Ni nani aliyeniumba? Na ni kwa nini aliniumba?Kila kitu kinaashiria kuwepo Muumba.
Makala hii imekwisha kutafsiriwa katika
- English - English
- български - Bulgarian
- português - Portuguese
- svenska - Swedish
- العربية - Arabic
- Wikang Tagalog - Tagalog
- Kurdî - Kurdish
- Français - French
- हिन्दी - Hindi
- español - Spanish
- čeština - Czech
- Русский - Russian
- Bahasa Indonesia - Indonesian
- ગુજરાતી - Unnamed
- অসমীয়া - Assamese
- አማርኛ - Amharic
- ไทย - Thai
- Deutsch - German
- Tiếng Việt - Vietnamese
- italiano - Italian
- فارسی دری - Unnamed
- বাংলা - Bengali
- Shqip - Albanian
- 中文 - Chinese
- Nederlands - Dutch
- اردو - Urdu
- Hausa - Hausa
- پښتو - Pashto
- සිංහල - Sinhala
- magyar - Hungarian
- ქართული - Georgian
- bamanankan - Bambara
- Akan - Akan
- Lingala - Unnamed
- ئۇيغۇرچە - Uyghur
- bosanski - Bosnian
Jamii ya vilivyomo
Full Description
Ni nani aliyeniumba? Na ni kwa nini aliniumba?Kila kitu kinaashiria kuwepo Muumba.
Ni nani aliziumba mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake, miongoni mwa viumbe vikubwa ambavyo havijulikani ukubwa wake?
Ni nani aliyetengeneza mpangilio huu mzuri zaidi katika mbingu na ardhi?
Ni nani aliyemuumba mwanadamu kisha akampa usikivu, uoni na akili, na akamjalia uwezo wa kujifunza maarifa na kufahamu uhakika wa mambo?
Vipi unafasiri uumbaji huu wa kiwango cha juu sana katika wa viungo vya mwili wako, na miili ya viumbe vilivyo hai? Na ni nani aliyeviumba kwa ustadi huu mkubwa?
Ni namna gani inajipanga vizuri na kutulia Dunia hii iliyo kubwa, pamoja na kanuni zake ambazo zinaipangilia mpangilio ulio madhubuti kwa miaka yote?
Ni nani ambaye ameweka nidhamu ambazo zinaendesha Dunia hii (uhai na kifo, kuzaana kwa vitu vilivyo hai, usiku na mchana, kubadilika kwa majira, na vinginevyo)?
Je, huu ulimwengu umejiumba wenyewe? Au ulikuja bila ya kutokana na kitu chochote? Au ulipatikana tu kwa ghafla?
Kwa nini mwanadamu anaamini uwepo wa vitu ambavyo havioni? Mfano wa hivyo ni kufahamu, akili, roho, hisia na mapenzi. Hivi siyo kwa sababu yeye anaona tu athari zake? Sasa kwa nini mwanadamu anapinga kuwepo kwa muumba wa ulimwengu huu mkubwa, ilhali anaona athari za viumbe wake na anaona athari ya uumbaji wake na rehema zake?!
Kamwe hawezi yeyote kukubali kuwa hii Nyumba ilipatikana pasi na kuwepo aliyeijenga! Au akasema kuihusu kuwa kutokuwepo ndiko kulikofanya nyumba hii kuwepo! Basi vipi baadhi ya watu wanawasadiki wenye kusema kuwa huu ulimwengu ulikuja bila ya muumba yeyote? Vipi mwenye akili timamu anaweza kukubali kuambiwa kuwa huu mpangilio madhubuti wa ulimwengu huu ulikuja ghafla tu?
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:(أَمۡ خُلِقُواْ مِنۡ غَيۡرِ شَيۡءٍ أَمۡ هُمُ ٱلۡخَٰلِقُونَ، أَمۡ خَلَقُواْ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ). "Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini."[Surat Tuur, aya ya 35-36]
Mwenyezi Mungu utakasifu ni wake na ametukuka.
Kuna mola mlezi na muumba mmoja, ana majina na sifa nyingi tukufu zinazoashiria ukamilifu wake. Miongoni mwa majina yake ni: Muumba, Mwenye huruma, Mwenye kuruzuku, Mwenye ukarimu, na "Allah" ndilo jina mashuhuri zaidi katika majina yake, aliyetakasika, Mtukufu, na maana yake ni: Anayestahiki kuabudiwa peke yake, hana mshirika yeyote.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur-ani tukufu [1]:﴿قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.* ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ * Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.*لَمۡ یَلِدۡ وَلَمۡ یُولَدۡ * Hakuzaa wala hakuzaliwa.*وَلَمۡ یَكُن لَّهُۥ كُفُوًا أَحَدُۢ﴾ * Wala hana anayefanana naye hata mmoja."[Suratul Ikhlaas, aya ya 1-4].
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:﴿اللَّهُ لا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلا نَوْمٌ لَهُ مَا فِي السَّمَوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَنْ ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ وَلا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ﴾ Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote vilivyomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kufanya uombezi mbele yake isipokuwa kwa idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui vyema chochote katika vilivyo katika elimu yake, ila kwa atakalo mwenyewe. Kursi (mahala pa kukanyagia) yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda viwili hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu mno, Mkuu.[Suratul Baqarah, Aya ya 255].
Sifa za Mola Mlezi, aliyetakasika,Mtukufu
Mola Mlezi ni yule ambaye aliiumba ardhi na akaifanya kuwa ni yenye kutii, na akaifanya kuwa ni yenye kufaa kwa viumbe wake, na yeye ndiye aliyeziumba mbingu na vilivyomo ndani yake miongoni mwa viumbe vikubwa, na akaliwekea jua, mwezi, usiku na mchana mpangilio huu madhubuti ambao unaashiria ukuu wake.
