahisishia njia ya kuingia Peponi".[239] Na sio kwamba Uislamu umehimiza kutafuta elimu ya kisheria peke yake,bali hata kutafuta elimu zingine za kidunia,ambazo tumesema ni elimu za ziada,maana mwanadamu ana haja nazo. Amesema Mwenyezi Mung Mtukufu: " Je !huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mawinguni!na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali.Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu,yenye rangi mbali mbali,na (myengine )myeusi sana.Na katika watu na wanyama wanao tambaa na wanyama (wengine),pia rangi zao ni mbali mbali. Kwa hakika wanao muogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu (wanavyuoni).Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu msamehevu".[240] Utaona katika aya hizi Mwenyezi Mungu anamtaka mwanadmu atafakari kwa kina na hatimaye aweze kutambua kuwa yupo Muumba aliye viumba vitu hivi,kisha mwanadamu anatakiwa anufaike na vitu hivi alivyo viweka Mwenyezi Mungu.Bila shaka elimu hii si ya watu wa sheria peke yao bali hata watu wengine walio zama zaidi katika elimu ya uvumbuzi vitu hivi.Kwa mfano huwezi kujua ni namna gani mawingu yanajikusanya na hatimaye mvua inanyesha ila kwa kusoma fizikia na kemia.Na huwezi kujua namna ya kuotesha mimea ila kwa kusoma elimu ya kilimo,pia huwezi kujua tofauti za rangi zilizomo katika milima na katika ardhi ila kwa kusoma elimu ya jiolojia…nakadhalika.
Dini ya Kiislamu ni Dini inayo mfanya mtu ajichunge mwenyewe bila ya kusimamiwa,na hili ndilo linamfanya Muislamu wa kweli anakuwa ni mwnye kutafuta radhi za Mola wake katika maneno yake na matendo yake,na kujitenga mbali nay ale yanayo mkasirisha Mola wake,maana anatambua fika kwamba Mola wake anamuona katika harakati zake zote. Kwa mfano Muislamu anapo acha kuiba ni kwa sababu ya kumuogopa Mola wake na sio kwa ajili ya kumuogopa milinzi au askari,hivyo hivyo katika makosa mengine.Uislamu unamlea Muislamu iwe tabia yake anapokuwa peke yake na anapokuwa na watu ni ileile.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na ukinena kwa sauti kubwa (au ndogo ni sawasawa) kwani hakika Yeye anajua (yaliyo dhahiri na ) yaliyo siri na yaliyofichikana zaidi (kuliko siri) ".[241] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katika kuelezea maana ya Ihsani (wema); "Ihsani ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama kwamba unamuona,na ikiwa wewe humuoni basi hakika yeye anakuona".[242] Na ukafundisha Uislamu katika kuweka misingi ya mtu kujichunga mwenyewe:-
Kwanza: Kuamini kwamba kuna Mungu mmoja ,mwenye uwezo,mwenye ukamilifu katika dhati yake na sifa zake,anatambua mambo yote yanayo jiri katika ulimwengu huu,halitendeki ila alitakalo. Amesema Mwenyezi Mungu:" Anayajua yanayo ingia katika ardhi na yanayo toka humo, na yanayo teremka kutoka mbinguni na yanayo panda humo.Naye yu pamoja na nyinyi popote mlipo.Na Mwenyezi Mungu anaona mnayo yatenda (yote) ".[243] Bali elimu yake Mwenyezi Mungu haikomi katika vitu vyenye kuoneka au vinavyo julikana kupitia hisia,imefikia mpaka anajua hata wasi wasi uliomo katika nafsi za wanadamu.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu; " Na billa shaka tumemuumba mwanadamu Nasi tunajua yanayo pita katika nafsi yake,Nasi tu karibu naye zaidi kuliko mshipa wa shimgo yake".[244]
Pili:Kuamini kuwa kuna kufufliwa.Amesema Mwenyezi Mungu:"Kwa yakini atakukusanyeni siku ya Kiyama..".[245]
Tatu: Kuwa na yakini kwamba kila mtu atahesabiwa kivyake. Amesem mwenyezi Mungu :"Wala mbebaji(mizigo yake ya dhambi)hatabeba mizigo ya mwingine kumsaidia".[246]
Kila mwanadamu atahesabiwa mbele ya Mola wake ju yakila analo lisema na analolitenda,liwe ni kubwa au dogo,la kheri au la shari,na atalipwa kheri kwa yale ya kheri na shari kwa yale ya shari.Amesema Mwenyezi Mung Mtukufu: "Basi anaye fanya wema (hata) wa kiasi cha uzito wa mdudu chungu ataona jazaa yake. Na anaye fanya uovu(hata)wa kiasi cha uzito wa mdudu chungu ataona jazaa yake".[247]
Nne: Imehimizwa kutanguliza utiifu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake,na kuwapenda kuliko kingine chochote. Amesema Mwenyezi Mungu: " Sema:Kama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mlizozichuma na biashara mnazo ogopa kuharibikiwa na majumba mnayo yapenda;(ikiwa vitu hivi)ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake,basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake..".[248]
Uislamu ni Dini ambayo malipo yanaongezwa maradufu,ama maovu yenyewe hulipwa kama yalivyo. Amesema Mwenyezi Mungu: " Afanyaye kitendo kizuri atalipwa mfano wake mara kumi,na afanyaye kitendo kibaya hatalipwa ila sawa nacho tu".[249] Bali Uislamu umeweka malipo hata kwa nia nzuri tu hata kama mtu hakulitenda jambo zuri alilo linuia,si hivyo tu bali hata akikusudia kutenda jambo baya na baadae akaliacha kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu,anaandikiwa malipo mema,maana kuacha kwake ni kwa ajili ya kumuogopa Mwenyezi Muungu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwamba amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Pindi mja wangu anapokusudia kufanya jambo baya msiliandike mpaka atakapo lifanya ndipo muliandike,na akiliacha kwa ajili yangu basi muandikieni ujira,na atakapo kusudia kufanya jambo jema na akawa hakulifanya basi muandikieni ujira wake,na kama atalifanya basi muandikieni kumi mfano wake mpaka mia saba".[250]
Bali katika Uislamu matamanio ya mtu yaliyo ya halali yanaweza kugeuka kuwa ni ibada na mtu akaandikiwa malipo pindi yatakapo ambatana na nia nzuri;kwa mfano kula na kunywa endapo mtu atakusudia kuuhifadhi na kuulinda mwili wake na kupata nguvu ili aweze kuchuma chumo la halali na ili aweze kutekeleza yale aliyo wajibishiwa na Mola wake kama vile ibada na kuihudumia familia yake,basi anaandikiwa ujira kwa nia yake hii. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Pindi mtu akiihudumia familia yake kwa ajili ya kutaka malipo kwa Mwenyezi mungu basi huandikiwa malipo ya swadaka".[251] Vile vile Muislamu katika kukidhi matamanio yake na haja zake za kimaumbile katika njia ya halali na mke wake,kama wataweka nia nzuri (wakajaalia tendo lao hilo ni njia ya kujizuia na haramu) uzinifu inahesabiwa wako katika ibada na wanapata thawabu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Na katika kitendo cha mmoja wenu kumuendea mke wake ni swadaka"maswahaba wakamuuliza:Vipi mtu akidhi matamanio yake kisha aandikiwe thawabu?! Akasema:" Mwaonaje kama angeyapeleka matamanio yake katika njia za haramu, angeandikiwa dhambi? Hivyo hivyo akiyapeleka katika njia halali anasitahiki thawabu" .[252] Bali kila jambo analo lifanya Muislamu kama ataitakasa nia yake huandikiwa malipo ya swadaka. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Kila Muislamu anawajibikiwa kutoa sadaka",alipo sema hivyo Maswahaba wakmuuliza:Vipi kama mtu hakupata cha kutoa? Akasema:"Afanye kwa mikono yake,na ainufaishe nafsi yake na atoe sadaka",wakasema;Na kama hawezi je?akasema:" Basi na amsaidie mwenye matatizo"wakasema:Je kama hakuweza kufanya? Akasema "Basi na aamrishe mema" wakasema :Na kama hakufanya? "akasema: " Basi na ajizuie na shari maana kufanya hivyo itakuwa kwake ni sadaka".[253]
Katika Uislamu wale wanao tubia kikweli kweli na wakajuta kutokana na makosa yao na wakaweka azma ya kutorejea tena katika makosa yao,basi hubadilishwa yale maovu yao yakawa ni mema. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " ila yule atakaye tubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri,basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema,na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu".[254] Haya ni katika haki zinazo muhusu Mwenyezi Mungu,ama haki za wanadamu ni lazima zirejeshwe na kuwaomba msamaha. Uislamu unazungumza na akili ya mtu aliye tenda dhambi na kuiondoa hofu kubwa aliyonayo kwa kumfungulia mlango wa toba ili aweze kutubu dhambi zake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Sema: Enyi waja wangu milio jidhulumu nafsi zenu! Msikate tama na rehma ya Mwenyezi mungu,bila shaka Mwenyezi Mung husamehe dhambi zote,hakika Yeye ni mwingi wa kusamehe ni mwingi wa kurehemu".[255] Na ukajaalia jambo la kutubia ni jepesi lisilo kuwa na uzito wowote. Amesema Mwenyezi Mungu: " Na mwenye kutenda uovu (wa kuwachukiza wenzie )au akadhulumu nafsi yake (kwa kufanya kosa la kumdhuru mwenyewe tu) kisha akaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu,atamkuta Mwenyezi Munu ni mwenye kughufiria na Mwenye kurehemu".[256]
Haya ni kwa wale ambao ni Wailamu,ama wasiokuwa waislamu kisha wakaingia katika Uislamu wao hupata malipo mara mbili,kwa sababu ya kumuami Mtume wao kisha kuamini Utume wa Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake. Amesema Mwenyezi Mung Mtukufu: "Wale tulio wapa kitabu (kabla ya hii Qur-ani) (baadhi yao)wanaiamini hii(Qur-ani).Na wanapo somewa husema:Tunaiamini ,bila shaka hii ni haki itokayo kwa Mola wetu,kwa yakini kabla ya haya tulikuwa wenye kujisalimisha(kwa Mola wetu).Basi hao watapewa ujira wao mara mbili (kwa kumfuata Nabii Musa au Nabii Isa zamani na sasa kumfuata Nabii muhamad) na kwa kuwa walistahamili,na huondoa ubaya kwa wema,na hutoa (sadaka na zaka)katika yale Tuliyo wapa'.[257] Na zaidi ya hayo ni kwamba Mwenyezi Mung anwafutia madhambi yao yote waliyokuwa nayo kabla ya kuwa waislamu.Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipo mwambia Amru bin al-aaswi wakati alipokuja kusilimu kisha akashartisha kwamba kama atasamehewa makosa yake yaliyo tangulia basi ataingia katika Uislamu,ndipo MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia: " Je hujui kwamba Uislamu unayaporomosha na kuyafuta yote yaliyo tangulia?! ".[258]
Dini ya Kiislamu imewadhamini waumini wake kuendelea kupata malipo ya matendo yao mema hata baada ya kufa kwao,kupitia mema yao waliyo yaacha duniani. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Pindi anapo kua mwanadamu matendo yake hukoma ispokuwa mambo matatu; Swadaka yenye kuendelea,au elimu yenye manufaa,au motto mwema anaye muombea dua njema".[259] Na amesema vile vile "Mwenye kulingania katika uongofu hupata malipo sawa na malipo ya watakao ufuata uongofu huo,bila wao kupungukiwa chochote katika malipo yao,na mwenye kulingania katika upotevu hupata madhambi sawa na madhambi ya watakao ufuata upotevu huo,bila wao kupunguziwa chochote katika madhambi yao".[260] Na hili ndilo linamfanya Mwislamu wa kweli anakuwa ni mwenye pupa katika kutengeneza jamii yake katika mambo mbali mbali ya kheri,na kupambana na uharibifu wa aina yoyote ,na kuzuia jambo lolote linalo pelekea kuharibu jamii,ili kurasa za matendo yake siku ya Kiyama ziwe safi.
Uislamu umeiheshimu akili na kuipa haki yake,na kuwataka watu kuzitumia vizuri akili zao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Bila shaka katika mbingu na ardhi ziko alama kubwa (za kuonesha kuwa yuko Mwenyez Mungu) kwa ajili ya wanao amini. Na katika umbo lenu na katika viumbe alivyo vitawanya zimo alama (vile vile) kwa watu wenye yakini. Na (katika) kupishana(kufuatana)usiku na mchana na katika riziki aliyo teremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni(mvua) na akaifufua kwayo ardhi baada ya kufa kwake,na katika mabadiliko ya pepo,zimo alama pia kwa watu wenye akili".[261] Hivyo hivyo utazikuta aya nyingi katika Qur-ani zinazungumza na akili ya mwanadamu,na kuiamsha,mara nyingi utakuta aya kama hizi; "Je !hawana akili"? "Je! Hawazingatii"? "Je! Hawafikiri" " Je! Hawatambuui" nakadhalika. Lakini pia akili imewekewa ukomo wake,ambao ni katika vitu vinavyo weza kujulikana kupitia njia za hisia (ambazo ni tano),ama mambo ya ghaibu (yasiyo onekana wala kujulikana kwa njia za hisia) hapa akili haina nafasi. Na Uislamu katika kuheshimu akili na kuipa nafasi yake ndio maana ukawalaumu wale wenye kuiga na kufuata tu bila kuzitumia akili zao.Akasema Mweyezi Mungu Mtukufu: " Na wanapo ambiwa fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu,husema;Bali tutafuata yale tuliyo wakuta nayo baba zetu, je hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka (watawafuata tu)? ".[262]
Dini ya Kiislamu ni Dini inayo endana na maumbile sahihi ya mwanadamu,na haipingani kabisa na maumbile aliyo waumbia Mwenyezi Mungu watu wote. Amesema Mwenyezi Mungu : "Ndilo umbile alilo waumbia Mwenyezi Mungu watu (yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana na umbo la binadamu).[263] Lakini maumbile haya yanaweza kuathiriwa kutokana na mazingira yanayo mzunguka mtu.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Kila mtoto huzaliwa katika maumbile sahihi (ya Kiislamu) ispokuwa wazazi wake ndio humbadilisha na kumpeleka katika uyahudi au ukiristo au umajusi(wenye kuabudu jua) ".[264] Na Uislamu ndio Dini ya njia iliyo nyooka.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu ameniongoza katika njia iliyo nyooka,(katika) Dini iliyo sawa kabisa ambayo ndiyo dini ya Ibrahimu aliye kuwa muongofu,wala hakuwa miongoni mwa washirikina".[265]
Katika mafundisho ya Uislamu hakuna hata jambo moja linalo pingana na akili iliyo sawasawa,bali akili zinashuhudia juu ya ukweli na usahihi wa mafundisho ya Uislamu,maana maamrisho yake yote na makatazo yake yote ni uadilifu mtupu.Haukuamrisha jambo ispokuwa ndani yake kuna maslahi ya wazi wazi,na haukukataza jambo ispokuwa ndani yake kuna shari moja kwa moja au manufaa yake ni machache kuliko madhara yake,na haya yako wazi kwa mwenye kuzisoma aya za Qur-ani na hadithi za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake zilizo sahihi kwa mazingatio.
Dini ya Kiislamu imezikomboa nafsi za wanadamu kutoka katika utumwa wa kuabudu vitu visivyo kuwa Mwenyezi Mungu,kwa kujenga misingi ya imani katika nafsi ya Muislamu ya kutomuogopa yoyote ila Mwenyezi Mungu,na kuamini kuwa hakuna anaye weza kunufaisha wala kudhuru ila Mwenyezi Mungu.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na badala ya Mwenyezi Mungu (wa haki),(wale makafiri) wameshika miungu ambao hawaumbi chochote ila wao ndio walio umbwa,wala hawajimiliki(kujiondoshea) dhara wala (kujivutia) manufaa,wala hawamiliki mauti(kufisha) wala uhai wala kufufua".[266] Mambo yote na maamuzi yote yamo mikononi mwa Mwenyezi Mungu.Amesema Mwenyezi Mungu. "Na kama Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara(taabu),basi hakuna yoyote awezaye kuyaondoa ila Yeye,na kama akikugusisha kheri(hakuna wa kuweza kuiondoa ila Yeye tu peke yake),Yeye ndiye Muweza juu ya kila kitu".[267] Hata Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake pamoja na cheo kikubwa alicho nacho mbele ya Mola wake yanamfika yanayo weza kuwafika watu wengine.Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu: "Sema: Sina mamlaka ya kujipa nafuu wala kujiondoshea madhara ila apendavyo Mwenyezi Mungu,na lau kama ningelijua ghaibu ningejizidishia mema mengi, wala isingelinigusa dhara, mimi si chochote ila ni muonyaji na mtoaji habari njema kwa watu wanao amini".[268]
Uislamu umeipa uhuru nafsi ya mwanadamu kutokana na kuwa na khofu na wasi wasi kwa kutibibu na kuondoa sababu zinazo pelekea katika hali hiyo. Kwamfano:-
ü Ikiwa mtu anaogopa kwa sababu ya kifo,basi Mwenyezi Mungu anasema :"Na nafsi yoyote haitaweza kufa ila kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwa ajali iliyo wekwa".[269] Na akasema vile vile: "Unapo fika muda wao hawakawii saa moja wala hawatangulii".[270] Na vyovyote atakavyo fanya mwanadamu ili kuyakimbia mauti hakika mauti yanamuwinda,hawezi kuyakimbia.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema:Hakika mauti haya mnayo yakimbia,bila shaka yatakutana nanyi".[271]
ü Na ikiwa hofu yake ni kwa sababu yakuogopa ufakiri na umaskini,basi Mwenyezi Mungu anasema: " Na hakuna mnyama yeyote(yaani kiumbe chochote) katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Mwenyezi Mungu.Na anajua makao yake ya milele na mahali pake pa kupita tu (napo ni hapa duniani).Yote yamo katika kitabu kinacho dhihirisha(kila kitu. Kitabu chake Mwenyezi Mungu anacho kijua Mwenyewe hakika yake,si kama vitabu tunavyo vijua sisi).[272]
ü Na ikiwa hofu ni kwa ajili ya maradhi na misiba,basi Mwenyezi Mungu anasema: "Hautokei msiba katika ardhi wal katika nafsi zenu ila umekwishaandikwa katika kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kabla Hatujaumba.Kwa yakini hilo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu. Ili msihuzunike sana juu ya kitu kilicho kupoteeni (na kinacho kupoteeni ),wala msifurahi sana kwa alicho kupeni (na kwa anacho kupeni).Na Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye ajifakharishaye".[273]
ü Na ikiwa hofu ni kwa sababu ya kuwaogopa viumbe wenzako,basi Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anasema : " Muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi,muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako (ni mwenye kukusaidia katika kila jambo),jikurubishe kwa Mola wako wakati wa raha naye atakutambua wakati wa matatizo,na utakapo omba baasi muombe Mwenyezi Mungu,na ukihitaji msaada basi taka msaada kwa Mwenyezi Mungu,maana kalamu ya Mwenyezi Mungu imekwisha andika yote yatakayo tokea,laiti watu wakijitahidi ili kukunufaisha kwa jambo ambalo Mwenyezi Mungu hakukupangia basi hawataweza,na kama watu watafanya kila juhudi ili kukudhuru kwa jambo ambalo hakupanga Mwenyezi Mungu likupate basi hawataweza,hivyo kama utaweza ewe mwanadamu kuwa na subra pamoja na yakini nzuri kwa Mola wako basi fanya hivyo,na kama hukuweza basi kuwa mvumilivu,maana kuvumilia juu ya jambo unalolichukia kuna kheri nyingi,na utambue kwamba nusura hupatikana baada ya uvumilivu,na kwamba baada ya dhiki faraja".[274]
Dini ya Kiislamu ni yenye msimamo wa kati na kati katika mambo ya Dini na kidunia.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na vivyo hivyo Tumekufanyeni umma wa kati na kati (kama qibla chenu tulivyo kifanya bora) ili muwe mashahidi juu ya watu,na Mtume awe shahidi juu yenu".[275]
-Ni Dini ya wepesi na nyepesi.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu hakunituma mimi niwe ni mwenye kuyatia uzito mambo,bali kanituma nikiwa mfundishaji mwenye kufanya wepesi katika mafundisho".[276]
-Na ni Dini ya upole na msamaha.Imepokewa kutoka kwa Bibi Aisha – Mungu amuwie radhi- kwamba amesema:Siku moja walikuja mayahudi kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake wakasema: Assaamu alaykum, (maneno haya yana maana ya kumuombea dua mbaya),Bibi Aisha akayasikia maneno yale kisha akawajibu kwa kusema:Na nyinyi juu yenu laana ya Mwenyezi Mungu,hapo Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia mkewe:"Taratibu ewe Aisha ,hakika Mwenyezi Mungu anapenda upole katika kila jambo" Bibi Aisha akamwambia Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake Hivi hukuyasikia maneno waliyo yasema?Mtume akasema :"Nami nimewajibu kwa kusema nanyinyi pia".[277]
-Na ni Dini ya kuwapendelea watu kheri. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Mtu anaye pendwa na Mwenyezi Mungu zaidi ni yule mwenye kuwanufaisha watu,na matendo anayo yapenda zaidi Mwenyezi Mungu ni kitendo cha kumuingizia furaha ndugu yako Muislamu,au kumuondolea tatizo lililo mfika,au kumkidhia deni lake,au kumuondolea njaa,na kutembea na ndugu yangu Muislamu katika kukidhi haja yake ni bora zaidi kuliko kukaa itikafu msikitini mwezi mzima,na mwenye kuzuia ghadhabu zake pindi anapo kasirika Mwenyezi Mungu atamsitiri aibu zake,na mwenye kusamehe wakati anauwezo wa kulipiza basi Mwenyezi Mungu ataujaza radhi moyo wake siku ya kiyama,na hakika tabia mbaya inaharibu matendo ya mtu kama vile siki inavyo weza kuharibu asali pindi ikichanganyika nayo".
-Na ni Dini ya wepesi,na maamrisho yake yamejengwa katika msingi huu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Nitakacho kukatazeni basi kiacheni,na nitakacho kuamrisheni basi kifanyeni kwa kadri ya uwezo wenu,maana kilicho waangamiza walio kuwa kabla yenu ni wingi wa maswali na kutofautiana na Mitume wao".[278] Na ushahidi wa wazi juu yahili ni kisa cha yule swahaba aliye kuja kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! hakika mimi nimeangamia,MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake akamuuliza :"Una tatizo gani"? Akasema: Nimemuingilia mke wangu hali ya kuwa nimefunga. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia: "Je una uwezo wa kumuacha huru mtumwa"? akasema :Hapana. Akamuuliza tena: "Je unaweza kufunga miezi miwili mfululizo"? akasema : Hapana. Akamuuliza tena: "Je unaweza kuwalisha maskini sitini"? akasema :Hapana. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akakaa kimya kwa muda kidogo,mara ghafla akaja mtu mmoja na chombo kikiwa na tende,kisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: "Yuko wapi yule mtu aliyekuwa akiniuliza"?Yule bwana akaitika,Mtume akamwambia:" chukua tende hizi ukazitoe sadaka".yule bwana akasema : Nitampa nani ambaye ni fakiri kuliko mimi ewe Mtume wa Mungu? Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba hakuna mtaani kwetu familia ambayo ni fakiri kuliko familia yangu.Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akacheka mpaka meno yake yakaonekana,kisha akasema:" Basi wapelekee familia yako".[279] Maamrisho yote na ibada zote katika uislamu zinazingatia uwezo wa watu katika kuzitekeleza,halazimishwi mtu kufanya jambo ambalo liko nje ya uwezo wake,bali kuna wakati maamrisho na ibada husamehewa . Kwamfano:
-Kusimama katika swala ni wajibu,lakini kama mtu atashindwa kusimama anaruhusiwa kuswali akiwa ameketi,na kama atashindwa pia anaruhusiwa kuswali hali yakuwa amelala,na akishindwapia anaruhusiwa kuswali kwa kutumia ishara.
-Kusamehewa ibada ya kutoa zaka kwa asiyekuwa na uwezo,bali anastahiki kupewa akiwa ni fakiri.
-Kusamehewa ibada ya Hija kwa asiye na uwezo wa kimali au kimwili kama ilivyo bainishwa katika vitabu vya kisheri.Kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hijja katika nyumba yake,yule awezaye kufunga safari kwenda huko".[280]
-Pindi mtu anapo hofia kupoteza maisha anaruhusiwa kula au kunywa katika vitu vilivyo haramishwa kama mizoga,au damu,au nyama ya nguruwe –kwa kadiri ya kujizuia kifo- kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu: "Atakaye fikwa na dharura(ya kula vitu hivi)bila kutamani wal kupita kiasi,yeye hana dhambi".[281]
Dini ya Uislamu inazikubali dini zingine zilizo tangulia na kuwataka waislamu kuziamini na kuwaheshimu Mitume walio kuja nazo.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale wanao mkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume yake,na wanataka kutenga baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume yake,kwa kusema:Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa…".[282] Na Uislamu unakataza kuwatukana watu pamoja na itikadi zao.Amesema Mwenyezi Mungu : "Wala msiwatukane wale ambao wanawaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu,wasije wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri zao bila kujua".[283] Na inaamrisha kujadiliana na wale tunao khalifiana nao kwa hekima na upole.Amesema Mwenyezi Mungu: "Waite wayu katika njia ya Mola wako kwa hikima na mauidha mema,na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora(sio kwa kuwatukana wao au kutukana dini yao.Kwa njia hii huwezi kumvuta mtu).Hakika Mola wako ndiye anaye mjua aliye potea katika njia yake naye ndiye anaye wajua walio ongoka".[284]
Dini ya Kiislamu ni Dini ya amani kwa maana yake halisi,kuanzia ngazi ya kijamii.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Muumini wa kweli ni yule ambaye watu wanamuamini juu ya mali zao na nafsi zao,na Muislamu wa kweli ni yule ambaye watu wanasalimika na ulimi wake na mikono yake,na mpiganaji wa kweli ni yule anaye pigana na nafsi yake katika kumtii Mola wake,na mhamaji wa kweli ni yule aliye yahama madhambi na makosa".[285] Mpaka kufikia katika ngazi ya ulimwengu mzima,kwa kujenga misingi ya nahusiano mazuri na mapenzi na kutofanyiana uadui kati ya jamii ya kiislamu na jamii nyingine,hasa jamii ambazo hazikejeli Uislamu wala haziweki vizuizi katika kuwalingania watu katika Dini sahihi. Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini !ingieni katika hukumu za uislamu zote,wala msifuate nyayo za shetani,kwa hakika yeye kwenu ni adui dhairi".[286] Na ili kuchunga usalama Uislamu umewaamrisha wafuasi wake kuzuia uadui na kupambana na dhulma.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Na wanao kushambulieni basi nayinyi washambulieni kwa kadiri walivyo kushambulieni".[287] Na kutokana na jinsi Uislamu unavyopupia sana swala la amani,umewaamrisha Waislamu hata wanapokuwa katika vita kasha adui akataka wasimamishe vita kwa kuwekeana mikataba na makubaliano wanatakiwa wakubali. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kama (hao maadui) wakielekea katika amani nawepia ielekee na umtake msaada Mwenyezi Mungu.Hakika Yeye ndiye asikiaye na ajuaye".[288] Lakinihata hivyo Uislamu haukuwataka Waislamu kujidhalilisha kwa ajili ya kulinda amani,bali wameamrishwa kuilinda amani pamoja na kuchunga utukufu wao na kutokubali kudhalilika. Amesema Mwenyezi Mungu: "Basi msilegee na kutaka suluhu,maana nyinyi ndio mtakao shinda,na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi wala hatakunyimeni (thawabu za ) vitendo vyenu".[289]
Katika Uislamu hakuna kumlazimisha mtu kusilimu, anatakiwa aingie kwa kukinai mwenyewe.Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: "Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini,uongofu umekwisha pambanuka na upotofu".[290] Pindi ujumbe ukiwafikia watu na wakabainishiwa ukweli,baada ya hapo wanakuwa na uhuru wa kufuata au kukataa.Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: "Basi anayetaka na aamini na anayetaka na akufuru".[291]Maana uongofu na kuongoka vyote vimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu.Amesema Mwenyezi Mungu: "Na kama anagelitaka Mola wako (kuwalazimisha kwa nguvu kuamini)bila shaka wangeliamini wote waliomo katika ardhi(asibaki hata mmoja)(Lakini Mwenyezi Mungu hataki kuwalazimisha watu),basi je wewe utawashurutisha watu kwa nguvu hata wawe waislamu"?[292] Na katika mauzri ya Uislamu ni kwamba umewapa uhuru watu wa kitabu kufanya ibada zao,bila kuwalazimisha wawe Waislamu. Imenukuliwa toka kwa Abubakari swidiq Khalifa wa kwanza wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipokuwa akiliusia jeshi likienda vitani,akasema; Na mtawakuta watu wakifanya ibada katika nyumba zao za ibada,basi waacheni wala msiwadhuru.."[293] Na pia wamepewa uhuru wa kula na kunywa vile ambavyo dini yao imewaruhusu,hakuna ruhusa ya kuuwa nguruwe wao,wala kumwaga pombe zao. Na katika mambo yanayo husiana na ndoa na talaka na mengineyo wana uhuru wa kuyatekeleza kwa mujibu wa dini yao kulingana na masharti yaliyo bainishwa katika vitabu vya kisheria kwa urefu sina haja ya kuyaeleza hapa.
