Uislamu ni dini ya Mitume wa Mwenyezi Mungu
Makala hii imekwisha kutafsiriwa katika
- italiano - Italian
- Français - French
- български - Bulgarian
- Türkçe - Turkish
- português - Portuguese
- Русский - Russian
- svenska - Swedish
- العربية - Arabic
- Wikang Tagalog - Tagalog
- English - English
- español - Spanish
- Kurdî - Kurdish
- čeština - Czech
- Deutsch - German
- অসমীয়া - Assamese
- 中文 - Chinese
- Tiếng Việt - Vietnamese
- ไทย - Thai
- тоҷикӣ - Tajik
- Bahasa Indonesia - Indonesian
- magyar - Hungarian
- Shqip - Albanian
- فارسی دری - Unnamed
- বাংলা - Bengali
- Кыргызча - Кyrgyz
- Hausa - Hausa
- فارسی - Persian
- bosanski - Bosnian
- bamanankan - Bambara
- Nederlands - Dutch
- پښتو - Pashto
- ქართული - Georgian
- ئۇيغۇرچە - Uyghur
- azərbaycanca - Azerbaijani
- Kinyarwanda - Kinyarwanda
- Lingala - Unnamed
- română - Romanian
- Luganda - Ganda
Jamii ya vilivyomo
Full Description
Uislamu ni dini ya Mitume wa Mwenyezi Mungu
Uislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa dunia na Mwenye kuiendesha dunia, na kujifungamanisha kwake kwa mapenzi na kumtukuza, na msingi wa Uislamu ni kumuamini Mwenyezi Mungu, na kuwa Yeye Mwenyezi Mungu ni Muumbaji, na kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu kimeumbwa, na kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anastahiki kuabudiwa peke yake asiye na mshirika, hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, majina mazuri yote ni yake na sifa za juu zote ni zake, na ni Mwenye ukamilifu wa moja kwa moja bila ya upungufu, hakuzaa wala hakuzaliwa wala hakuna wa kulinganishwa naye wala kufananishwa naye, wala haingii katika kiwiliwili, na wala hajifanyi mwili wa yeyote katika viumbe wake.
Na Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye hakubali kwa watu dini isiyokuwa Uislamu, nayo ni dini ambayo walikuja nayo Mitume wote rehema na amani ziwe juu yao.
Na miongoni mwa misingi ya Uislamu ni kuamini Mitume wote, nakuwa Mwenyezi Mungu aliwatuma Mitume ili wafikishe maamrisho yake kwenda kwa waja wake na akawateremshia vitabu, na akawa wa mwisho wao ni Muhammad rehema na amani ziwe juu yake, Mwenyezi Mungu alimtuma kwa sheria itokayo kwake sheria ya mwisho yenye kufuta sheria za Mitume wa kabla yake, Mwenyezi Mungu alimpa nguvu kwa alama kubwa, na miongoni mwa alama hizo ni Qur'ani tukufu, maneno ya Mola Mlezi wa viumbe, kitabu kitukufu walichokitambua viumbe, ni miujiza katika muundo wake na matamshi yake na mpangilio wake, ndani yake kuna uongofu wenye ukweli wenye kufikisha katika utukufu duniani na siku ya mwisho, na imehifadhiwa mpaka leo hii kwa lugha ya kiarabu ambayo Qur'ani imeshuka kwa lugha hiyo, haijabadilika wala kubadilishwa ndani yake hata herufi moja.
Na miongoni mwa misingi ya Uislamu ni kuamini Malaika, na kuamini siku ya mwisho na siku hiyo Mwenyezi Mungu atawafufua watu kutoka kwenye makaburi yao siku ya Kiyama ili awahesabu kwa matendo yao, basi atakayefanya mema hali yakuwa ni muumini atakuwa kwenye neema za kudumu ndani ya pepo, na atakaye pinga na akafanya makosa atapata adhabu kubwa ndani ya moto, na miongoni mwa misingi ya Uislamu ni kuamini yote aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu katika heri au shari.
Na waislamu wanaamini ya kwamba Issa (Yesu) ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na yeye si mwana wa Mwenyezi Mungu; kwakuwa Mwenyezi Mungu ni Mtukufu haiwezekani awe na mke au mwana, isipokuwa Mwenyezi Mungu ameeleza ndani ya Qur'ani kuwa Issa alikuwa Nabii aliyepewa miujiza mingi na Mwenyezi Mungu nakuwa Mwenyezi Mungu alimtuma kwa ajili ya kuwaita watu wake kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika, na Mwenyezi Mungu alitueleza kuwa Issa (Yesu) hakuhitaji kutoka kwa watu wamuabudu yeye, bali yeye mwenyewe alikuwa akimuabudu Muumba wake.
Na Uislamu ni dini inayoendana na akili iliyosalimika, na inakubaliwa na nafsi zilizo sawa sawa, Mwenyezi Mungu ameweka sheria ndani ya Uislamu kwa waja wake, nayo ni dini ya heri na utukufu kwa watu wote, Uislamu hauchagui kizazi hiki kuwa ni bora zaidi kuliko kizazi hiki, au rangi hii ni bora kuliko rangi hii, na watu wote ndani ya dini ni sawa sawa, hakuna yeyote anayeonekana bora ndani ya Uislamu juu ya mwingine isipokuwa kwa kiwango cha matendo yake mazuri.
Ni lazima kwa kila mtu mwenye akili timamu aamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi, na Uislamu ndiyo dini, na Muhammad kuwa ni Mtume, na jambo hili halina hiyari kwa mtu; kwakuwa Allah atamuuliza siku ya Kiyama nini aliwajibu Mitume; kama alikuwa ni mwenye imani basi atafaulu kufaulu kwa kiwango cha juu zaidi, na kama alikuwa ni mpingaji atakuwa mwenye kupata hasara kubwa na ya wazi.
Na mwenye kuhitaji kuingia katika Uislamu basi ni wajibu kwake aseme; Ash-hadu an laa Ilaaha illa llaah, wa ash-hadu anna Muhammadan Rasuulullaah (Ninakubali ya kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na ninakubali kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu), aseme hivyo kwa kujua maana yake na kuiamini pia, na kwa kutamka hivyo atakuwa muislamu; kisha atajifunza sheria zingine za Uislamu kidogo kidogo ili aweze kuyatekeleza yale aliyowajibishiwa na Mwenyezi Mungu juu yake.
Kwa faida zaidi tembelea: byenah.com
Uislamu ni dini ya Mitume wa Mwenyezi Mungu