Mola Mlezi ndiye ambaye aliyetudhalilishia hewa ambayo hatuwezi kuishi bila kuwepo kwake. Nna yeye ndiye anayetuteremshia mvua na akatudhalilishia bahari na mito. Na yeye ndiye aliyekuwa akitulisha ilhali tuko vijusi kwenye matumbo ya mama zetu hali ya kuwa hatuna nguvu. Na yeye ndiye aliyeifanya damu iweze kupita kwenye mishipa yetu na akaifanya mioyo yetu kupiga kwa kuendelea tangu siku ya kuzaliwa kwetu mpaka tutakapokufa.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:﴿وَاللَّهُ أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئًا وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴾ "Na Mwenyezi Mungu amekutoeni kutoka kwenye matumbo ya mama zenu, hali ya kuwa hamjui kitu chochote, na akakujaalieni usikivu na uoni na macho na nyoyo ili mpate kushukuru."(Surat An-Nahl, aya ya 78)
Mola Mlezi anayeabudiwa ni lazima asifike kwa sifa za ukamilifu
Muumba wetu ameturuzuku akili zinazotambua ukuu wake, na akapandikiza ndani yetu maumbile yanayoashiria ukamilifu wake na kwamba yeye hawezi kusifika kwa sifa za upungufu.
Ibada zote ni lazima ziwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, kwani yeye ndiye mkamilifu, anayestahiki kuabudiwa, na kila chenye kuabudiwa kando na yeye ni batili, ni chenye mapungufu, ni chenye kupatwa na mauti na kuangamia.
Mwenye kuabudiwa haiwezekani awe mwanadamu, au sanamu, au mti, au mnyama!
Haifailii mwenye akili timamu kuabudu isipokuwa Yule aliye kamili. Basi ataabudu vipi kiumbe kilicho chini zaidi yake!
Mola Mlezi hawezi kuwa kijusi katika tumbo la mwanamke, na azaliwe kama wanavyozaliwa watoto!
Mola Mlezi ndiye aliyeumba viumbe, na viumbe vyote vipo kwenye mshiko wake na chini ya nguvu zake. Kwa hivyo hawezi kudhuriwa na mwanadamu na wala hakuna yeyote anayeweza kumsulubisha, kumuadhibu na kumdhalilisha!
Mola Mlezi hawezi kufa!
Mola Mlezi ni yule ambaye hasahau wala halali, wala hali chakula, naye ni mtukufu, haiwezekani kwake kuwa na mke au kuwa na mtoto. Kwa hivyo, Muumba ana sifa za tukufu, na wala haiwezekani hata kidogo asifike kwa sifa za uhitajia au upungufu. Na kila maandiko ambayo ndani yake kuna chenye kuhalifu utukufu wa Muumba miongoni mwa sifa zinazonasibishwa kwa Manabii, basi hayo ni maandiko yaliyobadilishwa na siyo katika Ufunuo sahihi ambao alikuja nao Musa na Isa na wengineo miongoni mwa Manabii rehema na amani ziwe juu yao.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:يَا أَيُّهَا النَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ فَاسْتَمِعُوا لَهُ إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ لَنْ يَخْلُقُوا ذُبَابًا وَلَوِ اجْتَمَعُوا لَهُ وَإِنْ يَسْلُبْهُمُ الذُّبَابُ شَيْئًا لَا يَسْتَنْقِذُوهُ مِنْهُ ضَعُفَ الطَّالِبُ وَالْمَطْلُوبُ (73) "Enyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawatoumba hata nzi, hata kama watajumuika kwa ajili ya hilo. Na nzi akiwapokonya kitu, hawawezi kukichukua kutoka kwake. Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa.مَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ (74) Hawakumheshimu Mwenyezi Mungu anavyostahiki kuheshimiwa. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye nguvu, Mtukufu."[Suratul Hajj, aya ya 73-74].
Je, inaingia akilini ya kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kutuwacha hivi hivi pasi na kutuletea ufunuo?
Je, inaingia akilini kuwa Mwenyezi Mungu aliumba viumbe wote bila malengo. Je, aliviumba bure tu ilhali yeye ni Mwenye hekima, ajuaye zaidi?
Je, inaingia akilini kwamba yule ambaye alituumba kwa mpangilo huu mzuri na ustadi huu mkubwa, na akatudhalilishia vilivyomo mbinguni na ardhini, alituumba bila lengo lolote, au atuache bila majibu ya maswali muhimu zaidi ambayo yanatushughulisha, ka vile: Kwa nini tupo hapa? Na ni nini kitakuwa baada ya kifo? Na ni nini lengo la kutuumba?
Bali Mwenyezi Mungu aliwatuma Mitume ili tujuwe lengo la kuwepo kwetu, na ni kitu gani anataka kutoka kwetu!
Na Mwenyezi Mungu alituma Mitume ili watuelezee kuwa yeye peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, na ili tufahamu namna ya kumuabudu, na ili watufikishie maamrisho yake na makatazo yake, na watufundishe maadili mazuri ambayo tukiyachukua, maisha yetu yatakuwa mazuri, yenye heri na baraka tele.
Na kwa hakika Mwenyezi mungu aliwatuma Mitume wengi kama vile Nuhu, Ibrahim, Musa na Issa, na Mwenyezi Mungu akawapa Mitume hawa ishara na miujiza mbalimbali inayoonyesha ukweli wao na kwamba walitumwa kutoka kwa Muumba.
Na Mtume wa mwisho ni Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - na Mwenyezi mungu alimteremshia Qur-ani tukufu.
