Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya tano ambayo imeelezea makatazo ya kuoga katika maji yalio tuwama mahala pamoja, kisha akabainisha maana ya maneno ya hadithi na tafsiri ya hadithi kisha akafafanua kuhusu upokezi wa hadithi hii.
Sherhu Umdatul Ahkam 22 - (Kiswahili)
Sherhu Umdatul Ahkam 21 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya nne, ameeleza maana ya hadithi kwa jumla, kisha akabainisha faida za hadithi: kwamba inafaa kupandisha maji puani na kuyatoa, na nisheria kuosha mikono miwili baada ya kuamka usingizini, aliye lala bila kuambatanisha makalio yake anatakiwa atawadhe upya.
Sherhu Umdatul Ahkam 20 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: umuhimu wa kutawadha vizuri, na uhatari wa kuharakisha kutia udhu, kisha amewahusia watu waoshe viungo vizuri wakati wa kutawadha, katika hadithi: Udhu ni katika matendo mema, miguu inaoshwa katika kutawadha, mwenye kuacha mabaka katika kutawadha ataadhibiwa.
Sherhu Umdatul Ahkam 19 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: ufafanuzi wa hadithi ya tatu, amebainisha daraja ya hadithi hiyo na akafafanua baadhi ya maneno katika hadithi kama vile (waylu) na (aqaab).
Sherhu Umdatul Ahkam 18 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: umuhimu wa kujifunza mambo ya muhimu katika udhu kabla ya kuswali, kisha akataja faida zinazo tokana na hadithi: swala ya mwenye hadathi haikubaliwi, hadadhi ni katika vitenguzi vya udhu…
Sherhu Umdatul Ahkam 17 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya pili na amenukuu maneno ya shekh Albassam katika kufafanua maana ya hadithi, kisha amebainisha hukumu za hadithi kisha akasisitiza uwajibu wa kutawadha vizuri.
Sherhu Umdatul Ahkam 16 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: Maana ya hadithi kwa ujumla kisha historia fupi ya Swahaba Abuu Hurayra, kisha akabainisha maana ya kauli ya Mtume (s.a.w): (hakubali) katika hadithi, kisha akaweka wazi tofauti baina ya hadath na najsi.
Sherhu Umdatul Ahkam 15 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: marejeo mafupi ya hadithi iliyo tangulia kisha akaanza kufafanua hadithi ya pili katika hadithi za kitabu cha Umdatul Ahkam..
Sherhu Umdatul Ahkam 14 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: rai za wanachuoni kuhusiana na hadithi ya Omar bin khatwab, na kwamba hadithi hii ni msingi katika misingi ya kisheria, na kwamba ni nusu ya elimu.
Sherhu Umdatul Ahkam 13 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: ufafanuzi wa hadithi ya kwanza kazungumzia maana ya matendo, akaeleza tofauti baina ya niya na kuazimia, kisha akaeleza kusudio la kuhama katika uislam.
Sherhu Umdatul Ahkam 12 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: maana ya kuhama na kwamba niya inaweza kubadilisha matendo kisha akasema kuwa hadithi ya niya ni nusu ya elimu.
Sherhu Umdatul Ahkam 11 - (Kiswahili)
Shekh anazungumzia: mlango wa kwanza katika kitabu cha Umdatul Ahkam, kisha akabainisha maana ya twahara, kisha akaanza kusherehesha hadithi yakwanza na kutaja historia fupi ya maisha ya Omar bin Khatwab kwa ufupi (r.a).