Uislamu umekuja kuwaacha huru watumwa,na ukaweka malipo na thawabu nyingi kwa mwenye kumuacha huru mtumwa,na ukalizingatia jambo hilo ni sababu ya kuingia Peponi.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Mwenye kumuacha huru mtumwa basi Mwenyezi Mungu atamuacha huru na Moto kwa kila kiungo alicho nacho mtumwa huyo..".[294] Na Uislamu umeharamisha njia zote za utumwa ispokuwa njia moja tu ambayo ni utumwa kwa njia ya mateka vitani ikiwa kiongozi wa Waislamu ataona hivyo,maana wamteka katika Uislamu wana hukumu zao maalumu ambazo kazi bainisha Mwenyezi Mungu alipo sema : "Basi mnapo kutana(vitani )na wale walio kukfuru wapigeni katika shingo zao (wafe mara moja) mpaka mkiwashinda sana hapo wafungeni (muwachukue makwenu hali yakuwa ni mateka),tena wawacheni kwa ihsani (waende zao makwao) au kwa kujikomboa".[295] Baada yakuwa Uislamu umefunga njia za utumwa ispokuwa katika hali moja tu tuliyo itaja,kisha ukaweka njia za kupunguza watumwa,kwa kujaalia kitendo cha kuwaacha huru ni kafara ya baadhi ya madhambi kama vile:-
-Kuua kusiko kwa makusudi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:"Na mwenye kumuua Mwislamu kwa kukosea basi ampe uungwana mtumwa(wake mmoja)aliye Muislamu na (pia)atoe diya(malipo) kuwapa warithi wake (huyo mtu aliye muua).Ispokuwa wakiacha wenyewe kwa kufanya kuwa ni sadaka (yao).Na (aliye uawa) akiwa ni jamaa wa maadui zenu hali yeye ni Muislamu;basi ampe uungwana mtumwa aliye Muislamu,na kama (aliye uawa)ni mmoja wa watu ambao kuna ahadi baina yenu na baina yao;basi warithi wake wapewe malipo,na pia apewe uungwana mtumwa alliye Muislamu..".[296]
-Kuto kutekeleza kiapo mtu anapo apa. Amesema Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu hatakuteseni kwa viapo vyenu vya upuuzi,bali atakushikeni kwa sababu ya (vile viapo) mlivyoapa kwa nia mlioifunga barabara.Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha kati na kati mnacho walisha watu wa majumbani mwenu,au kuwavisha ,au kumpa uungwana mtumwa".[297]
-Kosa la mwanaume kumtamkia mkewe kuwa yeye ni sawa na mama yake. Amesema Mwenyezi Mungu: "na wale wawaitao wake zao mama zao,kisha wakarudi katika yale waliyo yasema (wakataka kuwarejea wake zao wakae kama desturi ya mke na mume) basi wampe uhuru mtumwa kabla ya kugusana".[298]
- Kumuingilia mke mchana wa mwezi wa ramadhani.Imepokewa kutoka kwa Abu huryra –Mungu amuwie radhi- kwamba mtu mmoja alimuingilia mkewe mchana katika mwezi wa ramadhani,akaja kumuuuliza MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake kuhusu hukumu yake ,Mtume akamuuliza "Je unaweza kumuacha huru mtumwa"? akasema hapana,akamuuliza "Je unaweza kufunga miezi miwili mfululizo"?akasema hapana,akamwambia :"Walishe masikini sitini".[299]
-Pia ni kafara ya kumfanyia uadui mtumwa. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Atakaye mpiga mtumwa wake kwa kumuonea pasina sababu basi kafara yake ni kumuacha huru".[300]
Na miongoni mwa mambo yanayo onyesha jinsi uislamu ulivyo himiza swala la kuwaacha huru watumwa ni:-
1-Kuamrisha kuwekeana mkataba baina ya mtumwa na bwana wake ,wanakubaliana atoe malipo maalumu ili aweze kuacha huru "N a wale wanao taka kuandikiwa (ili wapate uungwana) katika wale iliyo wamiliki mikono yenu ya kuume,basi waandikieni mkiona wema kwao.Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni".[301]
-Pia ukajaalia Uislamu miongoni mwa kazi za Zaka ni kutumika katika kuwakomboa watumwa na mateka. Amesema Mwenyezi Mungu: "Sadaka (hupewa watu hawa):Mafakiri na masikini na wanao zitumikia,na wano tiwa nguvu nyoyo za (juu ya Uislamu),na katika kuwapa uungwana watumwa,na katika kuwasaidia wenye deni,na katika (kutengeneza) mambo aliyo yaamrisha mwenyezi Mungu,na katika (kupewa) wasafiri (walio haribikiwa).Ni faradhi inayo toka kwa Mwenyezi Mungu,na Mwenyezi Mungu ni mjuzi Mwenye hikima".[302]
Dini ya Uislamu sheria zake zimegusa nyanja zote za maisha;katika matendeano, vita,ndoa, uchumi,siasa,ibada na kila jambo ambalo ni sababu ya kupatikana jamii iliyo bora.Na kadiri watu wanavyo jiweka mbali na utaratibu na mfumo wa Kiislamu ndivyo wanavyo haribikiwa mambo yao kidini na kidunia. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:"Na tumekutere-mshia kitabu hiki kielezacho kila kitu,na ambacho ni uongofu na rehema na habari za furaha kwa wanao jisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu) ".[303]
Uislamu umeweka nidhamu nzuri na mafungamano kati ya mja na Mola wake,na mahusiano ya mja na jamii yake na hata mazingira yaliyo mzunguka.Katika mafundisho ya Kiislamu hukuti jambo hata moja linalo pingana na akili au maumbile yaliyo sahihi,na ushahidi wa wazi juu ya hili unaonekana katika mafundisho yake ambayo yamegusa kila jambo amablo linahusiana na maisha ya watu ya kila siku,kama vile adabu za kukidhi haja (kwenda chooni),ameelekezwa Muislamu ni mambo gani anatakiwa kuyafanya kabla na baada ya kukidhi haja. Amesimulia swahaba Mtukufu Abdur-rahmani bin Zaid kwamba aliuylizwa Salman (ni mmoja katika maswahaba wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: Unadai kwamba Mtume wenu kawafundisha kila kitu,hata namna ya kukidhi haja? Akasema: Ndio katukataza kuelekea Kibla pindi tunapo kojoa au tunapo kidhi haja kubwa,na akatukataza pia kustanji (kujisafisha )kwa kutumia mkono wa kulia,na akatukataza kutumia chini ya mawe matatu tunapo jisafisha, na akatuzuia kutumia mifupa au kinyesi cha wanyama wakati wa kustanji".[304]
Uislamu umemnyanyua mwanamke na kumkirimu, na ukajaalia kitendo cha kumkirimu mwanamke ni dalili na alama ya ubora wa mtu.Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Muumini ambaye ni mkamilifu wa imani ni yule mwenye tabia njema,na aliye mbora miongoni mwenu ni yule mwenye tabia njema kwa wake zake".[305] Uislamu umehifadhi utukufu wa mwanamke,na haukumzingatia kwamba yeye ndio chanzo cha madhambi ,na kwamba yeye ni sababu ya kutoka baba yetu Adamu Peponi kama wanavyo dai watu wa dini zilizo tangulia. Amesema Mwenyezi Mungu: "Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asili) moja,na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile.Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao.Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana.
Na (muwatazame)jamaa.Hakika Mwenyezi Mungu ni mlinzi juu yenu(anayaona yote mnayo yafanya) ".[306] Na Uislamu umefuta nidhamu za kijeuri dhidi ya mwanamke zilizokuwa zimetawala,hasa ile dhana iliyo kuwepo kuwa mwanamke hana haki yoyote,dhana iliyo pelekea kumnyima mwanamke haki zake za kibinadamu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Hakika wanawake ni wenza (wanashirikiana) na wanaume".[307] Na ukaheshimiwa utu wake na karama yake,na ikawekwa adhabu kali kwa mwenye kuchezea heshima yake kwa kumtuhumu tuhuma ya kumvunjia heshima. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na wale wanao wasingizia wanawake watwahirifu (kuwa wamezini), kisha wasilete mashahidi wanne, basi wapigeni mijeledi thamanini, na msiwa-kubalie ushahidi wao tena,na hao ndio mafasiki".[308] Na ikahifadhiwa haki yake ya kurithi kama anavyo rithi mwanaume, wakati huko nyuma alikuwa hapewi chochote katika mirathi. Akasema Mwenyez Mungu : "Wanaume wanasehemu katika mali wanayo yaacha wazazi na jamaa walio karibu, na wanawake (pia) wanayo sehemu katika yale waliyo yaacha wazazi na jamaa walio karibu,yakiwa kidogo au mengi.(haya) ni mafungu yaliyofaradhishwa na Mwenyezi Mungu".[309] Pia Uislamu ukampa mwanamke uhuru kamili wa kutumia mali yake,na kuwa na haki ya kuuza na kununua bila ya kuingiliwa na mtu ila kama atakwenda kinyume na sheria. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini! Toeni katika vizuri mlivyo vichuma".[310] Na Uislamu ukawajibisha kumsomesha mwanamke.Akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " kutafuta elimu ni wajibu juu ya kila muislamu".[311] Na ukaamrisha kumlea malezi mazuri,na ukajaalia jambo hilo ni sababu ya kuingia Peponi. Akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Mwenye kuwalea mabinti watatu malezi yaliyo mema,kisha akawaozesha na akawafanyia wema,basi amesitahiki Pepo".[312]
Uislamu ni Dini ya usafi:
1- Wa nje (wenye kuonekana) kama vile ushirikina.Amesema Mwenyezi Mungu." Hakika ushirikina ni dhulma kubwa kabisa".[313] Au kufanya jambo kwa kutaka uonekane kwa watu au usifiwe. Amesema Mwenyezi Mungu: " Basi adhabu itawathibitikia wanao Sali.Ambao wanapuuza (maamrisho ya) sala zao.Ambao hufanya matendo yao ili watu wawaone tu. nao hunyima misaada".[314] Au tabia ya kujikweza na kujiona bora kuliko wengine. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala usiwatazame (usiwafanyie watu jeuri) kwa upande mmoja wa uso,wala usende katika ardhi kwa maringo,hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye,ajifaharishaye. Na ushike mwendo wa kati na kati,na uteremshe sauti yako,bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote(kwa makelele yake).[315] Au tabia ya kiburi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Hatoingia Peponi yeyote mwenye chembe ya kiburi ndani ya moyo wake"mtu mmoja akamuuliza Mtume kwa kusema : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu,bila kila mtu anapenda avae nguo nzuri, viatu vizuri na kadhalika!,hapo mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akambainishia makusudio ya maneno yake kwa kusema : "hakika Mwenyezi Mungu ni Mzuri na anapenda vilivyo vizuri,lakini kiburi maana yake ni kuikanusha haki na kuwadharau watu".[316] Au kuwa na tabia ya husuda.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Tahadharini san na tabia ya husuda,maana husuda inakula mema ya mtu kama vile moto unavyo kula kuni au nyasi".[317]
2- Usafi wa ndani. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini! Mnapo simama ili mkasali,basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni,na mpake vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu mpaka vifundoni,na mkiwa na janaba basi ogeni,na mkiwa wagonjwa au mmo safarini au mmoja wenu ametoka chooni,au mmeingiliana na wanawake na hamkupata maji ,basi kusudieni (tayamamuni)udongo(mchanga)ulio safi na kuupaka nyuso zenu na mikono yenu.Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu,bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru".[318]
Uislamu ni Dini yenye nguvu za dhati yenye uwezo wa kingia ndani ya nyoyo na akili za watu,na jambo hili ndilo limeifanya ni dini yenye kuenea kwa kasi ya ajabu na watu kuingia katika Uislamu kwa wingi pamoja na hali ya udhaifu wa kimali waliyo nayo waislamu katika kuutangaza uislamu,wakati maadui wa Uislamu wanamiliki nyenzo mbali mbali na wanafanya kazi usiku na mchana ili kupambana na Dini hii na kuipaka matope na kuwafanya watu wasiingie katika Uislamu,lakini pamoja na yote haya watu wanasilimu makundi kwa makundi,na ni nadra sana kumkuta Muislamu anatoka katika Uislamu na kuingia katika dini nyingine.Na nguvu hii ya Uislamu imekuwa na athari na mchango mkubwa katika kusilimu watu wengi ambao waliusoma Uislamu wakiwa na malengo ya kutaka kujua kasoro zilizomo ili wapate njia ya kuushambulia,badala yake wakakuta uzri wa Uislamu na mafundisho yake yanayo endana na aikili na maumbile sahihi ya mwanadamu,ikawafanya wabadili muelekeo wa maisha yao na kuingia katika Dini hii. Hata maadui wa Uislamu wameshuhudi akuwa Uislamu ni Dini ya haki,miongoni mwa watu hao ni huyu bwana aitwaye "Margoliouth"[319]amabaye uadui wake juu ya Uislamu ni maarufu,lakini alipouona utukufu wa qur-ani hakusita kusema ukweli,akasema:"Hakika katika mambo ambayo wanakubaliana watafiti wote juu ya dini ni kwamba Qur-ani imeshika nafasi ya juu katika vitabu vitakatifu vyote,japokuwa ni kitabu cha mwisho(yaani kimeteremshwa kikiwa ni cha mwisho) lakini kimevitangulia vitabu vyote katika kwa jinsi kinavyo weza kumuathiri mwanadamu taathira ya ajabu kabisa,kwa hakika kimekuja na fikra mpya kwa mwanadamu,na kikaweka misingi madhubuti ya kitabia".Mwisho wa kunukuu.
Uislamu ni Dini ianayo himiza kusaidiana ,imemuwajibishia Muislamu kuwajali ndugu zake waislamu popote pale watakapo kuwa.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Utawaona waumini (wa kweli ) katika kuhurumiana kwao na kupendana kwao ni mfano wa mwili mmoja,pindi kiungo kimoja kinapo patwa na maumivu basi mwili mzima huugua na kukesha".[320] Na uislamu umewaamrisha kutengeneza hali zao ima kwa njia ya sadaka ambazo ni za lazima kama vile Zaka au sadaka zinginezo. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hawi muumini wa kweli mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake vile anavyo vipenda mwenyewe katika nafsi yake".[321] Na kusaidiana nao wakati wa matatizo. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Muumini kwa Muumini mwenzie (katika kushirikiana kwao na kusaidiana kwao ) ni kama mfano wa jengo noja lililo kamatana madhubuti".[322] Na Uislamu umekataza mtu kumdhalilisha Mwislamu mwenzie.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Mtu yeyote atakaye mdhalilisha Muislamu mwenzie katika sehemu ambayo anavunjiwa heshima basi naye ajue kuwa Mwenyezi Mungu atamdhalilisha katika mazingira amabyo ni mwenye kuhitajia nusura,na yeyote atakaye mnusuru Mwislamu mwenzie katika mazingira ambayo anavunjiwa heshima yake,basi mwenyezi Mungu atamnusuru katika mazingira ambayo anahitajia nusura yake".[323]
Uislamu umekuja na nidhamu ya mirathi,amabpo hugawiwa urithi(baada ya kulipa madeni ya marehemu na kutoa wasia wake) kwa wanao stahiki kumrithi,wakubwa kwa wadogo,wake kwa waume,kwa ugawaji wenye uadilifu,ambao kila mwenye akili timamu anashuhudia hivyo,wnarithishwa kulingana na ukaribu wao kwa marehemu,na manufaa yao kwake. Uislamu haukumpa haki mtu yoyote kugawa mirathi kwa mujibu wa matamanio yake,bali Qur-ani tukufu imebainisha fungu wanalo sitahiki watoto,na wazazi,na mke au mume,na ndugu.Lakini hapa sio mahala pa kuyaeleza kwa ufafanuzi wake,mwenye kutaka kufahamu zaidi na arejee katika vitabu vilivyo eleza mambo hayo kwa urefu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Hakika Mwenyezi Mungu amempa kila mtu haki yake,hivyo hakuna ruhusa ya kuusia mali kwa mwenye kurithi".[324]
Uislamu umeweka nidhamu ya Wasia,Muislamu anayo haki ya kutoa wasia katika sehemu ya mali yake baada ya kufa kwake ipelekwe ktika mambo ya kheri (ifanyiwe kazi za kheri) ili iwe ni sadaka yake ambayo malipo yake ni yenye kuendelea hata baada ya kifo chake,lakini hata hivyo kimewekwa kiwango maalumu katika wasia huu,kwamba usivuke theluthi ya mali yake. Imepokewa kutoka kwa Aamir bin Saad- Mungu amuwie radhi- amesema: Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuwa akija kuniona nikiwa mgonjwa,nikiwa katika mji wa Makka,nikamuuliza nikasema: Mimi nina mali nyingi,je ninaruhusiwa kuusia mali yangu yote?akasema :"Hapana",nikasema basi nusu yake? Akasema: "Hapana", nikasema basi theluthi yake? akasema:"Theluthi sawa,hata hivyo pia theluthi ni nyingi,maana ukiwaacha warithi wako wakiwa ni matajiri ni bora zaidi kuliko kuwaacha wakiwa ni masikini ombaomba,na chochote ukitoacho hiyo ni sadaka kwako,hata tonge unalo litia katika kinywa cha mkeo pia ni sadaka". [325] Lakini wasia unakubalika kama hautakuwa na madhumuni ya kuwadhuru warithi.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Baada ya kutoa vilivyo usiwa au kulipa deni pasipo kuleta dhara.(Huu) ndio wasia ulio toka kwa Mwenyezi Mungu".[326]
Uislam umeweka nidhamu ya adhabu ambazo lengo lake ni kulinda amani na usalama wa jamii kutokana na kuenea kwa maovu.Hivyo adhabu hizi zinakuwa ni sababu ya kuhifadhi damu za watu na heshima zao na mali zao,na zinawazuia waovu na wale wenye tabia za kiadui,ndio maana Uislamu ukalipangia kila kosa adhabu yake inayo lingana na uzito wa kosa lenyewe,kwamfano kosa la kuua kwa makusudi ikawekwa hukumu ya kisasi.Amesema Mwenyezi Muungu Mtukufu: " Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika walio uawa.." .[327] ispokuwa kama ndugu wa marehemu wataamua kusamehe.Amesema Mwenyezi Mungu. "Na anaye samehewa na ndugu yake.. (yaani ndugu wa marehemu)".[328] Na katika kosa la wizi ikawekwa hukumu ya kukatwa mkono. Amesema Mwenyezi Mungu." Na mwizi mwanamumue na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao,malipo ya yale waliyoyachuma.Ndiyo adhabu itokayo kwa Mwenyezi Mungu.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu na Mwenye hekima".[329] Pindi mtu akitambua kwamba akiiba mkono wake utakatwa bila shaka atajizuia na kitendo hicho na hivyo kuuhifadhi mkono wake na kuzisalimisha mali za watu. Na ikawekwa adhabu ya mwenye kufanya uzinifu apigwe bakora endapo atakuwa hajaowa.Akassema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanaume, mpigeni kila mmoja katika wao bakora mia..".[330] Na ikawekwa pia adhabu ya bakora kwa kumvunjia mtu heshima kwa kuzushia uzinifu. Amesema Mwenyezi Mungu " Na wale wanao wasingizia wanawake watwaharifu (walio jihifadhi na uzinifu) kuwa wamezini kisha wasilete mashahidi wane basi wapigeni bakora thamanini na msiwakubalie ushahidi wao tena na hao ndio mafaasiq".[331] Kisha Uislamu ukaweka kanuni ambazo kwazo hukadiriwa adhabu sitahiki kwa kila kosa. Akasema Mwenyezi mungu: "Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na (ubaya) huo".[332] Akasema vile vile Mwenyezi Mungu "Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo onewa".[333] Lakini adhabu hizi tulizo zieleza kuna masharti maalumu katika kuzitekeleza,pia Uislamu haukujaalia kutekeleza adhabu hizi ni jambo lisilokuwa na khiyari ,bali mtu amepewa uhuru wa kusamehe kama akitaka kufanya hivyo katika makosa ambayo yanafungamana na haki za mtu.Amesema Mwenyezi Mung: "Lakini atakaye samehe na kusuluhisha ugomvi ujira wake uko kwa Mwenyezi Mungu".[334] Na Uislamu katika kuweka adhabu hizi makusdio yake makubwa ni kuhifadhi haki za watu na kuleta amani na utulivu katika jamii,na kutoa fundisho kwa kila mtu mwenye mawazo machafu ya kutaka kuharibu aman katika jamii,maana muuaji akijua kuwa nayeye atauawa,namwizi akajua kuwa atakatwa mkono,na mzinifu akajua kuwa atakaangwa bakora,na mwenye tabia ya kuwazushia watu akajua kuwa atakaangwa bakora pia,bila shaka atakoma,na hivyo atasalimika yeye na kuisalimisha jamii yake. Na hapa unabainika ukweli na uzito uliomo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema : "Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili ili msalimike".[335] Labda baadhi ya watu wanaweza kusema kwamba baadhi ya adhabu zilizo wekwa na Uislamu katika baadhi ya makosa ni adhabu kali sana na za kinyama! ,Mtu kama huyu tunamjibu ifuatavyo; Hakika watu wote wanakubaliana kwamba haya yaliyo tajwa hapo nyuma ni makosa yaliyo na madhara makubwa katika jamii,na tunakubaliana kwamba ni lazima yakomeshwe kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuyawekea adhabu,ispokuwa tunatofautiana katika aina ya adhabu inayo sitahiki juu ya makosa hayo. Lakini hebu kila mmoja aiulize nafsi yake na awe mkweli katika jawabu lake,je adhabu zilizo pangwa na Uislamu zinauwezo wa kukomesha na kutokomeza kabisa mako maovu hayo,au adhabu zilizowekwa na wanadamu na ambazo zimekuwa ni sababu ya kuongezeka maovu kila kukicha?! Ukweli ni kwamba kiungo flani katika mwili kinapo haribika njia sahihi ni kukiondoa ili kuusalimisha mwili!.
Uislamu umehalalisha njia zote za kutafuta mali,kama vile kufanya biashara na kadhalika maana ni katika njia za kuwafanyia watu wepesi katika maisha yao,lakini ni lazima iwe chini ya misingi inayo kubalika kisheria,ili kuweza kuhifadhi haki za watu kwa njia ya makubaliano kati ya pande mbili(muuzaji na mnunuzi),na kukijua vizuri chenye kuuzwa,na maasharti yake na wasifu wake,na Uislamu haukuharamisha kitu ispokuwa kinachokuwa na madhara,na dhulma ndani yake,kama vile riba,kamari,na biashara zinazokuwa hazieleweki vizuri katika pande zote.Na japo kuwa uhuru wa kutumia mali kwa njia zinazo kubalika ni haki ya kila mtu ila Uislamu umeweka nidhamu ya kumzuia mtu kuitumia mali yake pindi ikigundulika kwamba utumiaji wake unaweza kumsababishia madhara yeye mwenyewe au wengine,kwamfano sheria imeweka utaratibu wa kumzuilia majununi(taahira) na motto mdogo (amabye hajafikia baleghe),au mwenye madeni ambayo yamekuwa ni mengi kuliko mali yake,mpaka atakapo lipa madeniyote.Bila shaka katika nidhamu hii mna hekima kubwa kabisa isiyofichikana kwa kila mwenye akili timamu,na mna kuchunga haki za watu zisiweze kuchezewa na kupotea .
Uislamu ni Dini ya umoja na mshikamano,imewalingania waislamu wote kuwa katika safu moja na katika msimamo mmoja ili waweze kuwa na nguvu,wametakiwa kufanya hivyo kupitia mambo yafuatayo;
-Kuacha ubinafsi na kujikweza kwa sababu za kimadhehebu,na ukabila,na jinsia,mambo ambayo ni sababu ya kuletea mifarakano na mgawanyiko. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitilafiana baada ya kuwafikia dalili zilizo wazi(za kuwakataza hayo),na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa".[336] Hivyo swala la kuhitilafiana sio katika mafundisho wala muongozo wa Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale walio farikisha dini yao na wakawa makundi makundi,huna uhusiano nao wowote,bila shaka shauri yao(ya kuwaadhibu) iko kwa Mwenyezi Mungu,kisha (hapo wakati wa kuwaadhibu)Atawabainishia waliyokuwa wakitenda".[337] Maana kuhitilafiana na na kutofautiana ni sababu ya kuondokewa na heba na kushuka heshima na kutoogopwa na maadui. Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu: "Wala msizozane (msigombane)msije mkaharibikiwa na kupoteza nguvu zenu".[338]
-Kutakasa itikadi na ibada kutokana na mambo ya ushirikina na mambo ya uzushi.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wa kuitakidia Mola ni Mwenyezi Mungu tu,lakini wale wanaofanya wengine kuwa ni waungu badala yake (husema): Sisi hatuwaabudu hawa ila wapate kutufikisha karibu kabisa na Mwenyezi Mungu".[339]
Uislamu umewawekea wazi watu mambo ya ghaibu na kuwabainishia habari za nyumati zilizo tangulia, maana ukiisoma Qur-ani utakuta katika aya zake nyingi Mwenyezi Mungu anatusimulia habari za Mitume walio tangulia na kaumu zao na mambo yaliyo wakuta. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwa hakika tulimpeleka Musa pamoja na aya zetu na hoja zilizo wazi.Kwa Firauni na wakuu (wa umma) wake..".[340] Akasema tena Mwenyezi Mungu: "Na (wakumbushe) aliposema (Nabii)Isa bin Marya(kuwaambia mayahudi): Enyi wana wa Israili,Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nisadikishaye yaliyokuwa katika taurati..".[341] Akasema tena Mwenyezi Mungu:" Na kwa Adi (Tulimpeleka) ndugu yao Hud..".[342] Na hivyo hivyo Mitume wengine walio bakia Qur-ani imetusimlia yaliyojiri katiyao na watu wao.
Qur-ani imetoa chalenji kwa wanadamu wote pamoja na majini kwamba walete kitabu mfano wa qur-ani,na chalenjii hii ni yenye kuendelea mpaka siku ya Kiyama, hakutatokea mtu wa kuweza kufanya hivyo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Sema: Hata wakijikusanya watu wote na majini ili kuleta mfano wa hii Qur-ani basi hawangeliweza kuleta mfano wake, hata kama watasaidiana (vipi) wao kwa wao".[343] Chalenji haikuishia hapo tu katika kuleta Kitabu kizima mfano wa Qur-ani ,bali kawataka walete hata baadhi ya sura. Amesema Mwenyezi Mungu: "Ndio kweli wanasema kuwa; Amekitunga mwenyewe (Muhamad kitabu hiki)? sema: Basi leteni sura kumi za uongo zilizo tungwa mfano wa hii Qur-ani, na waiteni muwawezao (kuwaita) badala ya mwenyezi Mungu (waje kukusaidieni kutunga hivyo) ikiwa mnasema kweli".[344] Na ikaendelea zaidi ya hapo na kuwataka walete japo sura moja tu mfano wa hii Qur-ani. Akasema Mwenyezi Mungu: "Na ikiwa mnashaka kwa hayo tuliyo mteremshia Mja wetu(kuwa hakuteremshiwa na Mwenyezi Mungu), basi leteni sura moja iliyofanywa na (mtu) aliye mfano wake,na muwaite waungu wenu kinyume na Mwenyezi Mungu (wakusaidieni) ikiwa mnasema kweli".[345]
Dini ya Kiislamu ni moja ya dalili miongoni mwa dalili za kumalizika dunia na kusimama Kiyama,maana Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alibainisha kuwa Yeye ni Nabii ambaye kutumwa kwake ni dalili ya kukaribia Kiyama.Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki –Mungu amuwie radhi- amesema kuwa Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Nimetumwa ukiwa ujio wangu na kusimama kwa kiyama ni kama hivi.." kisha akaashiria kwa kuunganisha kidole cha kati na kidole cha shahada.[346] Na hii ni kwakuwa Yeye ndiye Mtume wa mwisho hakuna Mtume mwingine baada yake.
Mtazamo wa Uislamu juu ya siasa kwa kifupi:
Kama ilivyo katika mambo mengine pia katika swala la siasa Uislamu umeweka misingi na kanuni ambayo Dola ya Kiislamu inatakiwa kuifuata,na ukamzingatia mtawala katika dola ya Kiislamu ni mwenye kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu kupitia kanuni na misingi hii.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je wao wanataka hukumu za kijahili (ya zile siku za ujinga kabla ya kuletwa Mtume)? Na nani aliye mwema zaidi katika hukumu kuliko Mwenyezi Mungu;(yanafahamika haya) kwa watu wenye akili".[347] Hivyo mtawala katika Uislamu ni kama wakili wa umma mzima,na inamlazimu kwa mujibu wa uwakala huu:-
1. Afanye kila njia kuhakikisha anatekeleza sheria za Mwenyezi Mungu,na kurahisisha njia za maisha ya raia,na kuihifadhi dini yao,na amani yao,na kulinda nafsi zao na mali zao. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Mja yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atamkabidhi jukumu la kuwachunga raia wake kisha asitekeleze amana hiyo basi hatoipata harufu ya Pepo".[348] Kwahiyo mtawala katika dola ya Kiislamu anapaswa kuwa kama alivyo sema Umar bin Alkhatwab- Mungu amuwie radhi- siku moja akiwaambia raia wake: Nielekezeni mtu ambaye naweza kumpa majukumu ya jambo ambalo linaisumbua akili yangu, miongoni mwa mambo ya waislamu.Wakasema:Abdur-rahmani bin Auf anafaa kulisimamia jambo hilo, akasema huyo ni dhaifu,wakamtaja mwingine,akasema: Huyo pia simuhitaji, wakasema unamtaka yupi basi? akasema: Nataka mtu ambaye nitakapo mpa madaraka kwa watu hatajikweza bali atajiona yeye ni mmoja katika wao,na asipokuwa kiongozi wao basi ajione ana majukumu kama kiongozi.Wakasema: Mwenye sifa hizo ni Rabiu bin Haarith, akasema: Ni kweli huyo anastahili wadhifa huu,kisha akamtawalisha.