Na hakika wametueleza Mitume kwa uwazi ya kuwa maisha haya ni mtihani, na kwamba maisha ya uhakika yatakuwa baada ya kifo.
Na huko kutakuwa na Bustani ya mbinguni kwa waumini ambao walimuabudu Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika na wakaamini Mitume wote, na kuna moto ambao Mwenyezi Mungu ameuandaa kwa ajili ya makafiri ambao waliabudu miungu mingine pamoja na Mwenyezi Mungu au walimkufuru Mtume yeyote miongoni mwa Mitume wake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
يَابَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِنْكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي فَمَنِ اتَّقَى وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (35) "Enyi wanadamu! Watakapokujieni Mitume miongoni mwenu wakikusimulieni Ishara zangu, basi mwenye kumcha Mungu na akatengenea, haitakuwa hofu kwao, wala wao hawatahuzunika.وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا أُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (36) Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hao ndio wenza wa Moto, wao humo watadumu."[Suratul A'araf, aya ya 35-36].
Na amesema Mwenyezi Mungu aliyetakasika:﴿ أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ ﴾ "Je, mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure tu na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?"[Suratul Muuminun, aya ya 115].
Qur-ani Tukufu
Qur-ani tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu ambayo ameyateremsha kwa wa mwisho katika Mitume, Muhammad. Nayo ndio muujiza mkubwa zaidi unaoonyesha ukweli wa Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - nayo ndiyo Haki, na hukumu zake za kisheria, na ni ya ukweli katika habari zake. Na kwa hakika, Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto wale wenye kuikadhibisha Qur-ani ya kwamba walete japo sura moja mfano wa sura zilizopo kwenye Qur-ani hii, lakini wakashindwa kufanya hivyo kutokana na uzuri mtindo wake na ufasaha mkubwa wa maneno yake. Na kwa hakika Qur-ani imekusanya ushahidi mwingi wa kiakili, na hakika mbalimbali za kielimu yenye kuonyesha kwamba Kitabu hiki hakiwezi kikawa kimeundwa na mwanadamu. Bali ni katika maneno ya Mola Mlezi wa wanadamu, aliyetakasika, Mtukufu.
Kwa nini idadi ya Mitume ni nyingi?
Hakika Mwenyezi Mungu aliwatuma mitume tangu mwanzo wa nyakati zilipoanza ili wawalinganie watu kuelekea kwa Mola wao Mlezi, na ili wawafikishie watu hao amri zake na makatazo yake, na wito wao wote ulikuwa ni kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake aliyetukuka. Na kila umma fulani ulipokuwa ukianza kuwacha au kuyachafuwa yale aliyokuja nayo Mtume wao, kama vile jambo la kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu alikuwa akimjukumisha Mtume mwingine jukumu la kwenda kurekebisha njia, na kuwarudisha watu katika umbile lilo salama, la kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii, mpaka Mwenyezi Mungu alipowafunga Mitume hao kwa kumtuma Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - ambaye alikuja na sheria ya kudumu, yenye kuwajumuisha watu wote, yenye kukamilisha na kufutilia mbali sheria zilizokuwa kabla yake. Kisha Mola Mlezi, Mtukufu alichukua dhamana ya kuibakisha na kuidumisha sheria hii mpaka siku ya Kiyama.
Kwa ajili hiyo, sisi Waislamu tunaamini Mitume wote na Vitabu vyote vilivyotangulia kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:﴿ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَاۤ أُنزِلَ إِلَیۡهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰۤىِٕكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَیۡنَ أَحَدࣲ مِّن رُّسُلِهِۦۚ وَقَالُوا۟ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ غُفۡرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَیۡكَ ٱلۡمَصِیرُ﴾ "Mtume ameamini yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. (Wao husema) Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (pia) husema: Tumesikia na tumetii. Tunakuomba msamaha Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako."[2: 285]. [Suratul Baqarah, aya ya 285].
Mtu hawezi kuwa Muumini mpaka awaamini Mitume wote.
Ambaye aliwatuma Mitume ni Mwenyezi Mungu, na yeyote atakayemkufuru mmoja katika mitume hao, basi hakika atakuwa amewakufuru wote. Kwa hivyo, hakuna dhambi kubwa zaidi kuliko mwanadamu kuukata Ufunuo wa Mwenyezi Mungu. Na ili kuingia katika Bustani ya mbinguni, ni lazima kuwaamini Mitume wote.
Basi la wajibu kwa kila mmoja katika zama hizi ni awaamini Mitume wote wa Mwenyezi Mungu, wala hilo haliwezekani isipokuwa kwa kuamini na kumfuata wa mwisho wao ambaye ni Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Mwenyezi Mungu ametaja katika Qur-ani tukufu kuwa mwenye kukataa kumwamini mtume yeyote miongoni mwa mitume wa Mwenyezi Mungu, basi mtu huyo amemkufuru Mwenyezi Mungu, na amekadhibisha ufunuo wake:
Soma Aya zifuatazo:"إنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّهِ ورُسُلِهِ ويُرِيدُونَ أنْ يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّهِ ورُسُلِهِ ويَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ ونَكْفُرُ بِبَعْضٍ ويُرِيدُونَ أنْ يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَلِكَ سَبِيلًا "Hakika, wale wanaomkufuru Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanasema: 'Wengine tunawaamini na wengine tunawakufuru.' Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya.أُولَئِكَ هُمُ الكافِرُونَ حَقًّا وأعْتَدْنا لِلْكَفَرَيْنِ عَذابًا مُهِينًا﴾". Hao ndio makafiri kweli. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha."[Suratun-Nisaa, aya ya 150-151].
