HUKUMU YA MWANAMUME MZINIFU MWENYE MKE MWEMA NA WATOTO
Jamii ya vilivyomo
Full Description
بسم الله الرحمن الرحيم
HUKUMU YA MWANAMUME MZINIFU MWENYE MKE MWEMA NA WATOTO.
SWALI:
Ipi hukumu ya mwanamume anaefanya uzinifu haliyakua ana mke mwema aliyetulia nyumbani na watoto?
JAWABU:
Ikiwa itadhibiti kuwa mwanamume nimzinifu kwakukiri mwenyewe au kwa kukushuhudiwa na mashahidi wanne waadilifu kuwa amefanya uzinifu na wameona au akakiri mwenyewe kuwa amefanya kitendo hicho kichafu basi hukumu ya kisheria kwa mwanamume kama huyu nikama ifuatavyo:
1-Ikiwa kuna mahakama ya kiislam na dola ya kiislam basi hukumu yake nikupigwa mawe mpaka kufa.
2-Ikiwa hakuna dola ya kiislam mfano kama sisi tunavyo ishi katika nchi hizi za kikafiri basi mwanamke anatakiwa afanye yafuatayo:
(A)-Amkalishe chini mume wake kisha ampe nasaha na mawaidha amkhofishe na Adhabu za moto kwasababu anafanya madhambi miongoni mwa madhambi makubwa, huenda akatubiya na akajutia aliokuwa anafanya, na akaacha hiyo dhambi anayo ifanya ya UZINIFU.
(B)-Ikiwa hakuacha zinaa basi mwanamke anatakiwa aombe talaka haraka iwezekanavyo kwani hajui huyo mzinifu au hawara au kiruka njia anaefanya machafu na huyu mwanamume, ana afya gani!
Kwasababu kuna maradhi mengi na kuachana na mzinifu nikulinda afya njema ya yule mwanamke ambae mume wake nimzinifu kutokana na Maambukizi, pia nikwasababu kakosa sifa ya kua muislam wa kweli na muumini, kwani mtume (S.a.w) anasema :
(Muislam hazini).
Pia Mwanamume huyo anakuwa kapoteza vigezo vya mume kupewa mke ambavyo ni Dini na tabia njema, niwajibu mwanamke achane na huyo mume kwani sio mwema kwake na familia yake kwa ujumla.
(C)-Kama mwanamume huyo mzinifu hakutoa talaka basi atapeleka kesi mahakama ya Qadhi ili wamuachishe kwa lazima.
(D)-Kama haikuwezekana basi itabidi mwanamke ajikhuluu, yaani: kukubali mwanamke kutoa mahali aliyoitoa mume ili waachane, nahiyo nihaki ya mwanamke kwani ndoa sio jela nilazima mume akubaliane na hali hiyo.
KWANINI HATUA ZOTE HIZI?
Kwasababu kuishi na mume mzinifu madhara yake sio kwa mume pekeyake bali yanaenea katika familia nzima, na inakuwa ni sababu ya watoto kuziniwa mpaka wazazi pia.
Imamu Shafii anasema:
ZINAA nideni ukilikopesha basi malipo ni kwa watu wa familia yako.
Subhana Allah!!! Subhana Allah!!!
Na inaweza kupelekea yule mke mwema ambae katulia nyumbani akachezewa na shetani alie laaniwa eti nayeye alipize kisasi akaamuwa azini wakawa wameangamia wote na kizazi chao.
Inna lilah wainna ilahi rajiuna.
USHAURI KWA WAZAZI:
Usikubali kubaki katika maasi na madhambi makubwa eti kwa kisingizio cha kukosa cha kuwalisha watoto, kumbuka kuwa wewe ukikaa na hao watoto ndio bora zaidi kwasababu utawapa malezi bora kwasababu ya imani yako, na Allah atakuletea mtu wa kukusaidia kuwalea kwani mwenye kuacha dhambi kwa ajili ya Allah, Allah humpa jambo lililo bora zaidi.
Na wazazi wenye mabinti walio olewa msiwaache mabinti zenu katika shida bila kuwafatilia na kujua matatizo yao kwasababu Mtume s.a.w mbali nakumuoza binti yake bi Fatma alikuwa akienda kwake mpaka anakaa kitandani wanaongea.
Na yeye Mtume s.a.w ndiye kiigizo chetu na hatofaulu yeyote kama hajamfanya Mtume s.a.w kuwa ni kiigizo chake.
Tunamuomba Allah atukinge na kila shari na uovu. Ameen!