2. Asimuweke madarakani katika mambo yanayo wahusu waislamu mtu asiye na sifa za kubeba majukumu hayo,na asiye weza kuibeba amana,kama vile kumpa madaraka mtu kwa misingi ya urafiki,au ujamaa na ukaribu,na kuwaacha wenye sifa. Mfano hai tunaupata kwa Khalifa wa kwanza wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake Abubakari –Mungu amuwie radhi- alipo mwambia Yazid bin sufyani wakati alipo mtuma aende shamu kusimamia mambo ya Waislamu: Ewe Yazidi hakika wewe una jamaa zako huko uendako, tahadhari usije ukawapendelea na kuwapa madaraka, hakika mimi nakuhofia sana juu ya hilo,maana nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema:"" Atakaye tawalishwa jambo lolote katika mambo ya Waislamu kisha naye akamtawalisha mtu kiupendeleo,basi laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake,na Mwenyezi Mungu hatopokea chochote katika ibada zake na atamuingiza Motoni".[349]
Na miongoni mwa uzuri wa kanuni na misingi hii ni kwamba:-
Misingi hii kaiweka Mwenyezi Mungu Mwenyewe,na watu wote katika misngi hii wako sawa,hakuna tofauti yoyote kati ya mtawala na mwenye kutawaliwa,wala kati ya tajiri na masikini,wala kati ya mweupe na mweusi,na hakuna mtu yoyote mwenye haki ya kuhalifu sheria na kanuni hizi hata kama atakuwa na cheo cha aina gani,au akaweka sheria zinazo kwenda kinyume na sheria hizi.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haiwi kwa mwanaume aliye amini wal kwa mwanamke aliye amini,Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri wawe nahiyari katika shauri lao.Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amepotea upotofu ulio wazi kabisa".[350]
Watu wote wanawajibika kufuta sheria na kuziheshimu. Amesema Mwenyezi Mungu: "Haiwi kauli ya waislamu wanapo itwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao ila kusema:Tuanasikia na tunatii,na hao ndio watakao fuzu".[351] Katika uislamu hakuna mtu aliye na uhuru wa moja kwa moja,hata mtawala uhuru wake una mipaka iliyowekwa na sheria,ikitokea kaikhalifu basi hakuna haki ya kumtii.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Ni juu ya kila Muislamu kumsikiliza kiongozi na kumtii kwa yale ayapendayo na hata asiyo yapenda,ispokuwa kama ataamrishwa jambo ambalo ni maaswi (kumuasi Mwenyezi Mungu) hapo hakuna haki tena ya kumsikiza wala kumtii".[352]
Kukukubali ushauri na nasaha ni jambo muhimu sana katika nidhamu ya siasa katika Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mutkufu: "Na wale walio muitikia Mola wao (kwa kila amri zake) na wakasimamisha sala,na wanashauriana katika mambo yao,na wanatoa katika yale tuliyo waruzuku".[353] Na akasema pia Mwenyezi Mungu: "Basi kwa sababu ya rehma itokayo kwa Mwenyezi Mungu umekuwa lainikwao (Ewe Muhamad), na kama ungekuwa mkali na mweye moyo mgumu bila shaka wangelikukimbia, basi wasamehe wewe na uwaombee msamaha(kwa Mweneyzi Mungu) na ushauriane nao katika mambo".[354] Katika aya ya mwanzo MwenyeziMungu kataja jambo la kushauriana pamoja na swala ambayo ndiyo nguzo kubwa ya Uislamu ili kuonyesha utukufu na umuhimu wa jambo hilo,maana mambo yote yanayofungamana na maslahi ya umma ni lazima kutaka ushauri kwa watu wenye maarifa na hekima. Na mwisho wa aya Mwenyezi Mungu kawasifu waumini wote kwa kulifanya jambo la kushuriana baina yao katika mambo yao ni jambo la lazima. N akatika aya ya pili akamtaka Mtume wake ambaye ndiye kiongozi wa dola ya kiislamu atake ushauri katika mambo yanayo husu maslahi ya umma na ikawa haikuja hukumu ya Mwenyezi Mungu katika jambo hilo,ama katika mambo ambayo imekuja hukumu ya Mwenyezi Mungu hakuna nafasi ya ushauri wala mawazo ya mtu.Na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuwa akiwataka ushauri maswahaba wake,kama alivyo bainisha Abuhurayra- Mungu amuwie radhi-aliposema: Sikuwahi kuona mtu mwenye kutaka ushauri sana kwa wenzake kuliko Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ".[355] Na Uislamu umempa kila mtu haki ya kuelezea rai yake na kukosoa kwa njia sahihi zinazo kubalika ka kufuata muongozo wa Mwenyezi Mungu,bila kuanzisha wala kusababisha fitina. Hata khalifa wa kwanza wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake Abubakari –Mungu amuwie radhi- katika hotuba yake ya kwanza baada ya kutawalishwa kuwa kiongozi wa Waislamu pindi Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipo fariki,alisema : Enyi watu,mimi nimetawalishwa juu yenu,lakini mimi sio mbora zaidi yenu,endapo nitafuata haki basi nisaidieni katika haki,na kama mtaniona nimefuata batili basi niongozeni na mnielekeze,nitiini mda wakuwa mimi ninamtii Mwenyezi Mungu na endapo nitamuasi Mwenyezi Mungu basi hakuna haki ya kunitii. Pia Umar bin Alkhatwab,khalifa wa pili,siku moja alisimama juu ya mimbari akitoa khutuba akasema:Enyi watu,pindi mtakapo niona nimepinda basi ninyoosheni.Pale pale akasimama bedui mmoja akasema; Wallahi lau tukiona umepinda hata kidogo basi tutakunyoosha kwa upanga.Umar hakuonekana kukasirika wala kumchukulia hatua,bali alinyanyua mikono juu na akasema: Namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amejaalia katika utawala wangu watu ambao wako tayari kumnyoosha Umar anapo panda. Bali katika Uislamu kiongozi anahojiwa na kuulizwa.Mfano hai tunaupata pia kwa Umar-Mungu amuwie radhi- aliposimama siku moja akitoa khutuba hali yakuwa kavaa vipande viwili vya nguo,akasema: Enyi watu! Sikilizeni na mtii, pale pale akasimama mtu mmoja akasema : Hakuna kusikia wala kutii! Umar akamuuliza kulikoni? Akasema: Kwasababu wewe umevaa vipande viwili vya nguo na sisi tumevaa kipande kimoja kimoja.Na alikuwa kawagawia kila mtu nguo moja moja.Palepale Umar akapaza sauti yake akamuita mtoto wake Abdillahi,akasema waambie hii nguo ya pili nimeipata wapi? Akasema :Hii nguo ni ile ya kwangu nimempa mimi,ndipo yule mtu akasema: Sasa unaweza ukasema,tutasikia na kutii!
Mtazamo wa Uislamu kuhusu vita:
Na ndio inaitwa katika Uislamu (Jihadi),na jihadi kwa maana yake ya kiujumla ni kupambana na nafsi na kuilazimisha kuacha mambo ya haramu na makatazo yote na kutekeleza yaliyo ya wajibu kwa kadri ya uwezo ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu. Ama Jihadi kwa maana yake halisi: Ni kitendo cha kupigana vita ili kueneza Dini ya Mwenyezi Mungu na kuifikisha kwa watu wote. Na Jihadi kwa maana hii sio jambo jipya ambalo limeletwa na Uislamu,bali ilikuwepo hata katika sheria zilizo tangulia, katika Taurati katika agano la pili ambalo wanalimiliki mayahudi imekuja sheria ya kupigana vita tena kwa sura mbaya kabisa na maangamizi,inasema hivi: Utakapo ukaribia mji kwa ajili ya kuupiga vita,kwanza watake kufanya suluhu,kama watakubali na wakauruhusu kuingia katika mji wao,basi mji huo na watu wake wote watakuwa chini yako na wakutumikie,na kama hawakujisalimisha wakataka vita basi utauzingira mji huo,na kama Mola wako atakupa ushindi ukauteka mji huo baasi waue wanaume wote,ama wanawake na watoto na wanyama na kila kitu kilichopo katika mji huo vitakuwa ni ngawira zako ,utakula ngawira za maadui zako alizokupa Mola wako,hivi ndivyo utakavyo fanya kwa kila mji ulioko mbali na wewe sio kwa miji ya karibu na wewe.."
Pia katika Injili ya Mathayo kuanzia toleo la 24 nakuendelea yamekuja maneno haya:Msidhani kwamba mimi nimekuja kuleta amani ardhini,sikuja kuleta amani bali upanga,maana nimekuja kumfarikisha mtu na baba yake na binti na mama yake,na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani kwake,na atakaye mpenda baba yake au mama yake kuliko mimi basi huyo hanifai,na atakaye mpenda mtoto wake au binti yake zaidi yangu huyo hanifai,na asiye chukua msalaba wake na kunifuata huyo hanifai,na atakaye yapenda maisha yake basi atayakosa,na atakaye poteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.
Na Jihadi imegawanyika mafungu mawili:-
Jihadi ya kujihami: Nayo ni kupigana na watakao wafanyia uadui Waislamu (kwa kufanya uadui katika Dini,au kuwavunjia heshima waislamu,au mali zao au mji wao) na jihadi katika hali hii inakuwa ni wajibu kwa kila mwenye uwezo wa kubeba silaha na kupigana mpaka wazuie uadui huo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni,wala msipindukie mipaka (mkawapiga wasio kupigeni). Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi warukao mipaka".[356] Ikiwa wataweza kumzuia adui wao wenyewe basi inatosha,na endapo hawakuweza basi wakati huo inawalazimu waislamu walio miji ya jirani kuungana nao katika kupambana na adui mpaka aondoke,na hili ni jambo ambalo linajulikana na watu wote katika mila tofauti tofauti.
Jihadi ya kutafuta: Nayo ni vita inayo kuwa kwa ajili ya kuondoa utawala dhalimu ambao unakwa ni kizuizi kwa watu wanao taka kuwafikishia watu ujumbe wa Mwenyezi Mungu,au wakawa watawala hao wanawaadhibu watu wanao muamini Mwenyezi Mungu,au wanawazuia wanao taka kuingia katika Uislamu,maana Dini hii kama tulivyo eleza huko nyuma ni Dini ya ulimwengu mzima ,sio ya watu maalumu,hivyo ni lazima kila mtu afikishiwe ujumbe wa dini hii,na hii ndio sababu ya msingi inayo pelekea kupatikana jihadi. Hebu sikiliza maneno ya mmoja katika maswahaba wa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliyomwambia Rostom mfalme wa Roma alipo muuliza sababu ya kwenda kwao katika nchi yake,alisema : Tumekuja kuwakomboa watu kutoka katika utumwa wa kuwaabudu wanadamu wenzao na kuwaelekeza wamuabudu Mola aliye waumba wanadamu,na tumekuja kuwatoa katika dhiki ya dunia na kuwapeleka katika starehe ya akhera,na kuwatoa katika ujeuri wa dini zingine ili kuwatia katika uadilifu wa Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na piganeni nao mpaka yasiweko mateso (nyinyi kuteswa na wao kwa ajili ya Dini yenu kama wanavyo kuteseni hivi sasa)na Dini iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu".[357] Pia Jihadi inaruhusiwa katika hali ya kuondoa dhulma kwa watu ambao wanadhulumiwa ili kuwanusuru.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na mna nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na (katika kuwaokoa) wale walio dhaifu-katika wanaume na wanake na watoto –ambao husema: Molawetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhwalimu,na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako,na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako".[358] Lakini hatahivyo Uislamu umeweka utaratibu wa msaada huo isiwe ni katika kuvunja mikataba na makubaliano.Akasema Mwenyezi Mungu: "Na kama wakiomba msaada kwenu katika Dini,basi ni juu yenu kuwasaidia,ispokuwa juu ya watu ambao kuna mapatano baina yenu na wao(hapo msiwasaidie wao mkapigana na waitifaki wenu.Lakini jitahidini kupatanisha).[359]
Ama vita ambayo inakuwa ni kwa ajili ya kupanua mamlaka na utawala ambayo matokeo yake ni uharibifu na maangamizi Uislamu umekataza vita ya aina hii,maana vita katika uislamu kama tulivyo sema hapo mwanzo ni kwa ajili ya kuinua utajo wa Mwenyezi Mungu,na sio kwa matakwa binafsi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala msiwe kama wale walio toka katika majumba yao(miji yao) kwa fakhari na kujionyesha kwa watu ..".[360] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake wakati alipokuwa akimjibu mtu mmoja aliye muuliza kwa kkusema: Kati ya mtu anaye pigana kwa lengo la kupata ngawira na anaye pigana ili asifiwe kuwa ni mpiganaji hodari,kati yao nani anahesabika yuko katika njia sahihi ya Mwenyezi Mungu? Mtume akamjibu kwa kusema: "Mwenye kupigana kwa ajili ya kuinua utajo wa Mwenyezi Mungu huyo ndiye anaye pigania njia ya Mwenyezi Mungu".[361]
Na Jihadi katika uislamu ina kanuni na adabu maalumu;Hakuna ruhusa na kumuua mtu upande wamaadui ispokuwa yule tu anaye shiriki katika vita,ama wazee,na watoto na wanawake na wagonjwa,na wanao watibu wagonjwa,na watu walioko katika nyumba zao za ibada wakifanya ibada hawa hakuna ruhusa ya kuwaua.Pia hakuna ruhusa ya kuwakata kata viungo watu baada ya kuwaua(wale wanao pigana),na hakuna ruhusa ya kuuwa wanyama,wal kuvunja majumba,wala kuharibu visima vya maji,wala hakunaruhusa ya kumfukuza aliye kimbia vitani (kwa lengo la kuacha kupigana).Haya ndiyo yalikuwa maelekezo ya mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake pamoja na makhalifa wake baada yake pindi wanapo lituma jeshi kwa ajili ya kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Anasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Piganeni, kwa jina la Mwenyezi Mungu, katika njia ya Mwenyezi Mungu,(piganeni) na wale walio mkufuru Mwenyezi Mungu,piganeni wala msifanye uvamizi,wala msiwakate watu viungo baada ya kwisha kuwaua,wala msiue watoto..".[362] Na Abubakari –Mungu amuwie radhi -pindi alipolituma jeshi aliwausia makamanda wake akasema:Simameni niwausie mambo kumi muyahesabu;"Msifanye khiyana,wala msifiche ngawira,wala msiwavamie maadui zenu bila taarifa,wala msiwakate viungo watu baada ya kuwaua,wala msiue watoto wadogo,wala msiue wazee wala wanawake,wala msiue wanyama wala kuwachoma moto,wala msikate miti yenye matunda,wala msichinje ngamia wala ng`ombe au mbuzi ispokuwa kwa ajili ya chakula,na mtawakuta watu katika sehemu zao za ibada wakifanya ibada zao basi waacheni na ibada zao".[363]
Ama mateka wa kivita katika Uislamu wana haki zifuatazo: Hairuhusiwi kuwatesa au kuwadhalilisha au kuwakata viungo,au kuwanyima chakula na maji mpaka wakafa,bali inatakiwa kuwatendea wema. Amesema Mwenyezi Mungu: "Na huwalisha chakula masikini na mayatima na wafungwa na hali yakuwa wenyewe wankipenda(chakula hicho).(Husema wenyewe katika nyoyo zao wanapo wapa chakula hicho);Tunakulisheni kwa ajili ya kutak aradhi ya Mwenyezi Mungu(tu),hatutaki kwenu malipo wala shukurani".[364] Na katika mafundisho ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anasema: " Waacheni huru mateka na walisheni wenye njaa na watembeleeni wagonjwa".[365] Baada yapo dola ya Kiislamu inauhuru kuhusu uamuzigani iuchukue juu ya hawa mateka,ima kuwaacha huru bila fidia au kwa kutoa fidia ima ya mali au kubadilishana mateka,au wanauwawa ikiwa kiongozi wa waislamu ataona kufanya hivyo kuna maslani zaidi,maamuzi yote haya yako mikononi mwa mtawalawa kiislamu. Amesema Mwenyezi Mungu " Mpaka mkiwashinda sana hapo wafungeni) muwachukue kwenu,hali yakuwa ni mateka),tena wawacheni kwa ihsani (wende zao makwao) au kwa kujikomboa.(Kila vikitokea vita fanyeni hivyo)mpaka vita vitue mizigo yake(mpaka mambo ya vita yaondoke).[366] Ama kuhusu hali za raia na watu katika nchi ya walioshindwa katika vita,hakuna ruhusa ya kuwavunjia heshima,wala kupora mali zao,wal kuwadhalilisha,au kuharibu nyumba zao ,bali tumeamrishwa kuwatendea wema,na kuwaamrisha yaliyo mema na kuwakataza yaliyo mabaya, na kuwafanyia uadilifu.Na ushahidi wa wazi juu ya hili ni ile ahadi aliyowapa Umar bin Alkhatwab khalifa wa pili wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake watu wa Baytulmaqdis (palestina) wakati alipo ufungua mji huo, aliwaandikia mkataba ambao ulikuwa unasema hivi: (Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu,haya ndiyo aliyowapa Mja wa Mwenyezi Mungu Umar Kiongozi wa waislamu kuwapa watu wa baytul maqdis katika amani:Kawapa amani juu ya nafsi zao na mali zao na makanisa yao na masanamu yao…wala wasilazimishwe kuacha dini yao,wala asidhuriwe yeyote miongoni mwao..). Je historia imewahi kusajili uadilifu kama huu kwa jeshi ambalo limemshinda adui yake kisha likamfanyia uadilifu wa aina hii?! Japo kuwa alikuwa anauwezo wa kuwawekea masharti yoyote yale ayatakayo,lakini kwa sababu kalelewa katika mafundisho ya uadilifu,na lengo lake kubwa ni kueneza dini ya Mwenyezi Mungu,na kuwapendelea watu kheri. Na hii ni dalilitosha kabisa kwamba jihadi katika Uislamu haiwi kwa ajili ya tama za kidunia.
Na kabla ya kuingia vitani kwanza adui anakhiyarishwa kati ya mambo yafuatayo:Ima kuingia katika Uislamu, au vita, au kubaki katika Dini yao lakini watoe kodi. Na kodi yenyewe ni pesa kidogo sana ambayo inatolewa kwa dola ya Kiislamu. Nayo imegawanyika katika mafungu matatu:-
Iko inayo chukuliwa kwa matajiri
Iko inayo chukuliwa kwa watu wenye hali za kati nakati miongoni mwa wafanya biashara na wakulima.
Na iko inayo chukuliwa kwa wafanya kazi. Na mali hii inakuwa ni badala ya hifadhi wanayopewa juu ya mali zao na heshima na utu wao,na kuwa katika hali ya amani kama wanavyo ishi waislamu ambao wameufungua mji huo. Imepokewa kutoka kwa mmoja wa makomandoo wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwamba aliwaambia watu wa mji alio ufungua akasema: Hakika mimi nimewawekea mkataba kwamba mtatoa kodi na sisi tutawalinda..,na endapo tutakiuka basi hatutakuwa na haki ya kuchukua kodi kwenu.[367] Na kodi hii haichukuliwi kwa kila mtu bali maskini na watoto wadogo na wanawake na watumwa na vipofu na wasioeza kama vilema na kadhalika,wote hawa hawatozwi kodi,bali Uislamu umeiwajibisha dola kuwasaidia na kuwahudumia kutoka katika hazina ya mali za waislamu. Na hili limefanyika wakati wa utawala wa Umar- Mungu amuwie radhi- khalifa wa pili,wakati alipomuona mzee mmoja wa kiyahudi akipita kwa watu kuomba sadaka. Wakati alipo peleleza habari zake na akajua kuwa ni miongoni mwa watu walio wajibishiwa kutoa kodi alisema: kwa hakika tutakuwa hatukukufanyi auadilifu ikiwa tumechukua kodi kwako wakati bado una nguvu za kutafuta,halafu tukutelekeze baada ya kuzeeka,akamshika mkono na kwenda naye mpakanyumbani kwake,akampa chakula alicho kikuta pamoja na mavazi,kisha akatuma taarifa kwa msimamizi wa hazina ya mali za Waislamu akimwambia: Muangalie mzee huyu na wazee wengine mfano wake uwape mahitaji yatakayo watosha na familia zao kutoka katika hazina yetu,maana Mwenyezi Mungu anasema : "Hakika sadaka wapewe mafakiri na masikini.." Na mafakiri ni waislamu, ama maskini ni watu wa kitabu.[368]
Amesema Mtafiti mmoja wa Ujerumani(Lise Liktenstadter):Hakika hiyari waliyo pewa watu Fursi na Rom (Yaani waislamu walipo ifungua miji hii) haikuwa ima kuuawa au kuingia katika Uislamu,lakini walikhiyarishwa kati ya kuingia katika Uislamu au kubaki katika dini zao na kutoa kodi.Na hii ni hatua inayo sitahiki sifa kubwa kabisa maana ilifuatwa baadae Uingereza wakati wa utawala wa Malkia Elizabeth.[369]
Ama kuhusu wale wasio waislamu wanaoishi katika nchi ya kiislamu kwa makubaliano kati yao na kiongozi wa waislamu, hakuna ruhusa ya kuwadhulumu,wala kuwafanyia uadui au ubaya wowote. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu" Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia ihsani na uadilifu wale ambao hawakupigana na nyinyi kwa ajili ya dini, wala hawaku-kufukuzeni katika nchi zenu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao uadilifu".[370]
Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Tambueni! Yeyote atakaye mdhulumu mtu aliyechukua ahadi ya kuishi katika nchi ya kiislamu kwa amani,au akamdharau,au akamkalifisha kufanya jambo lililo nje ya uwezo wake,au akachukua kitu chake bila ya ridhaa yake, basi mimi nitahojiana naye mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya kiyama".[371]
Hizi ni baadhi ya dondoo kwa ufupi sana kuhusu jihadi katika Uislamu, mwenye kutaka maelezo zaidi basi arejee katika vitabu vilivyo andikwa maalumu kwa jambo hili tu.
Mtazamo wa Uislamu kuhusu uchumi:
Mali ndio uti wa mgongo wa maisha,na sheria ya Kiislamu kupitia mali inalenga kuandaa jamii iliyo na hali ya usawa na uadilifu,na maisha mazuri kwa watuwote.Mali ni kama alivyo ielezea mwenyezi Mungu mtukufu: "Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia".[372] Na kwakuwa mali katika mtazamo wa Uislamu ni miongoni mwa mahitaji ya msingi ambayo kila mmoja anayahitajia,ndio maana Uislamu ukaweka nidhamu maalumu katika njia za kuitafuta hiyo mali,pia nidhamu maalumu katika kuitumia,na ukaweka Uislamu pasenti maalumu katika mali inayo kadiriwa asilimia 2.5% inayoitwa zaka,ambayo huchukuliwa katika rasilimali ya matajiri baada ya kupitiwa na mwaka mzima,kisha inagawiwa kwa mafakiri kamatulivyo tangulia kueleza.Na hii ni haki miongoni mwa haki za mafakiri,hana haki ya kuizuia. Lakini hii haimaanishi kwamba Uislamu umeondoa haki ya mtu kumiliki mali yake wemyewe,na kufanya biahsara zake bila kuingiliwa,bali Uislamu unalikubali hilo na kuliheshimu,na zimekuja dalili nyingi mno katika kuharamisha kuingilia mali za watu,kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukfu: "Wala msiliane mali zenu kwa batili".[373] Uislamu ukaweka nidhamu ambayo itawezesha kufikia lengo, ambalo ni kupatikana maisha mazuri kwa kila mtu katika jamii ya Kiislamu, kupitia mambo yafuatayo:
1. Kuharamisha riba: Kwa sababu riba ni kuitumia nafasi yakuwa mwenzio ana matatizo,ukapora malizake bila ya haki yoyote.Na kuenea kwa riba ni sababu ya kupotea tabia ya kutendeana wema katika jamii,pia ni sababu inayofanya mali zimilikiwe na kundi fulani tu katika jamii.Amesema Mwenyezi Mungu " Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na acheni yaliyo bakia katika riba, ikiwa mmeamini. Na kama hamtafanya (hivyo), basi fahamuni mtakuwa na vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mkiwa mmetubu basi mtapata rasilimali zenu, msidhulumu wala msidhulumiwe".[374]
2. Uislamu umehimiza kukopeshana ikiwa ni njia ya kupiga vita riba.Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Atakaye mkopesha Muislamu mwenzie dirhamu mara mbili huandikiwa malipo ya mwenye kutoa sadaka".[375] Na amesema pia Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwenye kumuondolea ndugu yake Muislamu tatizo mongoni mwa matatizo,basi Mwenyezi Mugu atamuondoshea tatizo miongoni mwa matatizo ya siku ya kiyama".[376]
- Na Uislamu umeamrisha kumpa muda mwenye kudaiwa kama atakuwa bado ana matatizo hajaweza kulipa deni lake,na kuto kumghasi na kumsumbua,lakini amri hii sio ya lazima ,pia ruhusa hii anaipata mtu anaye julikana kuwa ni mlipaji na hana nia ya kudhulumu,ama mwenye kuchelewesha haki za watu makusudi huyo hapewi fursa hii.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kama (mkopaji ) ana dhiki, basi (mdai)angoje mpaka afarijike".[377] Na akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Atakaye mpa muda mdeni wake ambaye ana matatizo basi huandikiwa kila siku inayo pita malipo ya swadaka,na mwenye kumuongezea muda baada ya kufika muda walio kubaliana pia huandikiwa kila siku malipo ya swadaka".[378]
- Pia sheria imehimiza kuwasamehe wadaiwa pindi wanaposhindwa kulipa,lakini jambo hili sio lazima ,bali kubainishwa ujira na malipo makubwa anayo yapata mtu mwenye kusamehe. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kama nyinyi (mnao dai mkisamehe madeni yenu) mkazifanya kuwa ni sadaka,basi ni bora kwenu".[379] Na akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwenye kutaka Mweyezi Mungu amsalimishe na kumnusuru na matatizo ya siku ya kiyama, basi na ampe muda mdeni wake au amsamehe".[380]
3. Na Uislamu ukaharamisha kuweka (kuzuia ) chakula kwa lengo la kungoja kupanda kwa bei wakati watu wana haja,kwa sababu kufanya hivi ni kuidhuru jamii. Akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Atakaye zui chakula wakati watu wanahaja nacho basi anapata madhambi"[381] Na mtawala anayo haki ya kumlazimisha mtu aliye zuia chakula wakati wa matatizo kukiuza kwa bei amabyo atapata faida ya kawaida bila kuwadhuru watu wala yeye kupata hasara,na endapo atakataa kukiuza kwa nguvu.
4. Uislamu umeharamisha kurundika mali bila ya kuzitolea zaka na haki za Mwenyezi Mungu zilizomo katika mali hizo,kwa sababu lengo kusudiwa la mali ni kwamba izunguke kwa watu ili jamii iweze kunufaika na uchumi uchangamke. Amesema Mwenyezi Mungu: "Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya mwenyezi Mungu,wape habari za adhabu iumizayo (inayo wangoja) ".[382] Pamoja na Uislamu kuheshimu haki miliki ya mtu lakini umeweka katika mali yake haki maalumu anazo paswa kuzitekeleza; miongoni mwa haki hizo ziko ambazo ni wajibu juu ya nafsi yake,kama vile kuitumia mali yake kwa kunufaika nayo vizuri yeye mwenyewe na kkuwahudumia vizuri wanao mtegemea,na kuna haki zingine ambazo ni za baadhi ya watu katika jamii anayoishi nayo,kama vile Zaka,na sadaka na kutoa misaada,na kuna haki zingine pia ambazo ni za kijamii kama vile kusaidia katika mambo ya kijamii kama kujenga mashule,mahospitali,vituo vya kulea mayatima,kujenga misikiti na mengineyo amabayo ni katika mahitaji ya kijamii.
5. Pia uislamu ukaharamisha kupunja na kupunguza vipimo,kwa sababu hiyo ni moja katika njia za wizi na hiyana na udanganyifu.Amesema Mwenyezi MunguMtukufu:"Maangamizo yatawathibitikia wapunjaowenzao. Ambao wanapo jipimia kwa watu hupokea (vipimo)kamili. Lakini wanapo wapimia kwa (kipimo cha) vibaba au mizani (au vinginevyo), wao hupunguza".[383]
6. Pia ukaharamisha kuhodhi vitu ambavyo maslahi yake ni ya watu wote,kama vile maji,malisho na kuwazuia watu wasinufaike nayo. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Watu wa aina tatu Mwenyezi Mungu hatawasemeza siku ya kiyama wala hatawatazama kwa jicho la rehma:Mtu anaye apa wakati wa kuuza bidhaa zake kwamba kanunua kwa bei kubwa zaidi kuliko aliyouzia na hali ni muongo,na mtu aliye apa kiapo cha uongo ili kudhulumu mali ya ndugu yake Muislamu,na mtu aliye wazuilia watu maji hali yakuwa hana haja nayo.Atawaambia Mwenyezi Mungu siku hiyo:Siku ya leo nitakuzuilieni fadhila zangu kama mlivyo wazuilia watu vitu ambavyo hamkuviumba nyinyi".[384] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Vitu vitatu hivi watu hushirikiana katika matumizi yake :Majani (malisho),na maji na moto".[385]
7. Ukaweka nidhamu ya mirathi amabyo imegawa urithi kulingana na ukaribu na umbali wa mtu kwa marehemu,pia kulingana na manufaa yake.Na hakuna yeyote mwenye haki ya kugawa mirathi kwa kufuata matakwa yake,na katika uzuri wa nidhamu hii ni kwamba inaisambaza mali katika miliki ndogondogo nahivyo swala lakurundikana mali kwa kundi fulani tu linakuwa halipo tena.Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Hakika Mwenyezi Mungu alikwisha mpa kila mwenye haki haki yake,kwahiyo hakuna ruhusa ya kuusia mali kwa mtu anaye sitahiki kurithi".[386]
8. Nidhamu ya kuweka waqfu.Uislamu umehimiza sana juu ya jambo hili, na waqfu uko namna mbili:-
- Waqfu ambao ni maalumu kwa watu wake na kizazi chake (yaani huyo aliye toa waqfu) kwa lengo la kuwaepusha na umasikini na hali ya kuomba kwa baadae. Na katika masharti ya kukubalika waqfu wa namna hii nikwamba pindi kizazi cha huyo aliyeweka waqfukikimalizika basi manufaa ya waqfu huo yanatakiwa yatumiwe katika kazi mbali mbali za kheri.