Uislamu ni nini?
Uislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumpwekesha, kumtii na kutekeleza sheria yake kwa kuridhia na kukubali.
Na kwa hakika Mwenyezi Mungu alituma Mitume wake wote kwa ajili ya ujumbe mmoja, nao ni kulingania kwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya kumfanyia mshirika yeyote.
Na Uislamu ndiyo dini ya Manabii wote. Kwani wito wao wote ulikuwa mmoja, ingawa sheria zao zilikuwa tofauti. Ama katika zama hizi, Waislamu peke yao ndio bado wameshikamana na dini sahihi ambayo walikuja nayo Manabii wote, na ujumbe wa Uislamu katika nyakati hizi ndio wa haki. Kwa sababu, Mola Mlezi ambaye alimtuma Ibrahim, Musa na Isa ndiye aliyemtuma Mtume wa mwisho ambaye ni Muhammad, naye kwa hakika alikuja na sheria ya Kiislamu yenye kufutilia mbali sheria zilizokuwepo kabla ya sheria yake.
Dini zote ambazo watu leo hii wanaabudu kuzipitia - ukitoa dini ya Uislamu - ni dini zilizoanzishwa na watu, au zilikuwa ni dini za Mwenyezi Mungu, kisha zikachafuliwa na mikono ya watu zikawa ni zenye kuchanganywa na mrundikano wa ushirikina wa uliorithiwa na jitihada za kibinadamu. Ama itikadi ya Waislamu, hiyo ni itikadi ya aina moja iliyo wazi na haibadiliki. Basi itazame Qur-ani tukufu. Utakikuta ni kitabu cha aina moja katika miji yote ya Waislamu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur-ani Tukufu:
قُلْ آمَنَّا بِاللَّهِ وَمَا أُنْزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنْزِلَ عَلَى إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَى وَعِيسَى وَالنَّبِيُّونَ مِنْ رَبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ (84) "Sema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu, na yale tuliyoteremshiwa sisi, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wana wake, na yale aliyopewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatutofautishi yeyote baina yao, na sisi ni wenye kujisalimisha kwake.وَمَنْ يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَنْ يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ 85). Na atakayetaka dini isiyokuwa dini ya Uislamu, basi haitokubaliwa kutoka kwake. Naye akhera atakuwa katika wenye kuhasiri."[Surat Al-Imran, aya ya 84-85].
Waislamu wanaitakidi vipi kuhusu Isa - amani iwe juu yake?
Hivi wajuwa kuwa Waislamu wanapaswa kumwamini Nabii wa Mwenyezi Mungu, Isa, na ni wajibu kwao wampende na wamuheshimu na waamini ujumbe wake ambao ni kulingania kwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, asiyekuwa na mshirika yeyote! Waislamu wanaitakidi kwamba Nabii Isa na Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yao - walikuwa ni Manabii, na wao wawili walitumwa ili kuwaongoza watu kwenye njia ya Mwenyezi Mungu na njia ya kwenda katika Bustani za mbinguni.
Na tunaitakidi kwamba Isa, amani iwe juu yake, alikuwa ni katika Mitume watukufu zaidi ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwatuma, na tunaitakidi kwamba yeye alizaliwa kwa namna ya maajabu. Na kwa hakika Mwenyezi Mungu alitufahamisha katika Qur-ani kuwa yeye alimuumba Isa pasi na kuwa na baba kama ambavyo alimuumba Nabii Adam pasi na kuwa na baba wala mama. Kwani Mwenyezi Mungu ni Muweza zaidi wa kila kitu.
Na tunaitakidi kwamba Isa si mungu, wala si mtoto wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hakusulubishwa msalabani, bali yupo hai, Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwenda kwake ili aje ateremke katika zama za mwisho akiwa ni Hakimu Mwadilifu, na atakuwa na Waislamu; kwa sababu Waislamu ndio wanaoamini kumpwekesha Mwenyezi Mungu, itikadi ambayo alikuja nayo Nabii Isa na Manabii wote.
Hakika Mwenyezi Mungu alitufahamisha katika Qur-ani Tukufu kwamba ujumbe wa Isa, Manaswara waliubadilisha, na kwamba kuna wabadilishaji wapotevu ambao waliipindisha na kuibadilisha Injili na wakaongezea maandiko ambayo Isa hakuyasema, na kinachosadikisha hilo ni uwepo wa nakala tofautitofauti za Injili, na kuwepo ukinzani mwingi katika Injili hizo.
Hakika Mwenyezi Mungu alitufahamisha kwamba Isa alikuwa akimuabudu Mola wake Mlezi na wala hakumtaka yeyote amuabudu yeye. Bali alikuwa akiwaamrisha watu wake wamuabudu muumba wake. Lakini Shetani akawafanya Manaswara kumuabudu Isa, na Mwenyezi Mungu ametupa habari katika Qur-ani kwamba hatomsamehe yeyote anayemuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Isa ikifika siku ya Kiyama, atajitenga mbali na wale waliokuwa wakimuabudu, na atawaambia kwamba: 'Nilikuamrisheni kumuabudu Muumba, na wala sikuwataka muniabudu.' Miongoni mwa ushahidi wa hilo ni maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿یَـٰۤأَهۡلَ ٱلۡكِتَـٰبِ لَا تَغۡلُوا۟ فِی دِینِكُمۡ وَلَا تَقُولُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ إِنَّمَا ٱلۡمَسِیحُ عِیسَى ٱبۡنُ مَرۡیَمَ رَسُولُ ٱللَّهِ وَكَلِمَتُهُۥۤ أَلۡقَىٰهَاۤ إِلَىٰ مَرۡیَمَ وَرُوحࣱ مِّنۡهُۖ فَـَٔامِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۖ وَلَا تَقُولُوا۟ ثَلَـٰثَةٌۚ ٱنتَهُوا۟ خَیۡرࣰا لَّكُمۡۚ إِنَّمَا ٱللَّهُ إِلَـٰهࣱ وَ ٰحِدࣱۖ سُبۡحَـٰنَهُۥۤ أَن یَكُونَ لَهُۥ وَلَدࣱۘ لَّهُۥ مَا فِی ٱلسَّمَـٰوَ ٰتِ وَمَا فِی ٱلۡأَرۡضِۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِیلࣰا﴾ "Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msimse juu ya Mwenyezi Mungu ila kwa lililo la haki. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilompelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa heri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametakasika Yeye kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha."[Surat Nisaa, aya ya 171].