- Waqfu unatolewa kwa ajili ya mambo mbali mbali yakheri,kama kujenga misikiti,mahospitali,mashule,barabara na mambo mengineyo ya kheri kwa ajili ya jamii. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Pindi mwanadamu anapo kufa,amali zake zote hukatika,ispokuwa mambo matatu(malipo yake huendelea):Sadaka yenye kuendelea,au elimu yenye manufaa,au aliacha mtoto mwema amabye anamuombea dua".[387]
9. Nidhamu ya wasia. Uislamu umemhimiza Mwislamu kuusia sehemu ya mali yake baada ya kufa kwake ili itumike katika njia za kheri,lakini ukamuwekea kiwango maalumu,kuwa wasia huu usivuke theluthi ya mali yake,ili warithi wasidhurike. Imepokewa kutoka kwa Aamir bin Saad- Mungu amuwie radhi- amesema:Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuwa akija kunitembelea nikiwa mgonjwa nilipo kuwa Mkka,siku moja nikamuuliza nikasema: Hakika mimi ni mtu mwenye mali nyingi,waonaje kama nitausia mali yangu yote?akasema: "Hapana"nikasema basi nusu yake,akasema "Hapana",nikasema basi theluthi yake,akasema: " Theluthi sawa, lakini hata theluthi ni nyingi,kwa sababu ukiwaacha warithi wako wakiwa katika hali nzuri ni bora zaidi kuliko kuwaacha ni masikini omba omba,na chochote ukitoacho jua kuwa unaandikiwa ujira wa sadaka,hata tonge ulitialo katika kinywa cha mkeo,na huenda Mwenyezi Mungu akakuchukua halafu baadhi ya watu wakabaki wananufaika kwa sababu yako, na wengine wakabaki wanadhurika kwa sababu yako".[388]
10. Uislamu umeharamisha kila jambo linalo zingatiwa kuwa ni miongoni mwa kula mali za watu bila ya haki. Amesema Mwenyezi Mungu "Enyi mlio amini msiliane mali zenu kwa batili..".[389]
Kama vile uporaji,maana ni miongoni mwa njia za kuleta uharibifu katika jamii. AmesemaMtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Yeyote atakaye jihalalishia haki ya ndugu yake Muislamu kwa kutumia kiapo,basi Mwnyezi Mungu amemuwajibishia Moto,na amemuharamishia Pepo" ,mtu mmoja akauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! hata kama kitu chenyewe ni kidogo tu? Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamjibu akasema : "Hata kama ni tawi la mti".[390]
Au kwa njia ya wizi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Hafanyi uzinifu mwenye kuzini hali ya kuwa ni muumini,wala haibi mwenye kuiba hali yakuwa ni muumini,wala hanywi pombe mnywaji hali yakuwa ni muumini,lakini mlango wa kutubia iko wazi".[391]
Au kufanya udanganyifu. Amesema MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Yeyote atakaye tubebea silaha huyo si miongoni mwetu,na mwenye kufanya udanganyifu huyo si miongoni mwetu".[392]
Au kwa njia ya kupokea rushwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala msiliane mali zenu kwa batili na kuzipeleka kwa mahakimu ilimpate kula sehemu ya mali ya watu dhambi na hali mnajua".[393] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Mwenyezi Mungu amemlaani mtoa rushwa na mpokeaji rushwa katika hukumu".[394] Amelaaniwa mtoaji kwakuwa yeye ni sababu ya kuenea tabia hii chafu yenye madhara kwa jamii,na kalaaniwa mpokeaji kwa sababu kamdhuru mtoaji kwa kumlia mali yake bila ya haki yoyote,na amefanya hiyana katika amana kwa kuchukua malipo katika kufanya jambo ambalo ni wajibu kwake kulifanya hata bila malipo,pia kasababisha madhara kwa mtu ambaye pengine wanashitakiana na mtoa rushwa.
Uislamu pia ukaharamisha kitendo cha mtu kuuza katika biashara ya mwenzie (yaani kamkuta mwenzie anapatana na mteja halafu akaingilia kati ili kuharibu mapatano yao ili amuuzie yeye).Maana jambo hili ni chanzo cha kuwekeana uadui na chuki.amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Asiuze mmoja wenu juu ya biashara ya mwenzie,wala asipose mmoja wenu juu ya posa ya mwenzie,ispokuwa akipewa idhini".[395]
Mtazamo wa Uislamu kuhusu hali ya kijamii:
Uislamu umekuja na nidhamu za kijamii zenye kubainisha haki na majukumu ya kila mmoja katika jamii ili mambo yaweze kukaa shwari,miongoni mwa haki hizo ziko ambazo ni makhsusi na ziko ambazo ni za kiujumla. Miongoni mwa haki na mambo ambayo wajibu maalumu aliyo yawajibisha Mwenyezi Mungu ni:
Haki za mtawala (kiongozi) juu ya raia.
- Kumsikiliza na kumtii,maana kufanya hivyo ni katika kumtii Mwenyezi Mungu,na kumuas ni sawa na kumuasi Mwenyezi Mungu,ispokuwa katika maasi hapo hakuna ruhusa ya kumtii .Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu".[396]
- Kumpa nasaha kwa upole na adabu,kwa kumuongoza katika mambo yenye manufaa kwake na kwa raia,na kumkumbusha haki na matatizo ya raia. Tunaona Mwenyezi Mungu anamwambia NabiiMusa na ndugu yake Haruni wakati alipo watuma wende kwa Firauni kumlingania, akawambia: "Kamwambieni maneno laini huenda atashika mauidha au ataogopa ".[397] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Dini ni kupeana nasaha ", tukamuuliza kwa ajili ya nani ? akaema: "Kupeana nasaha kwa ajili ya MwenyeziMungu ,na kwa ajili ya kufuata kitabu chake na kumtii Mtume wake,na kuwatii viongozi wa waislamu".[398]
- Kusimama nao bega kwa bega wakati wa matatizo na shida,na kutokuwatangazia uasi na kuacha kuwanusuru. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Atakapo kujieni mtu yeyote anataka kukuvurugeni na kusambaratisha umoja wenu hali yakuwa mmekubaliana juu ya mtu mmoja (kuwa ndio kiongozi wenu) basi muueni mtu huyo".[399]
Haki za raia juu ya mtawala (kiongozi).
Miongoni mwa haki za raia zinazo mpasa mtawala kuzitekeleza ni :-
1. Kuwa muadlifu kwao kwa kumpa kila mmoja haki yake ,na kuwa muadilifu pia katika kugawa majukumu,na uadilifu katika hukumu,watu wote mbele yake wanatakiwa kuwa sawa,asitofautishe kundi moja juu ya lingine. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hakika katika watu wanao pendwa sana na Mwenyezi Mungu, na watakao kuwa karibu nami siku ya kiyama ni kiongozi muadilifu,na katika watu wanao chukiwa sana na Mwenyezi Mungu na watakao kuwa na adhabu kali sana ni kiongozi mwenye jeuri na dhulma" .[400]
2. Kuto kuwadhulumu na kuwafanyia udanganyifu raia wake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Mtu yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atambebesha majukumu juu ya raia wake kisha akafa hali yakuwa kafanya udanganyifu, Mwenyezi Mungu kaiharamisha Pepo kwa mtu huyo". [401]
3. Kuchukua ushauri wao katika mambo yao yanayo husiana na siasa,au ya kijamii na kiuchumi-lakini ushauri unakuwa katika mambo ambayo haikuja dalili yoyote juu ya jambo hilo-na kuwapa uhuru wa kutoa mawazo yao na mitazamo yao na kuzikubali rai zao zikionekana zina maslahi. Maana hata Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katika vita vya Badri alipofikia pahala Fulani na akalitaka jeshi likae hapo na mbele yao kukawa ndio kuna visima vya maji,mmoja wa maswahaba akamuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake 0 akasema : Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu! Je kufikia kwetu hapa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu?(Yaani umepewa wahyi kwamba tufikie hapa)au ni katika mbinu tu za kivita? Akasema: Bali ni katika mbinu za kivita,basi yule swahaba akamshauri Mtume kwamba kambi yao iwe mbeli ya visima vya maji ili maadui zao wasipate maji,Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakeakaifanyia kazi rai yake.
4. Hukumu zake anazo zitoa kwa raia ziwe zinatokana na sheria za Mwenyezi Mungu na sio kwa kufuata matamanio yake. Mfano hai tunaupata kwa khalifa w pili wa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake Umar bin Alkhatwab,baada yakuwa ni kiongozi wa waislamu alimwambia bwana mmoja aitwaye Abu maryamu as-saluuli ambaye alimuua ndugu yake Zidu bin Alkhatwab, akamwambia:Wallahi hakika mimi sikupendi,na nitakuchukia mpaka siku ardhi ikipenda damu.Yule bwana akamuuliza Umar:je hilo litanifanya nizikose haki zangu kwako? Umar akasema: Hapana. Yule bwana akasema :Basi kama sitakosa haki zangu kunichukia kwako hakutanidhuru chochote.
5. Asiwe ni mwenye kujificha kwa raia wake,na kujifungia ili raia wake wasikutane naye,na akawa ni mwenye kiburi,na kuweka vizingiti baina yake na raia ,kwa kuweka watu ambao wanamruhusu wamtakaye na kumzuia kumuona wamtakaye. Maana Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amesema:" Yeyote atakaye tawalia mambo ya waislamu kisha akajificha na kuzuia wenye shida na masikini wasimuone,basi Mwenyezi Mungu atazipuuza shida zake siku ya kiyama".[402]
6. Awe ni mwenye huruma kwa raia na asiwakalifishe mambo wasiyo yaweza,na asiwabane na kuwadhiki kimaisha. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Ewe Mola wangu! yeyote katika umati wangu atakaye beba jukumu lolote katika majukumu ya watu kisha akawafanyia uzito,basi mfanyie uzito nayeye,na atakaye wafanyia upole na wepesi basi mfanyie wepesi katika mambo yake".[403] Kiongozi wa kiislamu anatakiwa awe kama alivyo kuwa Umar bin Alkhatwab katika kuogopa amana aliyo bebeshwa,miongoni mwa maneno yaliyo nukuliwa kutoka kwake ni kauli yake : Wallahi laiti kama nyumbu aliyeko Iraki atajikwaa akaumia,nachelea kwamba Mwenyezi Mungu ataniuliza siku ya kiyama kwanini siku tengeneza njia.Aliyasema maneno haya yuko madina lakinianajua kwa kuwa yeye ndiye mtawala basi hata usalama wa mbali anawajibika kuhakikisha unapatikana. Pia mtawala anatakiwa kuwa awe kama alivyo msifu Alhasan Albaswari –Mungu amrehemu- katika barua yake aliyoituma kwa Umar bin Abdul-aziz akasema katika barua hiyo: (Tambua ewe kiongozi wa waislamu kwamba hakika mwenyezi Mungu kamjaalia kiongozi muadilifu kuwa ni mwenye kumnyoosha kila aliye pinda,na kumrekebisha kila aliye potoka,na mwenye kumtia nguvu kila aliye dhaifu,na ni mwenye kumnusuru kila aliye dhulumiwa na nikimbilio la kila mwenye matatizo.Na kiongozi muadilifu ni kama mchungaji mwenye huruma na wanyama wake ambaye huwatafutia malisho yaliyo mazuri,na anawaepusha na sehemu mbaya za hatari,na kuwachunga kutokana na adha ya joto na mvua. Kiongozi muadilifu ni sawa na baba mwenye huruma kwa wanae,anawajali wakiwa wadogo na kuwaelimisha wanapo kua,na anachuma mali kwa ajili yao katika uhai wake,na kuwawekea akiba itakayo wafaa baada ya kufa kwake. Kiongozi muadilifu ni sawa na mama mwenye huruma na mapenzi kwa mtoto wake,ambaye kabeba mimba yake kwa tabu na kumzaa kwa tabu,na akamlea akiwa mdogo,akikesha usiku kwa sababuyake,mara kamnyonyesha ,mara kambeba,mara hivi, anapokuwa na afya njema ndio furaha yake, na anapo umwa basi hana raha. Kiongozi muadilifu ni sawa na mtu aliye achiwa mayatima,na ni sawa na mtu mwenye kuweka hazina ya masikini,anawachunga na kuwalea wadogo na kuwahudumia wazee wasio jiweza. Kiongozi muadilifu ni sawa na thamani ya moyo kwa mwanadamu,ukitengenea basi naye anakuwa safi na unapo haribika nayeye huharibika.Kiongozi muadilifu ni kiunganishi muhimu baina ya Mwenyezi Mungu na waja wake, yeye anasikia maneno ya Mwenyezi Mungu kisha anawafikishia,na anamnyenyekea Mwenyezi Mungu kisha anawaelekeza waja wake katika unyenyekevu,basi usiwe ewe kiongozi wa waislamu katika vile alivyo kumilikisha Mwenyezi Mungu mfano wa mtumwa ambaye kapewa amana na bwana wake na akamuachia mali zake na familia yake ili aichunge lakini badala yake akaiteketeza mali na kuisambaratisha familia na kuwatia katika ufakiri. Na utambue ewe kiongozi wa waislamu kwamba Mwenyezi Mungu kateremsha adhabu ili watu waweze kuonyeka na kuacha maovu na machafu,lakini vipi ikiwa maovu yanatendwa na kiongozi!!,Mwenyezi Mungu kajaalia kisasi ili iwe ni sababu ya kupatikana uhai wa nafsi za watu,lakini vipi ikiwa msimamizi wa kisasi ndiye muuaji! .Na uyakumbuke mauti ewe kiongozi wa waislamu,na ukumbuke hali utakayo kuwanayo baada ya kufa kwako na kwamba hutakuwa na msaidizi yeyote mbele za Mungu,na ujiandae kwa ajili ya siku hiyo ya mfazaiko mkubwa.Na utambue kuwa una mafikio ambayo ni tofauti kabisa na mafikio yako ya sasa ambapo utakaa sana hapo,ukiwa umetenganishwa na marafiki zako,bali wao ndio watakutupa humo wakuache ukiwa mpweke,hivyo jiandae kwa kufanya matendo ambayo ndiyo yatakuwa mliwazaji wako katika sehemu hiyo. Na ikumbuke siku watakapo fufuliwa waliomo makaburini,na zikawekwa wazi siri za watu,na daftari zilizo sajiliwa matendo ya watu zikawekwa wazi.Itumie vizuri fursa hii kabla ya kukufika ajali. Usiwahukumu waja wa Mwenyezi Mungu kwa hukumu za kijahili, wala usiwatendee matendo ya kidhwalimu,wala usiwasalitishe wajeuri juu ya wanyonge,usije ukabeba mizigo yako pamoja na yao (madhambi yao na yako pia),wala wasije wakakuhadaa wale wanao neemeka kupitia kwako hali wanakuangamiza,na wanaponda raha kwa kukuzuilia raha zako za akhera,usiangalie uwezo wako ulio nao leo lakini angalia uwezo utakao kuwa nao kesho,wakati utakapokuwa umefungwa kamba za mauti,na umesimamishwa mbele ya Mola wako,katika kundi la Malaika na Manabii na Mitume,hali nyuso za watu zimesawijika mbele ya Mwenyezi Mungu Mwenye uhai wa milele. Ewe kiongozi wa waislamu! japokuwa mawaidha yangu haya hayalingani na mawaidha ya wema walio tangulia kabla yangu,lakini sitoacha kukuonea huruma na kukunasihi. Tafadhali jaalia barua yangu hii ni kama vile daktari anaye mtibu rafiki yake kipenzi, anamnywesha dawa chungu lakini anatarajia kuwa zitamsaidia na kuirejesha afya yake. Ewe kiongozi wa waislamu! amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako pamoja na baraka zake)
Haki za wazazi wawili.
Nazo ni kuwatii na kutokuwaasi -muda wa kuwa hawajaamrisha maasi-na kuwatendea wema,kwa kila hali kama vile kuwatimizia mahitaji yao ya lazima kama chakula mavazi, mahala pa kuishi ,na kuwanyenyekea,na kutonyanyua sauti yako juu ya sauti yao,na kuwa na subira katika kuwahudumia,na kuzijali hisia zao,kiasi kwamba usizungumze mazungumzo yanayo wakera,na usifanye jambo litakalo waudhi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtuktufu: "Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yeyote ila yeye tu. na (Ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee. (naye yuko) pamoja nawe,au wote wawili,basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa heshima.Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa (njia ya kuwaonea) huruma.Na useme:Mola wangu !warehemu (wazee wangu ) kama walivyo nillea nikiwa mtoto".[404]
Na Uislamu umelizingatia swala la kuwatelekeza na kutowajali ni katika madhambi makubwa. Imepokewa kutoka kwa Abdalla bin Amru –Mungu awawie radhi- amesema: Alikuja bedui mmoja kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakeakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niyapi madhambi makubwa? Mtume akamjibu akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu".akauliza tena kisha lipi? Mtume akasema: "Kuwatesa na kutowajali wazazi wawili". akauliza tena kisha lipi? Mtume akasema:"Kuapa kiapo cha uongo".Nikauliza ni kipi kiapo cha uongo? Akasema: Ni kile ambacho mtu anajihalalishia kwacho mali ya ndugu yake muislamu hali anajua kuwa anasema uongo".[405]
Na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katika kubainisha nafasi na daraja waliyo nayo wazazi wawili akasema: " Radhi za Mwenyezi Mungu zinapatikana katika kuwaridhisha wazazi wawili,na ghadhabu za Mwenyezi Mungu zinapatikana katika kuwaudhi wazazi wawili".[406]
Na haki hizi kwa wazazi ni za lazima hata kama mtakuwa mnatofautiana katika dini. Maana imepokewa toka kwa Asmaa binti Abibakar –Mungu awawie radhi- kwamba amesema:Siku moja alinitembele mama yangu Madina hali yakuwa ni mshirikina (sio Muislamu), nikamuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake nikasema: Mama yangu kanitembelea,je nimkirimu na kumtendea wema? Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: "Ndio mfanyie wema mama yako".[407]
Na katika kuwatendea wema mama anapewa kipaumbele zaidi kabla ya baba,kutokana na hadithi aliyoipokea Abu hurayra –Mungu amuwie radhi- kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!Nani katika watu mwenye haki zaidi kufanyiwa wema? Mtume akamjibu kwa kusema :"Mama yako,kisha mama yako, kisha mama yako,kisha baba yako ,kisha jamaa zako wengine kulingana na ukaribu wao kwako".[408] Mama akapewa daraja tatu na baba daraja moja,nahii ni kwa sababu mama anavumilia shida nyingi sana juu ya mtoto tofauti na baba ,kama alivyo muelezea Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na tumemuusia mwanadamu afanye wema kwa wazazi wake,mama yake amechukua mimba yake kwa tabu na akamzaa kwa taabu..".[409] Mama anapata tabu ya kumbeba angali bado ni mamba tumboni,chakula chake ndio lishe yake,kisha anapata tabu wakati wa kumzaa,halafu anapata taabu wakati wa kumnyonyesha na kukosa usingizi kwa ajili yake…
Haki za mume anazo takiwa kuzipata kwa mkewe.
- Usimamizi : Miongoni mwa haki zake,anatakiwa awe ndie msimamizi mkuu wa nyumba na kufanya kila jambo analoona lina maslahi kifamilia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wanaume (wawe) ni walinzi wa wanawake;kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine,na kwa sababu ya mali zao wanazo zitoa".[410] Na kwa sababu mara nyingi wanaume wanauwezo wa kuyakabili mambo kwa busara zaidi kuliko wanawake,maana mara nyingi wanawake hutanguliza zaidi hisia zao kuliko kila kitu,lakini haimaanishi kwamba mwanaume asitake ushauri kwa mkewe na kuchukua rai yake katika mambo yanayo husu maisha yao ya ndoa.
- Amtii na kutekeleza amri zake,maadamu hajamuamrisha jambo ambalo ni madhambi. Imepokewa Kutoka kwa Bibi Aisha mke wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwamba amesema: Nilimuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake nikasema:Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu,ni mtu gani mwenye haki zaidi kwa mwanamke?akasema:"Mume wake".nikamuuliza tena:Je nimtu gani mwenye haki zaidi kwa mwanaume? akasema: "Mama yake".[411]
- Asimnyime unyumba pindi atakapo muhitajia. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Pindi mume atakapo muita mkewe kitandani mke akakataa,na mumue akalala hali yakuwa amekasirika,basi mwanamke huyo hulaaniwa na Malaika mpaka asubuhi".[412]
- Asimkalifishe mume mambo asiyo yaweza,na ajitahidi kumridhisha kwa kila hali.Amesema Mtume Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Laiti ningepewa idhini ya kumuamrisha kiumbe amsujudie kiumbe mwenzie, basi ningelimuamrisha mwanamke amsujudie mumewe".[413]
- Ahifadhi na kulinda mali ya mume wake ,na watoto wake,na aichunge heshima yake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwanamke bora ni yule ambaye ukimtazama anakufurahisha, na ukimuamrisha anakutii,na ukisafiri analinda heshima yako na mali yako"kasha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akaisoma Aya hii: "Wanaume (wawe)ni walinzi wa wanawake….".[414]
- Asitoke nyumbani kwake bila ridhaa wala idhini ya mume wake,wala asimruhusu kuingia nyumbani kwake mtu yeyote ambaye mume wake hapendi aingie. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hakika nyinyi mnazo haki kwa wake zenu,na wake zenu wanazo haki juu yenu,ama haki zenu juu ya wake zenu,ni kwamba wasimuingize yeyote mnae mchukia katika majumba yenu,na hakiza zao juu yenu ni kuwatendea wema katika kuwalisha na kuwavisha".[415] Na waislamu wa mwanzo walikuwa wakitekeleza wasia huu wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake.Mfano hai tunaupata kwa mama mmoja Aufu binti Mahlam Ash-shaybany katika wasia wake akimuusia binti yake wakati alipoolewa, akamwambia: Ewe binti yangu!hakika leo unaondoka katika nyumba uliyo lelewa unakwenda kwa mwanaume ambaye humjui,mwenza ambaye hukumzoea, hivyo basi kuwa kwake kama mja kazi naye atakuwa kwako kama mtumwa,na yachunge kwako mambo kumi yatakuwa ni kama akiba yako:
Ama jambo la kwanza na la pili: Kuwa mnyenyekevu kwake,na uwe ni mwenye kumsikiliza na kumtii.
Na jambo la tatu na la nne: Yachunge sana macho ake na pua yake,jicho lake lisitazame kitu kibaya kutoka kwako,na asinuse kwako ispokuwa harufu nzuri.
Ama jambo la tano na la sita: Chung asana muda wake wa kula na muda wa kulala,maana njaa hulipua mambo mengi,na kumchelewesha kulala kutamtia hasira.
Ama jambo lasaba na la nane: Ni kuchunga mali zake na kulinda heshima ya familia yake.
Ama jambo la tisa na laa kumi:Usije ukaasi amri yake wal kutoa siri zake,endapo utaasi amri yake,baasi utamtia chuki ,na endapo utatoa siri zake basi hutasalimika na vitimbi vyake. Kisha tahadhari sana na kuonyesha furaha mbele yake anapo kuwa kakasirika,pia tahadhari na kukasirika na kuonyesha unyonge mbele yake anapokuwa ni mwenye furaha na bashasha.
Haki za mke juu ya mume.
- Kumpa mahari yake. Na hii ni haki ya msingi anayo sitahiki mwanamke kutoka kwa mumewe,haipatikani ndoa pasina haki hii,na haina msamaha hata kama mke ataridhia,ispokuwa kama atasamehe baada ya kufunga ndoa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na wapeni wanawake mahari yao hali yakuwa ni hadiya(aliyo wapa Mungu),(Lakini hao wake zenu)wakikupeni kwa ridhaa ya nafsi zao kitu katika hiyo mahari basi kuleni kwa furaha na kunufaika".[416]
- Kufanya uadilifu na usawa kwa mwenye wake zaidi ya mmoja,anawajibikiwa kufanya usawa kati yao katika chakula,mavazi,makaazi na zamu za kulala.Kwa mujibu wa kauli ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Yeyote mwenye kuwa na wake wawili kisha akamili upande mmoja,basi atafufuliwa siku ya kiyama hali yakuwa ubavu wake umepinda".[417]
- Kumpa matumizi yeye na wanawe. Mwanume anawajibika kuandaa makaazi mazuri kulingana na uwezo wake,na kutimiza mahitaji ya lazima katika maisha,na kumpa mkewe mahitaji yake anayo yataka kulingana na uwezo wake. Kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu : "Mwenye wasaa atoe matumizi kwa kadiri ya wasaa wake,na yule ambaye amepungukiwa riziki yake,atoe katika kile alichopewa na Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yeyote ila kwa kadiri ya alicho mpa".[418] Na uislamu katika kulihiza na kulihamasisha jambo hili umejaalia matumizi anayo yatoa mtu kwa familia yake ni moja katika sadaka ambazo anaandikiwa malipo yake. Alisema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kumwambia Saad bin Abii waqas:" Hakika chochote ukitoacho katika matumizi basi unaandikiwa malipo ya sadaka,hata tonge ulitialo katika kinywa cha mkeo..".[419] Na mwanamke ana haki ya kuchukua katika mali ya mume wake hata bila taarifa endapo ataacha kutekeleza wajibu wake wa kuwapa matumizi. Ushahidi wa hilo ni hadithi ya Hindu bint Utbah alipo mshitakia Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika mume wangu Abu sufyani ni mtu bakhili mno,hanipi matumizi ya kutosha mimi na wanangu,ispokuwa ninacho chukua bila yeye kujua.Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia: "Chukua kiasi kitakacho kutosha wewe na wanao kwa wema".[420]
- Kulala naye sehemu moja na kumpa haki ya unyumba. Na hii nikatika haki muhimu sana ambazo sheria imemtaka mume kuzitekeleza na kuzichunga,maana mwanamke kama mwanmke anahitaji kuwa na mume mwenye huruma na mapenzi,atakaye mliwaza na kumkidhia haja zake za kimaumbile,ili mke aweze kubakia katika sitara na asije akafikia katika hatua ya kufanya mambo ambayo sio mazuri. Kwa ushahidi wa maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipo muuliza Jaabir –Mungu amuwie radhi- akasema: "Umeoa ewe Jaabir"? akasema : Ndio nimeoa.Akamuuliza tena : "Umeoa bikira au thayib"? (yaani mwanamke ambaye kaisha wahi kuolewa) Jaabir akasema :Nimeoa thayib. Mtume akamwambia: "Kwanini hukuoa ambye ni mdogo,mtakaye weza kucheza naye na kufurahishana"!. Maneno haya yanamaanisha kuwa binti ambaye hajaolea sio sawa kimapenzi na mwanamke ambaye kaisha olewa.
- Kuhifadhi siri zake,na kutokutoa aibu zake,na kuhifadhi mambo yao ya ndani.Kutokana na kauli ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliposema: " Hakika miongoni mwa watu watakao kuwa na mafikio mabaya mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya kiyama ni mwanaume ambaye anakaa faragha na mkewe (wanafanya tendo la ndoa) kisha akatoa siri zake".[421]
- Kumtendea yaliyo mazuri na kuishi naye kwa wema,na kumshauri katika mambo yanayo husu maisha yao,asiwe ni mwenye kuchukua maamuzi yake peke yake nakupuuza ushauri wa mkewe,na amuonyeshe mapenzi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Muumini mwenye imani kamili ni yule mwenye tabia njema,na mbora wenu ni yule anaye ishi vizuri na wake zake ".[422]
- Awe ni mwenye kuvumilia maudhi yake na kumvumilia kwa yale mapungufu aliyo nayo. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Haiwezekani mumue akachukia kwa mkewe kila kitu,endapo itamchukiza kwake tabia fulani basi kuna tabia nyingine ataipenda".[423]
- Awe ni mwenye ghera juu yake na kumhifadhi,na kutomuweka katika mazingira yenye shari na fitna. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini jiokoeni nafsi zenu na watu wenu kutokana na Moto , ambao kuni zake ni watu na mawe..".[424]
- Kuichunga na kuiheshimu mali yake,asichukue chochote katika miliki yake ispokuwa kwa idhini na ridhaa yake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Si halali kwa mtu kutumia mali ya mtu mwengine ispokuwa kwa ridhaa yake".
Haki za ndugu na jamaa wa karibu.
Nao ni ndugu kiukoo,uislamu umehimiza kuwatendea wema na kuwasaidia ikiwa mtu anauwezo,kwa kukidhi haja zao,na kuwajulia hali na kushirikiana nao wakati wa furaha na wakati wa matatizo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana,na (muwatazame)jamaa".[425]
Na muislamu ameamrishwa kuunga udugu wake hata kama ndugu zake wanamtenga na kutaka kuvunja udugu,na awasamehe pindi wanapo mkosea hata kama wao wanamdhulumu na kumfanyia ubaya. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Hahesabiki ni mwenye kuunga udugu yule anaye fanya hivyo kwakuwa ndugu zake nao wanamuunga,lakini muunga udugu kikweli kweli ni yule ambaye pindi ndugu zake wanapo mtenga yeye anawaunga na kuwaweka karibu".[426] Na Uislamu umetahadharisha sana jambo la kukata udugu na kulifanya jambo hilo ni katika madhambi makubwa. Anasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Mwenyezi Mungu alipo maliza kuwaumba viumbe,udugu ukasimama na kusema;naombahifadhi kwako kutokana na faraka(tabia ya utengano),Mwenyezi Mungu akasema:Je hauko radhi kuwa nimuunge atakaye kuunga na nimtenge atakaye kutenga? Ukasema:Nimekubali, Akasema Mwenyezi mungu:Limekubaliwa ombi lako" Kisha Abuhurayra (Mpokezi wa hadithi hii) akasema :Someni mkipenda kuhusu jambo hili kauli ya Mwenyezi Mungu: "Ndiyo yanayo tarajiwa kwenu kufisidi katika ardhi na kuwakata jamaa zenu wakati mkipata ukubwa"?[427]
Haki za watoto.
Nazo ni pamoja na kuhifadhi na kulinda maisha yao,na kutimiza mahitaji yao ya lazima kama chakula ,mavazi, makaazi na kadhalika. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Yamtosha mtu kupata dhambi kwa kitendo cha kuwatelekeza watu wanao mtegemea".[428]
Na miongon mwa haki zao ni kuwachagulia majina mazuri. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Kwahakia nyinyi mtaitwa siku ya kiyama kwa majina yenu na kwa majina ya baba zenu,hiyvo basi chagueni majina mazuri".[429]
Na katika haki zao ni kuwafunza tabia njema,kama vile kuwa na haya,kuwaheshimu wakubwa,kuwa wakweli,waaminifu,kuwatii wazazi …na kuwatahadharisha na maneno machafu pamoja na tabia mbaya,kama uongo,udanganyifu,khiyana,wizi,kuwadharau
wazazi… Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Wakirimuni watoto wenu na muwafunze tabia njema".[430]
Na katika haki zao ni kuwapatia elimu yenye manufaa,na kuwapa malezi mema,na kuwachagulia marafiki wazuri. Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Kila mmoja wenu ni mchunga,na kila mchunga ataulizwa juu ya uchungaji wake,mama ni mchunga na atulizwa juu ya uchungaji wake,na mume ni mchunga juu ya familia yake na ataulizwa juu ya uchungaji wake, na mke katika nyumba ya mumewe ni mchunga na ataulizwa kuhusu uchungaji wake,na mtumishi ni mchunga juu ya mali ya tajiri yake naye ataulizwa juu ya uchungaji wake".[431]
Na katika haki zao ni kuwa na mapenzi nao na kuwaombea dua nzuri,sio kuwalaani na kuwaombea dua mbaya. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Msizilaani nafsi zenu wala msiwalaani watoto wenu,wala msiwalaani watumishi wenu,wal kuzilaani mali zenu,msije mkawafikiana na muda ambao Mwenyezi Mungu anapokea maombi kisha zikakubaliwa dua zenu mbaya,na yakawasibu miliyo yaomba".[432]
Na miongoni mwa haki zao ni kufanya uadilifu baina yao na kuto kuwatofautisha kwa kukwafadhilisha baadhi yao juu yaw engine,maana jambo hili ni sababu ya kuwajengea chuki baina yao, na kutowaheshimu na kuwapenda wazazi. Imepokewa kutoka kwa Nuuman ibnu Bashir –Mungu amuwie radhi- amsema : Baba yangu alinipa zawadi katika mali yake,kisha mama yangu akasema kumwambia baba:Sikuridhika na ugawaji huu mpaka umshuhudishe Mtume wa Mwenyezi Mungu juu ya hili,kisha baba yangu akaenda kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ili kumshuhudisha, Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamuuliza: "Je umefanya hivi kwa watoto wako wote"?akasema :hapana, Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: "Mcheni Mwenyezi Mungu na muwe waadilifu kwa watoto wenu".[433] Kisha baba yangu akarejea na akaninyanga`nya ile zawadi.
Haki za jirani.
Uislamu umempa jirani nafasi na daraja kubwa,kutokana na kauli ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Hakuacha Jibrilu kuniusia juu ya jirani mpaka nikadhani huenda itakuja hukumu ya kumpa haki ya kumrithi jirani yake".[434] Uislamu ukaamrisha kumtendea wema jirani.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote,na wafanyieni ihsani wazazi wawili,na jamaa na mayatima na masikini na jirani walio karibu na jirani walio mbali,na rafiki walio ubavuni (mwenu) na msafiri aliye haribikiwa,na wale iliyo wamiliki mikono yenu ya kuume.Bila shaka Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wajivunao".[435] Uislamu ukaharamisha kumfanyia maudhi jirani kwa namna yoyote ile,eidha kwa maneno au kwa vitendo,. Imepokewa kutoka kwa Abu huryra- Mungu amuwie radhi- amasema; Siku moja palisemwa mbele ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake Kwamba kuna mwanamke Fulani,yeye anafunga sana na anafanya ibada za usiku sana,lakini anamuudhi jirani yake kwa ulimi wake. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: " Huyo hana kheri yoyote,huyo ni miongoni mwa watu wa Motoni..".[436] Na umelizingatia swala la kumuudhi jirani ni ukosefu wa imani. Akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Wallahi hana imani,Wallahi hana imani,Wallahi hana imani"akaulizwa,ni nani huyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? akasema : " Mtu ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake".[437]
Na jirani wako aina tatu,na haki zao zinatofautiana vilevile:-
-Kuna jirani ambaye ni ndugu yako,huyu ana haki tatu;haki ya udugu na haki ya ujirani na haki ya Uislamu
-Na jirani ambaye ni Muislamu , yeye ana haki mbli;haki ya ujirani na haki ya Uislamu
- Na jirani ambae sio Muislamu, naye ana haki moja, ambayo ni haki ya ujirani. Imepokewa kwa swahaba mtukufu Abdullahi bin Amru, kwamba siku moja aliingia nyumbani kwake akakuta kazawadiwa nyama,akawauliza watu wa nyumbani kwake:Je mmempelekea na jirani yetu myahudi?!,maana nilimsikia Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuacha Jibrilu kuniusia juu ya jirani mpaka nikadhani huenda akamrithisha".[438]
Haki za marafiki.
Uislamu umehimiza sna juu ya kuwajali marafiki na ukaweka haki ambazo zinamlazimu rafiki kumtendea rafiki yake,kama vile kumfanyia wema na kumpa nasaha.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Rafiki aliye bora mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mbora wenu kwa marafiki zake,na jirani aliye bora mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mbora wenu kwa jirani zake".[439] Na ukajaalia haki zake ni zenye kuendelea hata baada ya kufa mmoja wao. Mtu mmoja katika kabila la bani salama alimuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je kuna wema wowote uliobakia wa kuwatendea wazazi wangu baada ya kufa kwao? Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema:"Ndio, kuwaombea dua,na kuwatakia msamaha kwa Mwenyezi Mungu,na kutekeleza ahadi zao,na kuunga udugu wao na kuwakirimu marafiki zao".[440]
Haki za mgeni.
Miongoni mwa haki za mgeni katika Uislamu ni kumkirimu, kutokana na mafundisho ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na mkirimu jirani yake,na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi amkirimu mgeni wake,na mwenye kumuaminiMwenyezi Mungu na siku ya mwisho,basi aseme maneno ya kheri au anyamaze".[441] Na Uislamu unalihesabu jambo la kumkirimu mgeni ni miongoni mwa matendo matukufu yenye malipo makubwa. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Katika watu hakuna aliye mfano wa mtu ambaye kashika hatamu ya farasi wake na anapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na anajiepusha na watu waovu,na mfano wa bedui anayeishi jangwani na mifugo yake,akawa ni mwenye kuwakirimu wageni wake na anatekeleza haki zake".[442] Na ukaweka adabu maalumu katika kumkirimu mgeni,kama vile kumpokea vizuri kwa uso wenye bashasha,na wakati wa kumuaga pia iwe ni kwa bashasha.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hakika miongoni mwa suna katika kumuaga mgeni ni kutoka naye mpaka mlangoni".[443]
Lakinipia inampasa mgeni kuchunga hali za mwenyeji wake,asimpe uzito aulioko nje ya uwezo wake,maana Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anasema: " Si halali kwa Muislamu kukaa kwa ndugu yake mpaka akampatisha madhambi "akaulizwa ni vipi atampatisha madhambi? Akasema: " Anakaa kwake mpaka ankosa kitu cha kumkirimu nacho".[444]a
Imamu Alghazal Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akimkirimu kila anayeingia kwake,mpaka wakati mwingine alikuwa akimtandikia katika kitabu (Ihyaau uluumuddin) amemuelezea Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ambaye ndiye kiigizo cha waislamu,akasema: Alikuwa Mtume (nguo yake kukalia mtu ambaye hana ukoo nae wala ukaribu wowote,na hakupata kumkaribisha mtu yoyote ispokuwa alisadikisha kwamba ni mfano bora katika ukarimu,na alikuwa akimpa kila mgeni miongoni mwa wageni wanao kuwa mbele yake haki yake katika kumtazama na kumsikiliza pindi anapo zungumza, na zaidi yahivyo alikuwa ni mtu mwenye hay asana,na mnyenyekevu sana, na muaminifu sana. Na alikuwa akiwatukuza sana maswahaba wake,na hakuwa ni mwenye kukasirika bila sababu.
Na kwa upande wa kazi na wafanya kazi,Uislamu umeweka misingi ambayo inabainisha haki za kila mmoja kati ya muajiri na muajiriwa na haki za wafanya kazi wao kwa wao. Miongoni mwa kanuni hizo ni :-
Haki za wafanya kazi.
Uislamu umeamrisha mahusiano kati ya muajiri na muajiriwa uwe ni uhusiano mzuri wa kiudugu,na usawa na kuchungiana heshima,kutokana na mafundisho ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliposema : " Ndugu zenu hawa (watumishi) Mwenyezi Mungu kawaweka chini ya mikono yenu,basi yeyote atakateye kuwa na ndugu yak echini ya mikono yake,basin a amlishe katika kile anacho kula yeye,na amvishe katika kile anacho vaa yeye, wala asimkalifishe kufanya kazi asizo ziweza,na mkiwakalifisha kazi ngumu basi wasaidieni".[445] Na Uislamu umelazimisha kumpa mtumishi haki yake.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Watu wa aina tatu watakuwa wagomvi wangu siku ya kiyama; Mtu aliyeaminiwa kitu kisha akafanya khiyana,na mtu aliye muuza binadamu mwenzie aliye huru kisha akala thamani yake,na mtu aliye muajiri mtu,yule muajiriwa akatimiza wajibu wake lakini yeye hakumpa haki yake".[446] Na ukaamrisha kukubaliana malipo kabla ya kuanza kazi,maana Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amekataza kumuajiri mtu mpaka umbainishie malipo yake. Na ukaamrisha kumpa malipo yake mara tu amalizapo kazi mliyo kubaliana . Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Wapeni waajiriwa malipo yao kabla kabla hata jasho zao hazijakauka".[447] Na ili kubainisha umuhimu wa kufanya kazi,na ubora wa watu wanao jituma na kufanya kazi uislamu umejaalia chumo alipatalo mtu kutokana na kazi ya halali kuwa ndio chumo bora.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Hajapata mtu kula chakula kizuri na chenye kheri kuliko chakula alicho kipata kutokana na chumo la mkono wake,na hakika Nabii wa Mwenyezi Mungu Dawud alikuwa akila kutokana na chumo la mkono wake".[448] Na uislamu umewahimiza sana watu kufanya kazi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Ni bora mtu akachukua kamba kisha akaenda porini kutafuta kuni na akazibeba kichwani kisha akaja kuziuza na kukidhi haja zake,kuliko kupita kwa watu akiomba omba,ima wampe au wamnyime".[449]
Haki za muajiri.
Kama alivyo takiwa muajiri kukchunga na kutekeleza haki za waajiriwa pia muajiriwa ametakiwa kuchunga haki za muajiri wake,pindi atakapo pewa majukumu ni lazima ayatekeze kiukamilifu bila ya kuchelewa. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake :" Hakika Mwenyezi Mungu anapenda pindi mmoja wenu anapo fanya kazi aifanye kwa ufanisi".[450]
Ama kuhusiana na wajibu na haki zinazo wahusu watu wote;
Uislamu umemtaka kila mmoja awe ni mwenye kujali hali za ndugu zake popote pale watakapo kuwa.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Utawaona Waislamu katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao,na kufanyiana upole,mfano wao ni kama mwili mmoja,pindi kinapo umia kiungo kimoja basi mwili mzima unashiriki katika maumivu na kupatwa homa na kukesha".[451] Na ukaamrisha kutengeneza mambo yao na hali zao.Akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Hawezi kuwa muumini wa kweli mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake kile anacho kipenda yeye ".[452] Na kushirikiana nao wakati wa matatizo . Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Muumini kwa muumini mwenzie ni mfano wa jingo moja ambalo limeshikana imara pande zake zote".[453] Na ukaamrisha kuwanusuru na kuwapa msaada pindi ukihitajika. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na wakiomba msaada kwenu katika Dini ,basi ni juu yenu kuwasaidia,ispokuwa juuya watu ambao kuna mapatano baina yenu na wao(hapo msiwasaidie wao mkapigana na mkapigana na waitifaki wenu.Lakini jitahidini kupatanisha) Na Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda".[454]
Upande wa tabia katika Uislamu.
Uislamu umekuja ili kutimiza tabia njema.Amesema MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Nimetumwa ili nije kutimiza tabia zilizo njema".[455]Hivyo basi hakuna tabia iliyo njiema ispokuwa Uislamu umeiamrisha ,na hakuna tabia iliyo mbaya ispokuwa umeikataza na kuitahadharish. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Shikamana na kusamehe na uamrishe mema na wapuuze masafihi".[456] Na ukabainisha utaratibu anao takiwa kuufuata Muislamu katika mahisiano yake na jamii yake. Akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Jitenge na mambo yaliyo haramishwa utakuwa ni mchamungu mkubwa,na ridhika na kile alicho kupangia Mwenyezi Mungu utakuwa ni katika watu walio kinai,na mtendee wema jirani yako utakuwa ni muumini wa kweli,na wapendelee watu vile uvipendavyo wewe utakuwa Muislamu wa kweli,wala usiwe ni mwenye kupenda kuchecheka sana,maana kucheka cheka ovyo kunaua moyo wa mtu".[457] Na amesema Pia Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Muislamu wa kweli ni yule ambaye waislamu wenzie wanasalimika na na shari za ulimi wake na mikono yake,na aliye hama kikweli ni yule aliye yahama mambo aliyo yakataza Mwenyezi Mungu".[458] Na siku moja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliwauliza maswahaba akasema: " Je mnamjua muflis ni nani"? wakasema: Muflis miongoni mwetu ni yule asiyekuwa na dirham wala kitu cha kumsaidia. Akasema: " Muflis katika umati wangu ni yule atakaye kuja siku ya Qiyama akiwa na swal na zaka na swaumu,lakini kumbe alimtukana mtu Fulani,na akamzushia huyu,na alimwaga damu ya yule,na akampiga Fulani…akiwa na makosa mbali mbali.Yatachukuliwa mema yake apewe Fulani na Fulani katika wale alio wadhulumu,na endapo mema yake yatamalizika wakati bado anadaiwa,yatachukuliwa madhambi yao abebeshwe yeye kisha atupwe Motoni".[459]
Na Uislamu kati maamrisho yake au makatazo yake unakusudia kujenga jamii yenye mshikamano na umoja na mapenzi. Pia haebu tutaje baadhi ya mambo ambayo Uislamu umeyaharamisha na kuyakataza,ingawaje ni vigumu kuyataja yote katika kitabu hiki,lakini nitataja baadhi tu:-
Uislamu umeharamisha ushirikina. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi (dhambi ya) kumshirikisha na kitu, (kukifanya ni mungu nacho ukakiabudu, ukakiomba…) lakini Yeye husamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakaye".[460]
Ukaharamisha uchawi. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu hurayra –Mungu amuwie radhi- kwamba Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Jiepuseni na madhambi yaangamizayo;Kumshirikisha Mwenyezi Mungu,na uchawi".[461]
Ukaharamisha dhulma na kuwafanyia uadui watu,eidha kwa maneno au vitendo,na kutowatekelezea watu haki zao. Amesema Mwenyezi Mungu: "Sema (uwaambie): Mola wangu ameharamisha (haya, ameharamisha) mambo machafu, yaliyo dhihirika na yaliyo fichika,na dhambi na kutoka katika utii (wa wakubwa ) pasipo haki ".[462]
Ukaharamisha kuiua nafsi pasina haki.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Na atakaye muua Muislamu kwa kukusudia basi malipo yake ni jahanamu,humo atakaa milele,na mwwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani na amemuandalia adhabu kubwa". Lakini anayeua au kuuliwa kwa katika hali ya kuitetea nafsi yake,au mali yake haingii katika hukumu hii. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Atakaye uawa katika kuitetea mali yake basi huyo kafa shahidi,na atakaye uawa katika kuuitetea familia yake pia kafa ni shahidi,na atakaye kufa katika kuitetea nafsi yake pia kafa shahidi,na atakaye uawa katika kuitetea Dini yake huyo kafa shahidi".[463]
Ukaharamisha kukata udugu na kuwatenga jamaa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ndiyo yanayo tarajiwa kwenu kufisidi katika ardhi na kuwakataa jamaa zenu wakati mkipata ukubwa?.hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani akawatia uziwi na kuyapofua macho yao".[464] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Hatoingia Peponi mtu aliye kata udugu".[465] Na makusudio ya kukata udugu ni kutowatembelea,na kuwajulia hali,na kujikweza juu yao,na kutowajali wenye hali duni endapo kama yeye kajaaliwa kihali,maana kumsaidia fakiri ambaye huna ukoo naye unapata malipo ya kutoa sadaka,lakini kumsaidia fakiri ambaye ni katika ukoo wako uanapata malipo ya sadaka na malipo ya kuunga udugu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Wafanyieni wema ndugu zenu japo kwa salamu".[466]
Ukaharamisha uzinifu na kila jambo ambalo ni sababu ya uzinifu. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala msikaribie zinaa,hakika hiyo zinaa ni uchafu (mkubwa )na ni njia mbaya(kabisa) ".[467] Na hii ni kwa ajili ya kulinda heshima za watu,na kuchunga tabia za watu,na kuilinda jamii kutokana na mgawanyiko,na kulinda nasabu za watu zisichanganyike na hatimaye ikapelekea kuwarithisha watu wasio sitahiki,na pia wasije kuona watu ambao ni ndugu,na pia ni katika kuihifadhi jamii kutokana na maradhi na majanga yanayo tokana na tabia hii chafu. Siku moja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliwahutubia maswahaba akasema : " Enyi kongamano la Muhajirina! (Yaani walio hama kutoka mji wa Maka kwenda Madina),kuna mambo matano,endapo yatakufikeni,lakini namuomba hifadhi Mwenyezi Mungu yasije yakawadiriki. Hautapata kudhihiri uchafu wa zinaa katika jamii yoyote mpaka wakafikia kuifanya wazi wazi,ispokuwa yatawakumba maradhi ambayo hayakuwepo kwa watu walio tangulia kabla yao…".[468] Na zinaa mbaya zaidi ni mtu kuzini na ndugu yake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Yeyote atakaye muingilia ndugu yake basi muueni".[469]
Na pia uislamu umeharamisha kulawiti.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwaelezea watu wa Nabii Lutwi: "Basi ilipofika amri yetu tuliifanya (ardhi ardhihiyo iwe juu chini) juu yake kuwa chini yake na tukawateremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu wa motoni ulio kamatana. (Changarawe) zilizo tiwa alama kwa Mola wako (kila moja kuwa ya mtu Fulani).Na (adhabu) hii haiku mbali na madhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanao fanya machafu haya) ".[470] Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Mwenyezi Mungu kawlaani watu wa aina saba katika viumbe wake,na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akaitaja laana ya kila mmoja katika hao mara tatu,kisha akasema: Amelaani ,amelaaniwa,amelaaniwa mwenye kufanya matendo ya watu wa Nabii Lutwi(kulawiti),amelaaniwa mwenye kumuoa mwanamke na binti yake (mama na mtoto),amelaaniwa mwenye kuwatukana wazazi wake,amelaaniwa mwenye kumuingilia mnyama,amelaaniwa mwenye kubadlisha mipaka,amelaaniwa mwenye kuchinja kwa kujikurubisha kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu,na amelaaniwa mtu ambaye alikuwa mtumwa kisha akaachwa huru halafu akajinasibisha na watu kinyume na walio muacha huru".[471]
Ukaharamisha kula mali za mayatima,maana kufanya hivo ni kupoteza haki za wanyonge. Amesema Mwenyezi Mungu "Hakika wale ambao wanakula mali ya mayatima kwa dhulma,bila shaka wanakula Moto matumboni mwao,na wataungua katika huo Moto( wa Jahannam) uwakao".[472] Lakini Mwenyezi Mungu kamtoa katika hukumu hii msimamizi na muangalizi wa mali za yatima,yeye ana haki ya kutumia katika mali yake kulingana na usimamizi wake na kwa kadiri ya haja ,kama vile chakula,mavazi,na anayo haki ya kuifanyia biashara mali ya yatima kwa nia ya kumnufaisha yatima katika kuikuza mali yake. Amesema Mwenyezi Mungu: "Na mwenye kuwa tajiri basi ajiepushe (na kuchukua ujira katika kuwafanyia kazi zao).Na atakaye kuwa muhitaji basi ale kwa namna inayo kubaliwa na sheria".[473]
Umeharamisha kutoa ushahidi wa uongo,na ukalizingatia jambo hilo ni miongoni mwa madhambi makubwa,maana kufanya hivo ni kupoteza haki za watu katika jamii na ni sababu ya kuenea kwa dhulma katika jamii. Siku moja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliwauliza maswahaba akasema:" Je nisikufahamisheni madhambi makubwa"?wakasema;Tufahamishe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: " Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu,na kuwatelekeza wazazi wawili"alikuwa kaegemea kasha akakaa sawa,akasema: "Tambueni na mzingatie;Na kusema uongo ni katika madhambi makubwa,na kushuhudia uongo"akaendelea kuyakariri maneno haya ,mpaka maswahaba kwa kumuonea huruma wakadhani hato nyamaza.[474]
Ukaharamisha kamari na kutazamia kwa sababu kufanya hivyo ni katika kupoteza mali na nguvu bila ya faida yoyote inayo patikana kwa mtu au kwa jamii. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini! bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa (na kuombwa) asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli (na kwa vinginevyo); (yote haya) ni uchafu ni katika kazoo ya shetani basi jiepusheni nayo ili mpate kufaulu".[475] Maana mwenye kucheza kamari ikiwa atachuma mali kupitia kamari basi atakuwa kaipata kwa njia isiyo halali,na endapo ataliwa basi atakuwa kaipoteza mali yake katika mambo yasiyo kuwa na faida yoyote.
Ukaharamisha pia ujambazi na uvamizi na kuuwa watu. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Basi malipo ya wale wanao pigana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (kwa kufanya aliyowakataza)na kufanya maovu katika nchi,ni kuuawa au kusulubiwa au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho (mkono wa kulia kwa mguu wa kushoto ,na mkono wa kushoto kwa mguu wa kulia) au kuhamishwa katika nchi ,hiindiyo fedheha yao katika dunia,na akhera watapata adhabu kubwa".[476] Na adhabu hizi zinatekelezwa kulinga na ukubwa wa kosa lenyewe. Imepokewa kutoka kwa Ibnu abasi – Mungu amuwie radhi- hukumu ya majambazi; kwamba kama wataua na kupora mali,basi hukumu yao ni kuuawa na kusulubiwa,na kama wataua lakini hawakuchukua mali basii hukumu yao ni kuuawa lakini hawatasulubiwa,na kama watapora mali bila y a kuua,hukumu yao ni kukatwa mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha,na kama watawatisha watu tu lakini hawakuchukua mali basi hukumu yao ni kuhamishwa katika nchi.[477]
Na umeharamisha viapo vya uongo,navyo ni viapo ambavyo mtu anaapa hali yakuwa anaju a kuwa ni muongo ili aweze kujipatia haki isiyo yake,na viapo vya namna hii vinamzamisha mtu Motoni. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa ajili ya thamani ndogo ya kilimwengu hao ndio hawatakuwa na sehemu ya kheri katika akhera,wala Mwenyezi Mungu hatasema nao (maneno mazuri) wala hatawatazama (jicho la rehma)siku hiyo ya kiyama wala hatawatakasa (na mnadhambi yao) nao watapata adhabu iumizayo".[478] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Mwenye kuchukua haki ya mwislamu mwenzie kwa njia ya kiapo,basi Mwenyezi Mungu kamuwajibishia Moto na kumharamishia Pepo"mtu mmoja akamuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! hata kama ni kitu kidogo?akasema : " Hata kama ni fimbo".[479]
Umeharamisha pia mtu kujiua mwenyewe. Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Wala msijiue(wala msiue wenzenu). hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kukuhurumieni. Na atakaye fanya haya kwa uadui na dhulma,basi huyo tutamuingiza Motoni,na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu".[480]
Umeharamisha uongo na khiyana ,na kuvunja ahadi,na kutotekeleza amana. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini! Msimfanyie khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume (mkaacha kufuata mliyo amrishwa)wala msikhini amana zenu (mnazo aminiana wenyewe kwa wenyewe) na hali mnajua (kuwa ni vibaya).[481] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake " Mambo manne akiwa nayo mtu basi huyo ni mnafiki halisi,na atakaye kuwa na jambo moja wapo basi huyo anakuwa na sifa miongoni mwa sifa za unafiki mpaka atakapo iwacha;Pindi akiaminiwa anafanya khiyana, na akizungumza anasema uongo,na anapo ahidi hatekelezi,na akikosana na mtu anachupa mipaka ".[482] na katika mapokezi mengine ya Imamu Muslimu amesema: "Hata kama mtu huyo ataswali na akafunga na kudai kuwa ni muislamu".
Umeharamisha pia mtu kumhama ndugu yake na kufanyiana husuda.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Msibughudhiane wala msifanyiane husuda wala msihamane,na kuweni enyi waja wa Mwenyezi Mungu ni ndugu,na si halali kwa Muislamu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu".[483] Na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katubainishia mambo yanayoweza kuambatana na husuda,akasema: " Jiepusheni na jitengeni mbali na husuda,maana husuda inakula mema ya mtu kama jinsi Moto unavyo kula kuni au majani".[484]
Ukaharamisha tabi ya kulaaniana ,na kusema maneno mabaya namatusi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika muumini wa kwli hawi ni mwenye kuwatuhumu watu,wala kuwalaani watu, wala hawi na maneno machafu".[485] Hata kwa maadui zetu Uislamu unatuelekeza kuacha maneno machafu. SIku moja maswahaba walimwambia Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : Kwanini hauwaombei dua mbaya maadui zetu? Akasema: " Mimi skiletwa kuwa ni mwenye kuwalaani watu,bali nimeletwa ili niwe ni rehma kwa viumbe".[486]
Uislamu umetahadharisha na kukataza tabia ya ubakhili,kwa sababu mtazano wa Uislamu juu ya mali ni kwamba mali ni za Mwenyezi Mungu,ispokuwa kampa mwanadamu kama amana,ili imsaidie kukidhi haja zake na wanao mtegemea,na katika mali hiyo kuna haki za wenye matatizo. Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Mtu mkarimu yuko karibu na Mwenyezi Mungu,na yuko karibu na Pepo ya Mwenyezi Mungu,na yuko karibu na watu,na yuko mbali na Moto,na mtu bakhili yuko mbali sana na mwenyezi Mungu,na yuko mbali na Pepo,na yuko mbali na watu na yuko karibu na Moto,na mja ambaye ni mjinga lakini ni mkarimu katika mali yake anapendwa na Mwenyezi Mungu kuliko mja ambaye anajitahidi katika ibada lakini ni bakhili".[487] Na mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amebainisha matokeo mabaya yanayo weza kuikumba jamii endapo yatadhihiri maradhi ya ubakhili katika jamii hiyo, akasema : "Tahadharini sana na dhulma, kwa sababu dhulma ni kiza siku ya kiyama,na tahadharini sana na ubakhili, maana umewaangamiza walio kuwa kabla yenu, uliwafikisha mahala wakamwaga damu zao (wakauwana) na wakayahalalisha mambo aliyo waharamishiaa Mwenyezi Mungu".[488]
Hakika Uislamu unamzingatia mtu ambaye ana uwezo lakini hawasaidii wenye matatizo wanao mjia na kueleza shida zao,kwamba mtu huyu yuko mbali sana na imani . Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Tabia za aina mbili kamwe hawezi kuwa nazo muumini wa kweli; Ubakhili na tabia mbaya".[489]
Umetahadharisha na kukemea tabia ya kuchezea mali na kuitumia kwa fujo katika mambo yasiyo na faida. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na umpe jamaa yako wa karibu haki yake,na masikini na msafiri aliye haribikiwa,wala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu.Hakika watumiao kwa ubadhirifu ni ndugu wa mashetani (wanamfuata shetani),na shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake".[490] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amekuharamishieni kuwatelekeza wazazi wawili,na tabia ya uchoyo (chako unazuia cha mwenzio unakitaka),na tabia ya kuwazika mabinti zenu wakiwa hai (tabia hii ilikuwepo zamani kwa waarabu kabla ya kutumwa Nabii Muhammad),na anachukia kwenu maneno yasiyokuwa na faida yoyote,na tabia ya kuuliza uliza maswali mengi,na kupoteza mali katika mambo yasiyo kuwa na faida".[491]
Umekataza na kutahadharisha kuchupa mipaka katika Dini. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Hakika Dini ni nyepesi,na yeyote atakaye ifanya kuwa ngumu basi itamshinda,basi jitahidini kadiri ya uwezo wenu,na kuweni ni wenye bishara njema,na jisaidieni katika hilo kwa kufanya ibada wakati wa asubuhi na jioni".[492]
Ukatahadharisha na kukemea tabia ya kujikweza na kiburi .Amesema Mwenyezi Mungu: " Wala usiwatazame watu kwa upande mmoja wa uso (usiwafanyie jeuri),wala usende katika ardhi kwa maringo,hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye,ajifaharishaye. Na ushike mwendo wa katikati na uteremshe sauti yako,bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote (kwa makelele yake ya bure)".[493] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuhusu kiburi : "Hatoingia Peponi yeyote ambaye ndani ya moyo wake kuna chembe ya kiburi hata mfano wa punje ya ulezi" mtu mmoja akauliza :Ewe Mtume wa mwenyezi Mungu ! Hakika kila mtu anapenda kuvaa nguo nzuri,viatu vizuri.. (je na hivi ni katika kiburi)? Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamjibu akasema: " Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri na anapenda vilivyo vizuri,lakini kiburi maana yake ni kuikanusha haki na kuwadharau watu".[494]
Ukaharamisha kuwachunguza chunguza watu na kufatilia mambo yasiyo mhusu mtu,na kuwadhania vibaya watu, na kuwateta. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini! Jiepusheni sana na (kuwadhania watu) dhana (mbaya)kwani (kuwadhania watu) dhana (mbaya) ni dhambi. Wala msipeleleze (habari za watu), wala baadhi yenu wasiwasenge-nye wengine. Je! mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliye kufa? La, hampendi; (basi na haya msiapende), na mcheni Mwenyezi Mungu.Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba (na ) Mwingi wa kurehemu".[495] Na siku moja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliwauliza Maswahaba wake akasema: "Je mnajua nini maana ya kuteta"? wakasema: Mungu na Mtume wake ndio wajuao. Akasema: "Kuteta ni kumtaja ndugu yako kwa jambo asilo lipenda" akaulizwa tena: Je kama kweli jambo hili analo? akasema: "Kama kweli analo basihuko ndiko kuteta kwenyewe,na kama hana basi utakuwa umemzulia".[496]
Na ukaharamisha kusikiliza mazungumzo ya watu bila idhini yao. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Na mwenye kusikiliza mazungumzo ya watu bila ridhaa yao,basi atamiminiwa risasi za Moto siku ya kiyama".[497]
Ukakataza mtu kuingilia mambo yasiyo muhusu. Amkasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hakika katika uzuri wa Uislamu wa mtu ni kuacha mambo yasiyo muhusu".[498]
Ukaharamisha kudharauliana kwa kuitana majina mabaya,na kuwabeza watu ima kwa maneno au vitendo. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini !wanaume wasiwadharau wanaume wenzao ,huenda wakawa bora kuliko wao,wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao huenda wakawa bora kuliko wao, wala msitukanane kwa kabila wala msiitane kwa majina mabaya.."[499]
Ukaharamisha kadhi kufanya ujeuri katika hukumu,maana kadhi katika Uislamu anazingatiwa ni mwenye kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu wala hana haki ya kuleta sheria zake yeye ni mtekelezaji tu,hivyo akifanya ujeuri ana kuwa kafanya khiyana katika amana aliyo pewa. Amesema Metume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Makadhi wa aina mbili wataingia Motoni na aina moja tu ndio wataingia peponi,kadhi aliye hukumu kwa haki huyo ataingia Peponi,na kadhi aliye hukumu kwa jeuri na kufuata matamanio ya nafsi yake huyo ataingia Motoni,na kadhi aliye hukumu kwa ujinga bila kujua hukumu ya Mwenyezi Mungu,huyo pia ataingia Motoni"akaulizwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake Huyu ambaye hakujua ana kosa gani? Akasema : "Hakupaswa kutoa hukumu bila ya ujuzi".[500]
Ukamharamishia mwanaume kuridhia machafu katika familia yake, na kutokuwa na ghera. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Watu wa aina tatu Mwenyezi Mungu hatawatazama siku ya kiyama;Mtu aliye watelekeza na kuwatesa wazazi wake,na mwanamke mwenye kujifananisha na wanaume,na mwanaume anaye ridhia vitendo vichafu nyumbani kwake".[501]
Umeharamisha kwa wanaume kujifananisha na wanawake,na wanawake kujifananisha na wanaume. Imepokewa kutoka kwa Ibnu abasi – Mungu awawie radhi – amesema: (Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake,na wanawake wenye kujifananisha na wanaume).[502]
Ukaharamisha kusimbulia,nacho ni kitendo cha mtu kumpa mwenzie kitu au kumtendea wema kisha akaanza kumuumbua mbele za watu au kumkera kwa sababu ya wema alio mtendea. Ame3sema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake "Tahadharini sana na tabia ya kusimbulia,maana kufanya hivyo kuna futa malipo na thawabu za mtu".kisha akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu : " Enyi mlio amini !msiziharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na udhia…"[503]
Ukaharamisha mtu kudai kitu ambacho kaisha kitoa kumpa mtu. Akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake" Mwnye kurudi kudai kitu ambacho kaisha kigawa ni sawa na mbwa anaye tapika kasha akarudi kula matapishi yake".[504]
Ukaharamisha tabia ya uchonganishi kwa kuhamisha maneno huku na kule kwa lengo la kuwafitini watu. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala usimtii kila muapaji san alite dhalili. Msengenyaji aendaye katika fitina".[505] Na akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Hatoingia Peponi Mtu msengenyaji na mfitinishaji watu".[506]
Ukaharamisha kujikweza juu ya wanyonge,eidha unyonge wa kimwili kama wagonjwa,na wazee ,au unyonge wa kimali kama vile kujikweza kwa masikini na mafakiri na wenye matatizo,au hata kwa watu wanao mtegemea,yote hiyo ni kutaka watu waishi katika jamii yenye umoja na mapenzi na udugu na kuoneana huruma. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Mwabuduni mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote,na wafanyieni ihsani wazazi wawili,na jamaa na mayatima,na masikini na jirani walio karibu na jirani walio mbali na rafiki walio ubavuni (mwenu) na msafiri aliye haribikiwa na wale iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia.Bila shaka Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wajivunao".[507] Siku moja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuwa kashika mswaki mkononi halafu akamuita mtumishi wake akawa kachelewa,alipokuja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia: "Lau kama sio kisasi ningekupiga na huu mswaki".[508]
Umeharamisha kusababisha madhara katika wasia,kama vile kuusia kwamba anadaiwa na mtu Fulani hali anajua kuwa ni uongo kwa lengo la kuwakosesha warithi mali hiyo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " ..Baada ya kutoa vilivyo usiwa au kulipa deni,pasipo kuleta dhara..".[509]
Vilivyo haramu katika vyakula na vinywaji na mavazi.