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:(وَإِذْ قَالَ اللَّهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ "Na kumbuka pale Mwenyezi Mungu atakaposema: 'Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: 'Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu?'' (Na Isa) atasema: 'Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa niliyasema, basi bila ya shaka umekwishayajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye ajuaye zaidi wa yaliyofichikana.'"[Suratul Maaidah, Aya ya 116].
Yeyote mwenye kutaka kuokoka katika maisha ya akhera, basi ni wajibu juu yake aingie kwenye Uislamu na amfuate Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake.
Miongoni mwa mambo ya uhakika ambayo wamekubaliana juu yake Manabii na Mitume - rehema na amani ziwe juu yao - ni kwamba hataokoka mtu yeyote katika maisha ya akhera isipokuwa Waislamu ambao walimuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na wala hawakumshirikisha na yeyote katika kumuabudu yeye, na wakawaamini Manabii na Mitume wote. Kwa hivyo, wale ambao walikuwa katika wakati wa Nabii Musa, wakamuamini na wakafuata mafundisho yake, hao ndio Waislamu na waumini wema. Lakini baada ya Mwenyezi Mungu kumtuma Isa, ikawa ni lazima wafuasi wa Musa wamuamini Isa na wamfuate. Basi yeyote aliyemuamini Isa, hao ndio Waislamu wema. Na yeyote aliyekataa kumuamini Isa na akasema kuwa nitabakia kwenye dini ya Musa, huyu sio muumini. Kwa sababu yeye alikataa kumuamini Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu. Kisha baada ya Mwenyezi Mungu kumtuma Mtume wa mwisho, Muhammad, ikawa ni lazima kwa watu wote wamuamini. Kwani Mola Mlezi ndiye aliyemtuma Musa na Isa, na ndiye aliyemtuma Muhammad kama mwisho wa Manabii. Basi yeyote atakayekufuru ujumbe wa Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - na akasema nitabakia tu nikimfuata Musa na Isa, basi huyu sio Muumini.
Wala haitoshi mtu kusema kuwa anawaheshimu Waislamu, wala haitoshi kumfanya awe amefaulu huko akhera kwa kutoa sadaka au kwa kuwasaidia masikini. Bali ni lazima amuamini Mwenyezi Mungu, Vitabu vyake, Mitume wake na Siku ya Mwisho, ili Mwenyezi amkubalie hayo! Hivyo basi, hakuna dhambi kubwa zaidi kuliko shirki, kumkufuru Mwenyezi Mungu na kuukataa Ufunuo ambao Mwenyezi Mungu aliuteremsha, au akakataa unabii wa Nabii wake wa mwisho, Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake. Kwa maana Mayahudi na Manaswara (Wakristo) waliosikia kuhusu kutumwa kwa Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakakataa kumuamini na wakakataa kuingia katika dini ya Uislamu, hao watakuwa katika moto wa Jahannam, watakaa humo milele, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ} "Hakika wale waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina, wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa."[Suratul Bayyinah, Aya ya 6].
Kwa kuwa umeshashuka ujumbe wa mwisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuja kwa wanadamu, basi ni wajibu kwa kila mmoja anayesikia kuhusu Uislamu na akasikia kuhusu Mtume wa mwisho, Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - anapaswa kumuamini na kufuata sheria zake na kumtii katika maamrisho yake na makatazo yake. Kwa hivyo, atakayesikia ujumbe huu wa mwisho na akaukataa, Mwenyezi Mungu hatakubali chochote kutoka kwake, na atamuadhibu huko akhera. Ushahidi wa hilo ni maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَمَن یَبۡتَغِ غَیۡرَ ٱلۡإِسۡلَـٰمِ دِینࣰا فَلَن یُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِی ٱلۡـَٔاخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَـٰسِرِینَ﴾ "Na anayetafuta dini isiyokuwa Uislamu, haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kuhasiri."[Suratul Imran, Aya ya 85].
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:(قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ) "Sema (ewe Muhammad): 'Enyi Watu wa Kitabu! (Mayahudi na Manaswara), njooni katika neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote, wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi semeni: 'Shuhudieni ya kwamba sisi hakika ni Waislamu.'"[Suratul Imran, Aya ya 64].
Ni mambo gani yananilazimu ili niwe Muislamu?
Ili kuingia katika Uislamu, ni lazima kuamini nguzo hizi sita:
Kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwamba yeye ndiye Muumba na Mwenye kuruzuku, Mwendeshaji mambo, Mmiliki, hapana kitu kama mfano wake, na wala hana mke wala mtoto, na kwamba yeye peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa.
Kuwaamini Malaika kwamba wao ni waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, amewaumba kwa nuru na katika akafanya kazi zao ni kuteremsha Ufunuo kwa Manabii wake.