Uislamu umeharamisha kunywa pombe, na kila chenye kulevya kama madawa ya kulevya kwa aina zake zote. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa (na kuombwa) asiyekuwa Mwenyezi Mungu,na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli (na kwa vinginevyo);(yote haya) ni uchafu ni katika kazi ya shetani. Basijiepusheni navyo ili mpate kufaulu. Hakika shetani anataka kukutilieni uadui na bughudha baina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari,na anataka kukuzuilieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na (kukuzuilieni) kusali .Basi je mtaacha"?[510] Na ili kukomesha kabisa unywaji wa pombe na ainazote zote za ulevi amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Mwenyezi Mungu ameilaani pombe na amemlaani muuzaji,na mnywaji, na mwenye kuitengeneza,na mbebaji,na mwenye kupelekewa,na muuzaji na mwenye kuinunua,na mwenye kula thamani yake".[511] Na lengo kubwa la makemeo ma kali kama haya ni kutaka kuihifadhi akili na hisia za mwanadamu kutokana na kila kitu kinacho weza kuiharibu,kwa sababu Uislamu unawataka watu wasijishushe katika daraja aliyowapa Mwenyezi Mungu na kujiweka katika daraja ya wanyama wengine wasio na akili wala utambuzi. BIla shaka kila mmoja anatambua kwamba mtu anapofikia kubobea katika ulevi na utumiaji wa madawa ya kulevya,basi yuko tayari kufanya kila awezacho ilimradi apate pesa ili kukidhi kiu yake ya ulevi,hata kma ni kwa kuiba au kuua, na akisha lewa anakuwa tayari kufanya jambo lolote maana tayari anakuwa kaisha ifunika akili yake,na kwa sababu hii ndio maana Uislamu umeiita pombe kuwa ni mama wa madhambi yote makubwa.
Umeharamisha kula nyama ya nguruwe na kila kitu kinacho ingia katika kauli Ya Mwenyezi Mungu: " Mme haramishiwa nyamafu na damu na nyama ya nguruwe,na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,na kilicho kufa kwa kusongeka koo,na kilicho kufa kwa kupigwa,na kilicho kufa kwa kuanguka,na kilicho kufa kwa kupigwa pembe(na mwengine), na alicho kila mnyama (kikafa) ila mkiwahi kukichinja (kabla hakijafa),na (pia mmeharamishiwa) kilicho chinjwa panapo fanyiwa ibada isiyo kuwa ya Mungu (kama mizimuni) na ni (haramu kwenu )kutaka kujua siri kwa kuagua kwa kupiga bao (na njia zingine zilizo kama hii).Hayo yote ni maasi".[512] Pia umeharamisha kila kilicho chinjwa bila kutajwa jina la Mwenyezi Mungu,eidha kwa makusudi au likatajwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Wala msile katika wale (wanyama) wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu maana (kula )huko ni uasi".[513]
Pia ukaharamisha kula wanyama na ndege ambao ni wakali. Katika wanyama ni wale wenye meno chonge,kama samba,chui,mbwa mwitu na mfano wa hao. Na katika ndege ni wale wenye kucha,kama vile kipanga,kunguru,na mfano wa hao.
Ukaharamisha kila kitu chenye madhara katika mwili wa mwanadamu. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala msijiue(wala msiue wenzenu).Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kukuhurumieni ".[514]
Ukaharamisha kuvaa dhahabu na nguo za hariri kwa wanaume,lakini kwa wanawake ikaruhusiwa. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Imehalalishwa kuvaa hariri na dhahabu kwa wanawake katika umati wangu na ikaharamishwa kwa wanaume".[515]
Sasa hebu tutaje kwa muhtasari baadhi ya mambo ambayo Uislamu umeyaamrisha na kuyahimiza:
Umeamrisha kufanya uadilifu katika maneno na vitendo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na kufanya ihsani,na kuwapa jamaa (na wengineo),na anakataza uchafu na uovu na dhulma.Anakunasihini ili mpate kufahamu".[516] Uadilifu unatakiwa kwa mtu ambaye ni jamaa wa karibu na hata kwa mtu ambaye si ndugu yako. Amesma Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na msemapo( katika kutoa ushahidi na penginepo) semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa(usimpendelee kwa ajili ya ujamaa uliyopo baina yenu au kwa sababu nyingine),na tekelezeni ahadi ya Mwenyezi Mungu.Amekuusieni haya ili mpate kukumbuka".[517] Uadilifu unatakiwa katika zote,anapo kuwa radhi na hata katika hali ya ghadhabu,sawa sawa iwe ni kwa Muislamu au hata kama sio Muislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Wala kule kuwachukia watu kwa kuwa walikuzuilieni kufika msikiti ulio tukuzwa (wa Makka)kusikupelekeeni kuwafanyia jeuri (ili kulipa jerui yao)".[518]
Umeamrisha kuwapendelea kheri watu na kuwatanguliza kuliko kujipenda,maana kufanya hivo ni dalili ya mapenzi ya kweli,ambayo athari zake zinaifanya jamii inakuwa nijamii iliyo jaa mshikamano na mapenzi .Amesema Mwenyezi Mungu katika kuwasifu wale wanao wafadhilisha watu na kuwapendelea kheri kuliko nafsi zao: " Na wanawapendelea kuliko nafsi zao ingawa wenyewe wana hali ndogo,na waepushwao na ubakhili wa nafsi zao hao ndio wenye kufaulu kweli kweli".[519]
Umeamrisha kushikamana na watu wema,na ukatahadhaarisha kushikamana na watu waovu na kukaa nao. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipiga mfano ambao anabainisha athari zinazo patikana katika kusuhubiana na watu wema ,na athari zipatikanazo katika kusuhubiana na watu waovu,akasema : " Mfano wa kusuhubiana na mtu mwema na kusuhubiana na mtu muovu ni kama vile muuza manukato na mfua vyuma; ama muuza miski ukisuhubiana naye ima atakuzawadia katika manukato aliyo nayo,au atakuuzia,au utaambulia kwake kupata harufu nzuri,ama mfua vyuma ukisuhubiana naye ima ataunguza nguo yako,au utaambulia kunuka harufu ya moshi".[520]
Umeamrisha kusuluhisha baina ya watu pindiyanap tokea matatizo na kutoelewana. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakun akheri katika mengi wanayo shauriana kwa siri isipokuwa (mashauri ya) wale wanao amrisha kutoa sadaka au kufanya mema au kupatanisha baina ya watu.Na atakaye fanya hivi kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu basi tutampa ujira mkubwa".[521] Kuwasuluhisha watu ni jabo lenye ujira mkubwa kabisa katika Uislamu,malipo yake hayako mbali na malipo ya swala wala funga na mambo ya wajibu mengine. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Nikufahamisheni jambo lililo bora na lenye thawabu nyingi kuliko thawabu za kufunga,na kuswali na kutoa sadaka?ni kupatanisha baina ya watu,maana kukosekana maelewano kati ya watu ni jambo kubwa sana".[522] Bali katika kuonyesha umuhimu wa jambo hili Uislamu umeruhusu hata kutumia uongo inapo bidi ili kutafuta suluhu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Siuzingatii kuwa ni uongo mtu kusema maneno kwa ajili ya kutafuta suluhu,na katika vita,na mume katika kumridhisha mkewe,na mke katika kumridhisha mumewe".[523] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Haesabiwi kuwa ni muongo mwenye kusema uongo kwa ajili ya kusuluhisha baina ya watu".[524]
Umeamuru kuamrishana mema na kukatazana mabaya kwa kila njia kila mtu kulingana na uwezo wake,maana jambo hili nidio sababu ianyo wafanya watu wawe katika msitari ulio nyooka na kufuata sheria za Mwenyezi Mungu na kuacha makatazo yake.Kwahiyo jambo hili ndilo linalo hifadhi umma kutokuenea dhulma na ufisadi na kupoteza haki za watu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Yeyote miongoni mwenu atakaye ona uovu unafanyika basin a auondoe kwa mkono wake,na kama hakuweza basi kwa ulimi wake ,na kama hakuweza basi japo moyo wako(kwa kulichukia jambo lile) ,lakini huo ni udhaifu wa imani".[525] Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na wawepo katika nyinyi watu wanao ilingania kheri (Uislamu),na wanao amrisha memma na wakakataza maovu,na hao ndio watakao tengenekewa".[526] Na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kapiga mfano ambao kabainisha katika mfano huo athari zinazo weza kupatikana endapo watu wataacha kuamrishana mema na kukatazana maovu,akasema : " Mfano wa mtu aliye simama katika mipanga ya Mwenyezi Mungu,na mfano wa mwenye kuchupa mipaka yake ni kama mfano wa watu walio panda katika jahazi wakagawana kila watu wakawa na sehemu yao,baadhi yao wakawa chini na wengine wakawa juu,ikawa wale walioko chini wakihitaji maji inawalazimu wapande juu,hilo likawakera ,kisha wakashaurina kuwa ni bora nao watoboe sehemu yao ya chini ili wapate maji kwa urahisi pasina kuwasumbua walioko juu yao; Endapo walioko juu wakiwaacha watekeleze maamuzi yao ,basi wataangamia wote,na kama wakiwazuia watasalimika wote kwa pamoja".[527] Na Mwenyezi Mungu akabainisha adhabu inayo weza kuwapata watu endapo wataacha kuamrishana mema na kukatazana mabaya.Akasema Mwenyezi Mungu Mtufu: " Walilaaniwa wale walio kufuru miongoni mwa wana wa Israili kwa ulimi wa Daudi na wa Isa bin Maryam.Hayo ni kwa sababu waliasi na wakipindukia mipaka sana. Hawakuwa wenye kuzuiana (kukatazana) mambo mabaya waliyo kuwa wakiyafanya,uovu ulioje wa jambo hili walilokuwa wakilifanya".[528]
Lakini huku kuamrisha mema na kukataza mabaya kuna masharti yake na adabu zake:
- Mwenye kuamrisha anatakiwa awe na ujuzi wa kutosha juu ya jambo analo liamrisha ili asij kuwaharibia watu dini yao. Imepokewa kutoka kwa Sufyani bin Abdillah athaqafy kwamba amesema : Nilimuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakenikasema : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!nielezo jambo ambalo nitashikamana nalo liwe kama ngao yangu. Akanijibu akasema: " Muamini Mwenyezi Mungu kisha uwe na msimamo wa kweli katika hilo" nikamuuliza tena nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni jambo gani ambalo uanlihofia zaidi juu yangu? Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akashika ulimi wake kisha akasema: " Nakuhofia kitu hiki" yaani ulimi wako.
- Isiwe kukataza jambo hilo kunapelekea kupatikana jambo ambalo ni baya zaidi.
- Asiwe mwenye kukataza jambo Fulani yeye mwenyewe analifanya,au anaamrisha jambo wakati yeye halianyi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlio amini!mbona mnasema msiyo yatenda? Ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kusema msiyo yatenda".[529]
- Awe mpole katika kuamrisha kwake na kukataza kwake. Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hakika upole hauwi katika jambo lolote ila hulipamba,na haukosekani katika jambo ispokuwa hulifanya likaonekana ni baya".[530]
- Awe ni mwenye uwezo wa kuyavumilia maudhi na matatizo yatakayo mfika kutokana na kazi hiyo ya kuamrisha mema na kukataza mabaya.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na uamrishe mema na ukataze mabaya na usubiri juu ya yale yatakayo kusibu ,hakika hayo ni katika mambo yanayositahiki kuazimiwa ".[531]
Pia Uislamu umeamrisha kujipamba na tabia njema zilizo kuwa bora.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hakika muumini aliye mkamilifu wa imani ni yule mwenye tabia njema,tena ni mpole kwa watu wake".[532]
Ukaamrisha kuwatendea wema watu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "watendee wema wanao sitahiki na wasio sitahiki,kama ukiwapata wanao sitahiki kufanyiwa wema basi wema wako utakuwa umefika kwa walengwa,na kama watakuwa hawasitahiki basi wewe utakuwa miongoni mwa watenda wema" [533]yaani utakuwa hujapata hasara yoyote. Na akabainisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake Ujira mkubwa na malipo ayapatayo mtu mwenye tabia njema,akasema: "Hakika nimpendae zaidi miongoni mwenu,na atakaye kuwa karibu zaidi na mimi siku ya kiyama ni yule mwenye tabia njema,na hakika nimchukiae zaidi na atayekuwa mbali na mimi siku ya kiyama ni mtu mwenye maneno mengi na mwenye tabia ya kiburi".[534]
Ukaamrisha kupata uhakika wa jambo kabla ya kulisema. Akasema Mwenyezi Mngu Mtukufu: "Enyi mlio amini kama fasiki atakujieni na habari (yoyote ile msimkubalie tu) bali pelelezeni(kwanza),msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyo yatenda".[535]
Ukaamrisha kupeana nasaha na kushauriana. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Dini ni kupeana nasaha" Tukamuuliza kwa ajili ya nani ? Akasema : "Lwa jili ya Mweneyzi Mungu,na kitabu chake ,na Mtume wake,na viongozi wa kiislamu na watu wote".[536]
- Kupeana nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu: Inakuwa ni kwa kumuamini,kumuabudu Yeye peke yake,na kumtukuza kwa majina yake na sifa zake.
- Na kupeana nasaha kwa ajili ya kitabu chake:Inakuwa kwa kuitakidi kuwa kweli ni maneno ya Mwenyezi Mungu,ambayo kayateremsha kutoka kwake,na kwamba kitabu hiki ndio kitabu cha mwisho,na kuzifuata sheria zote zilizo kuja katika kitabu hiki,na kukifanya kuwa ndio muongozo wa kufuatwa..
- Na kupeana nasaha kwa ajili ya Mtume wake: Inakuwa kwa kumtii kwa yote aliyo yaamrisha,na kumsadikisha juu ya yote aliyo yaelelza,na kujitenga na yote aliyo yakataza,na kumpenda pamoja na kumheshimu,na kuzifuata suna zake na kuzieneza kwa watu.
- Kupeana nasaha kwa ajili ya viongozi wa kiislamu: Inakuwa kwa kuwatii muda wa kuwa hawajaamrisha jambo ambalo linakwenda kinyume na Dini,na kuwaongoza katika kheri pamoja na kuwasaidia katika kheri,na kuwanasihi kwa upole na kuwakumbusha wajibu wao kwa raia na kutowatangazia uasi.
- Na kupeana nasaha kwa ajili ya watu wote:Inakuwa ni kwa kuwaongoza katika mambo yaliyo na kheri kwao katika Dini yao na dunia yao,na kuwasaidia katika kutatua haja zao,na kuwaondolea adha,na kuwapendelea kheri na kuwatanguliza katika kheri,na kuwatendea yale anayopenda kutendewa.
Pia Uislamu umeamrisha ukarimu,maana hiyo ni sababu ya kupendwa na watu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Tabia za aina mbili Mwenyezi Mungu anazipenda;Tabia njema na ukarimu,na tabia za aina mbili Mwenyezi Mungu anazichukia;kuwa na tabia baya,na ubakhili,na pindi Mwenyezi Mungu akimtakia kheri mja wake ,basi humjaalia tabia ya kukidhi haja za watu".[537] Na kipimo sahihi cha ukarimu ni kauli ya Mwenyezi Mungu alipo sema : "Wala usifanye mkono wako (kama) ulio fungwa shingoni mwako,wala usiukunjue ovyo ovyo (moja kwa moja) utakuwa n mwenye kulaumiwa (ukifanya hivyo) ".[538] Yaani usitoe kupita kiasi wala usizuie kupita kiasi,bali kuwa kati kwa kati.
Umeamrisha kuwasitiri watu na kuwakidhia haja zao na kuwarahisishia mabo yao. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwenye kumtatulia Muislamu mwenzie tatizo miongoni mwa matatizo ya kidunia,basi Mwenyezi Mungu atamtatulia katika matatizo ya siku ya kiyama,na atakaye mrahisishia mtu aliye tingwa na jambo,basi nayeye Mwenyezi Mungu atamrahisishia mambo yake hapa duniani na akhera pia,na atakaye msitiri ndugu yake muislamu,basi nayeye Mwenyezi Mungu atamsitiri hapa duniani na akhera pia,na Mwenyezi Mungu anamsaidia mja muda wakuwa mja ni mwenye kumsaidia ndugu yake".[539]
Umeamrisha na kuhimiza sana kuwa na subira,sawa sawa iwe ni subira katika kutekeleza yale aliyo yaamrisha Mwenyezi Mungu au subira katika kujitenga na makatazo yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na kuwa na subira (ingoje )hukumu ya Mola wako,na hakika wewe uko mbele ya macho Yetu".[540] Au hata kama ni subira juu ya mambo aliyo yakadiria Mwenyezi Mungu,kama vile kuwa mvumilivu katika hali ya ufakiri,au njaa,au maradhi na mengineyo. Amesema Mwenyezi Mungu :" Na tutakutieni katika msukosuko wa (baadhi ya mabo haya);hofu na njaa na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wape habari njema wanao subiri.Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema,na ndio wenye kuongoka".[541]
Ukawaamrisha watu kuzuia hasira zao na kusamehe wakati mtu anapokuwa na uwezo wa kulipiza. Na hii yote ni kutaka kujenga moyo wa upendo katika jamii,na kuondoa chuki baina yao,na ukajaalia jambo hili lina malipo makubwa kabisa. Na ndio maana Mwenyezi Mungu amewasifu sana watu wenye tabia hii,akasema : " Na uendeeni upesi upesi msamaha wa Mola wenu na Pepo (yake) ambayo upana wake (tu)ni (sawa na ) mbingu na ardhi.(Pepo hii) wamewekewa wamchao Mwenyezi Mungu. Ambao hutoa katika (hali ya ) wasaa na katika (hali ya dhiki) na wazuiao ghadhabu (zao) na wanao samehe watu.Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsani".[542]
Ukaamrisha kuyakabili mabaya kwa mazuri kwa ajili ya kufuta chuki na tabia ya kulipiza visasi.Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ondosha (ubaya unao fanyiwa kwa wema) ;Tahamaki yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui atakuwa kama ni jamaa yako mwenye kukufia uchungu".[543]
Baadhi ya adabu za Kiislamu:-
Hakika sheria ya Kiislamu imekuja na adabu mbali mbali,ambazo imewahimiza waislamu kuzitekeleza kwa ajili ya kukamilisha Uislamu wao,miongoni mwa adabu hizo ni hizi zifuatazo:-
Adabu za chakula
1. Kusema Bismillahi (kutaja jina la Mwenyezi Mungu) kablaya kuanza kula,na kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kumaliza kula, ,na kula chakula kilicho kuelekea mbele yako, na kula kwa kutumia mkono wa kulia,maana mkono wa kushoto mara nyingi unatumiwa kwa ajili ya kujisafishia. Ametusimlia Swahaba mtukufu Umar bin abi salama akasema: Nilikuwa ni kijana anaye lelewa katika nyumba ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake,siku moja akaniona wakti wa kula mkono wangu unaruka huku na kule katika chakula,akasema kunambia: "Ewe kijana wangu! Utakapo kula anza kwa kusema Bismillahi,naule kwa mkono wako wa kulia,naule chaakula kilicho kuelekea mbele yako".[544]
2. Kutokukitoa kasoro chakula kwa hali yoyote kitakavyo kuwa,kutokana na hadithi aliyo ipokea abu hurayra –Mungu amuwie radhi- amesema :"Hakuwahi Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kukitoa kasoro chakula hata mara moja,bali alikuwa kikimfurahisha anakula na asipo kipenda anakiacha".[545]
3. Asipitilize kiwango katika kula au kunywa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri).Lakini msipite kiasi tu.Hakika Yeye Mwenyezi Mungu hawapendi wapitao kiasi (wapindukiao mipaka) ".[546] Na amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hajapata mwanaadamu kujaza chombo ambacho ni shari kwake kama tumbo lake,inamtosha mtu kula kiasi tu kitakachomuwezesha kuishi,na kama hana budi (yaani ni mpenda kula sana, basi aligawe tumbo lake sehemu tatu),theluthi kwa ajili ya chakula,na theluthi nyingine kwa ajili ya maji,na theluthi nyingine kwa ajili ya kupumua".[547]
4. Kutopumulia katika chombo au kupuliza wakati wa kunywa. Amesema Ibnu Abasi – Mungu awawie radhi- kwamba :((Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amekataza kupumulia katika chombo au kupuliza )yaani wakati wa kunywa.[548]
5. Asimuharibie mwenzie chakula au kinywaji.kama vile kunywea katika chombo kikubwa ambacho ndani yake mna kinywaji kingi na wengine wanahitajia.
6. Ale pamoja na wenzie na asile peke yake. Mtu mmoja alimuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: Kwanini sisi tunakula sana lakini hatushibi?! Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamuuliza: " Je mnapo kula mnakula pamoja au kila mtu anakula peke yake"? akasema : Bali kila mtu anakula peke yake. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia: "Jumuikeni pamoja katika chakulachenu ,na mtaje jina la Mola wenu,kwa kufanya hivyo mtazipata baraka za chakula".[549]
7. Atakaye karibishwa chakula kisha naye akafuatwa na mtu mwingine, basi amuombee idhini huyo aliye fuatana naye. Mtu mmoja katika Maanswari(watu wa Madina) alimkaribisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake pamoja na watu wengine watano,kisha mtu mwingine akawafuata,walipo fika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema:" huyu bwana katufuata,ukimruhusu kuingia basi aingie na kama hutamruhusu basi arejee" yule bwana akasema: Nimempa idhini ya kuingia.[550]
Adabu za kuomba idhini ya kuingia nyumbani kwa mtu.
Adabu hizi zimegawanyika mara mbili:-
- Kutaka idhini mtu akiwa nje. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Enyi mlio amini! Msiingie nyumba ambazo sio nyumba zenu mpaka muombe ruhusa (mpige hodi) na muwatolee salamu waliomo humo".[551]
- Kutaka idhini ndani ya nyumba. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Na watoto miongoni mwenu watakapo baleghe basi nawapige hodi kama walivyo piga hodi wale wa kabla yao".[552] Yote hii ni kwa ajili ya kuhifadhi siri zinazo kuwa ndani ya majumba na kusitiri baadhi ya mambo ambayo hayapaswi kujulikana na watu wengine.
- Kuto kulazimisha kuingia,yaani kupiga hodi mpaka ikawa kero kwa watu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "kuomba idhini (kupiga hodi ) ni mara tatu tu,kama ukiruhusiwa kuingia basi ingia,na kama hukuruhusiwa basi rudi".[553]
- Mwenye kupiga hodi ajitambulishe kwa jina lake akiwa bado yuko nje. Imepokewa kutoka kwa Jaabir – Mungu amuwie radh- amesema: Siku moja nilimuendea Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kutaka msaada kutokana na deni lililokuwa linamkabili baba yangu, nikagonga mlango, Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akauliza: "Wewe ni nani"? Nikasema: Ni mimi. Akasema: "Mimi?mimi?! "yaani kanakwamba Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alichukia kitendo hicho.[554]
Adabu za kutoa salamu.
Uislamu umehimiza watu kusalimiana ,kwasababu jambo hili linaleta mapenzi baina ya watu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake,hamtaingia Peponi mpaka muwe na imani,na hamtakuwa na imani mpaka mpendane.Je nikujulisheni jambo ambalo mkilifanya mtapendana? Toleaneni salamu baina yenu ".[555]
-Na ni wajibu kumjibu aliye kusalimia,maana Mwenyezi Mungu anasema: "Na mnapo amkiwa kwa maamkizi yoyote yale, basiitikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo,au rejesheni hayo hayo".[556]
Na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akabainisha haki za salamu ,akasema: " Aliyoko katika kipandwa anatakiwa amsalimie mwenye kutembea kwa miguu,na mwenye kutembea amsalimie aliye kaa,na wachache wawasalimie wengi".[557]
Adabu za vikao.
- Kutoa salamu kwa ulio wakuta wakati wa kuingia na wakati wa kutoka. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake:" Pindi mmoja wenu atakapo ingia katika kikao basi atoe salamu,endapo atataka kukaa basi akae na atakapo amka kuondoka basi ile salamu ya mwanzo haitoshelezi".[558]
- Kutoa nafasi kwa anaye kuja kukaa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:" Enyi mlio amini! Mnapo ambiwa (katika mikutano) wafanyie wasaa wenzenu katika (nafasi za) kukaa basi wafanyieni nafasi.Na Mwenyez Mungu atakufanyieni nafasi (duniani na akhera),na (hata ) ikisemwa: Simameni (ondokeni muwapishe wenzenu),basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua wale walio amini miongon mwenu,na walio pewa elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayo yatenda yote".[559]
- Kuto kumsimamisha mtu ili ukae katika nafasi yake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake :" Asimsimamishe mmoja wenu mtu katika nafasi yake ili akae yeye,lakini peaneni nafasi(sogeleaneni) ".[560]
- Kama mtu akinyanyuka katika nafasi yake kasha akarejea,basi yeye ana haki zaidi ya kukaa katika nafasi hiyo kuliko mtu mwingine. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Mwenye kusimama katika nafasi yake kisha akarudi basi ana haki nayo zaidi kuliko mwingine yeyote".[561]
- Kuto watenganisha watu walio kaa pamoja ila kwa idhini yao. Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake:" Si halali kwa mtu kuwatenganisha watu wawili walio kaa pamoja ila kwa idhini yao".[562]
- Kama wamekaa watatu basi wasinong`onezane wawili bila ya mwenzao kusikia. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Mtakapo kuwa watatu basi wasinongo`ne zane waili bila kumshirikisha wa tatu wao ,mpaka mtakapo changanyika na wengine,maana hilo litamtia simanzi".[563]
- Kikao kisitawaliwe na mazungumzo ya kipuuzi bila ya kumtaja Mwenyezi Mungu,au kuzungumza mambo yenye manufaa kwa jamii,katika mambo ya dini yao au dunia yao.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Watu wanapo kaa katika kikao chochote kisha wakanyanyuka bila ya kumtaja Mwenyezi Mungu katika kikao hicho,basi ni sawa na watu walio nyanyuka kutoka katika mzoga,na watakuwa na majuto juu ya kikao hicho siku ya kiyama ".[564]
Adabu za mikutano.
Uislamu ni dini ambayo inajali sana hisia za watu,hasa wanapokuwa wamekusanyika na kuchanganyika mahala Fulani. Hii yote ni kwa ajili ya kuwafnya watu wapende kuchangayika na ipatikane faida inayo tarajiwa katika mikutano. Na uislamu umejitahidi sana katika kuondoa na kuzuia kila kitu ambacho kinaweza kuwa ni sababu ya watu kuchukia mikutano na mchanganyiko, ndio maana Uislamu ukawaamrisha waislamu wawe wasafi kuanzia katika miili yao,wasiwe na harufu mbaya zitakazo wakera watu ,na mavazi yao pia yawe masafi. Pia Uislamu ukawafundisha waislamu adabu za mikutano, ukawaamrisha kumsikiza mzungumzaji na kuheshimu rai yake,na si ruhusa kumkatisha kabla hajamaliza kuzungumza. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akizungumza katika mkutano miongoni mwa mikutano ya waislamu,ambayo ni siku ya ijumaa,akasema: "Mwenye kuoga siku ya Ijumaa na akajipaka manukato mazuri kama atakuwa nayo,na akavaa nguo zake nzuri,kisha akaja msikitini,akawa hakuwa kanyaga kanyaga watu kwa kutaka akae nafasi ya mbele,kisha akaswali kiasi alivyo wezeshwa,kisha akakaa kimya baada ya kuingia imamu wake,mpaka akaswali ijumaa,basihiyo inakuwa kwake ni kafara ya makosa yake yaliyo patikana baina ya ijumaa hiyo na ijumaa iliyo tangulia".[565]
-Anatakiwa atakaye piga chafya amshukuru Mweyezi Mungu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Pindi atakapo piga chafya mmoja wenu,basi aseme:Alhamdu lilahi,na mwenzake aliye karibu naye amuombee dua kwa kusema: Mwenyezi Mungu akurehemu. Kisha nayeye amuombee kwa kusema: Mwenyezi Mungu akuongoze na akunyooshee mambo yako".[566] Na miongoni mwa adabu za kupiga chafya,nizile alizozieleza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Pindi atakapo piga chafya mmoja wenu basi na aweke mikono yake usoni mwake (ajistiri),na ainamishe sauti yake".[567]
-Mwenye kuijiwa na hali ya kupiga myayo anatakiwa kujizui kadiri ya uwezo wake,maana hiyo ni dalili ya uvivu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hakika Mwenyezi Mungu anapenda chafya na anachukia myayo,pindi mtu akipiga chafya na akamshukuru Mwenyezi Mungu basi inampasa kila aliye sikia amuombee dua,lakini kuoiga myayo kunatokana na shetani,basi na ajizui kadiri ya uwezo wake,maana anapofanya haaaaa,basi shetani humcheka".[568]
Adabu za mazungumzo.
-Kumsikiliza mwenye kuzungumza na kutokumkatisha wakati akiongea mpaka amalize. Maana Mtume (s.a.e)alipo taka kuwahutubia watu katika hija yake ya kuaga alimuamuru mmoja katika maswahaba wake akasema:" Wanyamazishe watu"[569]
- Kutumia ibara zilizo wazi ili msikilizaji apate kufahamu vizuri.Amesema Bibi Aisha Mke wa Mtume katika kuelezea uzungumzaji wake: " Alikuwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akiongea kwa kituo anayafahamu maneno yake kila anaye yasikia".[570]
-Anatakiwa mzungumzaji na msikilizaji wote wawe wachangamfu. Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Usije ukadharau wema hata Kama nidogo namna gani, japo kukutana na nduguyo kwa uso wa bashasha".[571]
-Kusema na watu kwa maneno mazuri. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Kila kiungo cha mwanadamu kinayo sadaka yake,kila siku inayo chomozewa na jua ukawafanyia uadilifu watu waili hiyo kwako inakuwa ni sadaka,na kumsaidia mtu katika yakipandwa chake,kwa kumpandisha au kumpandishia mzigo wake hiyo pia ni sadaka,na maneno mazuri pia ni sadaka,na kila hatua anayopiga kuelekea msikitini kwa ajili ya swala pia ni sadaka,na kuondoa maudhi njiani pia ni sadaka".[572]
Adabu za kuwatembelea wagonjwa.
Uislamu umehimiza sana kuwatembelea wagonjwa,na ukakifanya kitendo hicho ni miongoni mwa haki za lazima kwa kila muislamu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Haki za Muislamu juu ya ndugu yake muisilamu ni tano; Kuitikia salamu, kuwatembelea wagonjwa, kusindikiza jeneza, kuitikia wito pindi unapo itwa, na kumuombea dua mtu akipiga chafya kisha akamshukuru Mwenyezi Mungu".[573]
Na ili kuwahimiza watu kuwatembelea wagonjwa Uislamu umebainisha malipo makubwa anayo yapata mwenye kuwatembelea wagonjwa,akasema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwenye kumtembelea mgonjwa anakuwa ni mwenye kutembea katika viwanja vya Pepo".[574]
-Kuwaonyesh ahuruma na mapenzi wakati wa kuwatembelea. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Ukamilifu wa kumtembelea mgonjwa ni pamoja na kumshika kichwani au mkono na kumuuliza hali yake na maendeleo yake".[575]
- Kumuombea dua. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwenye kumtembelea mgonjwa ambaye ajali yake haijafika,kisha akamuombea dua hii mara saba: Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ,Bwana wa arshi tukufu akuponye,basi Mwenyezi Mungu humpa nafuu kutokana na maradhi yake".[576]
Adabu za mizaha na utani.
Hakika maisha katika uislamu sio kama wanavyo dhani baadhi ya watu kwamba hakuna nafasi ya kufanya utani na kucheza michezo iliyo halali. Anatusimlia swahaba mmoja aitwaye Handhwala anasema: Siku moja nilikutana na Abubakari ,akaniuliza ;Vipi hali yako ? Nikamwambia,mimi najiona nimekuwa mnafiki. Akashangaa sana na kusema: Subuhaana llah! Unasema nini ?! Nikasema: Tunapokuwa na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akitukumbusha Moto na Pepo, tunaathirika mpaka tunakuwa kama kwamba tunauona Moto na Pepo kwa macho yetu,lakini tunapo achana na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na tukachanganyika na wake zetu na watoto wetu,na tukashughulishwa na mambo ya kidunia tunasahau kila kitu!. Abubakari akamwambi: Wallahi sote hali hiyo inatukuta. Tukaondoka pamoja mpaka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, kisha nikasema mbele ya MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake: Hakika Handhwala kawa mnafiki ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akaniuliza kwa nini? nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika sisi tunapokuwa mbele yako ukitukumbusha kuhusu Pepo na Moto tunakuwa kama kwamba tunaviona kwa macho, lakini tunapoondoka tukaingia majumbani mwetu na kuchanganyika na wake zetu na watoto wetu tunayasahau mengi. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema : "Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, laiti mngekuwa mnadumu katika hali mnayo kuwa nayo pindi mnapo kuwa na mimi ,na hali mnayo kuwa nayo wakati mnapo kuwa katika kumtaja Mwenyezi Mungu,basi mngekuwa mnapeana mikono na Malaika katika vikao vyenu na njiani,lakini kila wakati na mambo yake,akalikariri neon hili mara tatu".[577]
Katika hadithi hii Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amebainisha kwamba michezo na utani na mizaha ambayo ni halali na kuipumzisha nafsi ni jambo ambalo linatakiwa. Na amewabainishia maswahaba wake adabu za mizaha, wakati walipo muuliza wakasema: Ewe Mtume wa Mungu! Kuna wakati tunakuona ukitutania! , Akasema: "Ndio,lakini hata hivyo sisemi ispokuwa la kweli".[578]
-Mizaha inakuwa kwa maneno na kwa vitendo pia. Na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuwa akiwatania maswahaba wake kwa vitendo. Imepokewa kutoka kwa Anasi bin Maaliki – Mungu amuwie radhi – kwamba mtu mmoja miongoni mwa mabedui,jina lake anaitwa Zahir,alikuwa akimletea zawadi Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kutoka shamba,kisha anapo takak kurudi na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake naye anamuandalia zawadi. Mpaka Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: "Hakika Zahir anatusaidia kwa vitu vya shamba nasisi tunamfaa kwa vitu vya mjini". Siku moja akiwa sokoni anauza vitu vyake Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alimtokea kwa nyuma bila yeye kumuona,kisha akamshika, yule bwana akawa anauliza,wewe ni nani?hebu niachie. Alipo euka akamkuta ni Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, akawa anamuegemea Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na Mtume akaanza kunadi: Nani atamnunua mtumwa huyu?! Zahir akamuuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: Yaani unaniona nina thamani ndogo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Mtume akamjibu akasema:Hapana bali wewe unathamani sana mbele ya Mwenyezi Mungu".[579]
-Mizaha isipelekee kumudhi mwislamu mwenzio au kumkosea adabu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Si halali kwa Muislamu kumtisha Muislamu wenzie".[580]
-Kufanya utani kusimpelekee kusema uongo ili kuwafurahisha watu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Adhabu kali itampata kila mwenye kusema uongo ili kuwachekesha watu,ole wake tena ole wake".[581]
Adabu za kumuhani aliye fiwa
Kitendo hiki kimeamrishwa ili kuwapunguzia huzuni wafiwa .amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Muumini yoyote atakaye muhani ndugu yake kutokana na msiba ulio mfika,bais Mwenyezi Mungu atambvisha vazi la karama siku ya kiyama".[582]
-Kuwaombea dua wafiwa na kuwausia kuwa na subira na kutaraji malipo kwa Mwenyezi Mungu. Imepokewa kutoka kwa Usama bin Zaid –Mungu amuwie radhi- amesema: Siku moja tulikuwa nyumbani kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake,mmoja kati ya mabinti zake akamtumia ujumbe anamuita kwamba mwanae yuko katika hali ya kufikwa na mauti. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia aliyetumwa kumuita kwamba:" Nenda ukamwambie kuwa Mwenyezi Mungu alitoa na sasa anatwaa,na kila kitu kwa Mwenyezi Mungu kina muda wake maalumu,na umuamrishe awe na subira". Yule mjumbe akarudi tena na kumwambia Mtume kuwa :Ameapa kwamba lazima uende.Hapo Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakeakanyanyuka pamoja na Saad bin ubaada na Muadhi bin Jabal na mimi nikaenda nao,tulipo fika akaletwa yule kijana hali yakuwa anaelekea kukata roho, MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yakeakatokwa na machozi,Saad akamuuliza kwa mshangao :Vipi unalia Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?! Mtume akamjibu akasema: Hii ni huruma ambayo Mwenyezi Mungu kaiweka katika nyoyo za waja wake,na hakika Mwenyezi Mungu huwarehemu waja wake wenye huruma".[583]
- Kumuombea msamaha maiti. Na ni vizuri kumuombea mfiwa dua hii: (Mwenyezi Mungu ayafanye makubwa malipo yako,na amsamehe maiti wako).
- Ni vizuri kuwatengenezea chakula wafiwa ,na sio wao wawaandalie chakula watu wanao kuja msibani,kufanya hivi ni kinyume.Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliesema wakati alipo kufa Jaafar bin Abii twaalib:" Waandalieni familia ya Jaafar chakula maana wamefikwa na jambo la kuwashughulisha,hawawezi hata kupika".[584]
Adabu za kulala.
Anatakiwa mtu anapo lala ataje jina la Mwenyezi Mungu (aseme: Bismillahi),kisha alalie ubavu wa kulia,na ahakikishe ktandani hakuna kitu chochote kinachoweza kumsababishia maudhi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Pindi mmoja wenu atakapo elekea kitandani kwake kwa ajili ya kulala,basi na akung`ute tandiko lake na ataje jina la Mwenyezi Mungu,maana mmoja wenu hajui nini kimetokea baada ya kuamka kwake,kisha alalie ubavu wa kulia na asome dua hii: " Umetakasika ewe Mola wangu,kwa uwezo wako sasa nauweka ubavu wangu,na kwa uwezo wako nitaunyanyua asubuhi,endapo utaichukua nafsi yangu basi nisamehe,na kama utairejesha basi nihifadhi pamoja na waja wako wema".[585]
-Na anapo amka anatakiwa aombe dua iliyopokelewa kwa MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake. Amesema Hudhayfatu –Mungu amuwie radhi- alikuwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anapo panda kitanda usiku husema: " Ewe Mola wangu kwa jina lako ninakufa na kwa jina lako ninahuika,".na akiamka husema : "Shukurani zote zinamsitahiki Mwenyezi Mungu ambaye katuhuisha baada ya kuwa alitufisha,na kwake tutafufuliwa".[586]
-Ajitahidi kulala mapema isipokuwa kama atakuwa na dharura ya kumchelewesha .imepokelewa kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuwa alikuwa anachukia kulala kabla ya kuswali swala ya Isha,na mazungumzo baada ya swala ya Isha".[587]
-Sio vizuri kulalia tumbo. Amepokea Abu hurayra –Mungu amuwie radhi-kwamba MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake alimkuta mtu mmoja akiwa amelala hali yakuwa kalalia tumbo,Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamtingisha kwa mguu wake,kisha akamwambia ulalaji huu haupendi Mwenyezi Mungu".[588]
- Kuchukua tahadhari kabla ya kulala kutokana na vitu vya hatari. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika huu Moto ni adui yenu,basi mkilala uzimeni".[589]
Adabu za kukidhi haja.
-Kuomba dua kabla ya kuingia chooni na baada ya kutoka. Amesimulia Anasi ibnu Maaliki anasema: Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuwa anapoingia chooni husema: " Kwa jina la Mwenyezi Mungu,ewe Mola wangu hakika mimi nataka hifadhi kwako kutokana na mashetani wa kike na wa kiume". na anapo toka husema: "Shukurani zote zinamsitahiki Mwenyezi Mungu ambaye kaniondolea udhia nilio kuwa nao na kunirejeshea afya".[590]
- Asielekee upande wa kibla wakati wa kukidhi haja wala asikipe mgongo.Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Hakika mimi kwenu nyinyi ni sawa na mzazi na watoto wake,asielekee mmoja wenu kibla wa asikipe mgongo wakati wa kukidhi haja,wala asiyumie chini ya madongo matatu" .[591] yaani katika kuchamba,kama hakupata maji.
-Wakati anapo kidhi haja awe sehemu ambayo haonekani na watu. Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Atakapo kidhi haja mmoja wenu basi ajisitiri..".[592]
-Asitumie mkono wa kulia wakati wa kujisafisha. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Pindi atakapo kunywa mmoja wenu ,basi asipumulie katika chombo,na atakapo kwenda chooni asiguse utupu wake kwa mkono wa kulia,na atakapo jisafisha asitumie mkono wa kulia".[593]
Adabu za kufanya tendo la ndoa na mke.
-Aanze kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake : " Laiti kama mmoja wenu anapotaka kukutana na mkewe anasema: Kwa jina la MwenyeziMungu,ewe Mola wetu tuepushe na shetani,pia ukiepushe na shetani kile utakacho turuzuku,basi wakijaaliwa kupata mtoto katika tendo lao hilo, hatadhuriwa na shetani".[594]
-Kufanya maandalizi pamoja na kuchezeana. Siku moja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alimuuliza Jaabir akasema: " Umeoa ewe Jaabir? Jaabir akasema : Ndio, akamuuliza tena : Je umeoa bikra au alikwisha olewa kabla? Akasema:Alikwisha olewa. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia: Mbona hukuoa bikra ambaye utacheza nae nayeye akakuchezea, ukamchekesha nayeye akakuchekesha".[595]
-Kuonyeshana mapenzi, ikiwa ni pamoja na kupeana busu na mambo mengine..Amesimlia Bibi Aisha mke wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikuwa akimbusu hata anapokuwa amefunga...".[596]
-Kila mmoja amridhishe na kumfurahisha mwenzie kwa kila njia,lakini kwa sharti alili libainisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kumwambia Umar-Mungu amuwie radhi- wakati alipo kuja kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: Hakika mimi nimeangamia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akamuuliza ni kipi kilicho kuangamiza? Akasema: Usiku wa leo nimemuingilia mke wangu mbele lakini kwa kupitia nyuma! MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake hakumjibu chochote, akakaa kimya, kisha akateremshiwa ufunuo, ambayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Wake zenu ni kama maashamba yenu,basi yaendeeni mashamba yenu mpendavyo". Ukipitia mbele au nyuma ni sawa,ispokuwa huruhusiwi kuingia sehemu ya haja kubwa,na kumingilia mwanamke wakati wa hedhi.[597]
-Kuhifadhi siri zinazo husiana na mambo ya kitandani.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika miongoni mwa watu watakao kuwa na mafikio mabaya kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya kiyama,ni mtu ambaye anakutana na mkewe kisha anatoa siri zinazo husiana na mambo yao ya ndani".[598]
Adabu za safari.
- Aurejeshe haki za watu kabla ya kusafiri,na kama anadaiwa basi alipe deni lake kwanza,na kuwaachia familia yake matumizi yao.Amesema mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Mtu yoyote ambaye kamdhulumu ndugu yake kitu chochote basin a akirejeshe mapema,kabla haijafika siku ambayo hakutakuwa kulipana dinari wal dirhau, kabla haiafika siku ambayo yatachukuliwa mema yake apewe anaye mdai,na kama hatakuwa na mema ya kuwalipa basiyatachukuliwa madhambi yao abebeshwe yeye kisha atupwe Motoni".[599]
- Asipendelee kusafiri peke yake, maana Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kakataza jambo hilo. Ispokuwa kama atakuwa kalazimika kufanya hivyo.
- Kama atasafiri na wenzie basi achague watu ambao ni wenye tabia njema, na wamchague kiongozi katika msafara wao. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Pindi watakapo safari watu kuanzia watatu ,basi wamchague mmoja wao awe ni kiongozi wa msafara".[600]
- Atakapo taka kurejea basi awataarifu familia yake muda wa kufika kwake,maana huu ulikuwa ndio mwenendo wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na asiingie nyumbani kwake usiku. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Pindi mmoja wenu akisafiri mda mrefu, basi siku ya kurejea asiingie nyumbani kwake usiku".[601]
- Anapo safiri awaage rafiki zake na jamaa zake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Pindi mmoja wenu atakapo taka kusafiri,basi awaage ndugu zake maana watamuombea dua, pamoja na dua yake yeye,inakuwa ni kheri juu ya kheri".[602]
- Afanye haraka kurudi mara tu amalizapo haja zake zilizo mpeleka. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Safari ni kipande cha adhabu,maana inamnyima mmoja wenu kula vizuri na kunywa vizuri na kupata usingizi mzuri,basi pindi mtu amalizapo haja zake arejee upesi kwa watu wake".[603]
Adabu za njia.
Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alibainisha adabu za njia,alipo sema: "Jiepusheni na kukaa sehemu za njia". Maswahaba wakasema:Hizi nisehemu ambazo tumezoea kukaa kwa ajili ya mazungumzo na kubadilishana mawazo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.Akasema: "Kama hamna budi kukaa sehemu hizo basi ipeni njia haki zake", wakamuuliza: Ni zipi haki za njia ewe mtume wa Mungu? akasema: "Ni kuinamisha macho,na kuondoa maudhi njiani, na kuitikia salamu ,na kuamrisha mema na kukataza mabaya".[604] Na katika mapokezi mengine zikatajwa pia katika haki za njia ni pamoja na (kuwasaidia wenye matatizo, na kuwaelekeza walio potea njia).[605]
-Achunge adabu za njia na asiharibu manufaa yanayo wahusu watu wote. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Jiepusheni na watu waiwili wenye kulaaniwa" wakamuuliza ni nani hao ?akasema: "Mwenye kujisaidia njiani,au kwenye vivuli wanavyo kaa watu".[606]
Adabu za kuuza na kununua.
Asili katika biashara ni halali,maana makusudio yake ni kubadilishana manufaa,baina ya muuzaji na mnunuzi,lakini pindi yanapo patikana madhara kwa mmoja wao au kwao wote basi wakati huo inatoka katika hukumu ya uhalali na inakuwa ni haramu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Enyi mlio amini! Msiliane mali zenu kwa njia za batili".[607]
Na Uislamu umejaalia chumo litokanalo na biashara ni miongoni mwa machumo yaliyo bora. Maswahaba wali muuliza Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuhusu chumo lililo bora zaidi,akasema: " Ni lile alipatalo mtu kutoka na kazi ya mikono yake,na kila biashara iliyo kuwa nzuri".[608]
Uislamu umehimiza sana juu ya uaminifu katika biashara. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mfanya biashara ambaye ni muislamu,mkweli ,muaminifu,atakuwa pamoja na mashahidi sik ya kiyama".[609]
-Kama bidhaa yake inakasoro ambazo mteja hawezi kuzijua basi anatakiwa azibainishe. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " si halali kwa mtu kuuza kitu chenye kasoro ila baada ya kuibainisha".[610]
-Asimfanyie udanyifu mnunuzi na kumtapeli. Siku moja Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipita kwa mtu anauza unga,akaingiza mkono wake ndani ya ule unga akagundua kuwa ulioko chini umelowa,akamu uliza: "Ni kitu gani hiki ewe muuzaji"? yule bwana ajasema: Umenyeshewa na mvua ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: "Kwanini basi hukuuweka juu ili wanunuzi wakaona? mwenye kutuhadaa sio miongoni mwetu".[611]
Awe mkweli katika biashara yake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Wenye kuuziana wawili kila mmoja kati yao anayo khiyari,muda wa kuwa hawajaachana ,ikiwa watakuwa wakweli na kila mmoja akabainisha kasoro ya bidhaa yake,basi Mwenyezi Mungu huwatilia baraka katika biashara yao,na ikiwa wataficha na wakasema uongo,basi Mwenyezi Mungu huondoa baraka katika biashara yao".[612]
-Ukarimu na upole katika biashara ,na kutokuwa na moyo wa tamaa bila kujali ubinadamu,maana hiyo ndiyo njia ya kujenga mapenzi baina ya watu. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: " Mwenyezi Mungu amemrehemu mja ambaye ni mkarimu pindi anapo uza, na ni mkarimu anapo nunua, na ni mkarimu pia anapo lipa".[613]
Kuto kuapa apa katika biashara.Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: ' Jiepusheni na kuapa apa sana katika biashara,maana kufanya hivyo kunaondoa baraka katika biashara".[614]
-Pia Uislamu umehimiza sana kuwa na moyo wa kusamehe endapo mtu atanunua bidhaa kisha akaomba kuirejesha kutokana na dharura ambayo iko nje ya uwezo wake. Amesema MtumeRehma na amani za Allah ziwe juu yake : "Ataye msamehe ndugu yake aliye kuja kumuomba arejeshe bidhaa baada ya kuwa wamekwisha uziana,basi Mwenyezi Mungu atamsamehe makosa yake siku ya kiyama".[615]
Hizi ni baadhi tu katika adabu mbali mbali za Uislamu,,lakini kuna adabu nyingi sana ambazo laiti kama tutataka kuzitaja zote hatuwezi kumaliza,bali inatosha tu kutambua kwamba hakuna jambo lolote linalo husiana na maisha ya watu ,eidha mtu mmoja mmoja au jamii ispokuwa kuna muongozo juu ya jambo hilo nadani ya Qur-ani tukufu au katika mafundisho ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake. Na hi yote ni kutaka kuyafanya maisha ya Muislamu yawe ni ibada,yaani muda wote awe anachuma thawabu nakujiongezea katika mizani ya mema yake .
HITIMISHO:
Napenda kuhitimisha kitabu changu hiki kwa kunukuu maneno ya watu wawili,miongoni mwa watu walio ingia katika Uislamu.
Amesema (F.Filweas)[616]: (( Kuna mapungufu makubwa sana upande wa kiroho katika nchi za kimagharibi,haijaweza kanuni yoyote miongoni mwa kanuni zinazo tungwa ,wala itikadi yoyote miongoni mwa itikadi walizo nazo,haijaweza kuziba mwanya huo,na kumletea mtu anaye ishi katika nchi hizo furaha na amani ndaniya nafsi yake,pamoja na utajiri mkubwa walio nao,na uwezo mkubwa wa kitekinolojia…na pamoja na kuwatimizia wananchi wao mahitaji yao muhimu yote,lakini mwanadamu anaye ishi katika nchi hizo bado anahisi kuwa kuna mapungufu makubwa katika maisha yake,na anajikuta mbele yake kuna maswali mengi kama haya: Kwanini naishi? Je ninaelekea wapi ? Na ni kwa nini? Na mpaka sasa hakuna yeyote ambaye amekwisha weza kutoa jibu sahihi la maswali haya. Lakini hakujua masikinikwamba dawa ya matatizo yote hayo ipo katika Dini iliyo sawa sawa,ambayo wao hawajui chochote juu ya dini hiyo ispokuwa upotoshaji tuwanao usikia. Lakini hata hivyo nuru imeanza kuchomoza,na asubuhi imeanza kupambazuka,kwa kusilimu baadhi ya watu katika nchi hizo japo ni wachache.Na wameanza kuonekana baadhi ya watu miongoni mwao wake kwa waume wakifuata mafundisho ya Uislamu katika maisha yao. Na kila siku watu wanaingia katika Dini ya haki,na huu ni mwanzo mzuri…)). Mwisho wa kunukuu.
Mwingine ni (D.potter)[617] anasema: (( …Uislamu ambao ni kanuni ya Mwenyezi Mungu,ni Dini ambayo tunauona ukweli wake wazi wazi hata katika mazingira yanayo tuzunguka, uataona milima ,bahari sayari,nyota vyote hivi vinatembea kwa sawaswa kwa amri ya Mwenyezi Mungu tu. Vyote vimetii na kunyenyekea amri ya Mungu muumbaji wake, kila kitu katika ulimwengu huu-hata vitu visivyo kuwa na roho-navyo pia vimejisalimisha na kunyenyekea amri ya muumba,lakini mwanadamu yeye ametolewa katika hukumu hii,maana Mwenyezi Mungu amemepa uhuru wa kuchagua na kuamua,anayo haki ya kujisalimisha katika amri za Mwenyezi Mungu,au kujiwekea kanuni zake mwenyewe,na kufuata muongozo autakao yeye. Lakinikwa bahati mbaya mara nyingi mwanadamu amechagua njia tofauti na njia ya aliyo itaka muumba wake…Hakika watu huko Ulaya na America hivi sasa wanaingia katika Uislamu makundi kwa makundi kwa sababu wana kiu kubwa ya kupata utulivu wa nafsi na utulivu wa kiroho,bali hata kundi kubwa la watu waliokuwa wamejitolea kufanya kazi ya kuuzima Uislamu na kuzidhihirisha kasoro zake kama wanavyo dai wao, pia wamejikuta wakivutiwa na Dini hii na hatimae kusilimu. Hii ni kwa sababu haki siku zote iko wazi wala hakuna namna ya kuweza kuikanusha).
[1] Al imran: 64
[2] Al aaraf :33
[3] Annahli :43
[4] Swahihul bukhari juzu ya 1 uk.50 hadithi no: 100
[5] Al muuminun: 12-14
[6] Al israa : 70
[7] Al jaathiya: 12-13
[8] Adh-dhariyaat : 56-58
[9] Al ikhlaas :1-4
[10] Al hadyd :3
[11] Al-raad:28
[12] Annahl:97
[13] Twaha :124-126
[14] Al maaidah :3
[15] Al imraan : 85
[16] Al hujraat :13
[17] Al mujaadila :11
[18] Al-imraan :185
[19] Yaasyn :78-82
[20] Al kahf :107
[21] Al bayinah 6-8
[22] Huyu alikuwa ni askari wa kimarekani wa kikosi cha majini,alishiriki katika vita ya kwanza ya dunia na ya pili,alikulia katika mazingira ya kikristo,na zikamuingia sana itikadi na desturi za kikristo,hata hivo alislimu baada ya kuisoma qur-ani tukufu.
[23] Annahl :125
[24] Huyu ni mtafiti mwenye asili ya Ufaransa,na ni mwalimu katika chuo cha Kiislamu Paris. Kanukuu katika kitabu kiitwacho:"Wasemavyo juu ya Uislamu," cha Dr.Imadi Kahalil.