Kuamini Vitabu vyote ambavyo vimeteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa manabii wake, kama vile Taurati na Injili - kabla ya kufanyiwa mabadiliko -, na kitabu cha mwisho, Qur-ani Tukufu.
Kuwaamini Mitume wote kama vile Nuhu, Ibrahim, Musa, Isa, na wa mwisho wao, Muhammad, na kwamba wao ni wanadamu ambao aliwapa nguvu kwa kuwapa ufunuo na akawapa ishara na miujiza ambayo inaonyesha ukweli wao.
Kuamini Siku ya Mwisho, pale ambapo Mwenyezi Mungu atawafufuwa wa mwanzo na wa mwisho, na atatoa hukumu baina ya viumbe wake, kisha atawaingiza waumini katika Bustani za mbinguni na awaingize makafiri katika Moto.
Kuamini mipango ya Mwenyezi Mungu, kwamba Mwenyezi Mungu anajua kila kitu kilichopita na kijacho mbeleni, na kwamba Mwenyezi Mungu alikwishayaandika hayo, akayataka, na akaumba kila kitu.
Uislamu ni njia ya furaha
Uislamu ndiyo dini ya Manabii wote, na sio dini maalumu kwa Waarabu tu.
Uislamu ndiyo njia yenye kuleta furaha ya hakika hapa duniani na yenye kuleta neema ya kudumu huko akhera.
Uislamu ndiyo dini ya kipekee yenye uwezo wa kukidhi haja za kiroho na za kimwili, na kutatua matatizo yote ya kibinadamu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{قَالَ اهْبِطَا مِنْهَا جَمِيعًا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلا يَضِلُّ وَلا يَشْقَى "(Mwenyezi Mungu) Akasema: 'Ondokeni humo nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu, basi atakayeufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى Na mwenye kuupa mgongo utajo wangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa ni kipofu.'"[Suratul Twaha, Aya ya 123-124].
Nitafaidika vipi kwa kuingia katika Uislamu?
Kuingia katika Uislamu kuna faida kubwa, miongoni mwazo ni:
Kufaulu na kupata utukufu duniani, kwa kuwa mwanadamu ambaye ni mja wa Mwenyezi Mungu, na kama sivyo, atakuwa ni mtumwa wa matamanio, Shetani na kila itakacho nafsi.
Mafanikio makubwa zaidi ya akhera ni kuepukana na adhabu ya Moto na kuingia katika Bustani za mbinguni, na kufaulu kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kudumu katika Bustani za mbinguni.
Na wale ambao Mwenyezi Mungu atawaingiza katika Bustani za mbinguni wataishi katika neema ya kudumu milele pasi na kufikwa na kifo wala maradhi ya aina yoyote ile wala maumivu wala huzuni wala kuzeeka, na watapata kila wanachokitaka.
Katika Bustani za mbinguni kuna starehe ambazo macho yajawahi kuona, wala masikio yajawahi kusikia, wala hazijawahi kupitia katika fikira za mwanadamu yeyote.
Katika ushahidi wa hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:﴿مَنۡ عَمِلَ صَـٰلِحࣰا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنࣱ فَلَنُحۡیِیَنَّهُۥ حَیَوٰةࣰ طَیِّبَةࣰۖ وَلَنَجۡزِیَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُوا۟ یَعۡمَلُونَ﴾ "Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, basi hakika tutamhuisha maisha mema, na katika tutawapa ujira wao kwa bora zaidi ya waliyokuwa wakiyatenda."[Suratun-Nahl, Aya ya 98].
Nitapata hasara gani nikiukataa Uislamu?
Mwanadamu atapata hasara ya kukosa elimu kubwa zaidi na maarifa, nayo ni maarifa na elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu. Na atapata hasara kwa kutomwamini Mwenyezi Mungu ambayo inampa mtu amani na utulivu hapa duniani na neema ya kudumu huko akhera.
Mtu atapata hasara ya kutoangalia katika Kitabu kikubwa zaidi cha Mwenyezi Mungu alichokiteremsha kwa watu, na atakosa kukiamini Kitabu hiki kitukufu.
Mtu atapata hasara ya kutoamini Manabii watukufu, na tena atakosa kuwa pamoja nao katika Bustani za mbinguni Siku ya Kiyama, na atakuwa rafiki wa mashetani na wahalifu na miungu inayoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu ndani ya moto wa Jahannam. Na hiyo ndiyo nyumba mbaya zaidi, na ujirani mbaya zaidi.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَلا ذَلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ (15) "Sema: 'Hakika waliohasirika ni wale waliojihasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri.لَهُمْ مِنْ فَوْقِهِمْ ظُلَلٌ مِنَ النَّارِ وَمِنْ تَحْتِهِمْ ظُلَلٌ ذَلِكَ يُخَوِّفُ اللَّهُ بِهِ عِبَادَهُ يَا عِبَادِ فَاتَّقُونِ } . Yatawekwa juu yao matabaka ya moto, na chini yao matabaka. Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni Mimi!"[Surat Az-Zumar, Aya ya 15-16].
Usicheleweshe kuamua!
Dunia sio nyumba ya kudumu milele...
Kila kizuri kitaisha humo, na kila matamanio yatazimika...
Na itakuja siku ambayo utahesabiwa ndani yake juu ya kila ulichokitanguliza, nayo ni Siku ya Kiyama. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَذَا الْكِتَابِ لاَ يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلاَ كَبِيرَةً إِلاَّ أَحْصَاهَا وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا وَلاَ يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا} "Na kitabu kitawekwa mbele. Basi utawaona wahalifu wanavyoogopa mno kwa sababu ya yale yaliyomo humo. Na watasema: 'Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika vyema?' Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote."[Suratul Kahf, Aya ya 49].
Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mtukufu ameeleza kwamba mwanadamu ambaye haukubali Uislamu, basi maishio yake ni kudumu milele ndani ya moto wa Jahannamu.
Hivyo basi hasara si ndogo, bali ni kubwa mno:{وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ } "Na anayetafuta dini isiyokuwa Uislamu, haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kuhasiri."[Surat Al-Imran, Aya ya 85].
Basi Uislamu ndiyo dini ya pekee ambayo Mwenyezi Mungu hatakubali isiyokuwa hiyo miongoni mwa dini zote.
Kwani Mwenyezi Mungu ndiye aliyetuumba, na kwake tutarudi, na dunia hii ni mtihani tu aliotupa.
Kuwa na yakini ya kwamba haya maisha ni mafupi kama ndoto... na hakuna yeyote ajuwaye kuwa atakufa lini!
Utampa jawabu gani Muumba wako atakapokuuliza Siku ya Kiyama: kwa nini hukufuata haki? Kwa nini hukumfuata Nabii wa mwisho?
Ni kwa jibu gani utamjibu Mola wako Mlezi Siku ya Kiyama, ilhali alishakutahadharisha kwa Uislamu kutokana na kuufuata mienendo ya ukafiri, na akakufahamisha kwamba mwisho wa makafiri ni kuangamia motoni milele?
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:﴿وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾ "Na wenye kukufuru na kuzikanusha ishara zetu, hao ndio watakaokuwa wenza wa Moto, humo watadumu."[2: 39]. [Suratul Baqara, Aya ya 39].
Hakuna udhuru kwa atakayeacha haki na akawaiga mababa na mababu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ametueleza kwamba wengi miongoni mwa watu wanakataa kuingia katika Uislamu kwa kuhofia mazingira ambayo wanaishi ndani yake.
Na wengi wao wanaukataa Uislamu kwa sababu ya kutotaka kubadilisha itikadi zao ambazo walizirithi kutoka kwa baba zao na wakazizoea, na wengi miongoni mwao huzuiwa na suala la kutetea kipofu batili ambayo waliirithi.
Na wote hao hawana udhuru kwa hayo, na watasimama mbele za Mwenyezi Mungu bila ya hoja.
Hivyo basi, mweye kukataa uwepo wa Muumba hawezi kutumia udhuru wa kwamba ati aseme: 'Nitabakia na itikadi ya kuamini kutokuwepo Muumba kwa sababu nilizaliwa katika familia isiyoamini uwepo wa Muumba!' Bali inamlazimu aitumie akili yake ambayo Mwenyezi Mungu alimtunuku, na azingatie ukubwa wa mbingu na ardhi, na afikirie kwa akili yake ambayo Muumba wake alimtunuku; ili aweze kutambua kwamba ulimwengu huu una aliyeuumba. Vile vile mwenye kuabudu mawe na masanamu, udhuru wowote katika kuwaiga babu zake, bali inamlazimu aitafute haki na ajiulize: "Vipi ninaabudu kisichokuwa na uhai, ambacho hakinisikii wala hakinioni, wala hakininufaishi chochote?!"
Vivyo hivyo Mkristo ambaye anaamini mambo yanayokwenda kinyume na maumbile ya asili ya mwanadamu na akili, inamlazimu ajiulize: 'Inakuaje Mola Mlezi amuuwe mtoto wake ambaye hakufanya kosa kwa ajili ya makosa ya watu wengine! Hii ni dhuluma! Inakuaje kwa watu kumsulubisha na kumuuwa mtoto wa Mola Mlezi! Je, Mola Mlezi si mwenye uwezo wa kusamehe madhambi ya viumbe bila ya kuwaacha kumuuwa mtoto wake?Je, hakuwa Mola Mlezi ni mwenye uwezo wa kumkinga mtoto wake?
Basi la wajibu kwa mwenye akili ni kwamba afuate haki, na asiwaige mababa na mababu katika batili yao.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:﴿وَإِذَا قِیلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡا۟ إِلَىٰ مَاۤ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ قَالُوا۟ حَسۡبُنَا مَا وَجَدۡنَا عَلَیۡهِ ءَابَاۤءَنَاۤۚ أَوَلَوۡ كَانَ ءَابَاۤؤُهُمۡ لَا یَعۡلَمُونَ شَیۡـࣰٔا وَلَا یَهۡتَدُونَ﴾ "Na wanapoambiwa: 'Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na kwa Mtume', husema: 'Yanatutosha tuliyowakuta nayo baba zetu.' Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?"[Suratul Maaidah, Aya ya 104].
Atafanya nini anayetaka kusalimika na anaogopa kudhuriwa ndugu zake wa karibu?
Anayetaka kusalimika na anahofu mazingira ambayo yanamzunguka, basi anaweza kusilimu na afiche Uislamu wake mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapomfanyia wepesi njia ya heri, ambapo ataweza kujitosheleza mwenyewe na akadhihirisha Uislamu wake.
Basi ni katika wajibu kwako kuukubali Uislamu haraka, lakini si wajibu kwako kumfahamisha aliyeko karibu nawe kuhusu kusilimu kwako, wala hata kuutangaza, ikiwa kufanya hivyo kuna madhara kwako.
Na tambua ya kwamba ukisilimu, utakuwa ndugu wa mamilioni ya Waislamu, na unaweza kuwasiliana na msikiti au kituo cha kiislamu katika mji wako na kutafuta ushauri wao na msaada, kwani hilo litawafurahisha.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِب} "Na mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, humtengezea njia ya kutokea (katika kila balaa). Na humruzuku kwa jiha asiyotazamia."[Surat At-Twalaq, Aya ya 2-3].