[25] Albaqara :170
[26] Swahihul-bukhari,juzuu ya 5,ukurasa 2247,hadithi nambari 5696
[27] Al-israa :33
[28] Annisaa :29
[29] Al-israa :32
[30] Al-baqara :188
[31] Al-maida :90-91
[32] Al-baqara :205
[33] Al-israa :23
[34] Adhuhaa :9
[35] Al-israa :34
[36] Al-an`aam :151
[37] Swahihul bukhari,juzu ya 3 ukurasa 1109,hadithi nambari 2881
[38] Swahihu ibnu hibaany,juzu ya 2,ukurasa 203,hadithi nambari 458
[39] Adhuha :10
[40] Swahihu Muslim,juzu ya 4 ukurasa 1996,hadithi nambari 2580
[41]Albaqara :256
[42] Annahl :125
[43] Annisaa :145
[44] Al-aaraf :54
[45] Al-mu`minun :91
[46] A-anbiyaa ;25
[47] Al-aaraf :180
[48] Ash-shuura :11
[49] Angalia: Ighaathatul-lahfaan,juzu ya 2 ukurasa 120
[50] Annaaziat : 5
[51] Adh`ariyaat :4
[52] Swahihu Muslim,juzu ya 4,ukurasa 2294,hadithi nambari 2996
[53] Maryam : 17-19
[54] Swahihul-bukhari, juzu ya 4 ukurasa 1840,hadithi nambari 4575
[55] Faatwir : 1
[56] Al-anbiyaa : 20
[57] Annisaa : 172
[58] Ash-shuaraa :193-195
[59] Annahl :50
[60] Al-anbiyaa : 26-27
[61] Al-imraan : 80
[62] Ash-shuaraa :193-194
[63] Albaqara :98
[64] As-sajda :11
[65] Al-muuminun :101
[66] Az-zukhruf : 77
[67] Al`lail :17-18
[68] Qaf :17-18
[69] Al-hadyd ;25
[70] Annajm :36-41
[71] Almaida : 44
[72] Al-fat-h :29
[73] Al maida :45
[74] Annisaa :163
[75] Al maida :46
[76] Al aaraf :156-157
[77] Attawba :111
[78] Ash-shu`araa :193-195
[79] Al maida ;48
[80] Al maida : 3
[81] Ibrahim : 1
[82] Mathayo :15:24
[83] Sunanu tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 175,hadithi nambari 2910
[84] Huyu ni mtafiti mkubwa mwenye jinsia ya kifaransa,na ni mwalimu katika chuo cha kiislamu huko Paris.Kanukuu kutoka katika kitabu kiitwacho: wasemavyo juuya uislamu
[85] Alhijri :9
[86] Al baqara :75
[87] Al maida :14-15
[88] At tawba 30
[89] Al-ikhlas :1-4
[90] Uislamu na Ukristo/aziz assamad
[91] Al-anbiyaa :25
[92] Al-an`am :48-49
[93] Al mu`min : 78
[94] Al-anbiyaa: 7-8
[95] Alkahf :110
[96] Al maida:75
[97] Al-aaraf: 188
[98] Ar-ra`d:38
[99] Annisaa : 150-151
[100] Al-an`aam :83-86
[101] Aal- imraan ;33
[102] Hud :50
[103] Hud : 61
[104] Hud 84
[105] Al-anbiyaa :85
[106] Al ahzab :40
[107] Al-ahzab:7
[108] Ar-rahman: 26-27
[109] Az-zumar: 68
[110] Al-mu`min:45-46
[111] Taghaabun:7
[112] Al-hajj: 5-7
[113] Al-ahqaf :33
[114] Az-zumar:42
[115] Yasyn :78-79
[116] Al-kahf :47-48
[117] Fuswilat :20-22
[118] As-swaafaat :24
[119] Maryam:71-72
[120] Al-anbiyaa:47
[121] Inshiqaaq :7-12
[122] Albayina: 7-8
[123] Al qamar :49
[124] Sunanu Tirmidhy,juzu ya 4 ukurasa 451,hadithi nambari 2144
[125] Al-mustadraku alas-swahihain,juzu ya 4,ukurasa 221,hadithi nambari 7431
[126] Al hadyd :22-23
[127] Swahihu Muslim juzu ya 4,ukurasa 2052,hadithi nambari 2664
[128] Swahihu ibnu Hiban juzu ya 2,ukurasa 510,hadithi nambari 731
[129] Al-ankabut :45
[130] At-tawba:10 3
[131] Albaqara:183
[132] Swahihul-bukhari juzu ya 5,ukurasa wa 2251,hadithi nambari:5710
[133] Al baqara :179
[134] Adh-dhaariyaat"56
[135] Al-anbiyaa: 25
[136] Al hujuraat:15
[137] As-swaafaat: 35
[138] Luqman:22
[139] Alfat-h:11
[140] Albayina:5
[141] At-tawba :24
[142] Al hashri : 7
[143] An-nisaa:80
[144] A-ahzaab:40
[145] Annajm:3-4
[146] Swahihul bukhari juzu ya 6 ukurasa 2555,hadithi nambari 6566
[147] Sabai :28
[148] Al-imraan:31
[149] Sunanu Tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 11,hadithi nambari 2616
[150] Al-bayina:5
[151] At-tawba: 60
[152] At-taghaabun:16
[153] Al-imraan: 180
[154] Swahihu Muslim juzu ya 2 ukurasa 680,hadithi nambari 987
[155] Albqara :183
[156] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 673,hadithi nambari 1804
[157] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa wa 673,hadithi nambari 1805
[158] Al-imran;97
[159] Swahihul bukhari juzu ya 3 ukurasa 1300,hadithi nambari 3342
[160] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 875,hadithi nambari 2344
[161] Ash-shura :13
[162] Almaida:48
[163] Al hijri:9
[164] Al-ahzab:40
[165] An-nisaa:50-51
[166] Al-maida:3
[167] Aal imraan:110
[168] Saba`I :28
[169] Al`aaraf:59
[170] Al`aaraf:65
[171] Al`aaraf:73
[172] Al`aaraf:80
[173] Al`aaraf:85
[174] Al`aaraf:103
[175] As-swaf: 6
[176] Albaqara:143
[177] Al maida :50
[178] Swahihu muslim juzu ya 3,ukurasa 1315 ,hadithi nambari 1688
[179] Swahihul bukhari juzu ya 4,ukurasa 1919 hadithi nambari 4739
[180] Sunanu Tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 175 hadithi nambari 2910
[181] An-nisaa:1
[182] Musnad Ahmad,juzu ya 2, ukurasa 361,hadithi nambari:8721
[183] Yunus: 19
[184] Alhujurat :13
[185] Sunanu abi daud juzu ya 4,ukurasa: 124 hadithi nambari: 4344
[186] An nisaa:32
[187] Sunanu ibnu maja juzu ya 1 ukurasa 81 hadithi nambari 224
[188] Al mulku: 15
[189] Musnad ahmad juzu ya 1 ukurasa wa 6 hadithi nambari 21
[190] Swahihul bukhari,juzu ya 5 ukurasa 2382,hadithi nambari 6131
[191] Az-zumar:3
[192] Al-a`raf:194
[193] An-nisaa:110
[194] Attauba: 31
[195] Sunanut-tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 278 hadithi nambari 3095
[196] Ash-shuura: 38
[197] Aal imran: 159
[198] Annisaa:36
[199] Swahihu Muslim juzu ya 4 ukurasa 1986 hadithi nambari:2564
[200] Swahihul bukhari juzu 1 kurasa wa 14 hadithi nambari:13
[201] Al-muujamus-swaghir,juzu ya 1 ukurasa 250,hadithi nambari:409
[202] Swahihu ibnu hiban juzu ya 13 ukurasa 214 hadithi nambari :5894
[203] Swahihu Muslim juzu ya 3 ukurasa 1550 hadithi nambari :1958
[204] Swahihu bin khuzayma ,juzu ya 4,ukurasa 143 hadithi nambari 2545
[205] Swahihul-bukhari ,juzu ya 1 ukurasa 182 hadithi nambari: 467
[206] Al-mustadraku alas-swahihain,juzu ya 4 ukurasa 175 hadithi nambari: 7274
[207] Swahihul bukhaari juzu ya 3 ukurasa 1284 hadithi nambari:3295
[208] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 870,hadithi nambari: 2334
[209] Al-israa:70
[210] Sunanu abidawud juzu ya 4 ukurasa 276, hadithi nambari:4904
[211] Al mustadraku alas2wahihayn,juzu ya 4 ukurasa 150,hadithi nambari:7188
[212] Al-jumua:9
[213] Al-jumua:10
[214] Annur: 37
[215] Zilzala:7-8
[216] Al-a1raf:32
[217] Al baqara:222
[218] Swahihu Muslimu juzu ya 1 ukurasa wa 204,hadithi nambari: 224
[219] Almaida :6
[220] Sunanu tirmidhy juzu ya 4 ukurasa 281, hadithi nambari:1846
[221] Swahihu Muslim ,juzu ya 1 ukurasa 220,hadithi nambari: 252
[222] Swahihul bukhari,juzu ya 5 ukurasa 2320,hadithi nambari:5939
[223] Albaqara:172
[224] Al-a`raf:31
[225] Swahihu ibnu hiban juzu ya 12 ukurasa 41 hadithi nambari;4236
[226] Albaqara:173
[227] Almaida:90-91
[228] Almustadraku alas-swahihayni,juzu ya 3 ukurasa 511 hadithi nambari:5903
[229] Swahihu ibnu hibani juzu ya 10 ukurasa 545 hadithi nambari:4691
[230] Sunanu abu dawud juzu ya 4 ukurasa 7,hadithi nambari; 3874
[231] Ar-raad:28
[232] Swahihulbukhari juzu ya 5 ukurasa wa 1949,hadithi nambari:4776
[233] Az-zumar:9
[234] Albaqara:67
[235] Twaha:114
[236] Musnadi Ahmad,juzu ya 5 ukurasa 323 hadithi nambari:22807
[237] Sunanu tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 50, hadithi nambari:2685
[238] Sunanu tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 29,hadithi nambari:2647
[239] Almustadraku alaswahihaynii juzu ya 1 ukurasa 165 hadithi nambari: 299
[240] Faatwir:27-28
[241] Twaha: 7
[242] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 27 hadithi nambari:50
[243] Al-hadyd:4
[244] Qaf:16
[245] Annisaa:87
[246] Al-an`aam;164
[247] Zilzala:7-8
[248] At-tawba;24
[249] Al-an`am:160
[250] Swahihul bukhari juzu ya 6 ukurasa 2724 hadithi nambari:7062
[251] Swahihulbukhari juzu yz 1 ukurasa wa 30,hadithi nambari:55
[252] Swahihu muslim juzu ya 2 ukurasa 697, hadithi nambari:1006
[253] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2241 hadithi nambari;5676
[254] Al-furqaan:70
[255] Az-zumar:53
[256] Annisaa:110
[257] Al-qasas; 53-54
[258] Swahihu muslim juzu ya 1 ukurasa 112,hadithi nambari:121
[259] Swahihu Muslim,juzu ya 3 ukurasa 1255,hadithi nambari: 1631
[260] Swahihu Muslimu juzu ya 4 ukurasa 2060,hadithi nambari: 2674
[261] Aljaathiya:3-5
[262] Albaqara:170
[263] Ar-rum:30
[264] Musnad Ahmad,juzu ya 12 ukurasa wa 413 hadithi nambari:7445
[265] Al-an`am:161
[266] Al-furqaan:3
[267] Al-an`am:17
[268] Al-a`raf:188
[269] Aal-imran:145
[270] Yunus:49
[271] Aljumua:8
[272] Hud:6
[273] Alhadyd: 22-23
[274] Al-mustadraku alaswahihayni,juzu ya 3 ukurasa 623 hadithi nambari:6303
[275] Al- baqara:143
[276] Swahihu Muslim juzu ya 2 ukurasa 1104, hadithi nambari:1478
[277] Swahihul bukhari ,hadithi nambari:6024
[278] Swahihu Muslimu juzu ya 4 ,ukurasa 1830, hadthi nambari:1337
[279] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 684 hadithi nambari:1834
[280] Al-imran:97
[281] Albaqara:173
[282] Annisaa:150
[283] Al-an`am:108
[284] Annahli:125
[285] Swahihu ibnu hibani juzu ya 11 ukurasa 203 hadithi nambari:4862
[286] Albaqara:108
[287] Albaqara:194
[288] Al-anfal:61
[289] Muhamad:35
[290] Albaqara:256
[291] Alkahf:29
[292] Yunus:99
[293] Tafsir Attwabari juzu ya 3 ukurasa:226
[294] Swahihu Muslim juzu ya 2 ukurasa 1147, hadithi nambari:1509
[295] Muhamad:4
[296] Annisaa:92
[297] Almaida 89
[298] Almujaadila:3
[299] Swahihu muslimu juzu ya 2 ukurasa 782,hadithi nambari:1111
[300] Swahihu muslimu juzu ya 3 ukurasa 1278 hadithi nambari:1657
[301] Annuur:33
[302] At-tawba:60
[303] Alnahl:89
[304] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 223,hadithi nambari:262
[305] Swahihu ibnu hiban juzu ya 9,ukurasa 483,hadithi nambari:4176
[306] Annisaa: 1
[307] Sunanu abidawud juzu ya 1 ukurasa 61, hadithi nambari:236
[308] Annuur:4
[309] Annisaa:7
[310] Albaqara:267
[311] Sunanu ibnu majah juzu ya 1 ukurasa 81,hadithi nambari:224
[312] Sunanu abi dawud juzu ya 4 ukurasa 338,hadithi nambari:5147
[313] Luqman:13
[314] Almaaun:4-7
[315] Luqman:18-19
[316] Swahihu muslim juzu ya 1 ukurasa 93,hadithi nambari:91
[317] Sunanu abi dawud juzu ya 4 ukurasa 276,hadithi nambari :4903
[318] Almaida:6
[319] Rew.G.Margoliouth:In Introduction to the Koran.By Rev.J.M.Rodwell.
London 1918
[320] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2238,hadithi nambari:5665
[321] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 14 hadithi nambari:13
[322] Swahiul bukhari juzu ya 2 ukurasa 863,hadithi nambari:2314
[323] Sunanu Abi dawud juzu ya 4 ukurasa 271, hadithi nambari:4884
[324] Sunanu abi daawud juzu ya 3 ukurasa 114,hadithi nambari:2870
[325] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 435,hadithi nambari:1233
[326] Annisaa:12
[327] Albaqara"178
[328] Albaqara"178
[329] Almaida:38
[330] Annur:2
[331] Annur:4
[332] Ash-shuura:40
[333] Annahl:126
[334] Ash-shuura:40
[335] Albaqara:179
[336] Aal imran:105
[337] Al-an`am:159
[338] Al-anfaal:46
[339] Az-zumar:3
[340] Hud:96
[341] As-saf:6
[342] Al-a`raf:65
[343] Al-israa:88
[344] Hud:13
[345] Albaqara:23
[346] Swahihu Muslimu
[347] Almaida:50
[348] Swahihul bukhari juzu ya 6 ukurasa 2614,hadithi nambari:6731
[349] Almustadraku als-swahihayn juzu ya 4 ukurasa 104,hadithi nambari :7024
[350] Al-ahzab:36
[351] An-nur:51
[352] Swahihul bukhari juzu ya 3 ukurasa 1469, hadithi nambari:1839
[353] Ash-shura:38
[354] Aal-imraan:159
[355] Sunanut-tirmidhy juzu ya 4 ukurasa 213,hadithi nambari:1714
[356] Albaqara:190
[357] Al-anfal:39
[358] An-nisaa:75
[359] Al-anfal:72
[360] Al-anfal:47
[361] Swahiul bukhari juzu ya 3 ukurasa 1034, hadithi nambari:2655
[362] Swahihu muslimu juzu ya 3 ukurasa 1357, hadithi nambari:1731
[363] At-twabari juzu ya 3,ukurasa 226
[364] Ad-dahri:8-9
[365] Swahihul bukhari juzu ya 3 ukurasa 1109,hadithi nambari:2881
[366] Muhamad:4
[367] Taarikhul balaadhri
[368] Alkharaj cha abu yusufu:126
[369] Rejea kitabu:uwiano kati ya dini mbali mbli,cha Dr.Ahmad shalaby,juzu ya 3 ukurasa:174.Kanukuu toka katika kitabu: Islam and the modern age,ukurasa:67
[370] Almumtahina:8
[371] Sunanu abi dawud juzu ya 3 ukurasa 170, hadithi nambari:3052
[372] Al-kahf;46
[373] Albaqara:188
[374] Al baqara:278-279
[375] Musnadu abuu yaala juzu ya 8 ukurasa 443,hadithi nambari:5030
[376] Shuabul-iman juzu ya 7 ukurasa 105, hadithi nambari:69
[377] Albaqara :280
[378] Sunanu ibnu majah juzu ya 2 ukurasa 808,hadithi nambari:2418
[379] Albaqara:280
[380] Sunanul bayhaqy alkubra,juzu ya5 ukurasa 356,hadithi nambari: 10756
[381] Swahihu muslimu juzu ya 3 ukurasa 1227,hadithinambari:1605
[382] At-tawba:34
[383] Al mutwafifina :1-3
[384] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 834,hadithi nambari:2240
[385] Musnadu Ahmad juzu ya 5 ukurasa 364,haithi nambari:23132
[386] Sunanu abi dawud juzu ya 3 ukurasa 114,hadithi nambari :2870
[387] Swahihu muslimu juzu ya 3 ukurasa 1255,hadithi nambari:1631
[388] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 435,hadithi nambari:1233
[389] Annisaa:29
[390] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 122, hadithinambari :137
[391] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 77,hadithi nambari:57
[392] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 99,hadithi nambari :101
[393] Albaqara:188
[394] Swahihu ibnu hiban juzu ya 11 ukurasa 467,hadithi nambari :5976
[395] Swahihu muslimu juzu ya 2 ukurasa 1032,hadithi nambari:1412
[396] Annisaa:59
[397] Twaha:44
[398] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 74,hadithi nambari:55
[399] Swahihu muslimu juzu ya 3 ukurasa 1480,hadithi nambari:1852
[400] Sunanut-tirmidhy juzu ya 3 ukurasa 617, hadithi nambari:1329
[401] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 125,hadithi nambari:142
[402] Almustadraku alas-swahihayn juzu ya 4 ukurasa 105,hadithi nambari:7027
[403] Swahihu muslimu juzu ya 3 ukurasa 1458,hadithi nambari :1828
[404] Al-israa:23-24
[405] Swahihul bukhari juzu ya 6 ukurasa 2535,hadithi nambari:6522
[406] Swahihu ibnu hibani juzu ya 2 ukurasa 172,hadithi nambari:429
[407] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 924,hadithi nambari:2477
[408] Swahihu muslim juzu ya 4 ukurasa 1974,hadithi nambari :2548
[409] Al-ahqaf:15
[410] Annisaa:34
[411] Almustadraku als-swahihayni juzu ya 4 ukurasa 167,hadithi nambari:7244
[412] Swahiu muslimu juzu ya 4 ukurasa 1060,hadithi nambari:1436
[413] Sunanut-tir midhy juzu ya 3 ukurasa 465,hadithi nambari:1159
[414] At-twayaalisy juzu ya 1 ukurasa 306,hadithi nambari:2325
[415] Sunanu ibnu maja juzu ya 1 ukurasa 594,hadithi nambari :1851
[416] Annisaa:4
[417] Sunanu abidawud juzu ya 2 ukurasa 242,hadithi nambari:2133
[418] At-twalaq:7
[419] Swahihul bukhari juzu ya 3 ukukrasa 1006,hadithi nambari :2591
[420] Swahihul bukhari juz ya 5 ukurasa 2052,hadithi nambari:5049
[421] Swahihu muslimu juzu ya 2 ukurasa 1060,hadithi nambari:1437
[422] Swahihu ibnu hiban juzu ya 9 ukurasa 483,hadithi nambari:4176
[423] Swahihu muslimu juzu ya 2 ukurasa 1091,hadithi nambari :1569
[424] At-tahrim:6
[425] An-nisaa:1
[426] Swahihul-bukhari juzu ya 5 ukurasa 2233, hadithi nambari:5645
[427] Muhammad:22
[428] Almustadraku alas-swahihayni juzu ya 4 ukurasa 545,hadithi nambari:8526
[429] Swahihu ibnu hiban juzu ya 13 ukurasa 135,hadithi nambari:5818
[430] Sunanu ibnu majah juz ya 2 ukurasa 1211,hadithi nambari:3671
[431] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 902,hadithi nambari:2419
[432] Sunanu abi dawud juzu yz 2 ukurasa 88,hadithi nambari:1532
[433] Swahihu muslimu juzu ya 3 ukurasa 1242,hadithi nambari:1623
[434] Swahihul bukhari juz ya 5 ukurasa 2239, hadithi nambari:5668
[435] Annisaa:36
[436] Almustaraku alas-swahihayni juz ya 4 ukurasa 184,hadithi nambari:7305
[437] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2240,hadithi nambari:5670
[438] Sunanu tirmidhy juz ya 4 ukurasa 333,hadithi nambari :1943
[439] Swahihu ibnu khuzayma juzu ya 4 ukurasa 140,hadithi nambari :2539
[440] Sunanu abu dawud juz ya 4 ukurasa 336,hadithi nambari:5142
[441] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2240,hadithi nambari:5673
[442] Almustadraku alas-swahihayni juzu ya 2 ukurasa 76,hadithi nambari:2378
[443] Sunanu ibnu majah juzu ya 2 ukurasa 1114,hadithi nambari:3358
[444] Swahihu muslimu juzu ya 3,ukurasa 1353,hadithi nambari:48
[445] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 20,hadithi nambari:30
[446] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 776,hadithi nambari:2114
[447] Sunanu ibnu majah juzu ya 2 ukurasa 817,hadithi nambari:2443
[448] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 730,hadithi nambari:1966
[449] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 535,hadithi nambari:1402
[450] Musnadu abiyaala juzu ya 7 ukurasa 349,hadithi nambari:4386
[451] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2238,hadithi nambari:5665
[452] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 14,hadithi nambari :13
[453] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 863,hadithi nambari :2314
[454] Al-anfaal:72
[455] Al mustadraku alas-swahihayni juzu ya 2 ukurasa 670 hadithi nambari:4221
[456] Al-a`raf:199
[457] Sunanu tir midhy juzu ya 4 ukurasa 551,hadithi nambari:2305
[458] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa13 hadithi nambari:10
[459] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 1997,hadithi nambari:2581
[460] Annisaa:116
[461] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2175,hadithi nambari:5431
[462] Al-a`raf :33
[463] Sunanu abi dawud juzu yz 4 ukurasa 246,hadithi nambari:4772
[464] Muhammad:22-23
[465] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 1981,hadithi nambari:2556
[466] Musnadu shihabu juzu ya 1 ukurasa 379,hadithi nambari:654
[467] Al-israa:32
[468] Sunanu ibnu majah juzu ya 2 ukurasa 1332,hadithi nambari:4019
[469] Almustadraku alas-swahihayni juzu ya 4 ukurasa 397,hadithi nambari :8054
[470] Hud:82-83
[471] Almustadraku alas-swahihayni juzu ya 4 ukurasa 396,hadithi nambari:8053
[472] Annisaa:10
[473] Annisaa:6
[474] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukuraasa 2229,hadithi nambari :5631
[475] Al-maida:90
[476] Almaida:33
[477] Sunanul bayhaqi juzu ya 8 ukurasa 283,hadithi nambari:17090
[478] Aal-imran:77
[479] Swahihu muslimu juzu ya 1ukurasa 122,hadithi nambari :137
[480] Annisaa:29-30
[481] Al-anfal:27
[482] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 21,hadithi nambari:34
[483] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 1983,hadithi nambari :2559
[484] Sunanu abu dawud juzu ya 4 ukurasa 276,hadithi nambari :4903
[485] Musnadu Ahmad juzu ya 1 ukurasa 416,hadith nambari :3948
[486] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 2006,hadithi nambari:2599
[487] Sunanu tirmidhy juzu ya 4ukurasa 342,hadithi nambari:1961
[488] Swahihu muslim juzu ya 4 ukurasa 1996, hadithi nambari:2578
[489] Sunanu tirmidhy juzu ya 4 ukurasa 343,hadithi nambari:1962
[490] Al-israa:26-27
[491] Swahihul bukkhari juzu ya 2 ukurasa 848,hadith nambari :2277
[492] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 23,hadithinambari:39
[493] Luqman:18-19
[494] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 93,hadithi nambari:91
[495] Al-hujuraat:12
[496] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 2001,hadithi nambari :2589
[497] Swahihul bukhari juzu ya 6 ukurasa 2581,hadithinambari :6635
[498] Sunanu ibnu maja juzu ya 1 ukurasa 466,hadithi nambari:229
[499] Alhujuraat:11
[500] Almustadraku alas-swahihayni juzu ya 4 ukurasa 102
[501] Sunanu nasai juzu ya 5 ukurasa 80
[502] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2207,hadithi nambari:5546
[503] Al baqara:264
[504] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 915,hadithi nambari :2449
[505] Alqalam: 10-11
[506] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 101,hadithi nambari:105
[507] Annisaa:36
[508] Musnadu abi yaala juzu ya 12 ukurasa 360,hadithi nambari :6928
[509] Annisaa:12
[510] Almaida:90-91
[511] Almustadraku alas-swahihayni juzu ya 2 ukurasa 37,hadithi nambari :2235
[512] Almaida :3
[513] Al-an`am:121
[514] Annisaa;29
[515] Musnadu ahmad juzu ya 4 ukurasa 407,hadithi nambari:19662
[516] An-nahl:90
[517] Al-an`am:152
[518] Almaida:1
[519] Al hashri:9
[520] Swwahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa hadithi nambari:5214
[521] Annisaa:114
[522] Sunanu tirmidhy juzu ya 4 ukurasa 663,hadithi nambari:2509
[523] Sunanu abu dawud juzu ya 4 ukurasa 281,hadithi nambari:4921
[524] Swahihul bukhari juz u ya 2 ukurasa 958,hadithinambari: 2546
[525] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukuasa 69,hadithi nambari:49
[526] Aal`imran:104
[527] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 882,hadithi nambari :2361
[528] Aal`imran:78-79
[529] As-saff:2-3
[530] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 2004,hadithi nambari :2594
[531] Luqman:17
[532] Sunanu tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 9,hadithi nambari:2612
[533] Musnadu shihab juzu ya 1 ukurasa 436,hadithi nambari:747
[534] Sunanu tirmidhy juzu ya 4 ukurasa 370,hadithi nambari:2918
[535] Alhujuraat:6
[536] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 74,hadithi nambari:55
[537] Shuabul iiman juzu ya 10 ukurasa 116,hadithi nambari:7253
[538] Al-israa:29
[539] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 2074,hadithi nambari:2699
[540] At-tuur:48
[541] Albaqara:155-157
[542] Aal`imran:133-134
[543] Fuswilat:34
[544] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2056,hadithi nambari:5061
[545] Swahihul bukhari juz ya 5 ukurasa 2065,hadith nambari :5093
[546] Al-a`raf:31
[547] Swahiu ibnu hibani juzu ya 12 ukurasa 41,hadithi nambari:5236
[548] Sunanu abi dawud juzu ya 3 ukurasa 338,hadithi nambari:3728
[549] Swahihu ibnu hibani juzu ya 12 ukurasa 27,hadithi nambari :5224
[550] Swahiul bukhari juzu ya 2 ukurasa 732,hadithi nambari:1975
[551] Annuur:27
[552] Annuur:59
[553] Swahihu muslimu juz ya 3 ukurasa 1696,hadithi nambari:2154
[554] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2306,hadithi nambari :5896
[555] Sunanu abi dawud juzu ya 4 ukurasa 350,hadithi nambari:5193
[556] Annisaa:85
[557] Swahihul buhari juzu ya 5 ukurasa 2301,hadithi nambari :5878
[558] Swahihu ibnu hibani juzu ya 2 ukurasa 247,hadithi nambari:494
[559] Almujaadila :11
[560] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 1714,hadithi nambari:2177
[561] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 1715,hadith nambari:2179
[562] Sunanu abi dawud juzu ya 4 ukurasa 262,hadith nambari:4845
[563] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2319,hadith nambari:5932
[564] Sunanu abu dawud juzu ya 4 ukurasa 264,hadithi nambari:4855
[565] Swahihu ibnu khuzayma juzu ya 3 ukurasa 130,hadithi nambari:1762
[566] Swahihul bukharu juzu ya 5 ukurasa 2298,hadithi nambari:5870
[567] Almustadraku alas-swahihayni juzu ya 4 ukurasa 293,hdithi nambari:7684
[568] Swahihullbukhari juzu ya 5 ukurasa 2297,hadithi nambari :5869
[569] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 56,hadithi nambari:121
[570] Sunanu abudawud juzu ya 4 ukurasa 261,hadithi nambari:4839
[571] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 2026,hadithi nambari:2626
[572] Swqhihul bukhari juzu ya 3 ukurasa 1090,hadithi nambari:2827
[573] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 418,hadithi nambari: 1183
[574] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 1989,hadithi nambari:2568
[575] Sunanu tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 76,hadithi nambari :2731
[576] Almustadraku alas-swahihayni juzu ya 1 ukurasa 493,hadithi nambari :1269
[577] Swahihu muslimu juzu ya 4 ukurasa 2106,hadithi nambari :2750
[578] Sunanu tirmidhy juzu ya 4 ukurasa 357,hadithi nambari:1990
[579] Swahihu ibnu hiban juzu ya 13 ukurasa 106,hadithi nambari:5790
[580] Musnadu Ahmad juzu ya 5 ukurasa 362,hadithi nambari :23114
[581] Sunanu Abudawud juzu ya 4 ukurasa 297, hadithi nambari :4990
[582] Sunanu ibnu maajah juzu ya 1 ukurasa 511,hadithi nambari:1601
[583] Swahihu Muslimu juzu ya 2 ukurasa 635,hadithi nambari: 923
[584] Almustadraku alas-swahihayni juau ya 1 ukurasa 527, hadithi nambari: 1377
[585] Swahihu ibnu hibani juzu ya 12 ukurasa 344,hadithi nabari: 5534
[586] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2327,hadithi nambari:5955
[587] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 208,hadithi nambari:543
[588] Swahihu ibnu hibani juzu ya 12 ukurasa 357,hadithi nambari:5549
[589] Swahihul bukhari juzu ya ukurasa 2319,hadithi nambari:5936
[590] Sunanu ibnu majah juzu ya 1 ukurasa 110,hadithi nambari: 301
[591] Swahihu ibnu khuzayma juzu ya 3 ukurasa 43,hadithi nambari : 80
[592] Sunanu ibnu majah juzu ya 1 ukurasa 121,hadithi nambari: 337
[593] Swahihu ibnu khuzayma juzu ya 1 ukurasa 43,hadithi nambari: 78
[594] Swahihul bukhari juzu ya 1 ukurasa 65,hadithi nambari: 141
[595] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2053,hadithi nambri: 5052
[596] Swahihu ibnu khuzyma juzu ya 3 ukurasa 246,hadithi nambari: 2003
[597] Sunanu tirmidhy juzu ya 5 ukurasa 216,hadithi nambari: 2980
[598] Swahihu muslimu juzu ya 2 ukurasa 1060,hadithi nambari: 1337
[599] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2394,hadithi nambari: 6169
[600] Sunanu abu dawud juzu ya 3 ukurasa 36,hadithi nambari: 2608
[601] Swahihul bukhari juzu ya 5 ukurasa 2008,hadithi nabari : 4946
[602] Musndu abi yaala:juzu ya 12ukurasa 42,hadithi nambari : 6686
[603] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 639,hadithi nambari: 1710
[604] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 870,hadithi nambari: 2333
[605] Sunanu abi dawud juzu ya 4 ukurasa 256,hadithi nambari: 4817
[606] Swahihu Muslimu juzu ya 1 ukurasa 226,hadithi nambari: 267
[607] Annisaa:29
[608] Almustadraku als-swahihayni juzu ya 2 ukurasa 12, hadithi nambari: 2158
[609] Almustadraku als-swahihayni juzu ya 2 ukursa wa 7 hadithi nambari: 2142
[610] Musnadu Ahmad juzu ya 3 ukurasa 491,hadith nambari: 16056
[611] Swahihu muslimu juzu ya 1 ukurasa 99,hadithinambari: 102
[612] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 732,hadithi nambari:1973
[613] Swahihul bukhari juzu ya 2 ukurasa 730,hadith nambari:1970
[614] Swahihu muslimu juzu ya 3 ukurasa 1228,hadithi nambari:1607
[615] Swahihu ibnu hiban juzu ya 11 ukurasa 402,hadithi nambri :5029
[616] Huyu ni askari wa kikosi cha majini wa uingereza ,alishiriki katika vita ya dunia ya kwanza na ya pili,alilelewa katika mazingira ya kikristo ,na akabobea sana katika itikadi za kikristo,hata hivyo alisilimu baada ya kuisoma Qur-ani tukufu,na vitabu mbali mbali vya kiislamu,ilikuwa mwaka 1924. Ni nukuu kutoka katika kitabu:"Wasemavyo juu ya Uislamu". Cha Dr.Imadudyn khalil.
[617] Kazaliwa mwaka 1954,katika mji wa trafirs katika wilaya ya Michigan America,na akasomea uandishi wa habari katika chuo cha Michigan. Ni nukuu kutoka katika kitabu:"Wasemavyo juu ya Uislamu". Cha Dr.Imadudyn khalil.