Ewe msomaji mkarimu,
hivi si kweli kwamba kumridhisha Mwenyezi Mungu, muumba wako - ambaye amekupa neema zake zote, na akawa anakulisha na hali ya kuwa wewe ni kijusi katika tumbo la mama yako, na anakuruzuku pumzi ambayo unaivuta sasa - kwamba yeye ndiye muhimu zaidi kuliko watu kukuridhia?
Hivi si kweli kwamba kufaulu kwa kidunia na kiakhera kunastahiki kujitolea mhanga kwa kila kisichokuwa hivyo miongoni mwa starehe za maisha zenye kuisha? Ni kweli, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu!
Usiyape nafasi maisha yako yaliyopita yakuzuie kusahihisha mwenendo wako mbovu na kufanya lilo sahihi.
Kuwa Muislamu wa kweli leo hii! Usimpe nafasi Shetani akuzuie kutoifuata haki!
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمْ بُرْهَانٌ مِنْ رَبِّكُمْ وَأَنزلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُبِينًا (174) "Enyi watu! Hakika, umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni nuru iliyo wazi.فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَاعْتَصَمُوا بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا (175) } Ama wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, na wakashikamana sawasawa naye, basi atawatia katika rehema yake na fadhila, na atawaongoa kwenye njia iliyonyooka."[Surat An-Nisaa, Aya ya 174-175]
Je, umejiandaa kuchukua uamuzi mkubwa zaidi katika maisha yako?
Ikiwa haya yote yaliyotangulia yanakubaliana na akili iliyo salama kulingana na wewe, na umeukubali uhakika katika moyo wako, basi ni wajibu kwako kupiga hatua ya kwanza ya kuwa Muislamu. Je, unataka nikusaidie katika kufanya uamuzi ulio bora zaidi katika maisha yako na kukuongoza kwenye namna ya kuwa Muislamu?
Usiache dhambi zako kukuzuia kuingia katika Uislamu, kwani kwa hakika Mwenyezi Mungu ametujulisha katika Qur-ani kwamba yeye anasamehe madhambi yote ya mwanadamu atakaposilimu na akatubia kwa muumba wake. Haata baada ya kukubali kwako Uislamu, ni jambo la kawaida kwamba utafanya baadhi ya makosa; kwa maana sisi ni wanadamu na si malaika walioepushwa kutenda dhambi. Lakini kinachotakikana kwetu ni kuomba msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu na tutubie kwake. Na Mwenyezi Mungu akikuona wewe ni mwenye kufanya haraka kukubali haki na ukaingia katika Uislamu, na ukatamka Shahada mbili, basi hakika yeye atakusaidia kuacha madhambi mengine. Kwani mwenye kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na akaifuata haki, Mwenyezi Mungu anamuwezesha kupata heri zaidi, kwa hivyo usisite kuingia sasa katika Uislamu.
Katika ushahidi wa hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:﴿قُل لِّلَّذِینَ كَفَرُوۤا۟ إِن یَنتَهُوا۟ یُغۡفَرۡ لَهُم مَّا قَدۡ سَلَفَ﴾ "Waambie wale waliokufuru, ikiwa wataacha yale mabaya waliyokuwa nayo, basi watasamehewa yaliyopita."[Suratul Anfaal, Aya ya 38].
Nifanye nini ili niwe Muislamu?
Kuingia katika Uislamu jambo lake ni lepesi wala halihitaji matambiko wala mambo maalumu wala kuhudhuria kwa mtu yeyote. Yamtosha mtu kutamka Shahada mbili akiwa anatambua maana yake huku ameziamini, na inakuwa hivyo kwa kusema: "Ninashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kwamba hakika Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu." Kama itakuwa wepesi kwako kuyasema kwa lugha ya Kiarabu, basi hilo ni vizuri. Lakini kama utapata uzito wa kufanya hivyo, basi itatosha uzitamke kwa lugha yako, na kwa kufanya hivyo utakuwa Muislamu. Kisha itakulazimu kwako kujifundisha dini yako ambayo itakuwa ndio msingi wa furaha yako duniani na kuokoka kwako huko akhera.
Ili kupata faida zaidi kuhusu Uislamu, ninakuusia kusoma kwenye tovuti hii:
Kiungo cha kutafsiri maana ya Qur-ani Tukufu kwa lugha ya....:
Na ili kujifunza jinsi ya kutekeleza Uislamu, tunakushauri uingie kwenye tovuti hii:
Ni nani aliyeniumba? Na ni kwa nini aliniumba?Kila kitu kinaashiria kuwepo Muumba.
Mwenyezi Mungu utakasifu ni wake na ametukuka.
Sifa za Mola Mlezi, aliyetakasika,Mtukufu
Mola Mlezi anayeabudiwa ni lazima asifike kwa sifa za ukamilifu
Je, inaingia akilini ya kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kutuwacha hivi hivi pasi na kutuletea ufunuo?
Kwa nini idadi ya Mitume ni nyingi?
Mtu hawezi kuwa Muumini mpaka awaamini Mitume wote.
Waislamu wanaitakidi vipi kuhusu Isa - amani iwe juu yake?
Ni mambo gani yananilazimu ili niwe Muislamu?
Nitafaidika vipi kwa kuingia katika Uislamu?
Nitapata hasara gani nikiukataa Uislamu?
Hakuna udhuru kwa atakayeacha haki na akawaiga mababa na mababu.
Atafanya nini anayetaka kusalimika na anaogopa kudhuriwa ndugu zake wa karibu?
Je, umejiandaa kuchukua uamuzi mkubwa zaidi katika maisha yako?
Nifanye nini ili niwe Muislamu?